Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Taaluma ya Madereva Tanzania (TATAMATA), Godlove Materu, ameachiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa Februari 5, 2026, kufuatia kudhaminiwa na mke wake Februari 9, 2026.
Materu alidaiwa kukamatwa Februari 5, 2026 na watu wasiojulikana, na Februari 8 viongozi wa TATAMATA waliwapa Polisi siku mbili awe amepatikana, usiku huohuo Jeshi la Polisi Songwe lilikiri kumshikilia kwa tuhuma za kijinai.