Naamka asubuhi na mapema nikiwa na njaa. Nachemsha chai nakumbuka kitafunwa sina. Natoka barabarani namwona mama muuza mihogo.
"Niuzie ya mia tano!"
"Subiri kidogo, ndiyo kwanza nimeiweka motoni."
Naamua kuketi juu ya jiwe kuisubiria.
Moshi mseto wa vifuu na kuni za kuokoteza, unasambaa...