Wapinzani jifunzeni kupitia siasa za Zanzibar, Nawaasa CHADEMA, ACT Wazalendo waende kwa hatua

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mada inahusika.

Hakuna kurudi nyuma na ni muhimu kusoma alama za nyakati kufikia malengo yaliyokusudiwa.

SOMO KUTOKA ZANZIBAR.
Huwezi kuzungumzia siasa za upinzani Zanzibar ukamuacha Maalim Seif na wenzake na siasa za wakati huo za CUF. Maalim Seif na wenzake walipitia hatua kadhaa katika kujenga upinzani wa kweli ingawa kuna wakati mazingira huwaelemea na kukaribia kupotea.

Kwa ufupi. Uhodari wa Uongozi wa Maalim na Wenzake mara zote umekuwa ukiwavusha salama kila baada ya uchaguzi licha ya vitimbi vya dhulma kutoka kwa watawala.

Miaka 25 ya vyama vingi kuweza kustahamili vitimbi vya watawala na ikawa hujatoka kwenye mstari si mchezo kwa viongozi wetu wa Afrika.

Haya yalifanyika kila baada ya chaguzi ili kubaki kwenye njia ya reli.

Waligoma kuyatambua matokeo kwa umoja wao na kutafuta kuungwa mkono kote duniani ingawa hakukupatikana suluhu ya mara moja. (1995)

Kulifanywa muafaka wa hadaa na wapinzani walikubali kutekeleza muafaka ingawa hakuna hatua kubwa. CUF wakati huo ilipata kujiimarisha na ili kupata influence ya kimataifa haikutizama jambo lengine.

Waligoma chaguzi za marejeo, waliwekewa pingamizi, walikwenda mahakamani na njia za kususia kijamii (social Boycott).

Kwa mbinu hizo na kwa mazingira ya Zanzibar walifanikiwa kuwatikisa watawala kisawa sawa na kuufanya utawala kuwa mgumu.

Siri yake ilikuwa ni uongozi imara wa Upinzani ukiongozwa na Maalim Seif wenye maono, umoja na mshikamano kwa kipindi chote hicho hadi 2015.

Jambo lengine ni kuwa na AJENDA. Zanzibar tofauti na bara kuna Ajenda, Tabia na tamaduni za watu ni tofauti. Kwa hivyo Vyama vijuwe Fursa zilizopo na kuzitumia ili ukifanya maamuzi yawe na athari.

CUF wakati huo ilitumia Fursa hizo Zanzibar kujijenga na kupeleka Ajenda mbele ya HAKI SAWA KWA WOTE.

Kitu cha kujifunza kutoka Zanzibar ni kwamnba upinzani umetumia njia zote zikiwemo za kususa, kugoma, mahakama, maridhiano, kujikweza na kujishusha ilimradi wasitoke kwenye Lengo.

Siri nyengine nikwamba watawala waliokuwepo walau walikuwa na hisia japo ya mbali ya Diplomasia na Demokrasia na ndio maana Upinzani ulitumia njia zinazokubalika kujiimarisha.

Kilele cha yote na kilicho live hadi sasa ni PRODUCT ya GNU kama ndio matokeo chanya ya JASHO NA DAMU kwa Upinzani kwa miaka yote 25 ya vyama vingi. Bahati mbaya hili liko Zanzibar Pekee na Tanzania Bara. Ingawa kuna changamoto ya KATIBA kupuuzwa.

Nakusudia kuwaambia CHADEMA na ACT kufika hatua hiyo kunahitaji SACRIFICE ya kutosha ya roho za watu kupotea, kuteswa kufungwa na kudhalilishwa. Hili halikuja bure.

Jifunzeni mbinu, mikakati, uongozi, ujasiri, umakini kutoka Upinzani Zanzibar

Someni mazingira kwa nini kuna wakati wapinzani waligoma? kwa nini walienda mahakamani kwa ishu gani? kwa nini walifanya maandamano na sababu zake? kwa nini walifanya miafaka zaidi ya 3 japo kama ilikuwa feki? kwa Nini?

Someni mazingira ya UTAWALA ULIOPO wa 2015- 2025 ili uwasaidie kuwa na mikakati imara na yenye Result.

NIWASAIDIE KUTAZAMA HAYA.
i. Je, mazingira ya kitabia na hulka ya Mkuu wa nchi yanaamini katika Diplomasia na Demokrasia?

ii. Je, kuna mbinu gani mlizotumia za kuleta madai yenu zilizofanikiwa?
iii. Je, vyombo vya Dola vina mtazamo gani kuhusu Upinzani? Vipi Mahakama? Vipi Bunge? Vipi mihimili ya kitaasisi kama Polisi N.K?

iv. Je, mna ungwa mkono vipi kimataifa hadi sasa na jee kuna mwelekeo wa kupata result za muda mfupi au bado sana?

v. Je, kuna fursa zozote za kimaridhiano kusaidia kutatua changamoto zenu kutoka kwa Utawala? Tambueni hili haliji bure mpaka muwe na nguvu za kumtikisa Mtawala Jee kwa sasa mnaweza kumtikisa? Jee mnaweza kuleta Social Boycott na ikaleta athari na Risk za kiuchumi na kijamii kwa Tanzania mzima kama ilivyokuwa Zanzibar miaka ile?

MWISHO KWA LEO

Nadhani kuna cha kujifunza. Tambueni mbinu sio moja tu ya kugomea kila pahali. Kuna mbinu nyengine unatazama wakati na kusogeza ajenda zenu mbele.

Kwa maoni yangu UTAWALA wa sasa hauamini katika DIPLOMASIA NA DEMOKRASIA, unaamini nguvu na kutweza ili maendeleo yafikiwe.

Fukueni vitabu na uzoefu wenu ili mngamue kilicho nyuma ya pazia muweze kusnitch mwelekeo wa huu Utawala kwa miaka mitano hadi kumi ijayo.

Fanyeni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi ili badala ya kuamini kujijenga na kusogeza ajenda zenu mbele msije mkajifuta na kupoteana kutokana na wakati.

Kwangu mimi the best aproach ni ile dhaifu ya struggle within and Outside. Hii ni ya kubahatisha lakini ina guarantee moja muhimu .HUWEZI KUKOSA KOTE KOTE.

Wakati unawataka ACT na CHADEMA kuweza kuservive zaidi kuliko kutwaa madaraka na kuwa na nguvu za maamuzi. Aina ya Utawala uliopo unataka kujificha zaidi na kuilinda network isipotee na isionekanwe pale mambo yanapoelekea kuharibika unatumia njia ya kujifichua na kupaza sauti ikibidi.

Tumieni fursa zilizopo kulinda hicho kidogo na fursa ndogo iliyopo na pambaneni huko nje kuangalia bahati yenu.

Afrika mapambano ya Demokrasia yamefeli na nyinyi msiwe wepesi wa kupotezwa mazima.

Kishada.
 
CCM inataka jino kwa jino , kama na wao hawajaathirika kama wapinzani, katu hawawezi kupata akili, wamelewa madaraka vibaya sana na kiburi kisicho kipimo.
 
Katika vurumai hii ya CCM, upinzani unahitaji utulivu sana na kuonesha maana halisi ya uongozi.

Wawe na uwezo wa kupima kote na kufanya maamuzi sahihi.
 
Assalaam Aleykum Warahmatullahi wabarakatuh

Niliongea naye na anataka namba zako
Akuunge
 
Hata Lissu alikua anatokwa povu kuliko wewe mwisho wa siku?
 
Mada inahusika.

Hakuna kurudi nyuma na ni muhimu kusoma alama za nyakati kufikia malengo yaliyokusudiwa.

SOMO KUTOKA ZANZIBAR.
Huwezi kuzungumzia siasa za upinzani Zanzibar ukamuacha Maalim Seif na wenzake na siasa za wakati huo za CUF. Maalim Seif na wenzake walipitia hatua kadhaa katika kujenga upinzani wa kweli ingawa kuna wakati mazingira huwaelemea na kukaribia kupotea.

Kwa ufupi. Uhodari wa Uongozi wa Maalim na Wenzake mara zote umekuwa ukiwavusha salama kila baada ya uchaguzi licha ya vitimbi vya dh
Unazungumza as if Maalim Seif amewahi kupata anachokitafuta? Anavukaje salama wakati hadi CUF amenyang'anywa, kuna wenzake wameumizwa, wengine kuwekwa ndani mkuu.
 
Hapana. Nakusudia hatua walizopita kwa kutumia weledi mpaka wakafika hatua ya kuufanya upinzani kuwa strong. Safari haijafika mwisho. Sasa mtawala anatafuta option ya kutumia dola kupora vyama na kuwapa mamluki.

ACT na CHADEMA safari yao ya kupambana kuleta mabadiliko wasitoe fursa ya kuvurugwa.

Wakati mwengine unajifanya mjinga, wakati mwengine unakubali udhaifu, wakati mwengine unakomaa, wakati mwengine unapembejea, wakati mwengine unasusa, wakati mwengine unaomba maridhiano.

Inategemea time calculation imeegemea wapi kwenye safari yenu.

Ndio nikasema wakati mwengine unatuliza mzuka ili kuwapa akhuweni wafuasi wako waliovurugwa na dola kiuchumi, kiakili, kimwili n.k sio kwamba eti utaonekana dhaifu, hapana.

Kipindi hiki wapinzani wapambane kwa akili sana ili waservive ndani ya taasisi zao kwanza na kujiimarisha kuponya baadhi ya madonda had I upepo mbaya uitwao stone wind upite.

Wake na mikakati hata ya kujilaza chini kuepuka huo upepo usiwabebe wakiwa wamesimama.

Mnao elewa mnielewe.
 
Back
Top Bottom