Tujikumbushe Tamthilia ya Bashe na Kigwangala!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
BASHE:Sikuwahi kuwa member wa hii forum lakini nimeguswa na kuvutiwa kutokana na mjadala ambao umemhusisha Mbunge wangu MH HAMIS ANDREA KIGWANGALA (SAIDI NASSOR BAGAILE) sikutaka kujadili jambo lolote lakini kilichonileta hapa kuchangia ni mambo makubwa mawili ambayo nitayataja hapa chini, leo nimefahamu kwanini Mh Kigwangala tulipokutana mara ya mwisho pale MOVENPICK Ijumaa katika kujadili baadhi ya mambo na umuhimu wa social network nikamwambia nataka nijiunge na wana bidii, alinishauri NISIJIUNGE WANABIDII KWAKUWA NI SEHEMU ISYOFAA WATU WANAPINGA KILA KITU, nimefahamu sababu kumbe hakutaka nifahamu kuwa mbunge wagu yupo huku akipotosha taarifa nyingi sana. Sikupenda kujibu hoja zake imenibidi,hizi chini ni sababu kuu zilizonisukuma kujibu.(1) Mbunge wangu amenitaja kwa jina katika baadhi ya mambo.(2) Kuweka rikodi sawa sawa juu ya baadhi maswala ya Msingi.Hizo ni sababu kubwa zilizonifanya niingie na kujibu baadhi ya mambo,nimesoma hoja za Mbunge ameongelea maeneo makuu yafuatayo, (1) UHALALI WA JINA LAKE (2) URAIA WA BASHE (MIMI BINAFSI) (3) AMESEMA HAKUBEBWA ( 4) AMONGELEA USHINDI WANGU (5) AMEONGELEA SWALA LA WAMA ( 6) AMEONGELEA KUWA ALIRUDISHA UNITY KTK CHAMA (7) ASILI YAKE. Haya ni maeneo makuu niliyoweza kuyaona katika majibu yake alotoa hapa.Nianze kwa kusema HAKUNA JAMBO BORA DUNIANI KAMA KUFAHAMU MAPUNGUFU YAKO, KUYAKUBALI NA KUKUBALI KUYAFANYIA KAZI, PIA HAKUNA JAMBO BORA KAMA KUMSHUKURU MUNGU KWA JAMBO LOLOTE UNALOKUTANA NALO kama nilivoshukuru mimi tar 2 august 2010 baada ya kuapata ushindi wa kura za maoni, na kushukuru pia baada ya kutoteuliwa na chama vyote nilimshukuru mungu.

Nimesema haya maneno kutokana na mbunge wangu kutokuwa mtu wakushsukuru mungu kwa bahati alopata ambayo imetokana na tabia na mila za watu kumalizana kutokana na kuwa na misimamo,mitazamo,fikra,na maoni tofauti tofauti juu ya baadhi ya mambo.SAIDI be a Gentleman kubali ubunge wa jimbo la Nzega haukuwa wako hukuwa na political Vission, Mission, wala strategy ya kupata ubunge ule,bcs of CCM politics Mimi na Lucas selelii hatukuteuliwa and you KNOW it.


NIANZE NA UHALALI WA JINA:


Usipotoshe watu jina la Hamis Andrea si jina lako kijana mwenye jina hili yupo Nzega unafahamu na baada ya Wewe KUTEULIWA Chama na Wana CCM kilikushauri uende mahakamani kuapa kupata kiapo cha mahakama kubadili jina na kulichukua rasmi jina la Hamis Andrea na ulifanya hivo, jina la hamis andrea umelichukua Rasmi baada ya KUTEULIWA na kabla ya kuchukwa Form na kuhisi utawekewa Pingamizi, lakini deep in your heart uanafahamu wewe na mimi tumesoma same primary school na mimi na wewe hatukufaulu DARASA LA SABA KITONGO PRIMARY SCHOOL. Baada ya hapo kutumia nafasi ya mama yako ambae wakati huo alikua ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega ulienda mwanzoli ukachukua jina la HAMIS ANDREA na kuanza kulitumia kijana huyu alifaulu yeye na watoto wa MZEE MTANGA WAKIKE AMBAO NI TWINS kwakuwa hakuwa na taarifa mapema na kwa kuwa kijana huyu baada ya kumaliza pale mwanzoli alienda kuishi KITANGILI baada ya mitihani taarifa za ufaulu wake zilichelewa kumfikia kijana huyu, ulichukua nafasi yake na wewe kwenda KIGOMA SEKONDARI.


Ni kweli kama ulivosema kwamba wewe nimjukuu wa mzee KIGWANGALLAH,huu ni ukoo wa mama yako na si BABA yako,na tulipokuwa tunasoma Primary ulikuwa unaitwa Jina la SAIDI NASSORO BAGAILE, nayo haya majina ( nassoro bagaile) ni ya ukoo wa mama yako tumekuwa wote hatumjui BABA YAKO na hakuna mtu wa Nzega ambae anamfahamu baba yako na siku zote imekuwa HIVYO until utakapo prove otherwise ( tunaweza kuchanga fedha hapa wanabidii watafute team ya watu wakafanye uchunguzi walete ripoti hapa tujue nani mkweli). Wanabidii mkiangalia HOJA ya kuhalalisha na U TANZANIA WA KIGWANGALA SIKU ZOTE ATAELEZA KWA KIREFU HISTORIA YA UPANDE WA MAMA YAKE UPANDE WA BABA UTABAKI UNCLEAR HATA MAELEZO YAKE HAPA YANAONYESHA HIVO,ingawa haikuwa strategy yangu kum disqualify SAIDI baada ya kuteuliwa katika uchaguzi kwa HOJA YA UIRAI bcs mimi si MUUMINI WA UKABURU HUO.


URAIA WA BASHE:


Nimesema mara Nyingi na leo nasema Tena URAIA WANGU HAUNA MASHAKA hata kidogo, labda nitoe maelezo mafupi hapa, Kutokana na sheria yetu ya UHAMIAJI KUNA AINA MBILI WATU kuna watanzania ambao wanaomba uraia kwakuwa hawajazaliwa TANZANIA inabidi baada ya muda wakaiishi kwa kutumia HATI MAALUM (PARMIT) Ambayo inakuwa re newable wataomba na watatangazwa katika magazeti na hawa wanatakiwa waishi si chini ya miaka 10.


Kundi la pili ni Mtanzania ambae anazaliwa Tanzania na ambae mzazi wake hasa wa kiume wakati mtoto huyo anazaliwa HAKUWA RAIA wa Tanzania,now Commenting on my setuation, BABU MZAA BABA alihamia Tanzania 1949, akiwa na baba yangu waliishi mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini,BABU MZAA MAMA aliahamia Tanzania 1902 akiwa na BABA yake aliishi maeneo ya SUMBAWANGA NA BAADAE ENEO LINALOITWA LAHELA NA ALIKUWA AKIJULIKANA KAMA MZEE ABDI ALI WAJINGA, BIBI MZAA MAMA ALIZALIWA BOMA NG"OMBE MOSHI Mwaka 1920, mama yangu mzazi alizaliwa Tabora mjini mtaa wa Mwanza Road.


Ukitazama that background utaona mzazi ambae alihamia Tanzania ni BABA yangu, kwa wanaofahamu historia ya Nchii hii watakumbuka 1957 wakati waingereza wanaandaa mazingira ya kukabidhi uhuru wa TANGANYIKA waliita all MINIORITY SOCIETY ambao walikuwa chini ya British Ambrella, na kuwaambia wana uhuru wakuchagua kubaki na URAIA wanchi walizotoka.


Na wakati huo babu zangu wote walikua na BRITISH PASPORT KWA SABABU WALIKUA WAMETOKA ENEO LA KASKAZINI LA SOMALIA LILIKUA CHINI YA BRITSH COLONY LILIKUA LINAITWA SOMALILAND, ama wachukue UHURU WA TANGANYIKA.

Babu zangu waliamua kuacha URAIA wanchi walizotoka na kuchukua uraia wa TANGANYIKA.

Waliasiliwa na kuandikishwa kama RAIA wa Tanganyika na kukabidhi HATI za uingereza na wao kutambulika kama WATANGANYIKA hiyo ilikua 1957.Hi unaweza kwenda RITA katika Registry za 1957 utakuta ukoo wa babu mzaa mama na babu mzaa baba .kwa mantiki hii wazazi wangu wote ni RAIA wa Tanganyika toka 1957 mpaka 1964 wakawa Raia wa Tanzania. Kwahiyo hoja ya urai wangu haina la kujadili


Ukiangalia 1959 TANU branch office ya Nzega ambayo kwa sasa ni ofisi ya CCM kata, alieitoa na kumkabidhi ofisi ile MAMA AMINA MAUFI wakati huo akiwa ni Mwenyekiti wa Tanu Branch na katibu wake ni Mwl shija ambae sasa ni mkiti wa CCM wilaya ya Nzega alikuwa Marehemu Babu yangu.


Chumba kile lilikuwa DUKA lake nay eye aliwapa ili ofisi ya Tanu ifunguliwe pale,hii ni memory iliyonifanya 2008 nilikarabati Jengo lile liweze kutumika mpaka leo.


NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO:


Wazazi wangu walioana baadae na kuzaa watoto sita mm nikiwa mmoja wao,kilichotokea ni kwamba 1986 /7 mzee anaeitwa MZEE RASHID NYEMBO( marehemu) ambae alikuwa Rafiki mkubwa wa Mzee wangu walikuwa na Safari ya Maswala ya kidini mzee wangu hakuwa na Hati ya Kusafiria wakati huo na u can imagine wakati huo hakuona umuhimu wa swala hilo.

Alitakiwa kupata hati alifata utaratibu lakini AFISA uhamiaji wilaya ya Nzega alikuwa anaitwa MR MALONGO na wakati huo kulikuwa na opartion za kukamata wahamiaji na kila wakija watu kutoka makao makuu ama mkoani walikuwa wanamsumbua na kumtaka atoe maelezo ya WHO IS HE.

Alishauriwa ni vizuri aombe UARAI KWA UTARATIBU WA MTU ALIEHAMIA TANZANIA, mzee wangu alifata utaratibu na kupewa HATI YA URAIA CERTIFICATE OF NATURALISATION 1987 na alipata hati na mambo mengine.

Tukumbuke Sheria yetu inatambua MZAZI WA KIUME,kwakuwa niliamua kuingia katika SIASA na ninafahamu hata leo ukipata msichana unaempenda PROTECTION ni MUHIMU basi 2008. Niliamua kwenda mahakamani kukana UARAI WA BABA (si kwasababu sina sifa bali kujilinda kama mtu anapoamua kutumia kondom ni katika kujilinda na un forseen events) lakini bcs kutokana na DOCUMENTATION mzazi wangu wa kiume alipewa HATI ya URAIA 1987. Na mimi kwa kuwa najua in politics anything can HAPPEN hasa pale linapotakiwa jambo flani kufanyika basi wakati nagombea UENYEKITI WA UVCCM TAIFA NILIAMUA KUWA NA HATI YA KIAPO INCASE OF ANYTHING na hilo likaja kujitokeza likakosa nguvu nikatoa kiapo hoja ikafa, pamoja na kuwaeleza URAIA wangu haukuwa na shaka yoyote lakini pia nilisema nimeisha timiza sharti la kwenda mahakamani nikaitumia.

Na 2009 niliamua kutaka IDARA YA UHAMIAJI INIPATIE CERTIFICATE OF CITIZENSHIP ambayo utaratibu wake nitofauti na ule wa mtu anepewa CERTIFICATE OF NATURALIZATION, 2009 nilipatiwa hati hiyo ambayo mpaka leo ninayo . Kwahiyo MH MASHA hakupotosha ,mkurugenzi wa UHAMIAJI HAKUPOTOSHA, wala mkurugenzi mkuu wa RITA hakupotosha pale alipotoa ushuhuda wa kimaandishi juu ya uhalali wa wazazi wangu kuwa katika registry ya mkoloni ya 1957 na wote hawa walikiandikia chama BARUA kuthibitisha tena baada ya mimi kutoteuliwa na mimi kuwaandikia Barua ni kitaka kauli yao juu ya upotoshaji uliofanyika,nakala ya Barua hizo ninazo mpaka leo, NIMSHAURI mbunge wangu usiongelee usilolifahamu usiwe mmoja wa wale wanaofumbia macho ukweli kujipa maliwazo ya MOYO. USHINDI WANGU 2010 Mh Saidi/kigwangala amekuwa mara nyingi akitaka kupotosha ukweli juu ya ushindi wangu labda watu wengi wajue historia ya mimi na wewe katika siasa za JIMBO LA NZEGA,2005 wote tukiwa tumetoka mashuleni na ajira zetu za mwanzo tuligombea ubunge jimbo la nzega wewe ukitumia Gari aina ya Mark 11 na mimi Suzuki vitara ukiwa na mkeo mimi single ukipita kuwaambia wananzega wakuchague kwakuwa wewe ni msomi, kijana na una mke. Huku mimi nikipita na kuwaambia wanichague kwa kuwa mimi ni kijana wao wamenisomesha na sasa nina taka kusimamia yale ambayo waliotangulia walishindwa kuyafanya.

Wana CCM wajimbo la Nzega walinipa kura 109 na wewe kura 24 chini ya 25% ndicho ulichopata ukifananisha ushindi wangu na wako, wakati huo kaka yetu LUCAS SELELII akipata ushindi wakura zaidi ya 300. Baada ya hapo wewe ulikimbia jimbo hukushiriki jambo lolote wakati mimi nikiendelea kutekeleza yake niliyoahidi kwa wapiga kura kama ninavyofanya sasa, 2007 ulifanyika uchaguzi wa chama nikapa kura 1947 kati ya kura 1982 zilizopigwa na mimi kuchaguliwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM TAIFA.

Then katika mktano mkuu wa mkao wa Tabora nilipata kura 487 kati ya kura 550 zilizopigwa na kuchaguliwa Mjumbe wa Halmshauri kuu ya CCM mkoa wa Tabora, chaguzi hiz wewe hukishiriki nilishinda huku nikipingwa na watu wote wenye Nguvu katika MKOA namaanisha WOTE. Na hapa nilizuia wizi wkura na GAZETI LA MWANANCHI LILIANDIKA STORY CCM WAONYESHA NAMNA YA KUIBA KURA.

2010 KATIKA UCHAGUZI

Katika uchaguzi huu nilishinda kihalali katika vitua 152 wewe uliongoza vituo 3,ambavyo nata CENTRE ulinizidi kura 7,isanzu centre,na shila,wakati kaka yetu SELELII alishinda vituo Viwili ambavyo ni SILIMUKA akinizidi kura 52,na ITILO akinizidi kura 17 kama sikosei.

LAKINI VITUO HIVO SI KATA KIKATA MIMI NILISHINDA KATA ZOTE 21, na wewe unalifahamu hili tulikua na Vituo 152 katika kata 21,vituo vyote tuliweka mawakala wote sisi wagombea wakuu 3 katika uchaguzi huo na matokea yakawa Bashe 14,420,SELELII 2500 KIGWANGALA(SAIDI)1530 kama sijakosea ukitazama kura hizo ni sawa ni 11 to 12% ya kra nilizopata.

Wana Bidii hata leo tukirudia Uchaguzi JIMBO LA NZEGA NITASHINDA KWA KURA NYINGI SANA na ikiwezekana tuakaandikishane tukafanye kampeni nauhakika nitamshinda lakini UBUNGE aendelee nao hili sina shaka juu yake.


Utakumbuka wakati wa kura za maoni niliwaahidi kuwashinda kwakuwa nilikuwa nafahamu kuna njama hizi nilikuambia wewe na wengine ,ninafahamu mpango wa kunikata jina lakini nitahakikisha ninawashinda kwa kura nyingi sana ili hatamtakaponikata watanzania na wananzega watapiga kelele kwa niaba yangu na historia itakuwa imeandikwa na hili lilitokea.


Wapo wanahabari waliokuwa wananieleza juu ya mipango hii mliokuwa mnaifanya na ilifahamika mapema ,but I said to my self sijajiunga CCM kwa ajili ya UBUNGE tu nitagombea nitashindwa nitakatwa lakini nitabaki ndani ya CCM kutimiza wajibu wangu,na unafahamu hili kwa 2015 u will face me again if god wish,politically u have never been threat to me jimbo la nzega ninafahamu mtu pekee ambae ninaamini ni threat kwangu ni LUCAS LUMAMBO SELELII not you.


HOJA YA WAMA


Sipendi kuliongelea sana hili lakini ni AJABU unapokana kuwa HUKUWAHI KUFANYA KAZI NA WAMA ni kama mimi nije katika PUBLIC nisema siajawahi kuajiriwa na ROSTAM AZIZ ni kukana ukweli ulio wazi binafsi sina uhakika kama uteuzi wako una mahusiano na kazi zako WAMA.

Bali nina uhakika umefanya kazi za WAMA kama MUWEZESHAJI na MTOA mafunzo yapo maeneo ambayo uliwahikutoa TRAINING ambayo mimi nafahamu,mfano KANDA YA ZIWA umewahi kufanya maeneo kama shinynga ,BARAZA KUU LA UVCCM ambalo mimi nilikuwepo DODOMA 2008 feb uliletwa na WAMA why useme UONGO jambo baya sana najisikia AIBU MBUNGE WANGU ANAPO DANGANYA.inawezekana mpaka leo tunasubiri maandamano ya kufunga mgodi hakuna umetudanganya naanza kupata mashaka na wewe.

USHINDI WA JIMBO LA NZEGA


Be honest huweza kufanya mkutano wa HADHARA hata mmoja mpaka ALIPOKUJA MH RAIS na sote tuliahidi kukusaidia,mimi ni mmoja wa watu ambao waligombana na MARAFIKI zangu kuja kukuombea KURA ni utamaduni mwema mtu kushukuru unafahumu deep inside in ur heart hukuwa na team ya kampeni aliekuwa kampeni meneja wako MR RWANGISA ndie aliekuwa kampeni MENEJA WA KAKA YETU SELELII,leo unasema HUKUBEBWA ULIBEBWA NA CCM na wana nzega walichagua chama kilichotuokoa NZEGA kama chama ni UPINZANI kugawanyika CUF na CHADEMA ur un popular katika JIMBO NA HILI UNALIFAHAMU.


UNITY KATIKA CHAMA


SAIDI/KIGWANGALA wana ccm waliungana kukisaidia chama chetu nah ii haikuwa jitihada yako binafsi wala jitihada ya mtu mwingine wewe si ulieleta umoja katika chama bali itikadi z wana ccm ndizo zilizo waunganisha watu wa nzega na ukiangalia katika historia yetu ya jimbo this time ni mwaka ambao watu walijitokeza kidogo kuliko waliojiandikisha,hukupata hata kura za wanachama wa ccm walipiga kura wote,utakumbuka binafsi nilipita maeneo yote ambayo wewe ulishindwa kuyafikia ulienda maeneo hayo baada ya mimi kuwa nimepita na kueleza why wachague CCM na sikuwahi kutumia JINA lako kuombea kura chama BCS nilijua the only instrument ya kuwafanya wana Nzega wakuchague ni kutumia CCM


HITIMISHO


Wana bidii mara nyingi MH mbunge wangu amekuwa akitaka tuamini kwamba yeye A kumbe ni B its good kusimama kwa RANGI yako sikupanga kuyaongea haya lakini imenilazimu kufanya hivo baada ya kuwa mara zote nikiangalia mkuu wangu akipotosha ukweli juu ya mambo mengi. Jambo la msingi kubali hukushinda nzega ,hukuwa chaguo la wana nzega,umefaidika na migogoro ya kisiasa ndani ya mkoa na Taifa hili,leo usilazimishe watu wakaanza kufanya kazi kuangalia CREDIBILLITY ya hata ELIMU YAKO NI QUESTIONABLE, ukiangalia unaongela umesoma MASTERS ya Bsness Administration, KAROLINSKA institute a lot of questions with no answer.

Tutaangalia credibility ya Degree yako ya Muhimbili,tutaangalia uhalali wa wewe kuchukua kiapo cha kubadili jina siku tatu kabla ya kujaza fomu,usilazimishe tujadili ambayo si sawa kuyajadili wewe ni kiongozi sasa acha siasa za uongo,upotoshaji,simamia unachokiamini na si wanachokiamini wengine.

Tutahoji moral authority juu ya mambo mengi unayoongea wakati wewe ni mmoja wa walio benefit na STIMULUS package 2009/10 ambazo hazikuwafaidisha wakulima zaidi ya kujinufaisha wewe binafsi kununua ma Range mjini na kuja kugombea ubunge Nzega kwa Fedha za walipa Kodi kupitia kampuni ya MSK ambayo wananchi wa Nzega hiuta jina la Ambalo unalifahamu,,tutakuhoji uadilifu wako wakati wewe ni mtu alilazimisha wananchi wa nzega waache kulima mazao ya chakula walime PAMBA kujinufaisha wewe binafsi na biashara yako na kushindwa kuwapa pembejeo matokea yake PAMBA wakose na chakula wakose.

Na sasa wanakabiliwa na njaa ukitumia nafasi yako ya ubunge kuhamasisha kilimo cha pamba na matokeo yake kuwatia watu umasikini na sasa wana nzega wanakabiliwa na njaa, Umefika wakati wa wewe kusimamia ahadi ulizotupa jimboni Tunasubiri maandamano siku 21 zimeisha,na hapa nilikushangaa lakini nikakubali kujifunza kitu kipya Mgodi ule upo pale kisheria,ni ilani ya chama uliyoinadi,leo unaandaa maandamano kuondoa? Nikasema labda new approach ktk siasa zetu,Umetuahuahidi mikopo kina mama nzega umechukua viingilio vyetu hujatoa mkopo mpaka leo ni either urudishe 6000 ulizochukua ama uwape mikopo,sio kupita na kuchinja Ng"ombe na pilau vijijini ndio maendeleo tuliotaka wana nzega.

Sikutaka kujakutoa maelezo marefu hapa,kama nilivokushauri juzi wakati tunachangia mfuko wa maendeleo wa mkoa wa TABORA Yule kijana unajua unatumia jina lake unajisikiaje anabeba mizigo sokoni na GANAGANA,msaidie mtafutie mtaji akafanye biashara hata nje ya Nzega kwa Mungu utaoneka umeshukuru,bila ya Jina lake leo may be usingekuwa hapo ulipo una RESPONSIBILITY YA KIBINAADAMU

KUMSAIDIA YULE BWANA HAMIS.

Mwisho kuwa mkweli ukweli utakuweka HURU
 
kumbe wakina mulugo wako wengi move zinaendelea tena za series mpaka raha.Ngoja nisubiri nae aje kujibu alafu tupime hoja kwa hoja.kuna mengine nilikuwa nasikia nafikili uongo sasa naaza kuona kumbe lisemwalo lipo na kama halipo linakuja.
 
Well.... mr @HKigwangala

umepewa taarifa.., Je unaikubali taarifa hii na huu ushauri ?
 
Politics is a game of chance.Hongera Bashe kwa kutumia chance tusubiri chance ya Kigwangala tena.
 
Politics is a game of chance.Hongera Bashe kwa kutumia chance tusubiri chance ya Kigwangala tena.Mkuu vipi lile la kutekwa mbona haujagusia kidogo?
 
kigwangala na bashe kila mmoja akiongea utampa credit,ila credibility ya wanachoongea ndio issue,ila nimefurahi kujua kwamba ni watu wanaofahamiana sana toka maisha ya shule mpaka kijijini walikokulia
 
Hii kali kwani nimeamini UTUKUFU ni kitu kibaya sana kwani unaweza kuwa na mali lakini watu wasipokusujudia uanjiona bado hujakamilika.
UBUNGE wao Bashe na Kigwangala ndio wamefika kwali Siasa ni SIo hASA
 
Hapo hakuna msafi, yote majizi tu, hili li Bashe limeajiriwa na jizi la Igunga, hili jingine limekwapua majina kama Mulugo. Wanajamvi na watz wote ambao hawajui haya (ila watajua tu) Tujiulize je hii kwapua kwapua ya majina ina maana gani ndan ya CCM na je ndo sera yao? Maana hata katika wizi wa kura hawa jamaa wapo 1st class. Hebutazama
1. NAHUM - Nape
2. MADELU - Mwigulu
3. HAMIM - Mulugo
4. SAIDI - Hamis Kigwangwala
Na wengine kibao, halaf wote hawa wanatulazmisha tukubali walifika University na kutwambia wao ni 1st class. Kumbeee MBULULA HUTENGENEZA MAMBULULA eeh! usishangae mwaka huu ZIRO ZOTE
 
Taarifa hii ipo kwenye uzi mmoja humu in pdf format je ni inauhusiano gani na zengwe lenu

1 | P a g e
Maganga Masanja, NZEGA. TABORA +255786731566 (DSO) 18th Sept. 2012 Katibu Mkuu, Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu DODOMA. Mheshimiwa, Yah: Taarifa Kuhusu Ndugu Husein Mohamed Bashe Tafadhali husika na kichwa cha barua hii hapo juu. Mimi ni mkazi wa Nzega na ni mwanachama hai wa CCM hapa Nzega. Nimeshuhudia na kusikia mengi yakisemwa kuhusu wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hapa Nzega nikaona ni vyema kama mwanachama na kama raia mwema nikatoa taarifa nilizonazo ili mzifanyie kazi wakati mkiwajadili wagombea wa nafasi mbalimbali na pia mkajiridhisha kuhusu taarifa hizi ili mfanye maamuzi yanayofaa kwenye vikao vyenu. Mimi nimefuatilia swala hili kwa kusoma maelezo aliyoyachapisha Huseni Bashe kwenye mitandao na pia kuongea na baadhi ya wazee wa hapa mjini Nzega(walioipokea familia ya shehe Mohamed Ibrahim na mkewe) na kubaini ukweli ufuatao, pia nimesoma sheria ya uraia(The Tanzania citizenship act, principal legislation, Chapter 357 revised edition, 2002) Ndugu Husein Mohamed Bashe ama Husein Mohamed Ibrahim Bashir (tunashangaa kwa nini jina lake limekuwa likibadilika badilika – wengine wakidhani ni katika kutafuta uhalali wa kujiita Mnyamwezi kama nyaraka zake za kughushi Uraia zinavyoonyesha), ambaye anajulikana hapa Nzega kama mtoto wa Shehe Mohamed Ibrahim, alizaliwa Nzega Mnamo Tarehe 26/08/1975 (kumbukumbu rasmi za kuzaliwa kwake zinapatikana Ofisi ya Vizazi na Vifo, Nzega - kwenye cheti chake cha halali cha kuzaliwa; Shule ya Msingi Kitongo, Nzega, aliposajiliwa darasa la kwanza Mwaka 1984; na Chuo Kikuu Mzumbe alipodahiliwa kuanza masomo ya shahada ) na wazazi wake wote wawili wakiwa wasomali pure kutokea Somalia, na wote hawa hawakuwa Raia wakati Huseni akizaliwa. Baba yake Husein amepata Uraia 1987 kwa taratibu za kuomba kisheria. Mama yake Huseni anayejulikana kwa jina la Zainab Abdi hajawahi kuwa raia wa Tanzania na hajawahi kuomba na kupewa Uraia (hivyo anaishi nchini kinyume cha sheria). Kwa kuwa wazazi wote wawili wa Huseni hawakuwa raia wakati wanamzaa yeye na wadogo zake wote watano kwa mujibu wa sheria wote hawa si raia na wako ndani ya Tanzania kinyume cha sheria.
Kama raia mwema nimepata taarifa kwamba kuna mtandao wa wasomali ambao wameingia nchini siku hizi na wametengeneza genge la kutafuta uhalali wa kuishi nchini hapa na kutawala nyanja mbalimbali za uchumi na jamii na hivyo nikahofia kwamba isije kuwa ndugu Huseni naye ni mmoja wapo ukizingatia
2 | P a g e
amekuwa akifanya jitihada za kina na kwa kutumia nguvu kubwa sana ya pesa (ambazo hatujui anazipataje ukilinganisha na hali ya maisha ya familia yake na wazazi wake hapa Nzega) kutafuta ubunge na uongozi ndani ya chama tawala. Wengine hapa Nzega wamekuwa wakisema kwamba anatafuta ubunge kwa nguvu namna hii ili ahalalishe uraia wake wa uongo alionao na atafute namna ya kuingiza ndugu zake nchini Tanzania kwa kutumia nguvu ya kisiasa. Watu wengi wamepata mashaka hapa Nzega na kuna minong’ono kwamba anafadhiliwa na huo mtandao wa kiharamia wa kisomali wenye nia ya kutafuta namna ya kupenyeza watu wao kwenye system. Hili hasa ndiyo limenitisha na kunifanya niamue kutoa taarifa hii ili vyombo vya dola vilifanyie kazi na ukweli uthibitike. Mwaka 2005 aligombea Ubunge na alipewa alama ya D kwa sababu ya ‘utata’ wa Uraia wake. Mwaka 2008 aligombea uenyekiti wa UVCCM Taifa na vikao vilimjadili na kuonyesha utata kwenye uraia wake, na hapo alikimbia kutengeneza kiapo cha kugushi cha haraka haraka cha kuthibitisha uraia wake. Watu wengi, na mimi nikiwemo tulibaki na mashaka yetu kwamba ni katika mazingira gani mtanzania wa kuzaliwa atalazimika kula kiapo kuthibitisha uraia wake? Hivi ni wangapi kati yetu wamewahi kufanya hivyo? Kwangu hili limekuwa likinipa mashaka makubwa na kunifanya niamue kufanya ufuatiliaji wa kina. Mwaka 2010 aligombea ubunge na alikatwa jina na vikao vya juu vya CCM kwa sababu ile ile ya ‘utata’ kwenye uraia wake. Mwaka 2010 Waziri wa Mambo ya ndani Laurence Masha alithibitisha kwenye vyombo vya habari kuwa ndugu Huseni Bashe ni raia japokuwa hapa Nzega ambapo wanamfahamu ndugu huyu na chimbuko la familia yake toka wanaingia walibaki na mashaka yao. Hali hii na wasiwasi nilionao juu ya mtandao huu vimenifanya kuandika waraka huu ili kukiomba chama kitupe ukweli wa swala hili ni nini na pengine kumtaka Huseni Bashe, mama yake na wadogo zake wafuate taratibu za halali za kutafuta uraia wao. Hata hivyo pamoja na waziri wa mambo ya ndani kutoa uthibitisho huo kwenye vyombo vya habari hakumpa ndugu Huseni Bashe hati yoyote ile ya kumpa Uraia. Hivyo maneno yale yanabaki kuwa kauli ya kisiasa isiyo na mashiko yoyote yale kisheria kwa mujibu wa sheria hiyo niliyoitaja hapo juu. Kwa kuwa baba yake alipewa uraia tarehe 27/05/1987 baada ya kuishi kwa hati ya ukazi kwa muda mrefu na kuamua kuomba uraia na kufuata taratibu zote hakuna utata kwamba alikuwa raia wa Somalia kwa muda wote kabla ya hapo. Hata Huseni mwenyewe amejaza kwa kuthibitisha hili kwenye fomu yake ya kugombea Ubunge kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1947 sehemu inayoitwa Buroa, Mkoa wa Buroa kule Somalia. Japokuwa maelezo yaliyopo kwenye mtandao aliyoyatoa kumshambulia mbunge wa nzega mheshimiwa dr. Kingwangallah anaandika hadithi tofauti kwamba baba yake alizaliwa Tabora mjini.
Uraia wa mama yake unabaki kuwa ni swala lenye kuhitaji uchunguzi na uthibitisho. Huseni hutoa maelezo ya kwamba mama yake ni mnyamwezi wa Tabora jambo ambalo halikubaliki maana hata Kiswahili, achilia mbali kinyamwezi, hakifahamu vizuri na pia hata muonekano wake ni wa kisomali bila shaka yoyote. Kwa maelezo ya Husein Bashe kwenye andiko la kashfa kwa mbunge wa nzega dr. kingwangallah anadai kuwa wazazi wa mama yake ni wazaliwa wa Tanzania, Sumbawanga (Baba yake na Mama Husein) na Boma Ng’ombe (bibi yake na mama Husein) kwamba walichagua uraia wa Tanzania
3 | P a g e
kutoka ule wa Somaliland wakati wa Uhuru lakini hakuna kumbukumbu hata moja kuwa waliandikwa kwenye rejista ya raia wa Tanzania waliosajiliwa kama ‘aliens’ kwa mujibu wa sheria iliyokuwa inatambua uraia wa kuandikishwa, yaani ‘citizenship by registration’ ya watanzania minorities wakati tukipata uhuru. Habari hizi zinaonekana ni za uongo kwa kuwa tayari tuna ushahidi wa cheti cha kugushi cha mama yake na mama Husein Bashe (aliyejulikana kwa jina la Amina bint Ahmed) na tuna taarifa kwamba babu yake kizaa mama na Husein alitokea kijiji cha Belibeli kule Somaliland akiingia Tanzania na mkewe bi Amina na watoto (akiwemo mama Husein – Zainab bint Abdi). Alichokifanya Huseni Bashe ili apate Uraia Kwa mujibu wa sheria ili upate uraia wa Tanzania ni lazima uwe umeishi nchini kwa kibali cha ukazi na umeishi kwa kipindi kisichopungua miaka 10, saba kati ya hiyo uwe umeishi mfululizo huku ukiwa mwema na mwenye faida kwa nchi kijamii ama kiuchumi (second schedule, conditions for citizenship by naturalization, section 9(1) ya sheria niliyoitaja hapo juu) . Na maombi hayo yanaanzia kwenye kata unayoishi (kanuni namba 8 iliyomo kwenye Tanzania citizenship regulations (section 28)) pia alitakiwa mwombaji (Huseni Bashe) kutangaza kwenye magazeti ya kila siku kwa siku 2 zinazofuatana (kanuni ya 3 ya kanuni nilizozitaja hapo juu). Mpaka naandika hapa hakuna gazeti wala mtu hata mmoja katika niowahoji aliyekumbuka kuona tangazo la namna huyo kumhusu Husein Bashe. Kwa kufuata utaratibu huu unaoelekezwa na sheria na kanuni zake alijua angepoteza matumaini ya kuingia kwenye siasa mapema na ingewezekana kuwa ndiyo ukomo wake kabisa. Aliamua kutafuta njia fupi ya kupata uhalali wa uraia wake kwa kugushi hati za kuzaliwa za mama yake mzazi na za bibi yake kizaa mama (ambazo naziambatanisha hapa). Kwa kufanya hivi alijua atapata uhalali wa kutumia kipengele cha sheria kinachosema kama mzazi wako mmoja ni mtanzania na wewe umezaliwa Tanzania basi unaukana tu uraia wa mzazi mmoja ambaye hakuwa mtanzania wakati unazaliwa. Hivyo alipata mwanya wa kuukana uraia wa baba yake na kudai amebaki na uraia wa mama yake (ambaye alidai kuwa ni mnyamwezi na hata kwenye hati ya Husein Bashe inaonekana hivyo). Hati ya kuzaliwa ya mama yake mzazi na Husein Bashe ninayo kivuli chake na nitakiambatanisha na barua hii pia cha bibi yake. Vyeti vyote hivi ni vya kugushi na hili tumelithibitisha RITA. Cheti cha mama yake Huseni Bashe kina taarifa zifuatazo:- No. of Entry 3032, Namba ya cheti A. 17404 na kimesainiwa na L. M. Manson tarehe 14/02/1984, kimetolewa wilayani Tabora, na kinadai mama yake Husein Bashe, mwenye jina la Zainab bint Abdi alizaliwa Government European Hospital na ni wa kabila la Isihakia kutokea Somalia. Na kile cha Bibi yake Husein Bashe kina No. of entry 3508, na namba ya cheti A 17399, na kimesainiwa na A. B. Hodgson, kimetolewa wilaya ya Moshi tarehe 14/02/1984, amezaliwa Boma la Ng’ombe, na jina lake ni Amina Binti Abeid, na ni wa kabila la Isihakia. Jambo la kuvutia ni kwamba kwenye vyeti vyote hivi aliyesaini ni mtu mmoja (japokuwa ni mikoa miwili tofauti na siku moja).
Mbali na RITA kukana kutokuvitambua vyeti hivi kuna kila alama ya kugushi kwenye nyaraka hizi kwanza vyote vimesainiwa na kutolewa siku moja, na mtu mmoja kwenye mikoa tofauti na serial number za kufuatana (17404 na 17399!) pia walioandikwa kusaini wana majina tofauti yanayoonesha kuwa ni foreigners (Manson na Hodgson). Watu wenye majina hayo hawajawahi kuwepo Tabora wala Moshi. Pia hakujawahi kuwa na hospiali yenye jina hilo lililotajwa hapa Tabora na ni kitu kisichowezekana kwa ofisa
4 | P a g e
wa serikali kukosea jina la Boma Ng’ombe na kuandika Boma la Ng’ombe pia kuandika kwamba ipo wilaya ya Moshi badala ya wilaya ya Hai. Uchunguzi wangu umebaini kuwa mama yake hakuzaliwa Tanzania na kwamba aliingia Tanzania kupitia Rundugai akiambatana na wazazi wake na wajomba wa Huseni Bashe (mmoja yupo Dodoma – maarufu kama Charles mnene, na ambaye alinipa historia hii bila kujua ninachokifanya) wakati huo mama yake mzazi Husein akiwa na umri wa miaka 8/9. Alitafuta njia fupi ya kujipatia uraia ili kukwepa mlolongo wa taratibu kwa sababu za kisiasa. Kiuhalali – alitakiwa alipofikisha umri wa miaka 18 aanze kuishi kwa kibali cha ukazi kwa kipindi cha miaka 10 ndipo afanye maombi yake rasmi ya kupatiwa Uraia jambo ambalo lingemnyima sifa ya kugombea uenyekiti wa UVCCM Taifa mwaka 2008, hivyo alikwepa akapita njia fupi. Sasa kwa kufanya hivyo amevunja sheria kwa kugushi nyaraka za uraia za mama na bibi yake na ana kosa la kujibu kisheria, yeye na pamoja na bibi na mama yake. Anachotakiwa kufanya kwa sasa kuhusiana na Uraia wake Anatakiwa kuomba kibali cha ukazi na aishi kwa kipindi cha miaka 10, 7 kati ya hiyo ikiwa ni ya mfululizo na akiwa ni mtu mwema na mwenye faida kwa nchi kijamii na kiuchumi ndipo afanye upya maombi ya uraia. Tabia ya kugushi nyaraka na taarifa mbalimbali Amekuwa akidanganya umri wake kwa kuwa na siku mbalimbali za kuzaliwa – ushahidi ni taarifa alizojaza kwenye fomu mbalimbali za kugombea nafasi za Uongozi kwenye chama, mfano mwaka 2005 alipogombea ubunge alijaza amezaliwa mwaka 1976, mwaka 2010 alipogombea ubunge alijaza kuwa amezaliwa mwaka 1978. Pia mwaka 2007 alikuwa anagombea Ujumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa alijaza kuwa amezaliwa mwaka 1977. Siku yake ya kuzaliwa imekuwa ikibadilika badilika kutokana na mahitaji ya wakati huo. Siku yake ya kuzaliwa ilibadilika ili apate fursa ya kugombea UVCCM mwaka 2008 (kwa kushusha umri wake akidhi vigezo) na tarehe hiyo inapatikana pia kwenye kiapo chake cha Uraia anachotumia (hivyo nacho ni batili) na pia kwenye kitambulisho chake cha mpiga kura (kama inavyoonyesha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura). Ukitaka kuamini kuwa amedanganya umri linganisha taarifa hizi na za mdogo wake aliyemuachia ziwa anayejulikana kwa jina la Ismail Mohamed, ambaye naye amezaliwa mwaka huo huo wa 1978. Kiapo chake cha uraia kilipatikana tarehe 24/09/2008 akiwa na umri wa miaka 30, umri ukiwa ni wa uongo kwa kuwa alikuwa amefoji vyeti vya kuzaliwa. Pia mwaka 2005 akigombea Ubumbe aliandika kuwa ana digrii mbili, ya kwanza ya Mzumbe nay a pili (MBA) ya UNISA, ambayo hakuwa nayo na mpaka leo hii hana.
Pia amewahi kufukuzwa kazi sehemu mbalimbali kwa udanganyifu:- alidanganya NMB benki kuwa anaumwa kumbe amelala nyumbani kwa uvivu wa kwenda kazini. Bosi wake alipozidi kumtafuta na aliposikia kuwa kuna hatari ya kufukuzwa kazi aliamua kutafuta daktari wa uongo ili amfunge POP ndipo akaenda kuripoti huku akiwa anatembea akichechemea kwa msaada wa magongo mpaka kwa bosi, watu wakampa pole nyingi pale ofisini. Alipoingia na kumueleza bosi wake kuwa hakuja kazini kwa sababu
5 | P a g e
alivunjika mguu bosi alimhoji kwa nini hakuchukua seek sheet na kwa nini hakutoa taarifa, akashindwa kujibu. Pamoja na hali aliyokuwa nayo bosi aliamua kumkabidhi barua ya kumfukuza kazi; Husein alilia sana na kisha akatupa magongo akaondoka bila kuchechemea tena kama alivyoingia. Watu wakashangaa na kuangua vicheko. Pia amewahi kufukuzwa kazi pale Celtel kwa kosa la uzembe na kutokuweka sawa hesabu zake. Amewahi kufukuzwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya pesa na kampuni nyingine ya wazungu wa Afrika Kusini iliyokuwa inatengeneza kadi za mabenki. Haya ni baadhi ya mambo niliyoweza kukusanya dhidi ya mtu huyu ambayo nadhani mnahitaji kuyajua ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi. Je ni kweli Tanzania inahitaji kuongozwa na vijana wa namna hii? Natanguliza shukrani zangu za dhati nikitarajia mtu huyu atapata anachostahili. Wako mtiifu, Maganga Masanja (kwa sababu za kiusalama nimeficha jina halisi ila ukitaka kunipata kwa maswali ama kwa ushahidi fika kwa DSO Nzega na mimi nitajitambulisha pale) Mwanaccm Mwaminifu, Nzega. Nakala:
1. Mwenyekiti wa CCM – Kwa taarifa
2. Naibu Katibu Mkuu, Mh John Chiligati (Mb.) – kwa ufuatiliaji (maana amekuwa akikutaja kwenye hotuba zake kwamba ulimsingizia kwa chuki zako)
3. Mwenyekiti wa CCM (M) Tabora – kwa taarifa
4. Katibu wa CCM (M) Tabora – kwa ufuatiliaji na uthibitisho
5. Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
6. Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
7. Msajili wa vyama vya siasa – ndugu John Tendwa – kwa ufuatiliaji wa hatua zitakazochukuliwa na chama cha mapinduzi
8. DPP – kwa upelelezi na hatua za kisheria
9. DCI – kwa upelelezi na hatua za kisheria
10. Kamishna Mkuu Uhamiaji – kwa upelelezi na hatua za kisheria
11. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi – kwa taarifa
12. Uhamiaji, Nzega – kwa taarifa
13. Usalama wa Taifa, Nzega – kwa taarifa
14. Mbunge Nzega – kwa taarifa
15. DC Nzega – kwa taarifa
16. CCM Nzega – kwa taarifa

Ninatabia ya kusave vitu kwa kumbukumbu....
 
Kwa hiyo HAMIS KIGWANGALA jina. Lake halisi ni SAID BAGAILE hatari sana hivi huko CCM inaonekana wengi sana wameiba majina ya watu na hili tatizo inaonekana wengi walifel darasa la saba hivyo wazaz wao wakishirikiana na watendaj serkal walikwapua majina ya wanafunz waliofaulu na kuwanyima fursa ya kielimu

Swal la kujiuliza n wanafunz wangap wa kipind hiko ambao waliibiwa majina na fursa za kimasomo na mfano katoa bashe mwenye jina anateseka tu hapo GANAGANA SOKONI NZEGA halafu mpuuz aliyeiba jina anatesa tu na range
 
Back
Top Bottom