Featured content

Mhadhiri wa UDOM aliyetuhumiwa kwa Ugaidi aachiwa huru
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imemwachia huru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedek Kaijage, baada ya Serikali kueleza kuwa haina nia ya kuendelea na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, huku mahakama ikimwekea masharti ya mwenendo. Kaijage ameachiwa huru leo, Alhamisi, Septemba 10, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Denisi Mpelembwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali, Jonathan Chuwa, kuiambia mahakama Serikali haina nia ya...
Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Conrad Agonza Kahyoza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam, leo Septemba 10, 2026, baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia askari wa Usalama Barabarani katika eneo la Lugalo, Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea Jumanne Septemba 8, 2026 saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, Lugalo, wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew...
Heche: Nilikamatwa na Kusomewa Shtaka la Ugaidi la Kuchoma Vituo vya Mwendokasi Kimara hadi Magomeni
Baada ya jana Septemba 9, 2026 Makamu Mwenyeekiti wa CHADEMA Bara, Joun Heche kupanda Kizimbani na kuanza kutoa ushahidi wake katika Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyeekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na leo tena anaendelea. Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Septemba 10, 2026, huenda ikatoa uamuzi kuhusu pingamizi la Serikali katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Pingamizi hilo linahusu ombi la Lissu la kuwaita viongozi na maafisa...
Brenda: Hatukususia uchaguzi, tulitaka marekebisho ya Sheria na Uchaguzi wa Kidemokrasia
Shahidi wa nne katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia, leo Septemba 8, 2026 ataendelea kutoa ushahidi wake wa utetezi dhidi ya Tundu Lissu. Jana Septemba 7, 2026, shahidi huyo alianza kutoa utetezi wake, ambapo Lissu alianza kwa kumuongoza kujibu maswali kwamba mkutano wa tarehe 3 Aprili ulihusu nini na nani aliyeuandaa. Katika...
Maghorofa ya Samia Kawe kugeuzwa AirBnB? Hivi hawaoni Janga la Makazi linalotishia Dar? Je, mlengwa ni nani?
Habari wakuu, majuzi nikiwa naperuzi insta nilikutana na tangazo la dalali la apartment ya AirBnB. Nilikuwa tayari nimeshapita, lakini nikastuka baada ya kugundua kuwa jengo lile ni la mradi wa Samia Housing Scheme uliopo pale Kawe. Swali likanijia mara moja: Hivi hizi nyumba tunawajengea kina nani hasa? Watalii, wafanyabiashara matajiri wanaopita Dar, au maharusi wanaotafuta sehemu ya kulala usiku wa harusi yao? Tusisahau kwamba Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linajenga kwa kodi zetu...
Masoud: Alishinda Ubunge, akapewa cheti, akanyang’anywa akapewa mwingine ambaye yuko Bungeni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othuman Masoud, amesema uchaguzi wa Zanzibar haukuwa “smooth” kama baadhi ya watu wanavyodhani, akieleza kuwa kulikuwa na matukio mbalimbali ambayo chama chake, ACT-Wazalendo, kiliwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Uchaguzi. Soma pia >> Othman Masoud: Hakukuwa na Uchaguzi 2025, Vyombo vya dola kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi na CCM viliamua nani awe Mshindi Othuman amesema moja ya matukio yanayoonyesha mazingira ya uchaguzi huo ni kuwepo kwa...
Jaji Warioba: Amani haikuletwa na Bunduki na hutailinda kwa Bunduki
Akizungumza leo Septemba 7, 2026, kwenye Mkutano wa wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini uliondaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba amesema: "Kurudi kwenye amani ya kweli, ni lazima turudi kwenye misingi ile ya zamani. Tuwe na usawa, tusiwe na ubaguzi wa aina yoyote. Tutarudi kwenye misingi ya amani. Amani hailetwi na bunduki, na hutalinda amani kwa bunduki. Lakini kwa sasa tunafikiri bunduki ndiyo inaweza kulinda amani. Inaweza kuleta...
Imetimia Miaka 9 tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi, uchunguzi umefikia wapi?
Wakuu, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi. Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma. Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana. Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya...
Ramani mpya ya dunia, yaonesha ukubwa halisi wa Afrika
Umoja wa Mataifa umepiga kura ya kupitisha ramani mpya rasmi ya dunia iliyobuniwa kuonyesha ukubwa halisi wa kijiografia wa bara la Afrika na maeneo mengine ya kanda ya ikweta. Mabadiliko haya yanalenga kuchukua nafasi ya "Mercator projection" (ramani ya kale ya Mercator), ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu lakini imekuwa ikikosolewa kwa kupotosha vipimo—ikionyesha maeneo ya kaskazini mwa dunia (kama vile Ulaya na Marekani ya Kaskazini) kuwa makubwa zaidi kuliko yalivyo, huku...
Rais Duma: Unapoingia madarakani inaweza kukuchanganya na kukufanya ujione Mungu mdogo
Rais wa Botswana, Duma Boko, amezungumzia hatari zinazoweza kuambatana na madaraka ya kisiasa na jinsi kushika wadhifa kunaweza kumbadilisha kiongozi mtazamo wake kuhusu yeye mwenyewe. Akihojiwa na eNCA’s CheckPoint Podcast, amesema unapoingia madarakan inaweza kukuchanganya sana na kukufanya ujione kama nusu-mungu, na viongozi wengi hutumbukia kwenye mtego huo. Amesema kuwa viongozi wanaoingia madarakani wakiahidi kuwa tofauti na waliowatangulia wanaweza baadaye kujikuta wakitekwa na...
Mangula: Magufuli alitaka kujiondoa kutafuta Wadhamini kisa wenzake walikuwa wanatoa fedha
Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Philip Mangula, amesema hayo Septemba 4, 2026, wakati akihojiwa kupitia Clouds Media. "Magufuli alikuja nyumbani kwangu hapa Osterbay siku moja ya Jumapili, akaniambia, 'Mzee, mimi nataka kujiondoa kwenye hii mizunguko ya kutafuta wadhamini.' Nikasema, 'Kwa nini?' Akasema, 'Hapana, mimi sina pesa kabisa. Wenzangu wanatoa pesa, mimi nikienda mahali mnaongea nao, mnataka kuondoka wanasema, sasa mnatwachaje?' Basi yeye alikwenda Iringa kutafuta...
Kimbunga Saudel na mvua kubwa zasababisha mafuriko makubwa China
Mvua kubwa za mawe na dhoruba zilizosababishwa na Kimbunga Saudel zimekumba mikoa ya Fujian na Zhejiang mashariki mwa China, na kulazimisha mamlaka kutangaza hali ya dharura ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya mafuriko. Kimbunga hicho kilitua kwa mara ya tatu nchini China kwenye pwani ya Fujian siku ya Alhamisi (Sep 3), baada ya awali kupiga mkoa jirani wa Zhejiang mara mbili. Mamlaka katika mkoa wa Fujian zimefunga shule kwa muda na kusimamisha huduma za vivuko. ==== Torrential rains...
Mnyika kuhusu ToneTone Mahakamani: Mikono yetu ni safi, Serikali ndiyo inazuia ruzuku yetu!
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania? Mnyika: Ni sahihi. Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo? Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu. Job Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya...
Raia wa China, Zheng Xiangming ateuliwa kuwa Chifu nchini Ghana kwa kutoa fursa za ajira
Mfanyabiashara wa China, Zheng Xiangming, ametunukiwa cheo cha Chifu wa jadi nchini Ghana na kupewa jina la Hiowe Golaka Noryam Matse Nene Asumahtsu I, katika hafla iliyofanyika Agosti 29, 2026, kwa kutambua mchango wake katika uwekezaji na maendeleo ya jamii kupitia kampuni yake, Greenhouse International Development Group Ghana Limited. Xiangming, ambaye ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo, ametajwa kuchangia maendeleo kupitia uwekezaji katika kilimo, mifugo, misitu na miradi ya viwanda...
Malisa: Polisi hawajatuachia kwa dhamana, wala sijahojiwa kwa tuhuma za jinai
Godlisten Elisante Malisa amesema ameachiwa huru na Jeshi la Polisi leo asubuhi bila kudhaminiwa, akikanusha taarifa kwamba aliachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za jinai. Malisa amesema hajahojiwa wala kuandikiwa maelezo kuhusu tuhuma zozote za jinai, na kwamba mali zake zote ikiwemo simu, fedha na mabegi zimerudishwa kwake. Amesema Polisi walimtaka kuandika historia ya namna alivyokamatwa katika eneo la Namanga hadi kufikishwa Arusha, huku akisisitiza kuwa hakutakiwa kutoa...
CDF Mkunda: Kuhusu ugaidi kwa Tanzania mpaka sasa hali ni shwari
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda amebainisha kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini Tanzania bado ni shwari dhidi ya matishio ya ugaidi. Hata hivyo, amesisitiza kuwa kwa vile ugaidi ni "uhalifu wa kuvuka mipaka," Tanzania haiwezi kujitenga au kujiona kama kisiwa. Ameeleza kuwa nchi inaendelea kushirikiana kwa karibu na majirani zake, hususan Msumbiji kusaidia kupambana na magaidi waliopo Kaskazini mwa nchi hiyo (Cabo Delgado), pamoja na kupeleka vikosi vya ulinzi wa amani...
Tanzania yamkamata Mkosoaji wa DRC, Denise Mukendi Dusauchoy
Denise Mukendi Dusauchoy, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ubelgiji, ameripotiwa kukamatwa nchini Tanzania. Dusauchoy anajulikana nchini DRC kama mwanasiasa na mtu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii na amewahi kuhusishwa na shughuli za kisiasa za Alliance Fleuve Congo, AFC, pamoja na kundi la waasi la M23. Vyanzo kadhaa vya habari nchini DRC vinasema amekamatwa nchini Tanzania na baadaye kuhamishiwa Dar es Salaam, huku mamlaka za Congo zikitarajiwa kuomba arejeshwe nchini humo...
Malisa akamatwa na Polisi, Namanga na kupelekwa kusikojulikana
Malisa GJ Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi...
Wizara ya Ardhi: Kisiwa cha Lupita kimepangishwa, Tim Draper anaweza kuhamisha uwekezaji wake
TAARIFA KWA UMMA KUH: KISIWA CHA LUPITA KILICHOPO KATIKA ZIWA TANGANYIKA, ΤΑΝΖΑΝΙΑ Dodoma 31 Agosti 2026 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeona kupitia mitandao ya kijamii taarifa kuwa mwekezaji Bw. Tim Draper anakusudia kuuza ardhi katika kisiwa kilichopo Ziwa Tanganyika nchini Tanzania. Pia soma ~ Timothy ‘Tim’ Cook Draper, bilionea kutoka Marekani, atangaza kuuza kisiwa chake kilichopo Ziwa Tanganyika, Tanzania Wizara inapenda kuutaarifu umma kuwa, kisiwa kinachorejewa...
Sheikh Ponda: Kuna matukio makubwa ikiwemo Utekaji, Mauaji, Ripoti za CAG lakini hakuna anayewajibishwa
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesisitiza kuwa uwajibikaji ndio msingi mkuu wa haki za binadamu na usalama wa wananchi. Akizungumza katika mahojiano na Crown Media, Agosti 28, 2026, Sheikh Ponda ameeleza kuwa uwajibikaji unahakikisha viongozi na watendaji wanabeba dhamana ya makosa yao, hasa yanapokuwa ya makusudi, na kwamba bila uwajibikaji hakuna haki wala maendeleo yanayoweza kupatikana nchini. Sheikh Ponda ameeleza swala la uwajibikaji...
Back
Top Bottom