KERO TANESCO Mpanda wanakata umeme ovyo

KERO TANESCO Mpanda wanakata umeme ovyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari jamii forum,

Mimi ni mdau kutoka Mpanda, Katavi.

TANESCO Mpanda wanakata umeme ovyo ovyo. Ni kama vile hakuna mamlaka ya kusimamia.

Yaani kwa siku umeme lazima ukatwe zaidi ya mara 3 na bado weekend wanasema wanamatengenezo kila Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa11 jioni karibia kila weekend. Sasa ni maboresho gani hayo ambayo hayaishi. Wanatupa mashaka ni kama wanatengeneza tatizo makusudi ili wapate mianya ya upigaji.

Kwanini umeme kila kukicha unakatika na hali ya umeme taifa lilishasema hakuna upungufu tena msimu huu wa mvua. Wachunguzwe. Mpanda kuwa na umeme siku nzima imekuwa ni ngumu.

Nawasilisha
 
Nilikua hapo Mpanda nilihisi M27 wamevamia ofisi za Tanesco , kila dkk 5 unakatika ,hakuna Cha mvua Wala nini ni ujinga mtupu Mji kama wa Mpanda kykosa umeme.
 
Habari, Ndugu Mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kujibu ujumbe wako kupitia Jamii Forums. Tulipata changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.

Pole sana kwa changamoto uliyoipata. Tafadhali fahamu kuwa tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au kutokana na hitilafu za dharura, huwa tunatoa taarifa kupitia njia mbalimbali rasmi, ikiwemo ujumbe mfupi wa simu (SMS) na makundi yetu ya WhatsApp. Taarifa hizi huwasaidia wateja wetu kufahamu kinachoendelea katika maeneo yao na muda unaotarajiwa wa kurejea kwa huduma, kwa kuwa baadhi ya matengenezo huchukua muda mfupi na mengine muda mrefu zaidi.

Iwapo hukupokea taarifa hizo, au uliona hazikukidhi matarajio yako, tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.

Je, tayari umejiunga na mojawapo ya makundi yetu ya WhatsApp? Kupitia makundi hayo tunatoa taarifa muhimu kuhusu huduma zetu, pamoja na kupokea maoni na changamoto za wateja. Ikiwa bado hujajiunga, tafadhali tujulishe ili tukuunganishe.

Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako. ^GK
 
Back
Top Bottom