Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.
Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano...