#COVID19 Serikali: Chanjo ya Corona iliyoruhusiwa ni kwa wafanyakazi wa Balozi na taasisi za nje, kwa Watanzania bado hatujaamua

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,766
Msemaji mkuu wa serikali Mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona.

Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu.

Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa kina taarifa na mapendekezo ya tume ya Corona.

Chanzo: ITV habari
 
Kama ile kamati waliyoiunda ilitoa mapendekezo ya njia za kujikinga na Corona, na chanjo ni njia mojawapo ya kujikinga, sasa serikali mbona inajichanganya?

Naona hawa watu huko serikalini bado hawajielewi wanaelekea wapi.
 
Bwashee kamati ya Corona siyo serikali!
 
Msemaji mkuu wa serikali mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona.

Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu.
Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa kina taarifa na mapendekezo ya tume ya Corona.

Source: ITV habari
Ujumbe wa mheshimiwa Paul Kagame....
 
Msemaji mkuu wa serikali mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona.

Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu.
Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa kina taarifa na mapendekezo ya tume ya Corona.

Source: ITV habari
Ikianza kwa wafanyakazi wa ubalozini mwisho wake inaelekea wapi kama sio kwa watanzania wote? Corona naona imekuwa politics
 
CHANJO NI HIYARI. SERIKALI INAOGOPA NINI KULETA KWA WANANCHI?
IMG_20210603_173008_417.JPG
 
Msemaji mkuu wa serikali mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona.

Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu.
Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa kina taarifa na mapendekezo ya tume ya Corona.

Source: ITV habari
Chanjo ya corona haina madhara yoyote
 
Msemaji mkuu wa serikali mh Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi tangazo la serikali linalohusu chanjo ya Corona.

Msigwa amesema chanjo iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa balozi na taasisi za kigeni tu.
Kuhusu chanjo ya Corona kwa wananchi serikali itafanya uamuzi baada ya kupitia kwa kina taarifa na mapendekezo ya tume ya Corona.

Source: ITV habari
It is a beginning for the end. It will unfold eventually. The jab for all.
 
Kuna wakati napata shida kuamini kama mambo yanayosemwa chanzo chake ni serikali kweli au la. Asimilia kubwa ya hizi balozi na taasisi za kimataifa ni waTaznania. Je unaporuhusu taasisi hizo zilete chanjo huoni vipi kuwa waTanzania watachanjwa pia? Ninadhani taarifa nyingi zinatolewa kwa mkanganyo na usiri usiostahiki! Na hakuna shirika na balozi zitaruhusiwa kuingiza chanjo katika nchi yoyote kama nchi hiyo haijaridhia chanjo kwa wananchi wake. Ndio maana toka mwanzo taasisi hizo hazikufanya chanjo. Kwa kufanya sasa, hata wananchi watapewa chanjo. Naiona hii kama ni PR strategy - hakuna ukweli kuwa kuna mchakato tofauti katika chanjo za wananchi.

Iko hivi - mashirika ya Umoja wa Mataifa yanatoa fursa ya kuchanja (kwa hiari) kwa kila mfanyakazi (wa kitaifa na kimataifa) na watu wote wanaotambulika kama wategemezi wake (mara nyingi watoto na mke/mume).
 
Back
Top Bottom