tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Pakome

    JamiiForums Tanzania Operation ya funga na TCRA inazidi kutia kufuli, mtandao wa Signal umefungwa

    Mtandao wa Signal umefungwa Tanzania Hivi sasa unafanya kazi nje ya nchi ya Tanzania lakini kwa watumiaji wa Tanzania wanapotuma meseji au Call zinashindwa kufika
  2. P

    JamiiForums Tanzania Msaada kwa wanasheria: Nataka kuishtaki TCRA kwa kuendelea kuifungia Jamii Forums

    Ndugu wanasheria wote mlioko humu naomba mnipe muongozo juu ya jambo hili kwani kila kitu kipo wazi toka September jukwaa hili lilifungwa na December hii ilitakiwa lifunguliwe lakini bado. Sasa kama JamiiForums ilitimiza hukumu na sisi Wanajamiiforums, TCRA haijatimiza wajibu wake hvyo kuna...
  3. F

    JamiiForums Tanzania Hivi ni kwanini serikali ya CCM na wafanyakazi wa TCRA huwa fikra zao hazina uelewa kuhusu JAMII FORUMS

    Hoja inaeleweka sana, na hisia zangu zinawakilisha malalamiko ya watumiaji wengi wa JamiiForums. Kwa kifupi, sababu kuu zinazofanya serikali ya CCM na baadhi ya watendaji wa TCRA kuonekana kutokuwa na uelewa wa kina kuhusu JamiiForums ni hizi: 1. Uelewa mdogo wa dhana ya majukwaa ya mtandaoni...
  4. Traxtion

    JamiiForums Tanzania Wakuu, hizi nyumba zilizpostiwa na TCRA zipo wapi?

    Nimeona post inayoonesha tangazo la TCRA linalohamasisha kuwa na nyumba zenye namba kwani ni msingi wa mpangilio wa taifa Lakini picha za nyumba walizotumia mbona kama ni nyumba za mambele wakuu. Ina maana wameshindwa kutafuta nyumba za wananchi wao na kuzitumia kama sample mpaka wachukue picha...
  5. Kuchwizzy

    JamiiForums Tanzania TCRA watupe maelezo ya huu upuuzi

    Tuki entertain upuuzi kama huu, tutaua hata hiki kidogo tulichonacho kwenye tech..... Sijajua kwanini watu wamekua kimya kwenye hiki kitu, lakini ni moja kati ya policy ya kipuuzi kuwahi kutolewa na taasisi yenye mamlaka kama TCRA Nawa hakikishieni kwa 100% watu walionyuma ya hii policy...
  6. R

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri Simbachawene: Hadi sasa hakuna tishio TCRA kuzima internet

    Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema uamuzi wa kuzima mtandao wa internet ni chaguo la mwisho kabisa pale ambapo hali ya kiusalama inakwa mbaya ambapo amesema hadi kufikia sasa hali ya Tanzania bado ipo shwari na hakuna tishio la kuwafanya TCRA wazime internet kesho December...
  7. Fbn

    JamiiForums Tanzania Kuna mpango wa teknolojia ya simu kutumia direct kwenye setelite. Je, TCRA mtaweza kuzima kilichopo juu?

    Teknolojia zina shika kasi sana.Kwenye Iphone 17 nimeona mfumo wa setelite ina maana mbeleni kutaweza kuwafanya watu wapate wanachokitaka sehemu yoyote. Huku kwetu tumeona hii tabia ya kuzima internet likuwa jambo la kila uchaguzi unapofika. Je TCRA mumejibangaje kufika angani na mkasi.
  8. M

    JamiiForums Tanzania TCRA mmepata faida gani kuifungia JamiiForums? Acheni kuwa na maamuzi ya mihemuko

    Bonge wa Zimbabwe mwenyewe alipost picha akiwa na Mama. Rostam alikiri kununua mgodi wa makaa ya mawe. Tulitumia VPN na tukawa tunaingia bila tatizo JamiiForums. Vpn ni salama zaidi kuliko hata hivi mlivyofungua.
  9. Idugunde

    JamiiForums Tanzania TCRA wanakiuka ibara 18 ya katiba ya JMT . Mpaka sasa hawajaifungulia JamiiForums kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi hii

    Ibara ya 18 ya katiba ya JMT imempa kila mtanzania haki ya kushiriki katika mijadala, kupeana taarifa na kuwa huru kupata habari. Kifungo cha Jamii forum jukwaa ljnalowaunganisha dunia nzima Watanzania kilisha keo saa sita usiku. Lakini mpaka sasa hivi Jamii forum haijafunguliwa Jambo ambalo...
  10. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 TCRA: Hatukuzima intaneti Oktoba 29, 2025

    Wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima intaneti intaneti siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025, mamlaka hiyo imekanusha ikisema, “TCRA haikuzima intaneti bali ilichukua hatua za...
  11. Mudawote

    JamiiForums Tanzania Umuhimu wa Mawasiliano Wakati wa Mizozo ya Kitaifa

    GTs, Katika siku za karibuni tumeshuhudia kuzimwa kwa huduma za mtandao na vizuizi katika majukwaa ya kijamii nchini. Hatua kama hizi, ambazo mara nyingi hutolewa kama “za kiusalama,” zimeleta maswali mazito kutoka kwa wananchi kuhusu uwazi, usimamizi wa taarifa, na haki ya kupata habari...
  12. Lord Denning

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 TCRA kiko wapi? Ngebe zote za kuzima Mitandao leo Dunia yote imejua kilichotokea na nyie mnatajwa kama sehemu ya Watuhumiwa

    Kwenye Jinai kuna watu wanaoitwa accomplices yaaani Watu wanaoshiriki kutenda uhalifu au kufanikisha Uhalifu. Vyombo vya habari vya Kimataifa hasa CNN vimeeleza wazi kuhusu vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania kuuwa watu na kuficha ushahidi. Uzuri kwenye kuficha ushahidi vimesema wazi...
  13. The Watchman

    JamiiForums Tanzania TCRA yakanusha kutoa onyo kwa vyombo vya habari kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi za uhaini

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekanusha onyo lililodaiwa kutolewa na mamlaka hiyo likionya vyombo vya habari kusambaza maudhui yanayoweza kuhatarisha amani kutoka kwa watu wenye kesi za uhaini ambapo imesisitiza kuwa taarifa hiyo ni Potoshi. Soma TCRA yatoa onyo kwa vyombo vya habari...
  14. The Watchman

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 TCRA yatoa onyo kwa vyombo vya habari kusambaza maudhui yanayoweza kuhatarisha amani kutoka kwa watu wenye kesi za uhaini

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma na kuvikumbusha vyombo vyote vya habari nchini, ikiwemo televisheni, redio, machapisho, mitandao ya kijamii, tovuti na majukwaa ya kidijitali, juu ya wajibu wao wa kufuata sheria na kanuni za mawasiliano katika kutoa habari kwa...
  15. Pakome

    JamiiForums Tanzania Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, ruhusuni JamiiForums kwasababu kwa miaka mingi imekuwa ikitatua changamoto za Afrika kupitia habari

    Maendeleo makubwa hayawezi kuja pasipo kufahamu changamoto zinazozuia mafanikio JamiiForums kwa miaka mingi imekuwa ikitatua changamoto za Afrika hasa katika maswala yanayoigusa jamii kwa ujumla kupitia habari, jambo lililokuwa likisaidia Serikali kuona changamoto za Wananchi wake na kutatua...
  16. The Magnifico

    JamiiForums Tanzania Tiktok, Twitter, VPN, P*rn Sites zafunguliwa rasmi Tz. Ama TCRA aliyekuwa night shift amejisahau?

    Nimeamka leo asubuhi VPN yangu ikawa imejizima nilipolala. Kabla sijaiwasha kwa bahati mbaya nikawa nimebonyeza notification moja ya Twitter. Heeeh, cha kushangaza ikafunguka, narudi nyuma na kurefresh TL yangu nashangaa kila kitu kinafanya kazi bila shida. Nikaingia Tiktok nako vilevile, kila...
  17. Lord Denning

    JamiiForums Tanzania Watanganyika mliopo TCRA simameni kuiokoa Tanganyika kuangamizwa na Wazanzibar. Rudisheni mtandao

    Ujumbe kwa Watumishi wa TCRA ambao ni Watanganyika. Wazanzibari wanataka kuiteka Tanganyika na kututawala kwa nguvu. Wamelazimisha Samia atangazwe kwa uchaguzi ambao haukufanyika ba matokeo ambayo yametengenezwa na kila mtu kaona. Simameni kuiokoa Tanganyika dhidi ya huyu mshenzi mzanzibari...
  18. M

    JamiiForums Tanzania Dar es Salaam: Waandamanaji ‘waisalimia’ TCRA. Hii inaenda kubaya zaidi

    Mwanzo nilichukulia wanatania. Wanaonekana kudhamiria
  19. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Kituo kinachofuata ni TCRA - mtandao ni haki yetu, hawapaswi kutuzimia na kutuacha gizani

    Wakuu, Kinachofanyika sasa hivi ni kuhakikisha mawasiliano yanakata, wanafanya kila njia ili tusipate taarifa, tuwe disorganized kukataa udhalimu wa serikali hii. Tunatakiwa kufika TCRA ili tuendelee kupata mtandao, waambiwe kabisa tunachotaka ni mtandao na si kitu kingine, hawawezi...
  20. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania TCRA: Watumiaji wa Huduma ya Intaneti wameongezeka kutoka Milioni 54.1 (Juni 2025) hadi Milioni 56.3 (Septemba 2025) sawa na 4.1%

    Huduma ya intaneti inaonesha kuongezeka utumiaji kutoka milioni 54.1 mwezi Juni 2025 hadi kufikia milioni 56.3 mwezi Septemba 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.1. Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Septemba 2025 inaonesha idadi ya...
Back
Top Bottom