Kina Mbowe na wenzake wanazuka unapokaribia uchaguzi Mkuu tu

Kina Mbowe na wenzake wanazuka unapokaribia uchaguzi Mkuu tu

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Hili sina huruma nalo. Wananchi walio wengi huingizwa kwenye mkenge na viongozi hawa wa upande wa vyama vya upinzani na hata kuthubutu kuwaambia waandamane. Hivi sasa wamekaa kimya huwasikii kabisa na hata ukiwasikia sauti zao ni kama vile unatafuta station ya redio kwenye shortwave2, hatuwasikii kuzungumzia iwe kwenye vikao vya ndani au kuita vyombo vya habari yale mambo muhimu yahusuyo uchaguzi.

Wanasubiri mpaka bado mwezi uchaguzi ndio unawaona kiguu na njia maneno makubwa makubwa na makeke huku wakitoa vitisho kwa serikali iliyopo madarakani, madai yao yanarudi tume sio huru, uchaguzi huu utakuwa sio wa haki na vurugu kibao wakiwapiga virugu na kuwalainisha wananchi kama pweza ili waingie kikaangoni kuwapambanisha na dola.
 
Kusema kweli saa ingine huwaona kama matapeli kuwatapeli Wananchi kwa maneno ili matumbo yao yajae kwa ruzuku za uchaguzi.
Uchaguzi ukipita wananchi wanakuwa na masikio marefu kwa kusikiza mazingahombwe wao viongozi matumbo kama mgongo wa nyangumi.
 
Nyie mlio hapa mnafanya nini zaidi ya kukwapua mabillioni ya fedha za walipa kodi?
 
Kusema kweli saa ingine huwaona kama matapeli kuwatapeli wananchi kwa maneno ili matumbo yao yajae kwa ruzuku za uchaguzi.
Uchaguzi ukipita wananchi wanakuwa na masikio marefu kwa kusikiza mazingahombwe wao viongozi matumbo kama mgongo wa nyangumi.
Matapeli ni maccm waliowadanganya wananchi kuwa nchi haina tena ufisadi wakati ndiyo kwanza ufisadi ulikuwa ndiyo unastawi
 
Mpuuzi wewe kila wakitaka kufanya siasa wanakamatwa, acha na wao wanafamilia zao siyo zinawahitaji.
 
Mbona unakuwa msahaulifu mapema hivi? Si walipigwa ban ya kufanya siasa kwa miaka mitano na mwendazake? Ulitaka uwasikie wapi ikiwa hata vikao vya ndani mlikuwa mnawavamia na kuvuruga?
 
Kipindi wakati mda wote wanapiga kelele na kupambania haki yako kama mwananchi, wewe kama mwananchi ulifanya nini ku suport kupata haki yako?
 
We huna akili.
Eti sina huruma.

Huna huruma we kama nani?
 
Mbona unakuwa msahaulifu mapema hivi? Si walipigwa ban ya kufanya siasa kwa miaka mitano na mwendazake? Ulitaka uwasikie wapi ikiwa hata vikao vya ndani mlikuwa mnawavamia na kuvuruga?
Hakuna hawakupigwa banni ni waoga wa kupindukia, yaani ukitishwa ndio umepigwa bani wamewahi kustand na kupambana maana hilo halikuwepo kisheria waliwahi kwenda mahakamani kupinga,unakuwa kiongozi halafu unakuwa goigoi. waache siasa ,mmemuona Bob wayne?
 
kipindi wakati mda wote wanapiga kelele na kupambania haki yako kama mwananchi, wewe kama mwananchi ulifanya nini ku suport kupata haki yako??
Hili boya kesho tu litaanza kulilia mafao au makato ya heslib
 
... wanasubiri mpaka bado mwezi uchaguzi ndio unawaona kiguu na njia maneno makubwa makubwa na makeke huku wakitoa vitisho kwa serikali iliyopo madarakani,
Hawa wagombea urais CCM walisubiri pia mwaka wa uchaguzi

1617259765648.png
 
hakuna hawakupigwa banni ni waoga wa kupindukia,yaani ukitishwa ndio umepigwa bani wamewahi kustand na kupambana maana hilo halikuwepo kisheria waliwahi kwenda mahakamani kupinga,unakuwa kiongozi halafu unakuwa goigoi. waache siasa ,mmemuona Bob wayne ?
Vipi ulienda kutoa pole kwa walionusurika kifo kwa risasi za mbavu na pliers za meno? Waliopotezwa na kuuawa familia zao ulienda kuwafariji? Au wewe ni wale keyboard warriors ambao uraiani hakuna la maana mnafanya. Uko hapa kusisitiza viongozi wa upinzani wafanye jambo ambalo wewe hauko tayari kulipa gharama yake.
 
Hili sina huruma nalo,wananchi walio wengi huingizwa kwenye mkenge na viongozi hawa wa upande wa vyama vya upinzani na hata kuthubutu kuwaambia waandamane.
Hivi ssasa wamekaa kimya huwasikii kabisa na hata ukiwasikia sauti zao ni kama vile unatafuta station ya redio kwenye shortwave2 ,hatuwasikii kuzungumzia iwe kwenye vikao vya ndani au kuita vyombo vya habari yale mambo muhimu yahusuyo uchaguzi ,wanasubiri mpaka bado mwezi uchaguzi ndio unawaona kiguu na njia maneno makubwa makubwa na makeke huku wakitoa vitisho kwa serikali iliyopo madarakani,madai yao yanarudi tume sio huru ,uchaguzi huu utakuwa sio wa haki na virugu kibao wakiwapiga virugu na kuwalainisha wananchi kama pweza ili waingie kikaangoni kuwapambanisha na dola.
unachawa unawashwawashwa unataka waseme nini c tuliambiwa uchaguzi umeisha ni muda wa kufanya kazi hakuna siasa hadi kipindi cha uchaguzi,au wameruhusiwa kufanya siasa na mikusanyiko
 
Back
Top Bottom