Happy Feet, Ahahaha hahaha! samahni mkuu wangu imenitoka tu silidhani...
Shangazi unajua unapotoa hoja lazima uwe na ushahidi kama ingekuwa bungeni kila mtu anaingia kwa mpango wake sidhani kama government policies zingekuwa zinapita kirahisi, maana wakati wa majadiliano ya bunge la budget kunakuwa na malalamiko mengi sana hata kutoka kwa wabunge wa serikari kuhusu budget iliyopita na jinsi ambavyo aijawafikia walengwa huko majimboni mwao, lakini watu hao hao ndio wanaoipitisha government budget kwa sababu ya maslahi ya kundi ndio maana ya kuwa mwanasiasa unaetumikia chama in most cases ni maslahi ya wengi(kundi zima) sio yako binafsi.
Hapo sasa unaona ulivyojibu, kama bajeti ya serikali imetoka, inakuwaje hata baadhi wajumbe wa CCM wanaipinga? wengine wanauliza ni lini maendeleo yatafika kwao, lini barabara itajengwa yaani siku kabla ya bajeti ila mtu Kipofu hajui ule mfuko ni kama box la Chocolate. hii ina maana hata CCM wenyewe hawakuandaa bajeti yao kutokana na itikadi ama sera zao isipokuwa sera hutungwa pale pale bungeni na wao husubiri Ilani ya Mheshimiwa itawahifadhi lipi.
Leo wataamini Elimu bure ni right, kesho ni privilege mara haiwezekani rais akisema inaweekana shangwe na makofi, ili mradi tu wapo wapo. Na ndio maana siku zote husubiri kumsikia mkuu wa kaya atasema nini maana wao hawana msimamo na kama ingekuwa tunarushiwa moja kwa moja kura za wabunge basi utakuta hata wale wa Upinzani wameipitisha bajeti.
Nakuhakikishia kwamba pale Bungeni kila mtu huenda na hoja yake kichwani, kisha yeye mwenyewe hutafuta watu kumuunga mkono, wizara na mashirika ya serikali vivyo hivyo tena hubeba na posho mkononi, huoni kama hii ni ajabu hata katika swala la kisera utafute watu wa kuuunga mkono utadhani mkutano wa saccos!
Despite all that niliutetea sana ule mkakati uliomwondoa Prof.Kitila na kumplekea Zitto kuwa mmbunge wa mahakama kwa sababu niliamini principally they did not break the rules ingawa practically they broke the cultural code of their institution na dhahiri CDM ina utamaduni wake wa kufanya mambo kama unavyoona ingawa Zitto leo hayupo kwenye kinyan'ganyiro lakini sakata la kutaka Mbowe aendelee kubaki mwenyekiti alijaisha na kwa jinsi mambo yanavyoenda you know the fate is with Mbowe himself.
Kumbe upo upande huo ndio maana basi. Kama umemchoka mtu hata akisema nini huwezi kufurahia nilidhani upo open minded kumbe tayari ulishamhukumu, Aaah basi nimekuelewa maana yanayotoka upande wa pili hunaosema kwamba Zitto hivi na vile, Slaa hivi Slaa vile, Mbowe ndiye jembe hakuna zaidi yake na sio Chadema toka nazifuatilia siasa za Bongo.
Hakuna haja ya maelezo mengi ila kumbukeni mtakuja vuna mlichopanda..