tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. figganigga

    JamiiForums Tanzania GE2025 VODACOM: Kama hutaki tukutumie Meseji za Uchaguzi 2025, Kalalamike TCRA

    Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya Vodacom, iimewataka wananchi ambao hawataki kutumiwa meseji za Uchaguzi, waende kushitaki au kulalamika TCRA. Meseji utake usitake utapokea tu. Huna uhuru wala haki yoyote ya kuamua wala kuchagua kwa mtakwa yako. Pumzika kwa amani Alfonce Mawazo. Muda huu...
  2. Damaso

    JamiiForums Tanzania BBC Swahili na maswali kwa TCRA: JamiiForums Mbuzi wa Kafara?

    Ni takribani masaa 12 sasa tangu BBC Swahili kuchapisha habari inayomhusu mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Chivayo, ikiwemo picha yake akiwa Ikulu ya Tanzania. Tukio hili limeibua mjadala mzito huko mitandaoni: watu wanahoji je, TCRA itachukua hatua sawa na zile ilizochukua dhidi ya...
  3. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Hizi nafasi za kazi za PAPU zinazopitia TCRA hazina infomation za kutosha rekebisheni

    https://www.tcra.go.tz/uploads/documents/sw-1757859650-PAPU_Vacancies_1032107643381814476641029946369102376331757853088906.pdf Angalia kiunga hapo juu kuhusu hizi nafazi za Pan African Postal Union (PAPU) zinaonekana kabisa ni mpunga mrefu maana ni P3 na P4, maombi inabidi yapitie TCRA, hata...
  4. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Polepole asikitishwa na JamiiForums kufungiwa, TCRA mngemkanya Wicknell Chivayo

    Balozi aliyejiuzulu na Katibu wa zamani wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amesema kitendo cha TCRA kufungia Majukwaa ya JamiiForums wakati nchi ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 ni Udikteta, Unyanyasaji na Uvunjifu wa Uhuru wa kupata Taarifa. Polepole ameongeza kuwa...
  5. Fbn

    JamiiForums Tanzania Content wanazopenda TCRA ni mapenzi,umbeya wa wasanii na maisha hata siku moja siawahi kuona za kuchunguza wanyama masaa 180

    Hii nchi yani anaweza msanii kukosea ndani ya siku hiyo mpaka wiki inakwenda ni mwendo wa media uchwara kudili na mada hiyo. wajifunze swahili Max kuna jamaa alikufa mara 6 sasa nasikia huyu jamaa anaweza kwenda kimataifa wanasayansi na wenye nguvu zao wakamfata.Sasa tujiulize swahili max na...
  6. Ponjoro wa Kinondoni

    JamiiForums Tanzania Lazima Kutakuwa na Wafanyakazi wa TCRA Wanaoendelea Kutumia JamiiForums kwa VPN

    Watu wa namna hiyo wanaitwa WANAFIKI, ni watu wabaya sana. Wewe si umezima, sasa unafuata nini huku? Si uende huko FB?
  7. Isaka James

    JamiiForums Tanzania JamiiForums Imezuiwa Siku 90? TOR Ndiyo Suluhisho Bila Form ya TCRA!

    Habari za Jumapili wadau wa JamiiForums! Leo nimekujieni na hii thread, haswa baada ya jana kusikia kuwa JamiiForums imepigwa ban ya siku 90 na TCRA kwa kile wanachodai ni maudhui yanayopotosha! (Kulingana na taarifa rasmi za TCRA Septemba 6, 2025, hii suspension inaanza mara moja na...
  8. Common Folk

    JamiiForums Tanzania Kimahesabu, hakuna tofauti ya kutumia VPN iliyosajiliwa TCRA na kutotumia VPN

    Ikiwa nisipotumia VPN, digital address yangu inakuwa uchi uchi TCRA wananiona eneo niliko na nafanya nini mtandaoni, then TCRA hao hao wakanilazimisha nitumie VPN ili kuzifikia baadhi ya huduma mtandaoni walizozifungia, utaniambiaje tena nijisajili kutumia VPN ili unione nafanya nini mtandaoni...
  9. R

    JamiiForums Tanzania Coalition on Right to Information (CoRI) yaitaka TCRA kuondoa adhabu dhidi ya JamiiForums

    Muungano wa Asasi Za Kiraia unaotetea Haki ya Upatikanaji wa Taarifa (Coalition on Right to Information - CoRI) umelaani vikali uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuisimamisha kwa siku 90 JamiiForums, jukwaa maarufu la majadiliano na uwazi nchini Tanzania. Uamuzi huo umetangazwa...
  10. Fbn

    JamiiForums Tanzania JamiiForums, kama TCRA imefungia siku 90 basi habari zinazohusu CCM hapa uchaguzi hatutaki maana serikali ni CCM

    Adui siku zote anajibiwa kwa mambo yake.Hapa wamekufungia forum ila unachotakiwa ndani ya siku 90 hakuna habari yoyote ya CCm inayotakiwa kuwa kwenye uzi kuanzia sasa. JamiiForums hawa watu funga ID zao kwa siku 90 kwanza. Walichofanya mtandao X ambao twitter wanataka kuleta kwenu na hapo...
  11. JamiiForums

    JamiiForums Tanzania Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums...
  12. Ponjoro wa Kinondoni

    JamiiForums Tanzania TCRA na Jeshi la Polisi Waogopa Kumchukulia Hatua Diamond Platnumz kwa Kutukana Hadharani

    Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na Jeshi la Polisi kwapamoja wameogopa kabisa kumchukulia hatua ndugu Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz baada ya video yake ya matusi ya nguoni kusambaa. Katika video hiyo, Staa huyo wa muziki amewatukana akina mama wote wa Tanzania ambao vijana wao...
  13. Isaka James

    JamiiForums Tanzania Jaza Form ya TCRA Usijepatwa na Shida, Serikali Inakufuatilia Vipi? (Watumiaji wa VPN Special Thread)

    Habari wadau wa JamiiForums, Leo nimekuja na kichwa moto kuhusu hili swala la VPN ambalo limekuwa likiwaka kama moto wa gari la maji mitandaoni! Tangu 2023, serikali kupitia TCRA ikawavunja moyo wengi kwa kusema kila mtu anayetumia VPN, iwe mtu binafsi au kampuni, lazima ajaze form rasmi ya...
  14. Mkalukungone Mwamba

    JamiiForums Tanzania GE2025 TCRA yawataka Waandishi wa Habari kukemea vurugu Uchaguzi Mkuu 2025

    Meneja wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kukemea vurugu na migogoro yoyote itakayojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 badala ya kushiriki kwa njia ya kuripoti au kuchochea...
  15. McLaren

    JamiiForums Tanzania Andrew Kisaka wa TCRA: Wiki 2 zilizopita tulikaa na Tiktok kujadili kuhusu maudhui yasiyofaa

    Wakuu, Akiwa anazungumza leo kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari Kanda ya Mashariki Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, Meneja wa Kitengo cha Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka amesema kwamba mara kwa mara wamejaribu ku-engage na baadhi ya mitandao ya kijamii ili kujadili...
  16. Ponjoro wa Kinondoni

    JamiiForums Tanzania Anayekata internet anatumia akili gani?

    Anakata internet Polepole akiwa live, live ikiisha anarudisha internet na kutupa fursa ya kuangalia alichokisema polepole, yani hata kama ulikuwa umesahau basi ni lazima utakumbuka maana ukiona tu internet inasumbua, unajua kuna jambo, ikirudi tu unasearch. Huyu anamhujumu mama yetu kipenzi wa...
  17. Teknolojia ni Yetu sote

    JamiiForums Tanzania Tanzania kutumia satellite badala ya minara ya simu kufanya mawasiliano

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra) imetoa mwongozo mpya itakayoweza kubadilisha namna ambavyo Watanzania wanavyopata huduma za simu. 🗯️ Mwongozo mpya utoaji wa mawasiliano ya moja kwa moja toka kwenye simu kwenda kwenye satellite, iliyotolewa julai 2025, huruhusu simu za mkononi...
  18. B

    JamiiForums Tanzania TCRA yatoa onyo kali kwa wanaokiuka sheria na kanuni za huduma za utangazaji

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306, na Kanuni zake ina wajibu wa kusimamia huduma za mawasiliano ya Simu na Intaneti, Posta, na Utangazaji wa Redio, Televisheni na Maudhui Mtandaoni. Hivi...
  19. R

    JamiiForums Tanzania GE2025 TCRA:Wanahabari msibebe umbea, hojini sera za vyama

    Meneja wa Huduma za Utangazaji katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amewataka waandishi wa habari na watangazaji nchini kuzingatia sera za vyama vya siasa katika uripoti na mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, badala ya kuendesha mahojiano kwa misingi ya mambo...
  20. M

    JamiiForums Tanzania GE2025 TCRA: Masuala ya uchaguzi siyo kama kutangaza mpira, waandishi hakikisha hujatia chumvi au kusisitiza vitu ambavyo havipo

    Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amewataka watangazaji na waandishi wa habari nchini kuepuka kuonesha mitazamo yao binafsi au kuongeza “chumvi” wakati wa kuripoti Uchaguzi Mkuu wa 2025. Akizungumza tarehe 16 Agosti 2025 katika...
Back
Top Bottom