Kuna taarifa ambayo bado haijathibitishwa inadaiwa kuwa Askari Polisi mmoja amefariki Dunia kwa kujipiga risasi akiwa kazini, Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Haijajulikana wazi chanzo cha kujipiga risasi na ni kama kweli amejipiga risasi amepigwa risasi.
Taarifa hii nimeona inasambaa chinichini...
Abdilah Musa alimaaruf kama Banjoo alitikisa Arusha kwa ubabe wake na ujuzi wa kuishika na kuitumia bereta kwa ufanisi wa hali ya juu sana.
Alikuwa mwizi wa madini na magari na mbabe haswa.
Soma Jambazi Sugu "BANJOO" larudi uraiani
Aliwahi kwenda magereza kwa vipindi tofauti lakini kesi yake...
Mfanyabiashara Nassor Hamdan Seif, Maarufu kama Mzee NBS, Mmiliki wa Mabasi ya NBS Tabora, amefariki leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam
Mwili wa Marehemu Mzee NBS utasafirishwa kuelekea Tabora kwa Mazishi yake.
Apumzike kwa Amani
Mchungani wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Makimbilio, Manispaa ya Moshi, Jane Mwangalimi amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake alikokuwa akiishi na mjukuu wake wa miaka mitano.
Tukio hilo ambalo limetokea Januari 20, 2026 limegunduliwa na mjukuu wake huyo aliyekuwa...
Hamjambo!
1. Kuna nyumba hapa mwaka mpya na Christmas hawakusherehekea.
2. Hawakupika chakula cha maana.
3. Lakini Kila wakisikia taarifa msiba ya kiongozi wa kiserikali wanafanya tafrija. Wananunua pombe, wanapika chakula kizuri, wanachinia kuku.
4. Wanaweka Muziki. Katafrija kadogo kwa...
Kijana Deogratius James Ottaru (37), mkazi wa Kijiji cha Kirima Kati, Kata ya Kibosho Kirima, wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake aliyokuwa akiishi peke yake.
Taarifa zinaeleza Drogratius (marehemu) alifariki takribani siku mbili kabla ya...
Inasemekana kuwa kada mtiifu wa CCM sheikh Sharifu Majini alifariki tarehe 29 October kwa kupigwa risasi.
Sina uhakika wa hii taarifa, ila kama ni kweli Mungu ampumzishe anapostahili.
Hana haja ya kupewa R.I.P.
Ni magonjwa ya mfumo was upumuaji yamekatisha uhai wake akiwa na Miaka 41 tu.
Bavarians Msiba huu usiwapite na wale wenzangu wa PES ( pro evolution soceer ).
Winger teleza ameenda.
Pumzika kwa amani mkongwe.
Soka halikudai.
Bwana Giorgio Armani alizaliwa mwaka 1934 nchini Italia. Alisoma shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu, baada ya hapo alijiunga na jeshi kabla hajagundua kipaji chake cha ubunifu wa mavazi.
Bwana Armani Amani kubuni mavazi ya nyota jwa dunia katika ulimwengu wa filamu kama Julia Robert’s...
Wakuu
Hivi mmepita huko X hivi karibuni
Duru zinasema kuwa Donald Trump amefariki japo hakuna confirmation kutoka kwenye sources ambazo ni rasmi.
Kwanza hajaonekana kwa siku takriban mbili na pia hii weekend yote hana any official meeting au schedule, kitu ambacho sio cha kawaida
Lakini...
NDAGU, KITALA NA ADHABU YA MCHAWI
NDAGU maana yake ni ‘ramli'. Kwa desturi, baada ya kuondoa matanga, ndugu waliofiwa huenda kwa mganga wa ramli ili awajulishe sababu ya kifo kilichotokea. Ziko namna nyingi za ndagu, kwa mfano, ndagu ya kifo, ndagu ya ugonjwa, yaani ramli ya kubashiri maradhi...
Hamjambo Wote!
Leo nimepokea kwa Masikitiko makubwa Taarifa ya Msiba wa Aunt Dory, Moja ya Wamama ambao walikuwa wananikubali Sana enzi za uhai wake.
Taarifa hiyo nilipoipata moja kwa moja ikanirudisha Mwaka 2015 nilipokuwa Udsm Mwaka wa Pili.
Nikiwa na hekaheka, za ujana kukimbizana na kila...
Mwanasimba mwenzetu na mwandishi wa BBC Eric David Nampesya amefariki Dunia. Muda mfupi uliopita nimeongea na mke wake amenithibitishia kuwa Eric hatunaye.
Eric alikuwa shabiki na mpenzi mkubwa wa Simba na Liverpool ya England.
BWANA ametoa na BWANa ametwaa jina lake lihimidiwe Amen
Mwanamieleka maarufu Hulk Hogan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71, WWE imethibitisha.
-
Hulk Hogan alikuwa miongoni mwa nyota maarufu zaidi katika historia ya mieleka lakini pia alikuwa mmoja wa watu waliowagawa sana mashabiki.
-
Tukio lake la kumbwaga Andre the Giant litasalia katika...
Inalilah waina ilahi rajiun
Ibrahim sow kutoka Ivory coast.
Aliekuwa mshindi wa Quran mwaka Jana pale uwanja wa mkapa amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 16.
====
Mshindi wa Mashindano ya Quran Tukufu Ibrahim Sow raia wa Ivory Coast amefariki.
Taarifa kutoka vyombo mbalimbali Nchini Ivory...
Connie Francis, nyota wa muziki wa pop aliyejizolea umaarufu miaka ya 1950 na 1960 kwa nyimbo kama “Pretty Little Baby”, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87
Taarifa za kifo chake zimetolewa na rafiki yake pamoja na msemaji wake, Ron Roberts, ingawa hakutoa maelezo zaidi mara moja
Francis...
Leo hii majira ya saa 11 jioni katika Block Namba 4 ghorofa ya Saba, Kota za Magomeni Jijini Dar es Salaam imeungua moto ambao chanzo chake, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni umetokana na mtoto kuchezea kiberiti.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.