Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,184
- 11,607
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu, lazima tutuinze na kuithamini zawadi hii muhimu kwetu sote. Tufurahie uhai na mema mengi ya Mungu alieyoyajaza katika ulimwengu huu.
Imeibuka kasumba kwa wanywaji pombe hasa vijana, mathalani, anasafiri kutoka mkoa moja kuelekea mkoa mwingine, kutumia vilevi hususani pombe.
Unakuta abiria huyo ama ana mzinga mkubwa wa Konyagi, K-vant au hivi vipombe flani vyenye flavor tofauti tofauti lakini kilevi ni kilekile, ambazo konyagi nao pia wameiga.
Baadhi yao wanakua wamejaza kwenye chupa za maji kukwepa kuonekana wanakunywa pombe, lakini wengine bila soni wanafakamia na michupa vilevile. Mnafika mwisho wa safari kijana kalewa chakari.
Sasa, shaka langu hapa ni kwamba ikitokea ajali, mtu huyu si, ni rahisi sana kupoteza maisha, kwasabb kupata ajali katika hali ya ulevi, hali ambayo inaweza kupelekea ashindwe kujiokoa mwenyewe panapostahili kujiokoa. Na mtu akishalewa akili yake inakua slow kumake decision, lakini pia anaweza akapitiwa usingizi fofofo ambao hata akiamshwa anaweza asiweze kuamka kabisa.
Lakini pia kwasababu pombe huchochea msukumo na mgandamizo wa damu kuwa wa kasi zaidi mwilini, mtumiaji pombe huyu akiumia anaweza kupoteza damu nyingi zaidi na hatimae akapoteza maisha pia.
Rai yangu kwa vijana na wanywa pombe safarini.
Kuweni wastahimilivu na wenye subra hadi mwisho wa safari ndipo kuzitafuta na kuzinywa vilivyo hizo pombe.
Pili, makondakta wa mabasi ambao pia miongoni mwa hutumia pombe wakiwa kazini, kuacha mara moja tabia hii isiyo yakiungwana, na kuwakemea abiria wanao tumia pombe ndani ya mabasi.
Mwisho ni kwa dereva bodaboda wote, ndugu zangu acheni izo mtaisha na kuwa walemavu wote. Kunywa pombe zako baada ya kazi, itakusaidia kuepuka ajali na ulemavu.
Ni kero na usumbufu kwa abiria wasiotumia aina hiyo ya kinywaji.
Asante.