Hussein Bashe: Sina historia ya kukata tamaa, nitarudi tena Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hussein Bashe: Sina historia ya kukata tamaa, nitarudi tena Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Oct 6, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Hivi karibuni, vichwa vya habari katika vyombo vya habari vilitawaliwa na sakata la mmoja wa makada vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe kunyimwa fursa ya kuteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Nzega kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutokua kwake raia wa Tanzania.

  Mapana ya sakata hili la Bashe yaligusa viongozi wa juu wa CCM kwa kiwango cha kulihusisha hata jina la Rais Jakaya Kikwete, katika mahojiano haya na jarida la UMOJA, Bashe anaeleza masaibu aliyopambana nayo na malengo yake ya kisiasa kwa siku zijazo.


  UMOJA:
  Agosti 16 mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwatangazia Watanzania kuhusu uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kubatilisha ushindi ulioupata katika kura za maoni za kugombea ubunge wa Jimbo la Nzega baada ya kuibuka kwa utata kuhusu uraia wako. Uliupokeaje uamuzi huo?


  Bashe:
  Kwanza nianze kwa kukushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuhojiana nami na napenda nikupongeze wewe binafsi kwa kuja na wazo la kuanzisha jarida linalokwenda kwa jina la UMOJA. Jina tu la jarida linabeba maudhui muhimu. Kwanza nianze kwa kumzungumzia ndugu Chiligati...komredi Chiligati. Maamuzi ya mimi kutothibitishwa kuwa mgombea siyo tatizo kwani wako pia ambao hawakuteuliwa kuwa wagombea ingawa waliongoza katika kura za maoni.
  Mimi hilo sina tatizo nalo sana wala sikuwa na kinyongo nalo.

  Lililonisumbua ni lile la kunitangaza kuwa mimi si raia. Chiligati amepotosha Watanzania, alipotosha wana CCM wa jimbo la Nzega kwamba mwana CCM waliyempigia kura siyo raia wa Tanzania. Kwanza alikuwa ‘conclusive' wakati akijua hakuwa na mamlaka ya kisheria ya kutamka hilo. Lakini Chiligati alikwenda mbali zaidi na kusema nimevuliwa uanachama na akasema nimenyang'anywa kadi na nimevuliwa nyadhifa zangu zote na kwamba siruhusiwi hata kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu. Kilichonisikitisha kwenye kauli za Chiligati ni kwamba, amepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, na alichofanya ni ukiukwaji wa sheria kwa kuchukua mamlaka ya kumvua mtu uraia hadharani...amekiuka hata haki yangu ya kikatiba ya kuchagua viongozi kwamba siruhusiwi hata kupiga kura kuchagua viongozi wakati wa uchaguzi.

  Kwahiyo ndg yangu Kibanda nikuambie kitu kimoja URAIA wangu hauna utata na kuhusu mapokeo yangu juu ya kutoteuliwa sina tatizo kutoteuliwa na chama tatizo langu ilikua kauli ya chiligati alikwenda mbali kuongea vitu ambavyo hakua na mamlaka navyo kikatiba wala kisheria.

  UMOJA: Huoni kama alichokifanya Chiligati kilikuwa ni kutangaza maamuzi ya NEC ya CCM na hivyo kama ni kukiuka taratibu na sheria ni CCM waliofanya hivyo na si Chiligati?


  Bashe:
  Kwanza siamini maneno aliyoyatamka Chiligati ni maneno ya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu. Ninachofahamu Kamati Kuu haikujadili suala la mimi kunyang'anywa uanachama, Kamati Kuu haikutoa maagizo nirudhishe kadi ya chama, kamati kuu haikutoa maagizo kama siruhusiwi kupiga kura katika uchaguzi mkuu. Kamati Kuu haina mamlaka ya kumuambia Mtanzania yeyote kuwa wewe si raia na kwa hiyo huruhusiwi kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi,hiyo ni mamlaka yaliyochini ya Tume ya Uchaguzi si Maamuzi ya Chama cha Siasa wala Viongozi wake.


  UMOJA: Kwa hiyo unaamini kuwa Chiligati alitoa maneno yale kwa matakwa yake binafsi?


  Bashe:
  Ndiyo naamini hivyo kwakua maamuzi ya kumfuta mtu uanachama kuna utaratibu wake.


  UMOJA:
  Lakini katika siku za hivi karibuni maneno yanayofanana na yale ya Chiligati yalirudiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba. Huoni kwamba hilo linathibitisha kwamba ni maamuzi ya chama chako?


  Bashe:
  Katibu Mkuu hakutamka kuwa siruhusiwi kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu. Katibu Mkuu hakusema nitarudishwa Somalia. Katibu Mkuu hakusema naishi nchini kimazoea katibu mkuu hakusema mimi si mwanachama wa ccm. Kwa hiyo naamini yale aliyoyazungumza Chiligati ni ya kwake binafsi.


  UMOJA: Lakini hatujasikia CCM wakikanusha matamshi yale ya Chiligati na nakumbuka wakati akirudisha fomu ya kugombea urais Rais Kikwete alirudia kusema kwamba wewe si raia? Je umeshachukua hatua zozote za kufuatilia kuhusu jambo hili kwa kuwasiliana na mamlaka husika za dola?


  Bashe:
  Kwa mara ya kwanza nilipomsikia Chiligati akitamka hayo nilifanya mahojiano na BBC nikawaambia maneno haya nimeyasikia katika vyombo vya habari..kwani kwa taratibu za chama chetu hakiwasiliani na wanachama wake kupitia katika vyombo vya habari hasa kwenye jambo sensitive kama hilo la haki za mwanachama, nilitarajia kwamba, chama kiniambie, una mapungufu moja, mbili, tatu na tunakuomba urudishe kadi yetu. Chama hakikufanya hivyo. Kwa hiyo niliyachukuliwa kuwa ni maongezi ya Chiligati.


  Baada ya kusikia imefika level hiyo uliyoitaja (kuzungumziwa hadi na rais) nikaona huenda chama changu kina taarifa zisizo sahihi kwa hiyo nilichukua hatua. Nilimuandikia Waziri wa Mambo ya Ndani barua. Kwanza nikurudishe nyuma, Agosti 10 wakati sekretarieti ikienda kukaa, suala hili la uraia nililisikia kwenye corridors (viambaza) na kwa sababu najua kuwa katika siasa kuna kutengenezeana mabomu, niliiomba wizara kwa barua, imuandikie Katibu Mkuu wa CCM imueleze juu ya status yangu ya uraia. Agosti 13, kabla hata Kamati Kuu haijakaa, barua ile ilikwenda hadi kwa Katibu Mkuu, ikiwa imeambatatanishwa na vyeti vyangu vyote.


  UMOJA: Je, kama hivyo ndivyo ni nini kilitokea. vile vielelezo na barua havikuifikia sekretarieti, Kamati Kuu au Halmashauri Kuu au kuna mambo mengine yalitokea?


  Bashe:
  Mimi siwezi kubuni ni nini kilitokea kwa sababu nitapata dhambi ya dhana. Mimi nilichokifanya nilifanya jitihada baada ya kupata hizo taarifa nikapeleka nyaraka na barua inayotoka kwa Mkurugenzi wa Uhamiaji ikithibitisha kwamba mimi ni raia kwa kuzaliwa.


  UMOJA: Je kuna majibu yoyote uliyapata baada ya NEC kumaliza vikao vyake na suala lako kutangazwa kwa namna ilivyotokea ndani vya vikao hivyo vya CCM?


  Bashe:
  Nilichokifanya niliandika kwa Waziri wa Mambo ya Ndani nikimuomba mambo makubwa mawili, barua yangu ilikuwa bayana kabisa, kwanza tuelewe kitu kimoja,suala la uraia wangu na lile la kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi ni vitu tofauti. Suala la uraia wangu ni la Mambo ya Ndani suala la kuwa mgombea ni la chama. Kwa hiyo chama kina maamuzi ya kumchukua mgombea yeyote kuwa mgombea wake.


  Baada ya kuona Chiligati kaongea, nani kaongea! Mzee Makamba namuheshimu sana kuwa ni mzee wangu. Kwamba naye kaongea nikaona hili ni jambo serious...nikaamua kuandika tena wizara ya mambo ya ndani nikiomba mambo yafuatayo. Moja ikiandikie Chama Cha Mapinduzi kuhusu status yangu ya uraia na kama kuna tatizo juu ya uraia wangu niambiwe. Hilo la kwanza. Lakini la pili niliiandikia wizara nikiomba waziri anipe kimaandishi status yangu ya uraia kitu ambacho nashukuru waziri amenijibu, Septemba 3, ameniandikia barua na ninayo, akiendelea kusisitiza barua yake ya tarehe 10 mwezi wa nane na ya tarehe 13 na leo tena anasema nasisitiza na narejea kwamba Hussein Bashe Ibrahim ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.


  UMOJA: Baada ya majibu hayo tena umeamua kuchukua hatua gani pengine juu ya Chiligati, Makamba au chama chako?


  Bashe: Hapana hakuna hatua nilizochukua dhidi ya chama changu wala viongozi wake . Ninachoamini ni kwamba chama changu kimepelekewa taarifa na mimi naweza kukielewa kwamba Kamati Kuu imekaa Ijumaa usiku ikitanguliwa na vikao vya kamati ya maadili na Jumapili asubuhi ndiyo matokeo yametangazwa. Nadhani kulikuwa na tatizo la muda, labda ingekuwa vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati vina muda wangeweza kupata muda wa kulifuatilia hili jambo na kupata ukweli wake kwahiyo naamini maamuzi ya chama yalikua yana GOOD FAITH kutokana na taarifa walizopata waliona kuna hatari ya kuteua mgombea mwenye tatizo la uraia then jimbo likwa halina mgombea tukapoteza wakaamua kufanya maamuzi hayo ambayo yalikua magumu sana kwa chama na wana chama wa jimbo la Nzega na nadhani kutokana na hili CCM tumejifunza jambo.


  UMOJA: Awali ulizungumzia kuhusu tabia ya watu kuundiwa mabomu katika siasa. Hili lako unajua lilitoka wapi? Nzega au sehemu nyingine?


  Bashe:
  Labda nikupe historia kidogo, bomu hili lilitaka kujitokeza mwaka 2008 lakini kwa sababu nilikuwa na muda wa kulishughulikia halikuweza kufika. Waliokuwa wameliandaa wako na nawafahamu, na wengine wamediriki kujisifia na kuongea kwamba wameniweza.


  UMOJA: Kwa hiyo unasema lilitokea mwaka 2008 wakati ukigombea nini?


  Bashe: Wakati huo nilikuwa nagombea umakamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa


  UMOJA:
  Siyo kwamba ulikuwa ukigombea uenyekiti wa vijana?


  Bashe: Niligombea uenyekiti...? Sikugombea nilijaza fomu ya kugombea uenyekiti lakini chama kikaamua kutupeleka kugombea umakamu, wakati huo liliibuka hili, likatengenezwa tengenezwa likaibuka, lakini namshukuru mwenyekiti wa umoja wa vijana aliyemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi moja ya vipaji vyake huyu jamaa huwa hakurupuki anapofanya jambo, yalipoibuka haya, aliyafanyia uchunguzi kabla ya kupeleka katika vikao vya kamati ya utekelezaji ya vijana, akajiridhisha kwamba hakuna hoja bali ni fitina.


  Safari hii hawa watu waliolitengeneza hili waliangalia muda wa vikao kuwa ni mfupi, wakalitengeneza hili bomu wakalipeleka kwenye vikao likaingizwa, wakijua kuwa tu vikao havikuwa na muda wa kulifanyia uchunguzi, vinginevyo naamini haya yasingetokea.

  UMOJA: Lakini ninachojua mimi umoja wa vijana CCM unawakilishwa na viongozi wake katika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu sasa wao ni kwa nini hawakulisemea hili ndani ya vikao?


  Bashe:
  Katika hili pia naamini Dk. Nchimbi angekuwa kwenye kamati kuu leo au halmashauri kuu, hili lisingetokea au hata kama angekuwapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana aliyeondoka, Francis Isaac haya yasingefika huko yalikofika..,lakini Bahati mbaya Viongozi wetu wa sasa wa Jumuiya kwa maana ya Katibu mkuu na Makamu Mwenyekiti wakati wa 2008 hawakua katika nafasi walizo nazo sasa kwahiyo hawakuwahi kua na Historia nalo jambo hili,wangekua wanalifahamu naamini wangelisemea na kuweka Record sahihi.


  UMOJA: Ukiacha hilo, nakumbuka wakati alipolizungumzia suala lako la uraia, Chiligati kwanza alisema wazazi wako wote wawili baba na mama walikuwa ni raia wa Somalia lakini pili akaenda mbele na kusema kwa kuwa wewe ulizaliwa hapa Tanzania basi ulipaswa baada ya kufika umri wa miaka 18 uukane uraia wa wazazi wako jambo ambalo alisema hukupata kulifanya. Hata hivyo kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari ambazo zinaeleza ulipata kukana uraia wa Somalia kwa kiapo. Unaweza ukalitolea maelezo hili?


  Bashe:
  Ndiyo maana nikasema Chiligati aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amekuwa kiongozi kwa muda mrefu, nilitarajia kwa busara ya kawaida asingefikia hatua ya kuongea hiki kitu. Hakuna jambo baya kama kuongea bila kuwa na taarifa kamili juu ya jambo. Tulizungumzie la wazazi wangu, ndiyo maana nasema kuna upotoshwaji wa mambo mengi, kihistoria, familia ya upande wa mama yangu, yaani babu yangu walihamia Tanzania mwaka 1902 na babu yangu huyu kati ya mwaka 1902 hadi 1927 alikuwa akiishi maeneo ya Sumbawanga na Tabora na hususan Sumbawanga sehemu moja inaitwa Lahela. Babu yangu mzaa baba na baba yangu walihamia Tanganyika mwaka 1949. Ni sahihi kama alivyosema Chiligati, baba yangu kazaliwa Somalia, ni kweli. Lakini mama yangu hakuzaliwa Somalia, alizaliwa Tabora, mtaa wa Ujiji nyumba namba 4. na Chiligati anavyosema wazazi wangu wamehamia nchini miaka ya 1960 wakiwa wanatoka Somalia ni uongo, ni upotoshaji mkubwa sana.


  UMOJA:
  Au pengine alisema kwa kutojua?


  Bashe:
  Hapana ni upotoshaji, naamini ni upotoshaji, huyu amepata kuwa waziri wa mambo ya ndani, anajua sheria, kanuni na taratibu.Pia nikueleze jambo moja Kwa watu wanaojua historia ya nchi hii, mwaka 1957 wakati Mwingereza anaandaa uhuru wa Tanganyika, aliwaita watu wote wenye asili ya nje ya (Asians,wazungu n.k) akawapa chaguo la ama kuendelea kubakia katika himaya ya Uingereza na kuendelea kuwa na uraia wa nchi walizotoka au wawe Watanganyika kwa kuwa nchi ilikuwa inaelekea kupata uhuru. Babu zangu waliamua kwa dhati kuwa raia wa Tanganyika.


  UMOJA: Babu zako upande upi Kwa baba au kwa mama?


  Bashe:
  Wote. Waliamua kuwa Watanganyika. Chiligati anasema wazazi wangu wamehamia miaka ya 1960...hajui historia. Kwanza baba yangu alikuwa mwanachama wa TANU na kadi yake ninayo tena mwanachama hai wa TANU toka mwaka 1960 hadi mwaka 1975 akiwa analipia ada zake.


  UMOJA:
  Kama hivyo ndivyo, kimsingi unachokisema hapa ni kwamba hukupaswa hata kula kiapo cha kuukana uraia wako?


  Bashe:
  Technically yes...subiri nikueleze sikupaswa hata kuukana uraia wa baba lakini unajua ni kwa nini niliukana?. Niliukana kwa sababu mwaka 1984, ehee... mwaka 1984 kuliibuka operesheni ya kamatakamata wahamiaji. Baba yangu akahojiwa na yeye kuhusu URAIA wake. Aliyekuwa afisa uhamiaji wa wilaya ya Nzega kati ya mwaka 1986- na 87 alikua bwana Mmoja anaitwa Mr Malongo alimwita baba na akamshauri akisema ‘si uombe tu uraia ili uache kusumbuliwa kila mara wakija maafisa wageni wankufata kutaka maelezo yako? ili kuepuka usumbufu' Baba akafanya hivyo.


  UMOJA:Kwa hiyo aliomba ili kuepuka usumbufu?


  Bashe:
  Ndiyo alifanya hivyo kuepuka usumbufu,Pia Bibi yangu mzaa mama, kazaliwa Boma Ng'ombe Kilimanjaro mwaka 1921 na ukienda leo Rita (Wakala wa Uzazi na Vifo) utakuta wamesajiliwa, bibi yangu mzaa mama, mama yangu mzazi, mama mkubwa na mjomba wangu...katika hili nimeenda mwenyewe kufanya uchunguzi na wameandikwa utaifa wao ni Watanganyika na wamesajili 1958. Chiligati nasema bado amepotosha na alikurupuka. Mwaka 1961 vijana waliokwenda uwanja wa polisi Nzega kupandisha bendera ya Tanganyika mmoja wa Vijana wa Tanu wakati huo, ni baba yangu na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Nzega leo, mzee Mwalimu Shija, enzi hizo wakiwa vijana. Wakati huo Mzee Shija alikuwa ni katibu wa tawi la TANU Nzega Branch. Kwa hiyo nasema ni hatari, ni hatari kwa viongozi wetu wakubwa kutoka kwenye public na wakijiamini kuongea vitu wasivyo na taarifa kamili.


  UMOJA:
  Wewe huoni kama huenda hicho unachodhani ni upotoshaji kilifanywa kwa malengo fulani ya kisiasa?


  Bashe:
  Katika mazingira ya namna hii, lolote lile unaweza ukalifikiria. Ni vigumu kutoamini.


  UMOJA: Vyombo vya habari vimepata kuripoti kuwa chimbuko la sakata lako la uraia ni siasa za makundi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM ambako wewe ni kiongozi, hili unalisemaje?


  Bashe:
  Vyombo vya habari vina kila sababu ya kuandika hivyo kutokana na utamaduni mbaya ambao tumejijengea ndani ya umoja wetu tangu tulipomaliza uchaguzi wetu mwaka 2008, na mimi nimewaambia wenzangu kwamba utamaduni huu ni mbaya. Tulianza kwa kumshughulikia aliyekuwa Katibu Mkuu wetu, Francis Isaac. Na mimi mpaka leo msimamo wangu na imani yangu ni kwamba uamuzi wa kumshughulikia Isaac ulikuwa ni mkakati wa kisiasa.

  Ni mbegu mbaya tuliyoipandikiza siku ya kwanza. , hata hivyo, dhambi ya mbegu ile tuliyoipandikiza imesababisha lolote linalojitokeza liwe linajitokeza katika misingi sahihi au isiyo sahihi na maamuzi yanachukluliwa sahihi ama si Sahihi.

  Kinachofanywa na vyombo vya habari na jamii ni kuamini hivyo kwa kuunganisha dot. (watajiuliza) Huyu rafiki yake ni nani. Badala ya kuangalia ajenda. Changamoto kwetu kama jumuiya ya vijana ni lazima tutafute njia ya kujivua hilo koti. Baada ya Isaac likaja lile (Hamad) Masauni kung'olewa na sasa limenikuta mimi. Watu wanaunganisha haya mambo.


  Kwahiyo Binafsi siamini kwamba lililonotokea ni kutokana na siasa za Makundi ndani ya Jumuiya,Bali hili halina uhusiano wowote,inawezekana tunatofautiana Mitazamo kwa Maswala Flani Flani lakini naamini ukiangalia siasa za Uvccm zina Historia ya Namna hiyo Tangu wakati wa Guninita,Dk Nchimbi,kulikua na Makundi na Makundi haya yanaifanya Jumuiya kua Active tunatofautiana Hoja na Mitazamo kwa Maslahi ya Chama na Taifa letu na Hatijengi Uadui huo ni Mtazamo wangu


  UMOJA: Lakini tukianza na Isaac kwa mfano kulikuwa na tuhuma nzito dhidi yake?


  Bashe: Kwa Isaac naamini tuhuma zilizosemwa dhidi yake hazikuwa ni za kweli. Magazeti yaliandika ni ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka. Mpaka leo hakuna official statement (taarifa rasmi) iliyokuja kwenye Baraza Kuu (la Vijana) iliyosema sababu ya kumuondoa Isaac. Lakini tunamshukuru Mwenyekiti wa Taifa wa chama chetu. Tunaamini Rais Kikwete anazo taasisi zinazofanya kazi yake...tunaamini kama Isaac angekuwa mbadhirifu, angekuwa mtumiaji mbaya wa madaraka, nafasi aliyompa asingempa. Naamini Isaac ni mtu safi hakuwa na matatizo. That's why Rais alimpa Majukumu Mengine Makubwa.


  UMOJA:
  Na hili la Masauni ambalo umelitolea Mfano, maana huyu anatuhumiwa kufanya kosa la kijinai na ukiukwaji wa kanuni za umoja wa vijana wa CCM kwa kudanganya kuhusu umri wake jambo ambalo lilimuondolea sifa za uongozi. Je huoni kama unatetea uhalifu hapo?


  Bashe: Kwanza ningekuwapo kwenye Baraza Kuu Iringa alikong'olewa ningehoji vitu vingi ili nipate majibu, lakini sikuwepo bahati mbaya na ninamaanisha bahati mbaya.


  UMOJA: Kwa nini hukuwapo?


  Bashe: Nilichelewa nilikuwa Nzega, kutoka Nzega nikaharibikiwa gari na nikafika Dar es Salaam Jumatatu, wakati huo baraza lilikuwa limekwisha. Najiuliza maswali madogo, mwanachama anajaza fomu, vinaanza vikao vya kumjadili na kuchunguza taarifa hizo kama ni sahihi au siyo sahihi. Masauni hatukumjua kwenye uenyekiti tu, tumemjua akiwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (ya CCM) kupitia vijana ndiyo akaja hapo. Mpaka miaka miwili baadaye ndipo tunajua kuwa alidanganya umri.


  UMOJA:
  Kwa sababu hiyo wewe ulikuwa mmoja wa viongozi wa vijana waliomtetea Masauni?


  Bashe:
  Kwanza niliseme hili Masauni ni rafiki yangu


  Bashe: Ndiyo. Ni rafiki yangu , kama alivyo mwingine yeyote, na siwezi kumkimbia rafiki kwa sababu kakumbwa na matatizo...nadhani hiyo ndiyo falsafa yangu binafsi ya urafiki. Binafsi sikukubaliana na utaratibu uliotumika kumuondoa Masauni. Masauni kaghushi, kajaza taarifa zisizo sahihi...utaratibu wa chama chetu upo wazi, kama kuna jambo mimi nadhani linakwenda kinyume cha utaratibu siwezi kulipeleka kwenye magazeti.

  Utaratibu uliotumika kumng'oa Masauni ni pressure ya media (shinikizo la vyombo vya habari). Watu walichukua nyaraka wakapeleka kwenye vyombo vya habari, kesho yake taarifa hizo zikatoka kwenye magazeti. Huo ndiyo utaratibu uliotumika kumuondoa. Ni utaratibu mbaya. Hii ni mbegu mpya mbaya ambayo tumeipandikiza. Utaratibu wa chama uko wazi, kama mimi naamini wewe umejaza taarifa zisizo sahihi, naandika barua napeleka malalamiko yangu kwa Katibu Mkuu wa chama. Na yeye atakuitwa na utatakiwa kutoa maelezo na kama una utetezi unautoa na baada ya hapo chama kinatoa maamuzi. Hayo yote hayakufanyika kwa Masauni.


  UMOJA: Je, kama hali iko hivyo, unadhani leo hii kuna mshikamano wa kutosha ndani ya umoja wenu wa vijana?


  Bashe: Niseme kwamba ndani ya jumuiya yetu linapokuja suala la CCM dhidi ya wapinzani tuko united (tunashikamana) kwa sababu pale tunaangalia maslahi ya chama, tofauti zetu tunaziweka pembeni kwanza tunashughulikia hilo, lakini changamoto kubwa tuliyonayo leo tuna kitu wazungu wakiita mistrust.


  UMOJA: Unamaanisha hamuaminiani?


  Bashe: Ndiyo. Tatizo ni kutoaminiana


  UMOJA:
  Lakini katika hilo hilo la makundi, ziko taarifa ambazo zimepata kuripotiwa katika vyombo vya habari zinazosema kwamba, mahusiano yako mabaya na mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete ni moja ya chachu zilizokufikisha wewe hapa ulipo leo. Hili unalielezaje?


  Bashe:
  Mimi na Ridhiwani siwezi kusema kwamba tuna uhusiano mbaya. Inawezekana tunatofautiana mitazamo. Hili ni jambo la kawaida kibinadamu, si kila jambo nalofikiria mimi nawe utalifirikia hivyo hivyo. Yako mambo inawezekana kweli mimi na Ridhiwani hatukuwa tukikubaliana kimitazamo, lakini sidhani kama tuna uhusiano mbaya kwa kuwa hatujawahi kugombana. Hilo ni la kwanza na la pili niseme tu kwamba, siamini mpaka sasa hivi kama Ridhiwani kuwa anahusika katika tatizo lililonikuta, lakini kama anahusika basi namsamehe kwani hata maandiko matakatifu yanasema uwasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo. Lakini bado siliamini hilo. Hata hivyo wako ambao naamini wanahusika na hilo.


  UMOJA: Hao ndiyo wale uliosema awali unawafahamu?


  Bashe: Ndiyo hao. Ninawafahamu


  UMOJA:
  Wakati wa mchakato wa kusaka mgombea wa ubunge jimbo la Nzega ndani ya CCM mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo hilo, Lucas Selelii alipata kusikika akilalamika ndani ya Bunge kuwa amepandikiziwa watu wa kumng'oa na yalipotoka matokeo ya kura za awali ambazo wewe uliongoza akasikika akisema ameshindwa kutokana na nguvu ya fedha. Na akasema kwa uchache shilingi kama bilioni moja zilitumika kumng'oa. Huoni kwamba alikuwa akikulenga wewe katika matamshi yake hayo?


  Bashe: Kwanza hakunisema mimi kwa jina kuwa ndiye niliyetumwa kwani angenitaja ningemjibu. Siyo kweli hata kidogo kwamba eti Nzega zilitumika shilingi bilioni moja kumng'oa. Labda tu Watanzania hawajui. Selelii hana historia ya kushinda Nzega. Wazungu wanasema ‘he is unpopular' ni mwanasiasa asiyekuwa na ushawishi, najua yeye he is making lead stories kwa maana ya kuuza magazeti. Leo Selelii akisema ‘vuvuzela' basi neno vuvuzela linashika kasi kila sehemu, media zote (vyombo vya habari) zikawa zinaandika vuvuzela.

  Lakini Selelii ni mbunge ambaye hakuwa maarufu ndani ya jimbo lake. Mwaka 2000 alishinda bwana mmoja anaitwa Abdallah Nassoro na si Selelii. Mwaka 2005 alishinda kwa mizengwe, kwa vurugu na kwa kuleta wapigakura hewa na mimi nikiwa mgombea na kwenye kura za maoni mimi nikawa mtu wa tatu. Selelii hana mizizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu hajawahi kuwa kada ndani ya jimbo la Nzega na wilaya ya Nzega.


  Na katika Politics za Majimbo wanachi wanakua na Imani na Kiongozi ambae amewatendea Mema selelii amekua Mbunge ambae alikuwa Busy na Mengine akasahu Jimbo lake hiki kili Mgharimu,Pia ifahamike hajawahi kua hata Balozi wa Nyumba Kumi,na to be Honest Hakuna Mgombea alietumia Fedha Nyigi Kama Selelii kwa Jimbo la Nzega.

  UMOJA: Aliwezaje basi kuwa mbunge wa CCM?


  Bashe: Hajawahi kuwa active politician (mwanasiasa wa hadharani) ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Mwaka 1995 wakati wazee walipokuwa wanatafuta mgombea, walikwenda kumchukua akiwa counter (sehemu ya kulipia gharama) hotelini kwao, walikuwa na hoteli inaitwa Selelii ambayo hata mimi utotoni nilikuwa nikienda pale kula vitumbua na maandazi. Ilikuwa maarufu sana Nzega. Aliyekuwa maarufu kwao ni marehemu mdogo wake na ndiye aliyemshika mkono mwaka 1995 kumnadi. Kule kwetu usafiri mkubwa ni baiskeli. Mdogo wake alikuwa na duka linauza vifaa vya baiskeli alikuwa mtu maarufu na anajulikana na alikuwa mchangamfu na mtu wa watu na ndiye aliyemshika mkono Selelii mwaka 1995.

  Anaposema zimetumika shilingi bilioni moja, hakuna mwanasiasa ameingiza fedha nyingi katika jimbo kama Selelii. Kumbuka Selelii ndiye aliyetuletea vikoba, lakini siasa ni namna gani unakuwa na mahusiano na watu, Kwa watu walio nje ya Nzega walikuwa wanaona kupambana na Selelii ni muujiza...Nakumbuka miye kuna bwana mmoja aliniambia unagombea Nzega! Utamweza Selelii? Kugombea na Selelii kilikuwa kikionekana kuwa ni jambo gumu sana.


  UMOJA:
  Kumekuwa na taarifa kwamba msingi wa nguvu zako Nzega ni ushawishi alionao Mbunge wa Igunga aliyemaliza muda wake, Rostam Aziz ambaye inadaiwa kwamba yeye ndiye amekuwa nyuma ya kugombea kwako ubunge akifanya hivyo kutokana na siasa za upinzani ndani ya Bunge ambazo zilimfanya atofautiane na Selelii. Hili unalielezaje?


  Bashe:
  Watu wasiojua historia... Selelii amekuwa akimtaja mheshimiwa Rostam kwamba ananisaidia, watu wanasahau kwamba mwaka 2005 aliyemsaidia Selelii kushinda ubunge wa Nzega ni Rostam sijui umenielewa? Mimi hata wakati wa kampeni nilikuwa nikimuuliza Selelii, wewe unaninyoshea kidole cha mimi kusaidiwa na Rostam ,wewe na Urafiki wenu iliishia wapi? Kama mimi nasaidiwa leo, wewe mwaka,1995, 2000 ulisaidiwa, 2005 ulisaidiwa, sasa wewe ukisaidiwa ni halali, wengine wakisaidiwa ni haramu, lakini vile vile ndiyo maana nasema kwamba watu wasiomjua Selelii hawajui kuwa ni bingwa wa kutengeneza vitu, ni bingwa wa kutengeneza uongo. Siye tumekua tunamjua, hakuna mtu aliyemnyoshea kidole yeye kwamba alikuwa akisaidiwa na Mzee Reginald Mengi.


  Kibanda nikueleze kwamba Rostam ni Muajiri wangu, Ni Mjumbe wangu wa NEC kutoka Mkoa wangu wa Tabora,ni kweli amekua Ni mtu ambae ananisaidia ushauri kikazi na Kisiasa, na Politics lazima uwe na Marafiki huwezi leo kutuhumiwa kwa Jambo then Marafiki wote wakakukimbia kwahiyo nikuambie kwamba si kweli ushawishi wangu wa kisiasa katika jimbo la Nzega umtokana na Ushawishi wa Rostam Aziz.


  UMOJA: Mengi alimsaidiaje Selelii?


  Bashe:
  Kupitia katika Vikoba


  UMOJA: Kwa nini huoni kwamba Mengi alikuwa akiwasaidia wananchi wa Nzega na siyo Selelii binafsi?


  Bashe: No. Kwa nini hakupeleka fedha hizo Igunga? Kwa nini hakupeleka Bukene jimbo ambalo lina umaskini mkubwa kuliko Nzega? Deciding factor ni nini? Ni mahusiano yake yeye (Selelii) na Mengi. Watu wasiojua historia, mwaka 2005 mimi nimeenda kugombea Nzega nilisaidiwa na nani? Nikiwa sina base ya kisiasa nikiwa sina nini wala nani na nikawa mtu wa tatu kati ya wagombea tisa kwenye kura za maoni. Nilisaidiwa na nani?


  UMOJA: Ziko taarifa kwamba nguvu za kifamilia na hususan nafasi aliyonayo baba yako anayeongoza taasisi moja nyeti Nzega ndiyo iliyokusaidia au?


  Bashe: Sasa kwanini imesahaulika historia ya familia yangu imechukuliwa factor (kigezo) moja ya Rostam kama mtaji wa kunisaidia kushinda? Kwa hiyo wako wanasiasa na wengine hivi majuzi walikuwa kwenye wilaya yangu wanaongea wanasema ooh tunajua nguvu za Hussein zinatokana na Rostam. Nataka rekodi ziwekwe sahihi. Ni kweli Rostam anaweza akawa mtu ambae amekua ni Mshauri na Kiongozi wangu kama walivo wana siasa wengine ambao nashirikiana nao. Ndiyo. Lakini nguvu zangu za kisiasa na jitihada zangu za kisiasa katika jimbo la Nzega ni matokeo ya mahusiano yangu na watu wa Nzega. Mimi nimezaliwa wilaya ya Nzega, nimecheza cha ndimu Nzega, nimesoma shule za msingi tena za uswahilini, hawa hawa ambao leo ni vijana Nzega, wazee Nzega, ndiyo walionikuza na ukitazama kura nilizopata ni kura za imani. Kwa hiyo wako watu ambao nashirikiana nao kisiasa kwa kuwa nakubaliana nao kimtazamo na nakubaliana nao kimsimamo, lakini haina maana kwamba huwa hatutofautiana katika baadhi ya mambo.


  UMOJA: Kwa hiyo ni wazi umejipanga kugombea tena ubunge Nzega?


  Bashe:
  Why not? (Kwa nini nisifanye hivyo?)


  UMOJA:
  Unatarajia kugombea kupitia CCM au unafikiria kuhama chama?


  Bashe:
  Siwezi kuhama CCM


  UMOJA: Unakumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipata kusema CCM si baba yake wala mama yake na anaweza kuhama
  ?

  Bashe:
  Ndiyo alisema, lakini hakuhama CCM na Mimi Sitahama CCM kama kuna yanayoni kwaza ndani ya chama nitayasema ndani ya Vikao Husika na kuomba kufanyiwa Marekebisho,Am a Beliver wa Change from Within not From out Side.


  UMOJA: Naona hukati tamaa


  Bashe:
  Siwezi kukata tamaa kwa kuwa sababu mimi sina historia ya kukata tamaa


  UMOJA: Unawaambia nini basi wananchi wa Nzega?


  Bashe:
  Ningetaka tu niwaambie wananchi wa Nzega kwamba nashukuru kwa kura walizonipa. Kura 14,422 ni nyingi mno. Mgombea aliyeteuliwa na chama amepata karibu asilimia 10 tu ya kura nilizopata mimi. Alipata kura 1,500. kwa hiyo nataka niwaambie wananchi wa Nzega kwamba, kwanza nathamini kura zao na mchango wao kwangu. Imani waliyonionyesha inatokana na matendo yangu kwao. Ninawaahidi nitaendelea kushirikiana nao kama tulivyokuwa tukishirikiana kabla sijaja kugombea. Jitihada zangu na mchango wangu kwa wananchi wa Nzega na wana CCM vitaendelea vile vile kama zilivyokuwa siku za mwanzo. Tulishambulia wote tukapata ushindi, tukafurahi na wote tukapata mshtuko na majonzi makubwa. Ipo siku Tunafuta machozi pamoja.


  UMOJA: Kabla hatujamaliza mahojiano, hebu nirudi katika lile lililosemwa na viongozi wa juu wa CCM kama Chiligati kwamba umevuliwa nafasi zote za uongozi ndani ya chama hicho. Unalielezaje hili?


  Bashe:
  Kwanza Chiligati alisema nimevuliwa nyadhifa zangu zote. Siyo sahihi. Katiba yetu ya CCM iko bayana mtu kuondolewa nyadhifa, kuondolewa uanachama ni maamuzi ya vikao na kuna utaratibu hatuvuani madaraka na uanachama namna alosema chiligati,na Ili umvue mwana CCM madaraka kuna vitu vinvyopelekea mtu kuvuliwa Madaraka,kama alitumia kigezo cha URAIA mimi ni Raia


  UMOJA: Na hili kwamba umepoteza sifa za kuwa mwanachama?


  Bashe: Ndiyo ni maamuzi ya vikao vinavyomfanya mtu apoteze uanachama na apoteze nyadhifa zake. Hili nalo Mzee Chiligati alikosea, mimi bado ni mwanachama wa CCM mimi bado ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Tabora, ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa. Sijapoteza nafasi zangu kwa sababu kwanza hakuna kikao cha chama kilichokaa kufanya haya maamuzi. Na kama alitumia base (kigezo) ya uraia, mimi ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo alikosea.


  UMOJA: Lakini huoni kuwa ni vigumu sana kutofautisha matamshi ya Chiligati na maamuzi ya NEC?


  Bashe:
  Labda aje kiongozi wa juu wa CCM aseme matamshi ya Chiligati ni maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa, kwamba nilivuliwa uanachama na siwezi kupiga kura.na ili umvue mtu Uanachamakuna utaratibu wa kufata ambao kikao kile hakikua Agenda hiyo.


  UMOJA: Baada ya kupata barua hii ya sasa kwamba wewe ni raia, unawaangalieje basi viongozi wako wa CCM Taifa na wajumbe wa NEC?


  Bashe: Sijawahi kuwa na kinyongo na viongozi wangu wa chama na sintakuwa na kinyongo nao, leo kwa haya niliyoyaona yananikumbusha kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza katika kongamano la viongozi vijana lililofanyika katika hoteli ya Kempinski, aliposema ndoto yake ni kuona katika serikali yake ijayo, atafanya kazi na viongozi vijana. Nilipoangalia mkanda wa Chiligati wakati alipokuwa akitoa matamshi dhidi yangu nikajifunza kwamba mzee wangu huyo alikuwa amepitiliza, pengine kwa sababu ya uchovu. Unajua walianza sekretarieti, kamati ya maadili, kamati kuu usiku kucha, NEC hadi alfajiri ndipo akaja kuzungumza. Inawezekana alichoka kwa hiyo akapitiliza kwa sababu ya uchovu.


  UMOJA:Unazungumzia uchovu wa umri au?


  Bashe: Umri ndiyo, ukiangalia na majukumu, ndiyo kwanza alikuwa ametoka katika kura za maoni ambako alishinda kwa shida


  UMOJA: Sasa baada ya matukio ya mizozo katika kura za maoni ndani ya CCM na kwa jinsi mchakato wa kampeni za urais, ubunge na udiwani zinavyoendelea, ni matokeo ya namna gani ambayo Watanzania wanapaswa kuyatarajia katika uchaguzi wa mwaka huu?


  Bashe: Labda niseme kitu kimoja kwanza CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa tulishinda kwa zaidi ya asilimia 90. Tumetoka hapo. CCM itashinda kwa kura nyingi sana. Kwa sababu moja ya tatizo ninaloliona na kwa mtazamo wangu rais Kikwete atashinda kwa kura nyingi kama zile za mwaka 2005 au zaidi. Udiwani CCM tutapata over 90pc,ktk tutapata upinzani kwa baadhi ya maeneo lakini Tutashinda kwa Kura Nyingi.


  UMOJA:
  Yaani pamoja na joto kubwa la kisiasa lililoibuliwa na Chadema unasema hivyo?


  Bashe:
  Any political party lazima iwe na kitu kinaitwa party machinery. Jimbo la Nzega ninalotoka,Chadema wako Nzega mjini, lakini CUF wana ofisi katika kata saba.chadema hawana unatarajia watapataje ushindi,Pia kujenga chama kunahitaji Commitment ya chama kuanzia ktk Grassroot,nikupe Mfano kwa miaka mitano ilopita chama kama Chadema nzg hawajawhi kufanya Mikutano hata kumi unatarajia nini?CCM tuna strong Political Machinery,tuna Viongozi Commitment mpaka ktk Grassroot wenzetu hawana, kuna 'big gap' katika viongozi wa Taifa wa Upinzani na wale wenzao wa Mawilayani, Vyama vyao vimekua vya Matukio, ukiangalia maaeneo machache walio na Nguvu it is because of our Mistakes.


  UMOJA:
  Lakini wewe huoni kwamba CCM kushinda kwa kishindo si jambo jema kidemokrasia?


  Bashe:
  Ni kweli tunauhitaji upinzani na upinzani ni kitu cha afya uwe upinzani katika issues. Chama cha siasa kijengwe kiwe kinashindana katika sera, hiyo itatufanya katika CCM tuendelee kuwa active, tusijisahau lakini nikiangalia kampeni zinavyokwenda sasa hivi, mimi nafuatilia wagombea. Siasa za ushindani katika masuala zinaondoka, yanazungumzwa masuala binafsi. Tumebaki tunajadili watu, hatutumii makosa ya nyuma, kama yaliyokuwapo, mimi ningetegemea nchi hii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yametokea mambo mengi makubwa yalikuwapo yale ya EPA, Richmond hoja nyingi, lakini sijamuona mwanasiasa wa upinzani akiibuka na akasema kulikuwa na mapungufu haya ambayo yalisababisha matatizo haya ya Richmond kwa Watanzania ambayo imetugharibu shilingi milioni 450 za walipa kodi na miaka tatu ya muda wetu na tatizo letu lilikuwa ni sheria hii na hii. Mimi nikiingia madarakani nitarekebisha hili na hili. Sasa zimebakia hoja za EPA, mafisadi, tutawafunga, tutawafanya nini sijui.


  UMOJA: Bashe nini Mtazamo wako kuhusu Serekali ya awamu ya NNE?


  BASHE:
  Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa kipindi hiki cha awamu ya kwanza ukumbuke kwamba wakati Rais jakaya anaingia Madarakani amekumbana na mambo makubwa matatu, Moja UKAME, mbili NJAA, Tatu MTIKISIKO WA UCHUMI, na Mbaya zaidi Bunge LILIASI ambalo lilhama kujadili Isuues za kuwasaidia watanzania na kuanza kujadili issues zinazo wahusu watu Flani Flani kwa Almost miaka mitatu ,haya mambo yalikua ni mambo mazito kwa srekali yoyote ambayo ni ya Nchi Maskini,lakini tumevuka salama Pamoja na kwamba kuna athari tumekutana nazo kama Taifa,But Serekali hii imeweza kutuvusha salama na leo tunaona stability ambayo tunayo uchumi unakua hauja shuka kiwango kikubwa but inawezekana hatuja fika tulikotarajia.


  Pia serikali ya CCM imewekeza sana ktk seka ya Elimu,KILIMO na Afya, wapo wanao beza Shule za kata ndg yangu hawa watu wapo DAR na maeneo ya Mijini shule za kata zimekua ni UKOMBOZI kwa watoto wa Maskini Vijijini, sisi tuanotoka Vijijini tunaelewa umuhimu wa shule hizi.

  But nikiri tuna changamoto nyingi shule zina upungufu wa waalimu, maabara, mabweni, lakini watu tujiulize swali kipi kianze tujenge shule ama Tuanze kuaandaa waalimu, Tujenge zahanati ama Tuandae wauguzi, it's a question of a chicken and an egg. Lakini nikiri kwamba zipo changamoto ambazo ilani yetu ya 2010 to 2015 imeeleza nini tutafanya kuhusu haya maswala ya waalimu, wauguzi, kujenga maabara n.k lakini Serikali yetu imefanya kazi kubwa na hasa zinazoelekea kumsaidia mwananchi wa chini kabisa leo tunao vijana wanamaliza kidato cha nne ingawa tunaweza kuhoji quality ya elimu but chochote tunafanya kinakua na mkakati wa kufanyiwa IMPROVEMENT, lakini kibanda leo kijijini mwamko wa Vijana ni mkubwa tofauti na 15 yrs ago na huko hamna TV wala Magazeti,Niseme Watanzania wanaona tulofanya,lakini nakiri kuna changa moto ambazo ilani yetu imezieleza namna tutakavyo zikabili.

  UMOJA:
  Nini ushauri wako kwa Chama chako?


  Bashe:
  Kwanza nishukuru ccm kwa Fursa zote walizonipa na kunifanya who iama today. Yapo mamboa mabayo ningependa kushauri chama changu,lkwanza ningeshauri chama tukalipitia upya AZIMIO LA ARUSHA na kuandaa mjadala wa Kitaifa kuangalia uwezekano wakulirudisha, azimo la Arusha nimekua nikilisoma mara Nyingi 90% bado ni Relevant halina mapunguufu makubwa na ile ni Dira ya Taifa letu bado azimio la Arusha lina umuhimu wake tuliangalie upya ukitazama misingi yake bado tunalihitaji.

  Pili, ningeshauri chama chetu tukajenga PLATFORM ambayo itaturuhusu kufanya siasa above Party Politics tuangalie ni namna Gani tunaweza kuanzisha Mfumo ambao tutawaruhusu wenzetu wa upinzani nao mawazo yao kuyaingiza ktk mikakati yetu ya kuo ndoa Umaskini na Matatizo ya watanzania, kwakua sisi tunayo dola tuna kila kitu wao hawana Basi tuanze kuangalia ninamna Gani tunaweza kuchukua mawazo yao kuyaingiza ktk Sera zetu na kuwashirikisha kwakua na wao ni watanzania wana wajibu kwa letu. Tuhame kule ambapo tunawao si wenzetu,Lakini na wao wakubali kushirikishwa na kutuoa mawazo na si kupinga kila Jambo.


  Tatu, Viongozi kuheshimu Utawala wa Sheria CCM ni chama Tawala tuanwajibu wa kuonyesha mfano ktk kuheshimu utawala wa sheria. Mfano Tukio lililonikuta na Komrei Chiligati,Mzee wangu aliongea kama waziri mwenye mamlaka kuhusu URAIA wangu hapa hakuheshimu utawala wa sheria. Kwahiyo ni vizuri tukajifunza kuheshimu utawala wa sheria ili kuendelea kujenga taifa hili tukianzisha mfumo wa kutoheshimu utawala wa sheria italeta Vurugu siku moja.


  Nne, Ni Vizuri tukaangalia upya Mfumo wetu wa Kura za Maoni,hasa utaratibu wa Uteuzi,badala ya kuanza kura za maaoni,then tunawajadili wagombea ni muhimu tukawajadili kabla hawajapelekwa kwenye kura za maoni ili baada ya kura za maoni ziwe Final na kuheshimiwa, na katika hili la Mfumo wa sasa Ni mfumo Mzuri sana kushirikisha wana chama wote ni mfumo amabao tunatakiwa kuuboresha kwa kua kila mwanachama anapata haki ya kuchagua kiongozi wake, tuuboreshe kwa kuongeza muda wa Kampeni ili kuwapa nafasi wana ccm kupata muda mrefu kuwatambua wagombea na Mwisho kamati za maadili na Usalama za chama zifanye kazi yake na ziwezeshwe kufanya kazi ili tusiruhusu MAJUNGU NA FITNA KUUMIZA WATU.


  UMOJA:
  BASHE KAMA KIJANA VIONGOZI GANI WANAKUVUTIA NA UNAWAONA NI WAKUPIGIA MFANO na wewe unapenda kujifunza kutoka kwao?

  BASHE:
  Wapo walio Hai na ambao wametangulia kwenda ktk Haki na kila kiongozi ananivutia kwa Jambo lake,wa kwanza Mwl Nyerere, Mzee Kawawa, hawa wazee wetu navutiwa sana na Commitment yao na Uadilifu wao kwa Taifa letu nimekua nikipenda siku moja na mm niweze kuhukumiwa kwa sifa hizo mbili, Mwingine Rais Mkapa Uwezo wa Kufanya maamuzi na kusimamia kile anachokiamini ambacho amekifanya kwa Nia Njema Mzee mkapa nina mu admire sana kwa hilo, Mzee Mwinyi, Upole na uadilifu, Rais Kikwete Uvumilivu na ni Democratic. Hivi ni vitu ambavyo ninavutiwa navyo toka kwa Rais Kikwete, Mh Edward Lowasa, Hard working, Bold kwenye maamuzi, mfatiliaji, msimamo, Mvumilivu na Man of his word! Ninamu-admire sana mzee huyu kwa mambo haya na nina amini ni mmoja kati ya Viongozi shupavu tuliona sasa ktk Chama chetu. Dk Emanuel Nchimbi, amekuwa role model wangu ktk viongozi vijana, Msimamo na Mtenda Haki, Mvumilivu.

  Kibanda hawa ni Viongozi ambao wananivutia na ninajifunza kutoka kwao

  UMOJA:
  Nakushukuru sana Hussein kwa kutupa muda wako

  Bashe: Ahsante sana, Mungu Akubariki, Mungu Ibariki Tanzania
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bashe ukuu wa wilaya unakunukia naona...mwenzako yupo Nachingwea kule kimyaaaaa saivi...kwisha kelele zake...subiri zamu yako Bashe usikate tamaa!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Scapegoating at best. Huyu naye ni kama katumwa kumsafisha Makamba & JK
   
 4. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Hakyaani! FISADI ANAWEZA KUWA ROLE MODEL WAKO? Du! hakuna mwenye nafuu CCM.
   
 5. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Bashe ni Back up ya Rostam Azizi kwa 100% jamani

  Hebu mwulizeni Mzumbe Kasomeshwa na nani?
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Pamoja na Historia yake, na uhusiano wake na Mafisadi, but naona kijana ana kipaji cha kujieleza. Sijui kama ana kipaji cha uongozi.

  Nampa big up sana mwandishi aliyekuwa anamuhoji kwa maswali yake yaliyoenda shule na yaliyojiopanga vizuri, sure you are professional.

  All in all, Bashe anaweza kuwa na future nzuri katika siasa, kama tu akifight kusimama mwenyewe, na kuvua kamba za mafisadi miguuni...
   
 7. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maswali mazuri. Big up sana huyu mwandishi...Ni mwandishi anayejua anafanya nini.
   
 8. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza Nimpongeze Bashe amejieleza vizuri na amejibu vizuri maswali haya aloulizwa na pia kibanda nakupongeza sana, kwa muda mrefu nimekua nikijaribu kutaka kujua kulikoni na nini mawazo yake juu yahaya mambo yalimtokea.Pia Nikushukuru INVISSIBLE kutuwekea mahojiano haya ya BASHE na KIBANDA.

  Nikujibu BASHE AMESOMESHWA MZUMBE NA SEREKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,namaanisha kasoma kwa boom kama ulivosoma wewe.
   
 9. minda

  minda JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  bashe alishinda kwa utaratibu aliojiamulia makamba wa 'kila mwenye kadi ya ccm' kushiriki tofauti na ile ya wanachama walioorodheshwa katika orodha ya kila tawi.

  selelii alijiamini kushinda kwa kuwa wanachama waliohakikiwa jimboni nzega walikuwa wanajulikana. bashe alishinda kwa kura 14000 kwa msaada wa mafisadi kupitia kwa wanachama wapya wasioorodheshwa matawini; mpango uliobuniwa na mafisadi na kutekelezwa na makamba kama shambulio la ghafla kwa wapiganaji dhidi ya ufisadi.

  hivyo, kwa kuwasafisha mafisadi na ma associate wao, bashe hana kosa kwani ametekeleza alichotumwa huku akiwatoa kafara waropokaji kama akina kept chiligati.
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bashe anangangania CCM kwa sababu tuu ana mtaji wa mafisadi (RA,EL) ambao wamekuwaa wakimjenga ili wamtumie 2015 na kuendeleaaaa katika kukamataa nchii waitafunee VEMA..
   
 11. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  TUKO mm nimesoma na Bashe Mzumbe namfahamu amekua kiongozi wangu kwa kipindi cha masomo yangu hapo mzumbe Uni.

  Bashe alipoamua kuingia katika siasa sikushangaa kwakua jamaa ni kiongozi na ni mtu ambae husimamia anachotumwa na watu wake na kile anachoamini bila kuangalia kitamgharimu kiasi gani.

  Sitasahau tukio alofanya mwaka 2001 alopoamua kusimamia na kuuambia uongozi wa chuo ikiwa kama wanafunzi wanaojilipia hawataruhusiwa kufanya mitihani yao ya mwisho hasa Finalist basi atagomesha wanachuo wote wasiingie ktk mitihani na warudi nyumbani, kwani hoja yake ilikuwa kama mtu anadaiwa ada ni chuo hicho ni Public basi Public interest comes first ni heri mtu afanye mtihani na cheti kizuiliwe mpaka atakapo maliza deni la ada kuliko kumfanya mtu wa mwaka wa tatu arudie kufanya mitihani wakati wa supu.

  Mimi nilikua mmoja wa waliokuwa wanadaiwa kwa hoja za huyu bwana mdogo akiwa mwaka wa kwanza niliweza kufanya mtihani na leo natumikia taifa langu.

  Juu ya swala uwezo wa uongozi sina shaka,najiuliza anafanya nini ccm mpaka leo nimewahi kumuuliza swali hili jibu lake ni kwamba (sometimes we use hard ways to reach our goals) nimekua simuelewi na ninaamini BASHE HUKO ULIKO SIKOOOOOOOO ONDOKA
   
 12. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jimbo la Nzega lina matawi 152 Bashe aliongoza matawi 150, Lucas Seleli aliongoza tawi mmoja (1) la Itilo, Hamisi Kigwangala Aliongoza tawi mmoja (1) la Nata, Wapigakura waliokuwa wamejiandikisha kwenye daftari la wanachama ni 25,480 hawa ni wanachama halali wenye shaada za kupiga kura na kadi za CCM.

  Waliokuwa wamepiga kura ni wanachama wasiozidi 20,000 hawa ni wanachama halali wenye shaada za kupigia kura kwahiyo hoja ya Minda kwamba Bashe alishinda kwa utaratibu ulioamuliwa na makamba ,sio za kweli na minda ana lengo la kupotosha umma,na kitu kinachowachanganya CCM hadi leo ni kwamba wanachama 14,521 waliompigia kura Bashe ni wanachama halali wa CCM na wamejiandikisha katika daftari la wapigakura

  Ndugu yangu Minda Usipotoshe ukweli
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jinsi Bashe alivyoweza kujipambanua kujibu haya maswali kisiasa sasa naona sababu zilizowafanya wakina Ridhiwani wamuone tishio na kikwazo kwa udhalimu wao. All in all hiki ni kifisadi kinachokua!!
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli hizi kamwe wakaazi wa Tabora hawatakaa kurudia kosa la kumchagua mtu ambaye yaelekea yupo mbele kujipendekeza kwa wakubwa badala ya kudai haki yake. Kama hawezi kudai haki yake ya kimsingi ya uraia na ni ya kikatiba na kukishitaki CCM mahakamani wapigakura wataweza wapi kumtegemea awe mtetezi wao?

  Kwa kauli hizi za kinyonge jamaa huyu huu ndiyo mwisho wake kisiasa:-

  Isitoshe mwaka 2015 atakuta CCM ndicho chama kikuu cha upinzani na hata hela hakina maana Dr. Slaa atakuwa amekwisha kurejesha mali zote walizopora serikalini zikiwemo majengo, fedha taslimu zilizopo kwenye mabenki, viwanja vya mpira, n.k
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni imani tu,swala la yeye kurudi nzega ni unpredictable!
   
 16. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana kipaji cha kupanga hoja tatizo analinda maslahi binafsi ndani ya CCM. Namtakia heri
   
 17. M

  Mpwa Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Swala lililo mpiga chini Bashe ni uraia,na ukweli wa hilo ana lijua yeye na mafisadi wenzake walio mbeba kumpa uraia kwa sababu hakuomba.

  Ndio maana kama mkoa walijua kuwa bashe ana matatizo ya uraia sasa yeye kwa kujuana na vigogo wa ccm hasa masha wakamuhalalisha ndio maana wakapata kigugumizi kuelezea uraia wake maana walijua walivyo mpatia

  Kwa nini Idara husika irishindwa kutoa tamko?(Uhamiaji), Na waziri mwenye dhamana akashindwa pia likatolea kisiasa tu

  Kwa hiyo bado uraia wake unautata. Mahakama haimpi mtu uraia kama kiapo chake kinavyo someka kupitia chapisho za magazeti yaliyopita.

  Halafu hakuna mnyamwezi msomali,ila kuna raia wa tanzania wenye asili ya somalia sio msomalimnyamwezi haieleweki.

  Watufafanulie uraia wake na si kumpapatikia yakuwa yumakini wakati hanatofauti na Kinana.
   
 18. minda

  minda JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  mkuu, wewe ndiye unayejaribu kupotosha umma kwa sababu hutofautishi kati ya orodha ya wana ccm matawini na daftari la wapiga kura ambalo ni mali ya tume ya taifa ya uchaguzi. katika sakata la bashe, haijawahi kutamkwa na tume kuhusu hao waliompigia kura na tume yenyewe zaidi ya kapt chiligati kumtangaza bashe kama sio raia, angenyang'anywa kadi ya ccm na ya nec, akimfananisha bila aibu na jenerali ulimwengu.
   
 19. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  MPWA KARIBU JAMVINI
  Nimesoma post yako inasikitisha umeongelea kitu usichofahamu,kwa Mtanzania aina ya Bashe kwa maana mzaliwa ambae asili yake ni nje haombi URAIA kwa mtindo wa UHAMIAJI bashe alitakiwa kuukana URAIA wa BABA yake na yeye alifanya hivo na unapoukana URAIA unaenda mahakamani kupata KIAPO na mahakama ikikupa kiapo unaenda uhamiaji kupewa CERTIFICATE OF TANZANIAN tofauti na mtu aliehamia ambae anapewa CERTIFICATE OF NUTRALISATION bashe tuliona ktk vyombo vya habari alipewa cheti cha uraia wa tanzania kama mzaliwa na si muhamiaji hiyo ndio tofauti.

  From legal point of view HATI ya kiapo ya BASHE inaonyesha KABILA MNYAMWEZI ,kisheria hata wewe unaweza kwenda mahakamani kuapa kuacha kabila lako na kutambulika kabila jingine,BASHE asingeweza kusema ktk kiapo chake kwamba kabila lake ni Msomali,hakuna kabila linaitwa SOMALI hiyo ni nationality kwahiyo ikiwa kiapo cha bashe kinasema kabila mnyamwezi kisheria si kosa,lakini angesema kabila msomali huo ni utaifa hilo ni kosa,na kwakua Bashe alienda shule alitambua hilo akaamua kuapa atambulike Mtanzania wa kabila la Kinyamwezi na kwa kiapo kile Bashe si Msomali hapa Watu vilaza wengi walichanganyikiwa kama ww ndungu yangu.
   
 20. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndg yangu inaonyesha hujaelewa hoja ya AGWAMBO,alichosema wanachama waliompigia Bashe ni wale waliojiandikisha ktk Daftari la ccm ktk matawi na vile vile ni mpiga kura ambae ameandikishwa ktk Daftari la wapiga kura la Tume,kwani ktk utaratibu wa ccm wa safari hii wote waliopiga kura walitakiwa wawe na kadi ya ccm na shahada ya kupigia kura ktk uchaguzi mkuu.
  kwahiyo hoja yake ilikua kupinga hoja iliyopita kwamba bashe alipigiwa kura na watu ambao hawakua wameandikishwa ktk daftari la wanachama la ccm,huyu bwana kama takwimu zake ni sahihi basi hiyo ni sababu tosha ya ccm kupoteza jimbo hilo ikiwa kama hao wote 14,000 walikua ktk daftari la ccm ktk matawi means wote ni elligible voters wa general election kwakua mara hii wapiga kura wote wa ccm walitakiwa wawe na kadi yaccm na shahada ya kupigia kura ktk uchaguzi mkuu ili kuona anechaguliwa ni potential voters.
   
Loading...