#COVID19 Chanjo ya COVID-19 kwa wafanyakazi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyoko nchini iratibiwa na nani?

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
3,117
5,584
Baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani kuruhusu chanjo ya COVID-19 nchini baada ya kushauriwa na watalaamu wetu, na kwamba mashirika ya kimataifa yalioko hapa nchini yanaruhusiwa kufanya chanjo hiyo kwa wafanyakazi wake.

Sasa kitu ambacho sijakielewa/Sikifahamuni kuwa je ni hospitali gani ambako hizo chanjo zitatakiwa kufanyikia au kila shirika/Balozi watafanya chanjo zake ofisini kwao.

Na je, nchi inaidhinisha aina gani ya chanjo? maana ziko aina nyingi pia za hizo chanjo. Ikumbukwe kuwa katika hayo mashirika wafanyakazi wa Kitanzania ndiyo wengi zaidi na ndiyo watakuwa watanzani wa kwanza kwanza kupata hizo chanjo.

Nadhani pia kuna mshirika ambayo wameshachanja wafanyakazi wao tayari. Ila kisichojulikana/Nisichokijua mimo wanachanjia hospitali gani na pia hizo chanjo zinazoingizwa hapa nchini zinaratibiwa vipi na ni aina gani ya chanjo iliyoidhinishwa na Serikali kuingziwa nchini nakutumika hapa nchini.
 
Sasa na wewe si ukachanje au uache tu?

Unataka muongozo wa serikali isiyojua itakacho? Waziri na naibu wake walioongoza kupinga uwepo wa corona, wakaoinga chanjo, wakaongoza kampeni za kula mananasi, machungwa, mabungo, maparachichi na mafenesi na kujifukiza kwamba ndiyo kinga dhidi ya corona na si hizo chanjo.

Kama serikali ingekua serious ilitakiwa hao wawili wawekwe kando kwanza, kuliko kuongozwa na vigeugeu wasiijua wanachokisimamia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom