chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. SankaraBoukaka

    JamiiForums Tanzania CHADEMA, ACT na wengineo wana lipi jipya kwa wananchi zaidi ya kuikosoa CCM?

    Katika siasa za Tanzania, mara nyingi vyama vya upinzani kama CHADEMA, ACT na vingine huonekana kama sauti za ukosoaji dhidi ya chama tawala, CCM. Hata hivyo, swali kubwa ni: je, wana jipya la kuwapa wananchi zaidi ya maneno ya ukosoaji? Ukweli ni kwamba vyama hivi vimejikita katika mfumo ule...
  2. 0

    JamiiForums Tanzania Tuhuma za Heche zinafukuza matajiri kuchangia CHADEMA

    Kwenye Mwananchi ya Leo kuna habari hiyo. CHADEMA hakuna matajiri bali hohehae, akina mimi tunaochangia buku moja, au jero pale CDM inapoomba tone tone Chama cha Matajiri wanajijua .... wale wanaokitolea 10B Uzuri tunawajua mnaotaka kututoa kwenye reli Anyways kituo kinachofuata ni 88, kisha...
  3. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Ashura Masoud: Tunao ushahidi wa Picha, Video na Miamala ya Fedha kwa baadhi ya Wanachama, tutauweka hadharani

    Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Masoud, amesema chama hicho kina taarifa na ushahidi wa awali unaojumuisha picha, video, mawasiliano pamoja na miamala ya fedha inayodaiwa kutumwa kutoka kwa wanachama wa kile alichokiita "chama cha kikaragosi" kwenda kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA...
  4. Zack Abdul

    JamiiForums Tanzania Ukweli Kuhusu Michango ya Chadema: Niwape Data Kamili

    Chadema Tokea waanze kuchangisha ma michango yao asilimia kubwa ya hiyo michango haija timiza lengp. Waje hapa kubisha niwape data kamili
  5. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania Kwa nini CHADEMA inawapokea waliohama

    Katiba ya nchi na Sheria ya vyama vya siasa inaonesha vyama vya siasa ni vyama vya hiyari na ni mali ya umma. Katiba zote za vyama vya siasa havijaweka kipengere cha kuzuia mtu akihama asirudi tena kwenye chama husika kwa kuwa itakuwa ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi. Ila vyama vyote...
  6. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania CCM kuhusu CHADEMA jifunzeni kwa mfano wa Kaini na Habili

    Kwenye Biblia kuna masimulizi ya wana wawili wa Adamu na Hawa, ambao ni Habili na Kaini. Biblia inasimulia kuwa Kaini ambaye alikuwa ni mkubwa alikuwa Mkulima wakati mdogo wake Habili alikuwa ni mfugaji. Inasemwa kuwa Kaini aliona wivu jinsi mdogo wake Habili sadaka zake zilivyokuwa...
  7. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Baada ya Miezi Miwili kurejea CHADEMA, Selasini ataka Heche achunguzwe

    Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini, amekitaka chama hicho kutumia vyombo vyake vya ndani kuchunguza tuhuma za kifedha zinazowakabili baadhi ya viongozi wake, akisema hatua hiyo itasaidia kubaini ukweli, kuwasafisha watakaobainika kutokuwa na hatia na kuimarisha...
  8. L

    JamiiForums Tanzania CHADEMA wana Matatizo Kichwani. Wanataka Mahakama Ziwe huru Bila Kuingiliwa Halafu Hapo hapo wanataka Lissu Achiliwe Kwa Matakwa yao Na Hisia tu

    Ndugu zangu Watanzania, Kuna watu wana Akili Za Nyumbu Sijapata Kuona . CHADEMA wana Matatizo makubwa sana vichwani Mwao. Ni watu ambao hawajua wanapigania nini na wanataka nini. Ni watu wasio na Dira wala Muelekeo wala kujua wana pigania Nini na wanaelekea wapi. CHADEMA ni chama ambacho ni...
  9. D

    JamiiForums Tanzania KWANINI Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA utumie gharama kubwa kuliko wa CCM

    Wadau naomba kuuliza mnisaidie hili swali kwanini mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA lenye wajumbe wasiozidi 200 lakini ili ufanyike unahitaji zaidi ya Tsh 350 na hapo unafanyika kwa siku moja tu. Kwanza nianze kwa uzoefu miaka ya nyuma nilishakua msaidizi wa sehemu ya ofisi iliyoratibu mikutano...
  10. kavulata

    JamiiForums Tanzania CHADEMA walikosea kukubali kuichoma nchi wanayotaka kuiongoza

    Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya...
  11. Dalton elijah

    JamiiForums Tanzania SI KWELI Godbless Lema amesema "Tunaonekana wasaliti ndani ya CHADEMA"

    Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na machapisho mbalimbali yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mojawapo ya machapisho hayo yanadai kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema, amesema kuwa kwa sasa anaonekana...
  12. Troll JF

    JamiiForums Tanzania UFISADI: Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA kanda ya Kati Amshauri Mnyika kuunda Tume kumchunguza Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho

    John Wegese Heche akiwa bado ananuka Ufisadi wa pesa za Tone kwa Tone uliofanywa akiwa makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kanda ya Kati, Aquilin Claud ameshauri Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika aunde tume ya kumchunguza Makamu Mwenyekiti wa chama...
  13. Q

    JamiiForums Tanzania Marathon ya Millioni 334 ya CHADEMA, sijui kama CCM wanaelewa logic yake

    LIVE UPDATES Tshs. 255.000,000/=. Binafsi sidhani kama Chadema kinashindwa kukusanya kiasi hicho pasipo kuwashirikisha wanachama wake na wananchi wa kawaida. Nina uhakika kinaweza kuandika barua kwa watu binafsi, wafanyabiashara, diaspora 100 tu wakakusanya kiasi hicho. Lakini lengo hasa...
  14. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Mchange: Mnyika aliacha kugombea Ubungo mwaka 2015 kwasababu hakukubaliana na ujio wa Lowassa CHADEMA

    Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwanaharakati wa kisiasa, Habibu Mchange, amedai kuwa aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliamua kutogombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutokana na kutokubaliana na uamuzi wa CHADEMA kumpokea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward...
  15. Tlaatlaah

    JamiiForums Tanzania Huenda pakatokea mivutano ya kikatiba itakayopelekea fujo na vurugu katika mkutano wa Baraza kuu la CHADEMA taifa Septemba 15,2026

    Kuna kila dalili na uwezekano mkubwa sana wa kutokea mivutano ya kikatiba na kupelekea timbwili baya sana litakalo vuruga na kuchochea mkutano wa Baraza kuu la chadema taifa kuvunjika bila muafaka ikiwa sintofahamu ya ufujaji wa pesa za chama isipowekwa sawa mapema hasa kwa wenye dukuduku hilo...
  16. Idugunde

    JamiiForums Tanzania CHADEMA hii ya Lissu na Heche ichangiwe kwa moyo mweupe. Fedha zipo salama hii sio ile SACCOS ya Mbowe.

    Natoa wito kwa Watanganyika wote na Wazinzabari kuichangia Chadema hii maana ipo kwa ajili ya ukombozi wa taifa letu. Kutoa ni moyo. Watu wachangie bila kuwa na hofu . Pesa na michango ipo salama tofauti na zama za Mbowe. Propaganda mfu za wanaCCM waliokosa sera zisisikilizwe. Mimi binafsi...
  17. econonist

    JamiiForums Tanzania Kutoka kwenye CHADEMA haiwezi kuishi bila ruzuku mpaka kufuatilia tone tone

    Nakumbuka mwaka Jana baada ya uchaguzi wa CHADEMA, kundi la G55 lililohamia chaumma lilidai limehama kwa sababu ya CHADEMA kutokushiriki kwenye uchaguzi mkuu kupitia kauli mbiu ya no reform no election. Moja ya hoja za G55 ni kwamba CHADEMA haiwezi kumudu kujiendesha bila Ruzuku, hivyo chama...
  18. Tlaatlaah

    JamiiForums Tanzania Huenda changamoto nyingine kubwa ndani ya CHADEMA ni Katibu Mkuu wake kupwaya kwenye nafasi yake kama mtendaji

    Sote ni mashahidi, kwamba katibu mkuu wa chadema, hata kwa kumtazama tu kwa macho, achilia mbali kumskiliza, ni wazi kabisa anaweza kua ni kichochea cha ufisadi unaoendelea chadema na matumizi mabaya ya ofisi kwa viongozi mbalimbali wa chadema taifa. Ni dhaifu sana, ni muoga mno na kabisa...
  19. L

    JamiiForums Tanzania Kuifarakanisha CHADEMA kwa wizi wa Heche.

    Niliwaza kabla haijapendekezwa na wengine,kumbe NAMI niliwaza kama wengine walivyowaza. Kua kama wanasema Heche ni mwizi wa Hela za michango ya tonetone,basi nilitamani sana atokee mtu aombe namba ya akaunti ya Benki ya Heche binafsi ili tumchangie kwa sababu Heche anapiga kazi ya kibabe sana...
  20. N

    JamiiForums Tanzania Nini kifanyike ili kuthibiti wanaharakati,magaidi na CHADEMA wasikwamishe salamu za mama kwenye matamasha ya miaka 30 ya bongo fleva?

    Baada ya kufanya uchunguzi wa kina na timu yetu toka Lumumba tumegundua kuwa wanaharakati, magaidi na CHADEMA ndio walionzisha zomea zomea wakati mwana FA alipotaka kuwasilisha salamu za serikali kwenye tamasha la bongo fleva. Tuligundua wanaharakati , magaidi na vijana wengi wa CHADEMA...
Back
Top Bottom