Nimekuwa nikishuhudia baadhi ya ndugu zetu wa nchi jirani wakitumia mofimu "kwa" katika namna ambayo siyo sahihi kwa mjibu wa Kiswahili sanifu na fasaha. Ninaelewa kuwa kuna utofauti wa kilahaja na matumizi ya Kishengi lakini napenda kukumbusha juu ya matumizi sanifu na fasaha ya mofimu hiyo...