TANESCO wameanza kuibia wateja waziwazi

TANESCO wameanza kuibia wateja waziwazi

Joined
Dec 22, 2023
Posts
73
Reaction score
80
Habarini za jioni, kwa kweli leo nimepata changamoto kubwa kwa kuliwa pesa yangu. Tufupishe mada mimi nipo wilayani Kisarawe nilivuta umeme tarehe 7.2.2026 na kuanzia hapo nimekuwa nikikatwa kodi ya jengo kila mwezi tsh 1,500/=, cha ajabu leo nilitaka kununua umeme wa tsh 10,000/= muamala ukarudishwa na Yas ikabidi niwapigie wakasema kwa swala hili niwatafute Tanesco kwa namba 180.

Baada ya kuwasiliana na mtoa huduma Tanesco akasema unadaiwa malimbikizo ya kodi ya jengo na halmashauri yangu kwa kipindi cha miezi 10 nikahoji kivipi wakati nimevuta umeme mwezi wa pili na kila mwezi nimekatwa tsh 1,500/= kwa miezi 2?

Akajibu ooh utaratibu wa sasa makato yanaanza kukatwa kuanzia mwaka wa kiserikali unapoanza kwa maana hiyo wamepiga hesabu toka tarehe 01.7.2026. Kwa kweli serikali ibuni vyanzo vingine vya mapato vilevile tupunguze kukopa pesa nje ya nchi na kuzifuja maana mzigo wake wanabeba wananchi wa kawaida
 
Screenshot_20260407-164622.png
 
Akajibu ooh utaratibu wa sasa makato yanaanza kukatwa kuanzia mwaka wa kiserikali unapoanza kwa maana hiyo wamepiga hesabu toka tarehe 01.7.2026. Kwa kweli serikali ibuni vyanzo vingine vya mapato vilevile tupunguze kukopa pesa nje ya nchi na kuzifuja maana mzigo wake wanabeba wananchi wa kawaida
mtoa mada kilichotokea ni kweli ndo hua wanafanya hivyo kila siku. kwa mujibu wao wanasema tanesco inatumika kama mkusanyaji wa hizo hela.

swali la kizushi mkuu, mara ya mwisho umelipa kodi ya jengo ni lini?
 
Tulia hivo wewe usijali ndugu yangu. Tutanyonywa hadi tukome tena kila sector
 
mtoa mada kilichotokea ni kweli ndo hua wanafanya hivyo kila siku. kwa mujibu wao wanasema tanesco inatumika kama mkusanyaji wa hizo hela.

swali la kizushi mkuu, mara ya mwisho umelipa kodi ya jengo ni lini?
Mwezi march
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hii haijakaa sawa kabisa, luku mpya ya mwaka huu, afu ubebeshwe madeni ya mwaka uliopita,
Afu mbaya zaidi wana charge hiyo kodi ya kwa meter, kwa watu wenye apartments au frame za biashara, maana yake kila meter inachajiwa kivyake
 
Habarini za jioni, kwa kweli leo nimepata changamoto kubwa kwa kuliwa pesa yangu. Tufupishe mada mimi nipo wilayani Kisarawe nilivuta umeme tarehe 7.2.2026 na kuanzia hapo nimekuwa nikikatwa kodi ya jengo kila mwezi tsh 1,500/=, cha ajabu leo nilitaka kununua umeme wa tsh 10,000/= muamala ukarudishwa na Yas ikabidi niwapigie wakasema kwa swala hili niwatafute Tanesco kwa namba 180.

Baada ya kuwasiliana na mtoa huduma Tanesco akasema unadaiwa malimbikizo ya kodi ya jengo na halmashauri yangu kwa kipindi cha miezi 10 nikahoji kivipi wakati nimevuta umeme mwezi wa pili na kila mwezi nimekatwa tsh 1,500/= kwa miezi 2?

Akajibu ooh utaratibu wa sasa makato yanaanza kukatwa kuanzia mwaka wa kiserikali unapoanza kwa maana hiyo wamepiga hesabu toka tarehe 01.7.2026. Kwa kweli serikali ibuni vyanzo vingine vya mapato vilevile tupunguze kukopa pesa nje ya nchi na kuzifuja maana mzigo wake wanabeba wananchi wa kawaida
Habari, Ndugu Mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.

Kwanza kabisa, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu ujumbe wako. Akaunti yetu ilikuwa inakabiliwa na changamoto kwa muda, lakini sasa imerejea katika hali ya kawaida.

Kuhusu ujumbe wako, tunaomba tuipke kama maoni yakuzingatiwa kama sehemu ya maboresho ya huduma zetu.

Asante. ^HN
 
Back
Top Bottom