Featured content

Othman Masoud: Vyama vya Siasa vinaweza kuwa sababu ya kurejesha nyuma nchi
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ametoa wito kwa vyama vya siasa, utumishi wa umma pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuzingatia wajibu wao wa msingi ili kuiletea nchi maendeleo na kuepuka migogoro. Akizungumza leo Septemba 22, 2026 baada ya kuapa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza namna vyama vya siasa vinavyojiendesha na aina ya viongozi wanaopewa dhamana vinaweza kuingiza nchi kwenye vurugu na kuirejesha nyuma badala ya kuisogeza mbele...
Serikali ya Misri yalipa fidia kwa familia ya Mwanaharakati aliyeuawa 2015 kwa kupigwa risasi na Polisi
Fidia Baada ya Miaka Kumi Misri imelipa familia ya mwanaharakati na mshairi Shaimaa al-Sabbagh fidia ya pauni 300,000 za Misri (chini ya $6,000), zaidi ya miaka 10 tangu auawa na polisi. Hukumu ya mahakama ilitoka 2023, lakini Wizara ya Mambo ya Ndani ilichelewesha malipo hadi wiki iliyopita. Wakili Ali Suleiman alisema fedha hazikuwa lengo, bali kudhibitisha kosa la wizara. Mauaji Katika Uwanja wa Tahrir Mnamo Januari 24, 2015 (mkesha wa miaka 4 ya maasi ya Januari 25), Sabbagh (34)...
Wakili wa Sandaland: Waziri Makonda hatakiwi kuingilia uendeshaji wa Chama cha Soka
Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho. Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila...
TPDC: Gesi ya Mitungi tunayotumia nyumbani inatoka nje, bei yake inategemea soko la mafuta Duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Mohamed Makame amsema, Gesi ya mitungi tunayotumia majumbani kwa sasa yote inatoka nje, bei yake hupanda kulingana na bei za mafuta duniani. "Gesi, nyingi ambayo tunatumia majumbani ni ile ya kwenye mitungi (LPG). Ni tofauti na gesi asilia ambayo sisi tunaisafirisha kwenye mabomba na kupitia njia ya CNG na LNG. Ile inatokana na uzalishaji wa mafuta, na kwasasa, kwasababu hatujaanza uzalishaji wa mafuta, ile gesi...
Sandaland: Tumeshangazwa na kauli ya Makonda, tunakusudia kuchukua Hatua za Kisheria
Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliyoponda ubora na uhalali wa jezi mpya za timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars). Sakata hili limeibuka kufuatia taarifa iliyotolewa leo, Septemba 18, 2026, na kampuni hiyo nchini Tanzania, ikijibu ujumbe wa Waziri Makonda uliowekwa Septemba 16, 2026 kwenye...
Lissu: Kingai amesema hawezi kutoa ushahidi na atashangilia nikipatikana na hatia
KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu itaendelea tena mchana leo, Ijumaa Septemba 18.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam KESI hiyo inayosikilizwa mfululizo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru inakuja Mahakamani hapo leo kwaajili ya upande wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi wake, ambapo shahidi wa SITA (6), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) CP Ramadhan Kingai ataanza kutoa ushahidi...
Makonda: Tutaunda Kamati kuchunguza mkataba wa mzabuni wa Jezi za Timu za Taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema hatambui matangazo kwenye jezi za Timu za Taifa, akisema mchakato wa kuzibadilisha haukuishirikisha Wizara licha ya maelekezo aliyoyatoa Februari 2026, na kwamba ataunda Kamati kuchunguza mkataba wa mzabuni wa jezi hizo.
Meli yenye Bendera ya Tanzania yashambuliwa na 'Drone' ya Urusi
Wizara ya Miundombinu ya Ukraine imesema kuwa shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi dhidi ya meli yenye bendera ya Tanzania, iliyokuwa ikielekea bandari ya Ukraine, limesababisha kifo cha nahodha wa meli hiyo na kuwajeruhi wafanyakazi watatu. Meli hiyo iliyokuwa ikisafiri chini ya bendera ya Tanzania ilipigwa katika shambulio la Alhamisi, ambapo nahodha aliuawa na wafanyakazi watatu kujeruhiwa. Wizara ya Miundombinu ya Ukraine ilitoa taarifa hiyo kupitia Telegram, ikieleza hali...
Kesi ya uhaini ya Lissu yaahirishwa hadi Septemba 18, DCI, IGP na CDF wapo nje ya nchi
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Septemba 18, 2026, baada ya Mahakama kuelezwa kuwa mashahidi watatu, akiwemo DCI Ramadhani Kingai, CDF Jenerali Jacob Mkunda na IGP Camillus Wambura, wako nje ya nchi.
DRC | Wananchi waandamana kupinga Rais Tshisekedi kuongezewa muhula wa 3
Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kinshasa, kupinga pendekezo la serikali la kufanya marekebisho ya Katiba ambayo yanaweza kumruhusu Rais Félix Tshisekedi, aliyechaguliwa mwaka 2019 na kuchaguliwa tena mwaka 2023, kugombea muhula wa tatu endapo marekebisho hayo yatapitishwa kupitia kura ya maoni. Takriban watu 10 wamekamatwa kufuatia maandamano hayo yaliyofanyika Septemba 15, 2026 jijini Kinshasa pamoja na Lubumbashi, hata baada...
Kundi la EPP katika Bunge la Ulaya lampendekeza Lissu kuwania Tuzo ya Sakharov
Wakati sisi tukimfungulia kesi za Uhaini mataifa ya Ulaya yanathamini mchango wake. Kati ya viongozi mashuhuri Duniani waliopata tuzo hii ni pamoja na Nelson Mandela, Malala Yousafzai, Nadia Murad, Denis Mukwege, Aung San Suu Kyi, na Václav Havel. ======= Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu amependekezwa rasmi kuwania Tuzo ya Sakharov ya Mwaka 2026, ambayo ndiyo heshima ya juu zaidi inayotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa watetezi wa haki za binadamu na...
Padri Kitima: Waliokosewa ni wananchi sio vyama, wao ndio waongoze mchakato wa Maridhiano
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema dhana ya maridhiano nchini inapaswa kuanza kwa kukiri na kukubali ukweli kuhusu matatizo yaliyopo. Akifafanua kuhusu maana ya maridhiano, amesema neno hilo linapaswa kueleweka kwa upana, akitumia mfano wa neno la Kiingereza “reconciliation”, ambalo kwa mtazamo wa Wakristo na Waislamu linahusisha kwanza hatua ya kukiri makosa kabla ya kufikia hatua ya kupatana. Padre Kitima amesema ili kufikia...
Dkt. Kijo-Bisimba: Haukuwa Uchaguzi, siku tumeruhusiwa kutoka tulikuta maboksi mitaani
Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mwanaharakati mkongwe, Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amehoji uhalali wa uchaguzi, akisema alichokiona siku hiyo hakikidhi viwango vya uchaguzi. Akizungumza Septemba 15, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, Dkt. Kijo-Bisimba amesema; "Mimi hofu yangu ni kwamba sikujua kama kweli palikuwa na uchaguzi. Kwa sababu hiyo siku ya uchaguzi, bahati nzuri nilikuwepo hapa nchini, na mimi sikuwa nimejiandikisha kwa...
Lutgard Kagaruki: Marekebisho ya katiba sio suala la hiyari ya kisiasa ni hitaji la dharula
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania (TTCF), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Lutgard Kokulinda Kagaruki, amesema changamoto za kiutawala na vikwazo katika ushiriki wa wananchi vilivyojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 vimedhihirisha kuwa mfumo mzima wa utawala nchini unahitaji kufanyiwa marekebisho ya kina. Amesema marekebisho ya Katiba si suala la hiari ya kisiasa tena, bali ni hitaji la dharura, akisisitiza kuwa utawala...
Janeth Rithe: Mimi ni sadaka kwa wengine, kama wamejifunza kuua na sisi tunatakiwa kujifunza kufa
Akizungumza katika mahojiano na M & S Podcast yaliyorushwa Septemba 9, 2026, Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha ACT-Wazalendo, Janeth Rithe, ameeleza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa nchini yanahitaji viongozi wenye kujitolea kama "sadaka" kuwa tayari kufa ikiwa una dhamira ya kuwa sauti ya wananchi. "Kwa hiyo sasa hivi ukiingia kwenye siasa ni ujikane nafsi, na uwe kweli una dhamira ya kutaka kuwatetea na kuwasemea watu. Lakini kama huna dhamira hiyo huwezi. Utakuwa unajawa...
Ado Shaibu: Yuko wapi aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi?
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, ametoa wito kwa familia ya Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Emmanuel Nchimbi kujitokeza hadharani na kuwahahakishia Watanzania kuwa yuko salama. Ado ametoa wito huo Septemba 10, 2026 wakati akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Bugogwa, Mtaa wa Igomba huko Ilemela, Mwanza.
Utafiti: Kunywa Chai au Kahawa ya Moto sana inaweza kusababisha Saratani ya umio
Je, huwa unaagiza kahawa ya moto sana au unapenda chai ikiwa inachemka? Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford wamegundua uhusiano kati ya unywaji wa vinywaji vyenye joto kali sana na saratani ya umio, yaani mrija unaounganisha koo na tumbo. Tabia za unywaji wa karibu watu milioni moja nchini Uingereza zilifuatiliwa, na matokeo yakaonyesha kuwa watu wanaokunywa vinywaji vyenye joto kali sana walikuwa na hatari iliyoongezeka mara tatu ya kupata saratani hiyo. Pia, mara ngapi mtu anakunywa...
IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi kesi ya Lissu
Mahakama Kuu kupitia Jaji Dunstan Ndunguru imekataa ombi la mshtakiwa Tundu Lissu la kuwaita baadhi ya mashahidi wa utetezi katika Kesi ya Uhaini Na. 19605/2025, likieleza kuwa ushahidi wao hauna umuhimu kwa kuwa jukumu la kuthibitisha kosa ni la Jamhuri. Hata hivyo, Jaji Ndunguru ameagiza kutolewa kwa wito rasmi (summons) kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Mkuu wa Polisi (IGP) na DCI ili wafike Mahakamani kutoa ushahidi wa utetezi, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Septemba 11, 2026.
Mhadhiri wa UDOM aliyetuhumiwa kwa Ugaidi aachiwa huru
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imemwachia huru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedek Kaijage, baada ya Serikali kueleza kuwa haina nia ya kuendelea na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, huku mahakama ikimwekea masharti ya mwenendo. Kaijage ameachiwa huru leo, Alhamisi, Septemba 10, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Denisi Mpelembwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali, Jonathan Chuwa, kuiambia mahakama Serikali haina nia ya...
Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Conrad Agonza Kahyoza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam, leo Septemba 10, 2026, baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia askari wa Usalama Barabarani katika eneo la Lugalo, Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea Jumanne Septemba 8, 2026 saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, Lugalo, wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew...
Back
Top Bottom