Zitto: Wapambe wametufitini na Mbowe

Zitto: Wapambe wametufitini na Mbowe

Hivi Zitto ana kadi "yetu" au ya CHADEMA?....
 
Aende tu huyo kondakta wa kisiasa kila abiria anamtamani
bora kenda mkononi kuliko kumi isiyokuwepo
 
J.F Moderator
Zitto Z. Kabwe (Mbunge).
Pamoja na wadau woye wa Jamii Forum.
Itafaki imezingatiwa.

Nitangulie kwa kusema yafuatayo.
Mimi ni kijana niliyelelewa katika jamii ya siasa. Nimekua nikishuhudi Siasa za nchi hii zinavyendeshwa kupitia watu nilio nao karibu kabisa na wanaojjihisisha moja kwa moja na maswala ya siasa. Wengne ni Viongozi wa chama ,Madiwani,na Wabunge.
Hivyo nimejifunza mambo mbalimbali ,ambapo pengine yanaweza kunifanya nione siasa ni jambo lisilofaa kabisa wala na kumkatisha mtu taama ya kufanya siasa katika maisha yake.
Naelewa huwezi itenganisha jii yeyote na maswlaa ya siasa,na ndio maana mtu hushindwa kabisa kujindoa katika uwanja hio moja kwa moja.

Nirudi kwenye Mada.

Nimeongea hayo nikiamini huwenda ZZK umepitia historia mfanano na hiyo.
Umelelewa katika siasa,au huwenda ulijifunza na kuijua siasa toka ukiwa mdogo.Umepitia vikwazo vingi ,miiba ,mabonde na milima migumu,kitu ambacho huwenda kingekukatisha tamaa katika hatua za awali kabisa .

Ukiwa kama kijana mdogo ,tena kama ya upinzani ulinza harakati zako za kutetea wananchi na kuikosoa serikali.
Uliibua Mambo mbalimbali mazito na yaliyo na tija kwa uma.Ufisadi pamoja na Rushwa,mambo ambayo mtanzania wa kawaida alaikua hayajui kabisaa na wala asingeweza kupata fursa ya kujua lolote.
Ni kupitia ww ulikamua limao na kutia chachu katika upinzani,ulipelekea muamko mkubwa sana wa upinzani. Kutokea hapo hamasa ikataambaa nchi nzima ,watamzania waliokua waoga juu ya serikali yao,wakageuka wajasiri.
Vyama vua upinzani navyo kwa haraka vikapata nguvu.

Hakuna atakayebisha kua ,ongezeko la vijana katika siasa lililetwa na wewe.

Hata leo hii wabunge vijana wote hususani wapinzani walipata muamko kupitia wewe. 90% ya wabunge vinana wa CHADEMA walipata nguvu kutokana na jitihada zako.

Nawalaumu wabunge wengi vijana wa CHADEMA wanaosimama leo hii na kukusema vibaya bila ya wao kuangalia walipotoka. Bila wewe leo hii waaingekua na uthubutu wa siasa na wala wasingeitwa wabunge.
Huwenda waliingia bila malengo ,bali kutokana na tamaa ya pesa,madaraka na umaarufu ,wakidhani hayo ndio siasa kumbe siasa sio lelemama.

Niseme tu kuna mambo mawili makubwa yanayokutofautisha na wabunge wengi vijana .

1.Uwezo wa Kuzaliwa wa Kisiasa.(upembuzi wa maswala ya siasa,umakini,uvumilivu,na uahawaishi wa hali ya juu).

2. Elimu (uwezo wa kubadili elimu yako katika vitendo )

Nadhani wabunge wengi wameshindwa kua na mambo hayo na ndio maana wanapoteza aifa ya uongozi bora.

Na ndio maana nadharia ya ukombozi inapotea ,wabunge wamebaki kutii amri za viongozi wao bila kusimamia ukweli na tija za mioyo yao juu ya wananchi.
Akili za vijana zinauliwa kwa nguvu za watu wachache wenye malengo binafsi.

Kwa kazi kubwa ulizozifanya ndani ya chama chako na hata katika nchi huna budi kupongezwa.
Unastahili pongezi za dhati

1.Kwa kuujenga na kuupa nguvu upinzani nchini kwa ujumla.

2.Kwa kuwa na udhubutu wa kuikosoa nchi.

3.Na kwa kuleta muamko kwa vijana/ kujielewa juu ya mwenendo wa nchi yao.

Kumekuwa na sitofahamu inayoendelea ndani ya chama ulichopo CHADEMA ,kwa kukuita Msaliti ,ambapo hoja hiyo ilizuka pale tu ulipojaribu kuitetea Democrasia ndani ya chama kupitia katiba ya chama chama chako.
Sihitaji kuhukumu direct juu ya hili ,ila mwisho wa siku ukweli utajulikana . Nakusihii piga moyo konde,ulipotoka ni mbali,kwa namna moja au nyingine naaamini kwa lolote lisemwalo ni sehemu ya mapigano katika kuitetea Tanzania.

Lengo la Ujumbe wangu.

ZZK mimi kama kijana ,tupo wengi tuliotambua na tunaotambua mchango wako kwa serikali ya Tanzania pamoja na vyama pinzani hususani CHADEMA.
Kila binadamu ana kasoro yake na mapumgufu yake "no one is perfect".
Hivyo basi naungana na vijana wenzangu wnye uchungu wa nchi hii kukutia moyo juu ya changamoto unazozipitia . Tunaelewa mapungufu yaliyolo ndani ya CHADEMA kuanzia ngazi ya uwenyekiti mpaka chini kabisa .
Hivyo basi sioni haja ya wao kukuhukumu kua umetenda dhambi kubwa kiasi hicho. Ni mchezo wa kuzuia Demokrasia wanayoihubiri wao wenyewe.

Pambana ukiamini katika kutetea demokrasia popote pale .

Kama Vijana "hakuna asiyetambua mchango wako"husani katika upinzani ,umetujengea msingi mzuri wa kijiamini,kithubutu na kutamani kuijenga nchi yetu.

Ahsante.
 
Ahsante.[/QUOTE]
nina wasiwasi kama unajua unacho andika, kama unajua unachoandika basi unajifanya hamanazo...unaelewa maan ya usaliti...hii umeiandika kiushabiki wala si kiuchambuzi...na kama zitto ni kiomngozi wa kipekee si lazima ang'ang'anie kuwa chadema ili aonekane ni kiongozi bora...kama nyerere alitaka kuachana na CCM kwamba si mama wala baba yake sembuse Zitto na chadema...Zitto anajua laichokuwa akikifanya chadema akiwa anatumikishwa na mabwana wake wa chama cha kifisadi!
 
team Yuda Askariote wako Kazini mtajibeba kuwasafisha wasaliti ni sawa na kuosha kanzu kwa mkaa
 
Jamaa alijisahau akajiona kama yeye ni mtu wa kipekee, kwamba hakuana tene binadamu kama yeye, kumbe ni kujidanganya na kujipumbaza...na mbaya zaidi tamaa ya pesa na majivuno ya kijinga...lakini kama uko makini sana ukimsikiliza Zitto kwa utulivu utagundua huyu jamaa ni mbabashaji na hayuko moja kwa moja...kwa wajinga anawakoga sana!
 
Msizitafute huruma zawatu kwanduguyenu yeye nimwana siasa kijana jasiri na maalufu aende kwenye chama chake alicho andaliwa asitafute huruma yeye simarufu sana wananchi waliokua wakimkubali watamfuata huko.
 
nina wasiwasi kama unajua unacho andika, kama unajua unachoandika basi unajifanya hamanazo...unaelewa maan ya usaliti...hii umeiandika kiushabiki wala si kiuchambuzi...na kama zitto ni kiomngozi wa kipekee si lazima ang'ang'anie kuwa chadema ili aonekane ni kiongozi bora...kama nyerere alitaka kuachana na CCM kwamba si mama wala baba yake sembuse Zitto na chadema...Zitto anajua laichokuwa akikifanya chadema akiwa anatumikishwa na mabwana wake wa chama cha kifisadi![/QUOTE]

Mstari wa tatu kutoka chini .

nanukuu .

"pambana ukitafuta demokrasia popote pale" mwisho wa kunukuu .

popote pale anaweza kuitetea demokrasi .. sihamsibii abaki CHADEMA.
 
Mwache aendelee kutumikia CCM kupitia ACT.Na ubunge si anaendelea nao wa viti maalum vya mahakama.
 
Mtoa mada andika kiswahili kinachoeleweka. Jaribu kuiedit maada yako.
 
Uchaguzi wa mwenyekiti chadema taifa ukipita zitto atasamehewa, vuteni subira muone
 
Mamamamayee zako,unaandika kwa kutumia makalio.ACT msituchagulie wanachama
 
Hata Zitto anapaswa kumshukuru sana Mbowe kumfikisha hapo alipo. Ni kweli kuna vijana waliokuwa inspired kuingia kwenye siasa na ZZK lakini hao hao vijana wamekuwa disapointed sana baada ya kugundua beyond reasonable dought kuwa Zitto kageuka kuwa mcheza madili na CCM akina Mwigulu na Zoka. Aende salama katika chama alichoagizwa kukiunda na Kinana. Amekisaliti CHADEMA, amesaliti Tumaini pekee la watanzania. AMEGUSA Mboni ya Mungu na Mungu atamshughulikia kwa kipimo anachokistahili.
 
Back
Top Bottom