Ni kweli Tanzania inabana Matumizi kama viongozi wake wanavyodai?

Taeyong

Senior Member
Sep 29, 2019
157
201
Salaam wana JF,

Niende direct kwenye point. Tanzania imepeleka watu 736 katika mkutano wa mabadiliko tabia ya nchi huko Dubai #Cop28

Msafara ambao unajumiasha viongozi,wafanyabiashara,makatibu,wasaidizi nk.. Je nani anagharamia tiketi? Maradhi? Posho? Za kwenda na kurudi mpaka mkutano huo utakapokua umekwisha za wajumbe wote kwa taifa ambalo tunakopa kila kukicha !? Nina maswali mengi emu tuanzie hapo kwanza.

Kuangalia orodha ya majina ya wajumbe wote wa msafara fungua link 👉🏿 Mwango Capital: List of Tanzanian Attendees of COP 28

Nakaribiisha maoni.
 
Salaam wana JF, ...Niende direct kwenye point. Tanzania imepeleka watu 736 katika mkutano wa mabadiliko tabia ya nchi huko Dubai #Cop28

Msafara ambao unajumiasha viongozi,wafanyabiashara,makatibu,wasaidizi nk.. Je nani anagharamia tiketi? Maradhi? Posho? Za kwenda na kurudi mpaka mkutano huo utakapokua umekwisha za wajumbe wote kwa taifa ambalo tunakopa kila kukicha !? Nina maswali mengi emu tuanzie hapo kwanza.

Kuangalia orodha ya majina ya wajumbe wote wa msafara fungua link 👉🏿 Mwango Capital: List of Tanzanian Attendees of COP 28

Nakaribiisha maoni.
Wanabana matumizi ya pesa zao binafsi ili waweze kula na kusaza kifisadi pesa za maskini wanaokamuliwa kodi.
 
Wanabana matumizi ya pesa zao binafsi ili waweze kula na kusaza kifisadi pesa za maskini wanaokamuliwa kodi huku maendeleo yakiwa hayaonekani ila kwao wenyewe na familia zao.

Nchi maskini inayotegemea misaada ya wahisani inanunua mashangingi ya mabilioni kila mwaka wakati huo huo hospital hazina dawa na wanafunzi wanakaa chini. Mikopo ya elimu ya juu ni ya kusua sua.

Ukisikia watawala wanazungumza jambo wanakuwa wanajizungumzia wenyewe walio kwenye level moja sio wewe mlala hoi unaishi kwa kuunga unga. Yote wanayofanya ni kwa maendeleo yao binafsi sio wewe mwananchi maskini wanayekuona kama mbwa tu.
Hakika, kama taifa bado tuna safari ndefu sana kuja kupata wazelendo wa kweli kwa taifa hili.
 
Siku zote kwenye mambo ya kipumbavupumbavu yanayowahusu wao hela zipo ila ya maana yanayowahusu wananchi wengi hela hamna
Nchi ngumu imagine hao watu wote kuwalipia hotel, tiketi,vyakula na posho🙌🏿
 
Inaonekana kuwa ndege tunazonunua hazina route zinazoweza kurudisha gharama za uwekezaji.

Sio ajabu mwakani tukamsikia CAG akitoa tathmini ya Air Tanzania kujiendesha kwa hasara kwa kutegemea zaidi tenda za Serikali hasa kwenye safari za Rais na ujumbe wake.

Air Tanzania itakuwa na abiria wachache sana wanaosafiri kwenda India kwa Airbus 220-300 wakati Boeing 737-9 ikiwa imepaki Dubaï kusubiri wajumbe wa mkutano wa mazingira.....Matumizi mabaya ya pesa za umma kwa kiwango hiki yanaweza kutafsiriwa kama uhujumu uchumi kwa makusudi au kutokujali.
 
Hebu tuanze kuwa lama wenzetu na kufanya wenyewe kwa kuchanga hela na kufungua charity tuiite jf charity
Huu umasikini hautaisha labda tubadilike bila kuitegemea serikali sana
Hata wenzetu wana Charities za kila aina na kila leo wanachanga ili kwenye shida wasaidie
Misaada yao kwa wananchi ni mingi sana mpaka mingine kwa roho zao za huruma wanaamua kuwaletea na nyie

Kweli hii shule mtasema ni ya karne hii? Hebu tuanze kwa kusaidia ingawa hatuna utamaduni huo, ila kama mnataka mabadiliko ndio haya
Mloenda Ocean Road mbana mkaishia huko kwa safari mbili tu
1000022051.png
 
Back
Top Bottom