tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Pascal Mayalla

    Tribute to Dennis Busulwa (Ssebo), Aliiheshimu Sana TCRA na Kuiita Baba! Alitamani isiitwe Mamlaka ya Udhibiti, iitwe Mamlaka ya Ulezi wa Utangazaji!

    Wanabodi Leo tumemuaga mwana tasnia ya habari, Dennis Busulwa kwa jina maarufu la Ssebo Hii ni Tribute yangu to Dennis Busulwa (Ssebo), aliiheshimu sana TCRA na kuiita Baba!. Alitamani TCRA isiitwe Mamlaka ya Udhibiti, iitwe Mamlaka ya Ulezi wa Tasnia ya Utangazaji!, na kuiita Baba Mlezi wa...
  2. R

    TCRA mna ugomvi gani na JF?

    Mliwafungia miezi 3 , wametiii sheria bila shuruti, sasa tatizo liko wapi? Tueleze na sisi umma tujue tatizo ni nini!? Hii ni very very important news outlet kwa Tanzania na dunia kwa ujumla kwa watanzania walio je ya Tanzania na wadau wanaotaka kijia what is happening in Tanzania.
  3. Waufukweni

    TCRA: Wazazi msiwanyang'anye Watoto simu, fuatilieni wanachofanya, ulinzi wa mtoto mtandaoni ni mazungumzo

    Meneja wa Huduma kwa Wateja na Watumiaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kadaya Baluhye, amesema kuwa kuwaandaa watoto kukabiliana na ulimwengu wa kidijitali ni njia bora ya kuwalinda kwa pamoja kama kundi na kama jamii. Ameeleza kuwa badala ya kuwazuia watoto kutumia vifaa vya...
  4. Waufukweni

    TCRA: Picha zako za utupu zikivuja toa taarifa Polisi, usione aibu

    Meneja wa Huduma kwa Wateja na Watumiaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Kadaya Baluhye, amewataka waathirika wa unyanyasaji mitandaoni, ikiwemo uvujaji wa picha za utupu, kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wapate msaada unaostahili. Wito huo umetolewa wakati wa...
  5. olimpio

    Ubora wa mawasiliano nchini umeshuka sana, TCRA fanyeni kazi yenu

    Nimepitia ripoti ya robo ya pili ya mwaka ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania nimeona TCRA wametujulisha kuhusu kushuka kwa ubora wa mawasiliano ya simu nchini lakini hawajasema wanafanya nini baada ya mawasiliano hayo ubora wake kushuka. Ripoti imekaa vizuri sana na hawajataka kuficha kitu...
  6. Club Mate

    Tuisaidie JF yetu, tusambaze elimu ya matumizi ya VPN

    Wakuu, Inaonekana platform yetu pendwa bado imezuiliwa ingawa kifungo hicho kiliondolewa rasmi zaidi ya mwezi mmoja sasa. Bila VPN hutoboi... Tuunganishe nguvu zetu ili kuwafahamisha watu wengi zaidi jinsi ya kuingia JF, kama jinsi akina Erythrocyte walivyopotea mwanzoni, yaani tuhakikishe...
  7. JamiiForums

    Tamko kuhusu JamiiForums kuendelea kuzuiliwa kupatikana nchini Tanzania

    TAARIFA KWA UMMA Mnamo Septemba 6, 2025, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilisitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums na kuzuia upatikanaji wa jukwaa kwa siku 90, kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. Pamoja na kutambua athari kwa haki ya...
  8. Abraham Lincolnn

    Kwanini mpaka sasa Msigwa na TCRA hawajadhibiti habari za Wakatoliki feki kwa kigezo cha 'kubalance' na 'Kuzua Taharuki' Wala Polisi kuzuia maandamano

    Kuna wakati Gerson Msigwa alikuwa mstari wa mbele kuwasema waandishi wa habari kujikita katika kuleta habari zenye uhakika na zenye kuzingatia balance na uhakiki, na zisizo zua taharuki kwa jamii, Watanzania wazalendo tunashangaa si tu kwa press hizi za Wanaojiita wakatoliki ambao si tu kwamba...
  9. ngara23

    JamiiForums kwanini hamuwashitaki TCRA mahakamani?

    Jamii Forums ilifungiwa siku 90 ambayo adhabu hiyo imeisha tarehe 6 December, 2025 Hadi Leo hii Taasisi unahujumu jamii forums Kwa kiburi tu bila sababu ya msingi. 1. Jamii forums ni walipa Kodi wa serikali, kwanini wazuie huduma kibabe, bila taarifa Kwa umma 2. Jamii forums imeajiri vijana...
  10. Fbn

    Kuna matangazo mengi ya mtandaoni ya mikopo ila TCRA na BOT wanajua pesa waliolipwa kwa uongo na uchochezi.

    Watu wamejikuta wakitapeliwa kwa singizio cha unafuu. Hapa serikali ya wapaka mikorogo na ushungu wa FFU uwezi kuona wakisema ili. Embu tupate Futuhi ya watoa mikopo
  11. Pakome

    Operation ya funga na TCRA inazidi kutia kufuli, mtandao wa Signal umefungwa

    Mtandao wa Signal umefungwa Tanzania Hivi sasa unafanya kazi nje ya nchi ya Tanzania lakini kwa watumiaji wa Tanzania wanapotuma meseji au Call zinashindwa kufika
  12. P

    Msaada kwa wanasheria: Nataka kuishtaki TCRA kwa kuendelea kuifungia Jamii Forums

    Ndugu wanasheria wote mlioko humu naomba mnipe muongozo juu ya jambo hili kwani kila kitu kipo wazi toka September jukwaa hili lilifungwa na December hii ilitakiwa lifunguliwe lakini bado. Sasa kama JamiiForums ilitimiza hukumu na sisi Wanajamiiforums, TCRA haijatimiza wajibu wake hvyo kuna...
  13. F

    Hivi ni kwanini serikali ya CCM na wafanyakazi wa TCRA huwa fikra zao hazina uelewa kuhusu JAMII FORUMS

    Hoja inaeleweka sana, na hisia zangu zinawakilisha malalamiko ya watumiaji wengi wa JamiiForums. Kwa kifupi, sababu kuu zinazofanya serikali ya CCM na baadhi ya watendaji wa TCRA kuonekana kutokuwa na uelewa wa kina kuhusu JamiiForums ni hizi: 1. Uelewa mdogo wa dhana ya majukwaa ya mtandaoni...
  14. Traxtion

    Wakuu, hizi nyumba zilizpostiwa na TCRA zipo wapi?

    Nimeona post inayoonesha tangazo la TCRA linalohamasisha kuwa na nyumba zenye namba kwani ni msingi wa mpangilio wa taifa Lakini picha za nyumba walizotumia mbona kama ni nyumba za mambele wakuu. Ina maana wameshindwa kutafuta nyumba za wananchi wao na kuzitumia kama sample mpaka wachukue picha...
  15. Kuchwizzy

    TCRA watupe maelezo ya huu upuuzi

    Tuki entertain upuuzi kama huu, tutaua hata hiki kidogo tulichonacho kwenye tech..... Sijajua kwanini watu wamekua kimya kwenye hiki kitu, lakini ni moja kati ya policy ya kipuuzi kuwahi kutolewa na taasisi yenye mamlaka kama TCRA Nawa hakikishieni kwa 100% watu walionyuma ya hii policy...
  16. R

    PostGE2025 Waziri Simbachawene: Hadi sasa hakuna tishio TCRA kuzima internet

    Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema uamuzi wa kuzima mtandao wa internet ni chaguo la mwisho kabisa pale ambapo hali ya kiusalama inakwa mbaya ambapo amesema hadi kufikia sasa hali ya Tanzania bado ipo shwari na hakuna tishio la kuwafanya TCRA wazime internet kesho December...
  17. Fbn

    Kuna mpango wa teknolojia ya simu kutumia direct kwenye setelite. Je, TCRA mtaweza kuzima kilichopo juu?

    Teknolojia zina shika kasi sana.Kwenye Iphone 17 nimeona mfumo wa setelite ina maana mbeleni kutaweza kuwafanya watu wapate wanachokitaka sehemu yoyote. Huku kwetu tumeona hii tabia ya kuzima internet likuwa jambo la kila uchaguzi unapofika. Je TCRA mumejibangaje kufika angani na mkasi.
  18. M

    TCRA mmepata faida gani kuifungia JamiiForums? Acheni kuwa na maamuzi ya mihemuko

    Bonge wa Zimbabwe mwenyewe alipost picha akiwa na Mama. Rostam alikiri kununua mgodi wa makaa ya mawe. Tulitumia VPN na tukawa tunaingia bila tatizo JamiiForums. Vpn ni salama zaidi kuliko hata hivi mlivyofungua.
  19. Idugunde

    TCRA wanakiuka ibara 18 ya katiba ya JMT . Mpaka sasa hawajaifungulia JamiiForums kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi hii

    Ibara ya 18 ya katiba ya JMT imempa kila mtanzania haki ya kushiriki katika mijadala, kupeana taarifa na kuwa huru kupata habari. Kifungo cha Jamii forum jukwaa ljnalowaunganisha dunia nzima Watanzania kilisha keo saa sita usiku. Lakini mpaka sasa hivi Jamii forum haijafunguliwa Jambo ambalo...
  20. JanguKamaJangu

    PostGE2025 TCRA: Hatukuzima intaneti Oktoba 29, 2025

    Wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima intaneti intaneti siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025, mamlaka hiyo imekanusha ikisema, “TCRA haikuzima intaneti bali ilichukua hatua za...
Back
Top Bottom