kagoshima
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 2,638
- 5,143
Jumapili njema wakuu!
Huu ndo ukweli wenyewe!
Kwa kengo lile lile la CCM kutawala raia wasio na elimu, ndiyo chanzo cha nguvu kubwa ya kuzuia elimu ya katiba mpya isisambae kwa raia kwa kukataza uwepo wa mijadala ya katiba mpya. Tafiti za huko nyuma zinaonesha wazi shabiki wakubwa wa ccm ni wale ambao hawakwenda shule. Ule msemo wa " mnyime elimu umtawale " ndio unaotumiwa na ccm kwa sasa.
Ccm hawawezi kubali kuona RAIA wakipata elimu ya uraia, katiba na mambo mengine yanayohusu haki za kiraia. Kumbuka makamanda wa polis inchi nzima ni makada wa ccm. Hivyo wanaona kabisa anguko la ccm ni anguko lao. Hivyo basi juhudi za polis kuzuia raia wasielimike kuhusu katiba na umuhimu wake ni juhudi zile zile za chama mfu Ccm. Ccm hawawezi simama jukwaani kutetea katiba iliyopo hivyo hutumia polis kama nguvu yao Ku suppress mjadala wa katiba mpya kinguvu.
Ni wazi taifa linahitaji katiba mpya. Hata nyoka huvua gamba la zamani ili aweze kukua zaidi ndani ya gwanda jipya. Wao ccm hawana cha kupoteza. Kwao maslahi ya chama kwanza taifa baadaye. Huwezi ukaendelea kutumia mbinu zile zile, taratibu zile zile, maarifa yaleyale utegemee matokeo tofauti. Hakuna mabadiliko, kiuchumi, kisiasa, kidemocrasia yatapatikana hii inchi bila katiba mpya.
Cha kufanya , vuguvugu la katiba mpya liendelee kwa njia zozote zile iwezekanavyo, maana katiba ni kwa ajili ya kizazi hiki ni vizazi vijavyo.