Zyansiku: Bashe ametumwa na Mungu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zyansiku: Bashe ametumwa na Mungu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Aug 18, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wakuu,
  kwenye post inayopatikana hapa mwenzetu zyansiku ametoa mantiki ya ujio wa bashe huko nzega akidai ametumwa na mungu pale aliposema:

  ...nyuma ya bashe yupo mungu maana watu wa nzega tumetaabika vya kutosha , umeme wa Ndalla unasua sua kwa Mbunge wa jimbo kufanya kazi za kitaifa zaidi nyingine hazitusaidii sisi wa mwaka shahara. HONGERA SANA BASHE NYUMA YAKO YUPO MUNGU!


  my take:

  kama huyo bashe ni mtume wa mungu (yaani gabriel):
  • :frusty: iweje achakachue uraia?
  • :frusty: iweje apokwe uraia na chama chetu?
  • :frusty: iweje huyo mungu asimlinde dhidi ya hiyo hujmat ya kisiasa?
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tafadhali naomba unipatie maana ya ilo neno nililo likoza weusi.
   
 3. R

  Ramos JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa haoni utata katika uraia wa Bashe (source; Mwananchi ya leo).

  Swali; Bashe ana maamuzi gani? (kama yupo kati yetu aliye karibu naye)

  Je, Watanzania wana usalama kweli katika suala la uraia? Mtu yeyote hawezi kuzushiwa sio raia kwa manufaa ya kundi au mtu fulani kama ilivyofanya kwa Bwashee?
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ramos I tell you when people want to play dirty with you especially in politics they will do whatever they can to put dirt in you kwa kweli sijui itakuwaje au hatua gani atakazochukua but its too late with CCM nothing more he can do labda aende CHADEMA unajua CCM wakiona you are a threat kwao lazima tu watakuzushia kitu fulani DIRTY POLITICS :eyebrows:
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Katika vitu amabavyo CCM vimewashinda kwa miaka yote hii ni kula matapishi yao and it is because thery are blind arrogant. Katika hali ya kawaida ungetegemea wangeliweka sawa hili suala na probably kumrudisha kijana kugombea. Lakni hiyo kwa CCM thubutuuuuuuu!!!!

  Na of course watakuwa wanaamini itakuwa karata mbaya mno kwao kisiasa wakifanya what most of us could be thinking is the right thing..
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ndo tatizo la kuwa na viongozi wenye akili za panzi....nasikitika na kuchukia sana kuongozwa na JK kama rais wa nchi....maamuzi yake na chama chake yako soo mean!!!
   
 7. Amanda

  Amanda Senior Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Yaani mm hainiingii akilini jinsi tunavopelekwa na CCM, kama waziri haoni tatizo kwa Bashe at last moment.
  Kwann waziri hakusema haya last week? kwann hakutoa tamko wakati anaenguliwa?? Wooote ni wale:confused2:
  hakuna wakutueleza la maana ndani ya ccm, wanalindana bila kujali nani ataathirika na maamuzi yao.

  Mimi naona Bashe aende chama kingine maana hapafai tena hapo. hakuna haki ndani ya ccm.
   
 8. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukizoe kunywa damu ya mtu utakunywa hata ya mwanao.
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naomba mwenye details atuweke sawa. Nimejaribu kutafuta gazeti la Mwananchi sijalipata mtandaoni na hapa nilipo siwezi kupata nakala. Kwani Masha kasema kuwa haoni utata kwa hiyo Bashe ni raia au haoni utata wowote katika kauli za CCM kwa hiyo Bashe siyo raia?:confused2::confused2:
   
 10. dkims

  dkims Senior Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  masha hana nguvu ya kwenda against maamuzi ya chama,wote ni walewale tuuuuuuu
   
 11. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bashe mwenyewe anasema mama yake alizaliwa Tanzania ila baba yake ndiyo alikuja toka Somalia na Makamba juzi alisema iwapo moja ya wazazi wake angekua Mtanzania basi nae ni mtanzania so mi sijui nchi inakwenda wapi. so ingekua kwa TZ Obama asingekua Rais
   
 12. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Waziri: Uraia wa Bashe hauna utata Send to a friend Thursday, 19 August 2010 08:47 0diggsdigg  [​IMG] Waziri wa mambo ya nje Laurence masha(katikati),akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam jana walipotaka maelezoya sakata la uraia wa Hussein Bashe

  CCM YASEMA DK KIGWANGALA RAIA Boniface Meena na Ramadhan Semtawa RAIS Jakaya Kikwete anasubiriwa kutatua kitendawili cha uraia wa Hussein Bashe baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, kueleza kuwa uraia wa kada huyo wa CCM, hauna utata wowote.
  Hata hivyo, pamoja na Masha kusema kuwa hakuna utata katika uraia wa Bashe alipoulizwa na gazeti hili nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jana, alishindwa kueleza bayaba kana ni raia au si raia.
  Alipoulizwa zaidi kuhusu suala hilo, alisema litaisha baada ya rais Kikwete kuzinduza kampeni za uchaguzi. Masha ambaye awali alisema kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho kuzungumzia suala hilo, alisisitiza kuwa uraia wa Bashe hauna utata.
  Mahojiano kati ya Mwananchi na Waziri Masha nje ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam yalikuwa kama ifuatavyo; Mwananchi: Mheshimiwa sulala la Bashe unalizungumziaje? Masha: Hakuna utata kwenye uraia wa Bashe. Naweza kusema hivyo.
  Mwananchi: Kama hakuna utata je, Bashe ni raia au si raia (wa Tanzania)? Masha: Nasema hakuna utata kwenye uraia wa Bashe na siwezi kuzungumzia suala hilo zaidi. Sikilizeni, hili suala halina umuhimu kama mnavyolizungumzia.
  Mwananchi: Wewe ndiye unayethibitisha kuwa mtu ni raia au si raia. Sasa kwa nini usitueleze kuhusu hilo? Barua zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari unazizungumziaje? Masha: Kumbe unajua kuwa mimi ndiye wa mwisho kuzungumzia hilo.
  Sasa nasema hii 'issue' sio kama mnavyoizungumzia, nasisitiza hakuna utata. Nimekuja kuwaona msije mkasema kuwa waziri kagoma kutuona. Kuhusu barua zilizochapishwa, tunafuatilia tujue zimepatikana wapi. Mwananchi: Tunajua kiongozi wa juu ndiye aliyelizungumzia hilo na wewe uko chini yake, hilo unasemaje? Masha: Kumbe unajua. Mimi si msemaji wa Ikulu na hivyo tusubiri kampeni zianze tuendelee na michakato mingine. Mwananchi: Vipi kuhusu uraia wa Kigwangala ambaye tumesikia ni Mrundi? Masha: Nimeagiza watu wangu walifuatilie ili waweze kunipa taarifa.
  Waziri Masha pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji na vyombo vya dola, juzi waliitwa ili wajadili kuhusu uraia wa Hussein Bashe, ambaye CCM kimedai kuwa si raia wa Tanzania na kumuengua kwenye kinyang'anyiro cha ubunge.
  Masha, ambaye alikuwa jimboni kwake Nyamagana mkoani Mwanza akisaka wadhamini kwa ajili ya kutetea ubunge, aliwasili jijini Dar es Salaam kwa ndege ili kuhudhuria kikao hicho ambacho kilifanyika kuanzia saa 7:00 mchana pamoja na baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola.
  Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili ilizipata kutoka wizarani, viongozi hao walifanya kikao hicho kwenye ofisi za makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani. "Waziri alikuwa Mwanza, aliitwa kwa ajili ya kusimamia kikao kinachoendelea hadi hivi sasa," alieleza mpashaji wetu wa habari. Kabla ya kupatikana kwa taarifa hizo Mwananchi lilifika wizarani hapo kuonana na Waziri Masha, lakini lilielezwa kuwa yuko safarini Mwanza na kwamba, naibu wake alikuwa safarini.
  Baadaye Mwananchi ilipata taarifa kuwa waziri alirejea Dar es salaam kwa ajili ya kikao hicho kwa ajili ya kuweka sawa suala la Bashe. Masha alipopigiwa simu alisema kuwa hajatoa taarifa ya kikao hivyo apewe muda wa kulishughulikia tatizo hilo kisha atatoa taarifa zote. "Sijakaa ofisini nataka nipate muda wa kufuatilia na nitatoa taarifa zote," alisema Masha.
  Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba amesema mgombea wake Dk Kigwangala, ni raia. "Tunachojua mgombea wetu ni raia," alisema Makamba.

  Alisisitiza kwamba, kitendo cha Hussein Bashe kukumbwa na tuhuma za kutokuwa raia, zisijaribu kuwaingiza na watu wengine. Kwa mujibu wa Makamba, Dk Kigwangala ndiye aliyepitishwa na Nec kuwa mgombea ubunge na kwamba matokeo hayo hayawezi kubadilishwa.
  Alipoulizwa haoni chama kinaweza kupoteza nafasi kama Dk Kigangwala atakuwa na tatizo hilo la kisheria, Makamba alijibu: "Tatizo la nini wakati nimesema yeye ni raia?" Makamba alifafanua kwamba, Dk Kigwangala ana sifa zote zinazomfanya awe mgombea ndiyo maana Nec ilimpitisha.
  Kuhusu kama chama kinaweza kumrudisha Bashe kugombea nafasi hiyo, Makamba alisema: "Chama tayari kimeshamchagua mtu. Siwezi kuitisha uchaguzi halafu Nec, haya mambo yanafanyika kwa utaratibu wake, yaani leo hii niitishe Nec ijadili tena mgombea wa Nzega?"

  Vyama vyote vya siasa leo vinapaswa kupelekea orodha ya majina ya wagombea wa nafasi zake mbalimbali za uchaguzi kuanzia udiwani, ubunge na urais.
  Suala la Bashe lilizua utata mkubwa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kukataa kumpitisha kuwania ubunge wa Jimbo la Nzega akidaiwa kuwa si raia wa Tanzania kwa vile hakuukana uraia wa baba yake ambaye alikuwa Msomali wakati mwanasiasa huyo kijana akizaliwa.
  Baada ya Nec kumuengua, ilibainika kuwa Idara ya Uhamiaji ilishampa Bashe uraia wa Tanzania tangu mwaka 2009 na wakati CCM ikielekea kwenye kikao hicho, (uhamiaji) ilimuandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba kumueleza kuwa Bashe ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa.
  Kwa mujibu wa nyaraka nyingine kuhusu uthibisho wa uraia wa Bashe ambazo Mwananchi imeziona, inaonyesha kuwa baada ya kuomba uraia, Julai 10 ,2008 alipata barua kutoka Idara ya Uhamiaji ambayo ilisainiwa na Mashauri G.S kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uhamiaji kueleza kukiri kupokea ombi la Bashe na ilikuwa ikilifanyia kazi. Barua hiyo yenye kumbukumbu Na 109758 ilimtaka Bashe awe na subira wakati ombi lake likishughulikiwa na mara litakapokuwa tayari atajulishwa kwa barua.
  Septemba 24, 2008, Bashe alikula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo kuthibisha kuwa ni Mnyamwezi kikabila na ni mzaliwa wa Nzega Tabora. Barua ya Agosti 10 mwaka huu iliyotolewa na Idara ya Uhamiaji yenye kumbukumbu Na DN 109758 na kusainiwa na P .O Mgonja kwa niaba ya Kaimu Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, ilikuwa ikimjulisha Bashe kuwa haina barua nyingine zaidi ya aliyopewa yenye namba S/N 312 ya Agosti 10, 2009 iliyomthibitisha kuwa ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa kwa mujibu wa kifungu 5(1) au 7(8) cha sheria ya Uraia Na 6 ya mwaka 1995 ambayo alikabidhiwa.
  Tayari wanasheria wa Bashe wameshachukua hatua ya kufuatilia sakata zima la mteja wao kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji. Bashe aliongoza kura za maoni Jimbo la Nzega kwa kupata kura 14, 466, na kufuatiwa na Lucas Selelii aliyepata kura 2,706 wakati Khamis Kigwangala alipata kura 1,566. Kigwangala ndiye aliyepitishwa kupeperusha bendera ya CCM. Taarifa ya ziada ya CCM na Ramadhan Semtawa

  Waziri: Uraia wa Bashe hauna utata
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Samahani wakuu. Nimeona makala yenyewe kwenye gazeti la Mwananchi (mtandaoni) ila naona hii nchi inaongozwa kisanii sana. Yaani waziri anakwepa kujibu swali jamani? Mhhhh.
  Someni wenyewe,

  Waziri: Uraia wa Bashe hauna utata
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Bashe..Bashe, CCM haimtaki imemvua sio tu nafasi ya kugombea Ubunge pamoja na nafasi za uongozi kwenye UVCCM. Kwa kifupia sasa hivi Bashe sio tena mwanachama wa CCM kwa mujibu wa Chiligati.

  Sasa iwapo ni raia au sio raia; CCM haimtaki. Tena CCM imemvua huo aunachama kupitia NEC...mngejua uzito wa maamuzi ya NEC hili suala wala lisingeadiliwa tena.

  Bashe kama ana uhakika na uraia wake ajiunge na vyama vingine vya siasa...lakini huko CCM hatakiwi...period.
   
 15. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hadithi za hapo zamani za kale palitokea sungura na fisi.shame upon ccm mana sa ivi sijui wanadata.leo ivi kesho vile duh tusubiri tu kuuzwa sasa.
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Hakuna anayeweza kumjia Bashe uamuzi wake ni upi. Ila kwa kuwa Bashe ni memba hapa JF naomba aje ajibu mwenyewe na kututoa katika utata huu.
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kaka CCM wana visasi sana, kama bashe akiamua kuonyesha in public kwamba chama chake hakikuwa makini na uamuzi wa kumuengua kwamba hizo ni chuki binafsi na kutimkia chama kingine, CCM bado wanaweza kumshughulikia na kumaliza kabisa, mimi naona afuate maamuzi ya Mwakalebela kukubali yaishe. otherwise akiendelea kukomaa nao ni kijitafutia matatizo zaidi.

  Kuna tetesi tu alitofautiana na mtoto wa mwenye hekalu kwenye hiyo UVCCM yao, so issue inafukuta siku nyingi na haya ni matokeo tu...anyway chanzo sikiamini msininukuu.
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pata gazeti la MwanaHALISI halafu la 18-24 Aug 2010 halafu usome habari kuhusu Hussein Bashe iliyoandikwa na Ezekiel Kamwaga utaona kuwa mhusika mkuu katika hili sakata ni mwenyekiti wa CCM mwenyewe. CCM hawataki mtu wa kuhoji chochote!!!!
   
 19. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Viongozi "vijana" tuliowataka, waziri anakula "jinzi" kazini, tena siku anayoenda kukutana na waandishi mbele ya hadhara ya nchi.
   
 20. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yale yalikuwa ni maamuzi ya kihuni yaliyopewa baraka na NEC ambayo yanakidhalilisha chama cha CCM na kuwafumbua macho watanzania waliokua wamelala usingizi kiasi cha kushindwa kuelewa muelekeo wa chama hicho sasa ni wa maamuzi ya fitna na visasi.
   
Loading...