Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Chama cha upinzani cha kisoshalisti nchini Algeria FFS kimetangaza kitasusia uchaguzi wa bunge wa mapema uliopangwa kufanyika mnamo Juni 12 kikisema mazingira ya kufanyika uchaguzi huo hayaridhishi.
Baraza la Taifa la chama cha hicho limesema matayarisho kuelekea uchaguzi huo siyo rafiki na uchaguzi wenyewe hautatoa suluhisho la mizozo inayokabili sekta mbalimbali nchini Algeria.
Baada ya kutanagaz kulivunja Bunge mwezi uliopita, rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria alitoa amri ya kufanyika uchaguzi wa Bunge wa mapema Juni 12.
Hata hivyo maelfu ya raia waliandamana siku iliyofuata kwenye mji mkuu Algiers kupinga kufanyika uchaguzi katika wakati maandamano ya kila wiki ya vuguvuvu la kudai demokrasia la Hirak yakishika kasi.
Vuguvugu hilo ambalo lilifanikiwa kushinikiza kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika mwaka 2019 linataka mageuzi kwenye mfumo wa utawala wa Algeria ambao umekuwepo tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1962.