chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. Uamuzi wa wabunge wa CHADEMA kutohudhuria Bunge na kujiweka karantini ni sahihi kabisa

    Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe, alilitangazia Taifa kuwa wabunge wa Chadema, hawataendelea tena na vikao vya Bunge na wameamua kujiweka karantini kwa siku 14, ili kuangalia afya zao kama wameambukizwa ugonjwa huu wa COVID 19 au laa Ni uamuzi wa busara kabisa...
  2. Hivi RC Makonda ametekeleza ahadi yake ya kuwakamata wabunge wa Chadema, aliowaita wazururaji ambao aliwafananisha na changudoa?

    Jana mnamo majira ya saa 6 mchana, tulimsikia RC Makonda, akitoa amri kwa wabunge wa Chadema, ambao waliamua kutoendelea na vikao ya Bunge, kwa kile walichokiita kujiweka karantini kutokana na hofu ya ugonjwa wa COViD 19 Akawapa saa 24 wawe wamerejea kuendelea na vikao hivyo vya Bunge na kama...
  3. B

    CHADEMA wameweka rekodi ambayo itawagharimu katika harakati za kutaka Madaraka ya nchii hii

    Ni Sasa CHADEMA wameshafanya makosa makubwa ambayo yatawapa taabu sana huko mbeleni historia haitawaacha Salama. Dunia Sasa iko kwenye vita kubwa ya covid19, hili ni tukio kubwa kihistoria vizazi na vizazi watajifunza hili Janga Kama ambavyo leo historia inazungumzia WW-I na WW-II au kuhusu...
  4. Napata wasiwasi wabunge wa CHADEMA wanataka kuwafanya nini! Serikali, Bunge wote wanaacha kujadili bajeti wanawajadili

    Kuna anayefikiri kama mimi? 1. Walipoondoka bungeni spika alifurahi na kusema hata wasipokuwepo ccm wanatosha kupitisha mambo yao na cdm hawana madhara yoyote na hawajavunja sheria wala kanuni yoyote. 2. Akaja Rais Magufuli akaonyesha kuumia sana kwa wao kuondoka akatoa amri wasilipwe posho...
  5. Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

    SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu. Amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019...
  6. K

    CHADEMA haijafa, na bila muujiza haitakufa kabla ya Oktoba

    Nimeona niandike juu ya CHADEMA na si kwa Upinzani kwa jumla kwa sababu ndio waliolengwa wafe. Sijui kama ACT-Wazalendo nao wanatakiwa wafe, au wao watavumiliwa wawepo pamoja na usumbufu wanaowapa watawala. CHADEMA sio kwamba wapo tu na wana - 'savaivu' bali wanatambuliwa kuwa ni tishio kubwa...
  7. Baada ya Uchaguzi, Je Chadema itweza kuishi bila ruzuku?

    Najiuliza hili suali sababu projections za wataalamu was siasa wanaona kama Chadema imeshakufa. Na kwenye uchaguzi ujao huenda isipate hata 5% ya kura zote za uchaguzi ili wapate ruzuku hata kidogo. Maana kila siku wanazidi kuumbuka na kukosa imani kwa wananchi. Hasa hii drama ya kutudanganya...
  8. Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

    Spika Job Ndugai amesema wabunge wa CHADEMA ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini wanahesabika kama watoro na wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni. Pia wamepaswa kufanya kipimo cha Covid19 kabla hawajaingia bungeni ==...
  9. CHADEMA kwanini inacheza ngoma za Rais Magufuli?

    Kila mtu anajua mpango wa kuivuruga Chadema unavyokwenda. Sasa why Chadema Wana play na mchezo huo? Kwanini wasijifunze kucheza tofauti? Kama mpango ni kuwavuruga mfukuzane ..why msiamue 'hafukuzwi' mtu Kwa sasa? Muache anaetaka kutoka atoke Tu mwenyewe? Why kumjibu mtu kama Makonda...
  10. J

    Zamani CCM walisema Zidumu fikra " sahihi" za mwenyekiti Sasa Chadema wanasema ' Zidumu fikra za mwenyekiti'

    Najaribu kukumbuka tu kiapo changu cha uanachama na salamu zetu ndani ya chama wakati ule wa awamu ya kwanza. Kwanza tuliitana " ndugu" pili tuliamini katika uhai wa chama ndio tulisema " kidumu chama cha mapinduzi" na tatu tuliamini katika uwezo wa mwenyekiti wetu na tulifahamu kuwa yeye ni...
  11. RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

    Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku. RC Makonda amesema kwa...
  12. T

    Udhaifu wa Chadema sio Uimara wa CCM!

    Nimeona mjadala mkali na wa kuvutia ukiendelea kuhusu uhai wa vyama vya upinzani hususan Chadema kuelekea 2020. Nikiri mapema kuwa, hatuna vyama vya siasa Bali tuna vikundi vinavyopambana na dola. Hata CCM yenyewe ilikwisha acha siku nyingi kuwa Chama cha siasa badala yake uhai wake unategemea...
  13. Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

    Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi...
  14. J

    Kwanini wabunge wanaotoka Chadema na kuhamia CCM wanakuwa na " chuki binafsi" na chama chao cha zamani?

    Tofauti na wabunge wa vyama vingine wanaohamia chama tawala CCM, wabunge wanaotoka Chadema huwa na chuki sana na chama chao cha zamani kana kwamba walifukuzwa. Wabunge wote wa Chadema waliotoka CCM labda ukimtoa Ole millya wakisimama tu bungeni jambo la kwanza ni kuikejeli Chadema. Hata huyu...
  15. J

    Dkt. Slaa: Bunge la bajeti ni takwa la kikatiba haliwezi kuahirishwa, Chadema wanatafuta huruma ya kisiasa lakini wamechelewa

    Balozi wetu huko Sweden amesema bunge la bajeti ni takwa la kikatiba hivyo haliwezi kuahirishwa kwa sababu zozote. Katiba inatamka wazi kuwa bunge la kbajeti litakaa kwa siku zisizozidi 45 ukiondoa week end na sikukuu hivyo hakuna namna unaweza kuahirisha na wabunge wanalijua hilo. Pili Dr...
  16. Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

    Wabunge wawili wa Chadema, David Silende (Momba) na Peter Lijualikali (Kilombero) wamehudhuria bungeni leo licha ya chama chao kuwataka wabunge wake kutohudhuria vikao vya Bunge ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, Hivi karibuni...
  17. J

    Mbowe ameathirika na " Hofu" baada ya kijana wake kupambana na Corona lakini CHADEMA ni kubwa kuliko familia

    Binafsi nakubaliana kabisa na wabunge wa CHADEMA kujiweka katika karantini kwa sababu hiyo ni haki yao ya kikatiba ya kulinda uhai. Kilichonishangaza kidogo ni namna Chadema inavyofanya maamuzi bila vikao rasmi vya kikatiba kuketi. Kwa mfano wabunge wa chama kutoingia bungeni ni muhimu wakapata...
  18. J

    Mkurugenzi Manispaa Ubungo amfukuza Meya Jacob kwa kutumia katiba ya zamani ya CHADEMA ambayo haitumiki

    Meya Jacob wa manispaa ya ubungo amesema yeye bado ni mwanachama halali wa Chadema na kwamba mkurugenzi wa manispaa hiyo ametumia katiba ya zamani ya Chadema ambayo ilishafanyiwa marekebisho kumuengua. Bonny anasema aliletewa barua ya kufukuzwa umeya jana Jumapili saa 3 usiku nyumbani kwake...
  19. Inadaiwa kuna Wabunge wa CHADEMA wataenda bungeni kesho

    Nashauri Chadema iwapuuze maana ni wale walio kwe list ya kuunga mkono juhudi na kwenda Ccm kabla ya uchaguzi october. Chadema wapuuzeni waacheni waende wakapambane na Corona.
  20. J

    Askofu Gwajima: Chadema wana mapepo ndio maana wamesusia bunge na wanalazimisha makanisa yafungwe, Wameshindwa katika jina la Yesu!

    Mambo ni moto mambo ni fire ndani ya Kanisa la ufufuo na uzima. Askofu Gwajima amesema wabunge wa Chadema wamesusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona ila ukweli ni kwamba wabunge hao wamepagawa na mapepo. Askofu Gwajima amewaambia waumini wake ambao ni wapenzi wa Chadema kuwa chama...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…