CHADEMA mnaweza kuwekwa mtegoni kwa kuingiziwa ruzuku itokanayo na Wabunge wa Viti Maalum msiowatambua

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kwangu mimi huu naona unaweza kuwa ni mtego unaofuata kwa CHADEMA ambapo chama kinaweza kupewa ruzuku kwa kigezo cha kuwa na wabunge wa viti maalamu katika Bunge hili la sasa unless utaratibu unaotakiwa kufuata hauruhusu mbinu hii kutumika (unaweka mazingira magumu).

Kwahiyo, kama ni swala la kuingiziwa tu fedha kwenye akaunti ya chama kulingana na idadi ya wabunge, basi CHADEMA mjiandae kwa hili kwani linaweza tokea wakati wowote ule.

Hata hivyo, ni Imani yangu mtazirudisha hizo fedha iwapo jambo la aina hii litatokea.

Fedha kwa sasa ndio imekuwa silaha ya watu fulani katika juhudi zao za kutaka kuua upinzani na hasa CHADEMA hivyo mjipange kukabiliana na mambo ya aina hii.
 
Njia pekee ya CCM iliyobakia kujikwamua kwenye hili sakata ni kujaribu kutumia ndoano na chambo kuwavua samaki wenye tamaa...ili kuudanganya umma kwamba uchaguzi huu ulikuwa Huru na Haki. Leo hii wale 19 ukiwauliza watakwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Ndoano ya kwanza ishawakamata wale 19 tayari - wacha tuone game linaendelea - fedha ilishindwa kumuumba na kumfufua mwanadamu tu - mengine inaweza.

Ndoano ya pili itakuwa ni kurusha fuko la ruzuku kwenye chama - hapo sasa!!
 
Kuna hatari ya kuwa hio ruzuku inaweza Kupelekwa kwa hao wabunge na wao wakatambulika kuwa ndio chadema rasmi,kama walofanyiwa cuf,hali ipo pabaya sana chochote cha ajabu kinawezekana na kitaonekana si sawa tu
Ikiwa hivyo kutakua na kubadili gear angani kama alivyofanya Maalim Seif
 
La pesa halikwepeki, watahakikisha wanabariki uwepo wa 19 kwenye bunge ili ruzuku isaidie kulipa gharama za kiutawala, mishahara nk, Mbowe ni muelewa hatakubali kuwa na msimamo mkali wakati kuna ulaji usio na maswali.
 
What if kwenye kikao cha kamati kuu ya chama kitakachofanyika Ijumaa hao viti maalum wakafukuzwa uanachama wa chadema?
1606376695940.jpeg
 
Hata hivyo, ni Imani yangu mtazirudisha hizo fedha iwapo jambo la aina hii litatokea.
Kaka Salary, mnachoamini wafuasi wa CHADEMA linapokuja suala la kujenga taasisi financially most likely sio wanachoamini na kupractice genuinely viongozi wakuu wa Chama

The fact kwamba Aida alienda Bungeni kuapa na hakuna kiongozi hata mmoja aliyempigia japo simu tu ya kumuonya kabla na baada ya kuingia ni indicator tosha.

Time will tell maana tarehe 27 Nov 2020 sio mbali. La msingi tu ni ninyi kuwa na akiba ya maneno maana mtarudi tu kutetea maamuzi ya chama vyovyote yatakavyokuwa
 
Back
Top Bottom