Mnyika usiwe Katibu wa kwanza katika historia ya CHADEMA aliyeua Baraza la Wanawake (BAWACHA), thamini juhudi zao kukufikisheni mahali mlipo leo

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
180
380
Unapozungumzia Viti maalum wa 2020 hawa 19 WALIOCHAGUANA unazungumzia ngome kongwe ya viongozi wa wanawake wa chadema (BAWACHA).

Nakukumbusha katibu mkuu utendaji wako juu ya hili kundi sio tu unawaathiri wao kama viti maalum bali unaathiri mfumo mzima wa balaza lako la wanawake ambalo ndio linaunda moja ya mabalaza unayoyaongoza.

Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa kujishusha ili kulinda image na maslahi mapana ya mtaji wa watu wako, na jambo hili liko kwa kila mwanasiasa hata magufuli ambaye tunamuona ni mkali nayeye anaukomo katika kuamua hata kwa majizi yaliyomo ndani ya chama chake, kama tunavoona hajaweza hayatumbua yote sababu mengine akiyatumbua anatumbua mzizi au mfumo mzima wa chama, bali labda tu ameweza kupunguza kidogo kiwango cha ulaji wao kisiwe kikubwa cha kutisha kama tunavojua CCM ni ILE ILE.

Na ww mheshishimiwa katika hili jambo unapaswa kujishusha, sabab ukipima faida gani utaipata kwa kusimamia msimamo wako au wakamati kuu..? Utagundua hakuna faida maana hao wabunge hata ukiwafukuza uwanachama bado wataendelea kulindwa na spika na watapata haki zao zote, lakin hasara kubwa utakayopata ni kupoteza kundi kubwa sana la wanawake ambao limeibuka kwa kasi tena kwa nguvu ya hao hao kina halima mdee na wenzie, pia utakosa ruzuku ya bure.

Najua utasema nalinda value ya chama chetu na maamuzi ya vikao ya chama , katika hili nakwambia kuwa hakuna kitu kinaitwa maamuzi kama wanachama wako hawayapi thamani maamuzi hayo, bali huonekana ni maamuzi hewa yasio akisi mtazamo wa wanachama walio wengi, kwaiyo tukianzia kwenye mzizi wa jambo je maamuzi yenu walikuwa sahihi..? Utagundua haya kuwa sahihi mbele ya wanachama, sabab kama yangekuwa sahihi mbele yao wangetoka kuandamana kupinga matokeo kama mlivotangaza, kwaiyo kama wanachama hawajaona value ya maamuzi yenu na nyinyi mnaongoza kwa niaba yao mnapaswa kukaa mguu sawa kuna mahali mmekosea, ima wanachama wenu hawajui itikadi yenu au hawajui namna gani unapaswa kulinda value ya itikidi yenu.

Na kukumbusha kuwa pamoja ya kuwa mfumo wenu wa maamuzi ni kamati kuu ya chama lakin unapaswa kuamini na kuthamini mtazamo wa hawa wamama wa chadema ambao kimsingi ndio nguzo kubwa ya BAWACHA.

Haiwezekani watu makini kama wale ambao wamekesha magerezani wakitetea chama na wengine juzi tu ndio wamefutiwa mashtaka wakubali hivi hivi tu kuwa viti maalum bila kuwa na MTAZAMO SAHIHI.

Sio kila kitu kiongozi unaweza kukiona, hata kwenye familia sio kila kitu baba utakiona kuna vingine mama ataviona na vikaleta manufaa, hivo hivo wamama wa chadema wameona hayo ndio maamuzi sahihi lakin hayawezi kufanikiwa sabab wababa mmeyakalia wameamua kujichukulia hatua mnapaswa kuyathamini.

La sivyo chagua baina kubakiwa na kiti bila wanachama au kujishusha na kurekebisha muelekeo wa kisiasa.

Alijishusha Mandela baada ya kufungwa miaka mingi na akakaa nao meza moja wasaliti wake hatimae akawa rais na nyinyi hamuwezi kushindwa , wekeni karata zenu sawa sawa.
 
CCM mlichokifanya ni kibaya sana, mnatumia resources za nchi kujaribu ku-justify madudu mliyoyafanay kwenye uchaguzi mkuu? hawa ma dada mmewaponza tayari, sasa watakuwa ni wabunge wa mahakana kwa muda wote wa miaka mitano.

Watakayosema Bungeni haitakuwa kwa niaba ya CDM bali watayasema kwa niamba ya Kambi rasmi ya Mahakamana na Ndugai.
 
Hao wanawake wote fukuza uanachama,kisha chama kipeleke majina mengine tofauti na hao 19 iwe fundisho kwa wengine!
 
Ninaamini kuwa Mnyika anajua ya kuwa wabunge hawa 19 hawajiendea tu ...hata km yeye hakuhusika....ila Kuna jambo limejificha hapa....Huenda mh.MBOWE akawa anahusika ila katibu Mnyika anacheza mchezo wa KADENGE kwa ile theory kuntu: THESIS +ANTI-THESIS=SYNTHESIS....

Hapa ni hiyo SYNTHESIS itafutwayo.

Haitokuwa mara ya kwanza kwa mh.Spika Ndugai kumlinda MBUNGE aliyefukuzwa na CHAMA CHAKE.

Alifanya kwa wengi tu.

Hata Spika wa nyuma alimlinda mh.ZITTO KABWE alipofurushwa kutoka CHADEMA. Kwa hiyo Nina imani kabisa MNYIKA ameshapima hayo ya kuwa WAKIFUKUZWA basi WATABAKI tena kama wanaCHADEMA na mbeleni watakuwa WABUNGE wa upinzani wasio na CHAMA kwa miaka yote hii 5.

Mbowe amebadilisha GIA ANGANI kama alivyofanya 2015?!!!

Kwanini Katibu wake Mnyika anazungukazunguka baada ya HAYO?!!!
 
Mwelekeo sahihi ni kususia bunge na Serikali ya kidikteta ya Magufuli
Dunia inaona na mapambano yanaendelea
 
CCM mlichokifanya ni kibaya sana, mnatumia resources za nchi kujaribu ku-justify madudu mliyoyafanay kwenye uchaguzi mkuu? hawa ma dada mmewaponza tayari, sasa watakuwa ni wabunge wa mahakana kwa muda wote wa miaka mitano.

Watakayosema Bungeni haitakuwa kwa niaba ya CDM bali watayasema kwa niamba ya Kambi rasmi ya Mahakamana na Ndugai.
Yaani mambo yafanyike chadema alaumiwe ccm. Ndiyo maana chama kinaenda kufa hakuna brain mle
 
Bawacha siyo Mdee na hao wakina Bukaya peke yao.

Lazima wafuate sheria na taratibu za chama chao, kama hawawezi wakaunde chama kipya naamini watasajiliwa upesi sana kwa msaada wa marafiki zao wa CCM.
 
Inakuaje hii issue wanaccm ndio mnaifurahia sana kuliko CDM ambao msimamo wao ulikua hautambui matokeo yote na kutopeleka hao viti maalum iweje CCM ndio wafurahi? Tafakari hayo
 
Chakula chenye sumu hakiliwi, hata ukiwa na njaa vipi.

Hii BAWACHA ishakuwa sumu.... kama wanajiweza wakaanzishe chama chao. Sikio haliwezi kuzidi kichwa.
 
Yaani mambo yafanyike chadema alaumiwe ccm. Ndiyo maana chama kinaenda kufa hakuna brain mle
Kwahiyo CHADEMA ndio ilimfutia mashtaka binti fulani alafu asbuhi yake ikampeleka kuapa?

Unajua kuna vitu mnafanya hata wapuuzi wanafahamu ni nyie. TISS hakuna bright people
 
Kuwatetea kina mdee unahitajika kuwa mnafiki Sana.Unamrukaje katibu mkuu kwa kuhalalisha usaliti?
 
Back
Top Bottom