Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic...

Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic...

Mawazo Bora ndani ya mawazo Bora ni uchakachuaji

nakumbuka tulipokuwa shule, kwenye ile elimu ya sekondari kubwa ya miaka miwili, mkaka mmoja ambaye mara zote alipenda group discussion ambayo ladies wako kibao, yeye alijifanya mtaalam sana wa hesabu za minyororo, na mkipata kipande cha swali na mkakukuruka nalo kwa muda na kupata jibu, yeye huchomoka akajitenga pembeni na kukukuruka nalo zaidi ili tu apate njia nyingine mbadala wa kulifanya swali hilo hata kama njia yake ni ya kubuni ili mradi jibu analijua basi ataungaunga mpaka nae aonekane kidume flan wa mafiga hayo yaliyoitwa mase au mets au 'nyuma ya nyumba' (backhouse). Basi akishajitengenezea njia yake anavamia kwenye group ambapo nyie that time mmeshasolve mafiga kama kumi hivi..utaskia.. 'eheee nimeshapata njia nyingine ya kufanya lile swali'.. basi atawabugudhi mpaka awaonyeshee na sometimes anasahau anarudi kuundaunda jibu anakuja tena.. yaaani kero tu.. hatimae aliruka na Div Zero ukingoni mwa shule..

samahani Mwanakijiji .. sasa nadhani jamaa yetu huyu mnaweza kuwa mnafanana fanana kimtazamo.. Wabunge leo wameweka Historia ya kuthubutu, hata kama si kweli kiranja huyu wa mawaziri atang'oka, ila hatua hii ni ukomavu wa uthubutu ambao kwa miongo mingi ya uhai wa Bunge ZOTOTO haikuwahi kufikia. Ingepongezwa hatua kama hii na kuweka imani kwamba kuna hatua zaidi hapo baadae inaweza kuchukuiwa. ukisema hatua hii ifie mkononi utakuwa na udhaifu wa kuwaza..

ungeanza na Kichwa cha habari kwamba PELEKA hoja ila kuwe na strategy baadae ya desh..........desh........ na desh........... hapo ungeeleweka ila ulipotumia neno USIPELEKE.. hapo ndipo uzi wako ulipopotokea mkuu.. si kila shambulio au si kila pambano unalenga ushindi, sometime unapima nguvu ya adui.. ukimuona adui yuko kimya unarusha bomu moja kupima upepo, ukiona linajibiwa na makombora ya kufa mtu ujue hapo usiguse tangaza hali ya amani haraka urudi ukajipange upya.. kama huamini angalia masumbwi, unamkuta mtaalam anaanza kurusha kikonde kwa mkono wa kushoto anapima mtikisiko wa adui na kufanya tathimini yakinifu kwamba akivurumsha konde la kulia itakuwaje..

Bravo wabunge.. sogezeni ukuni Jumatatu .. kisha serikali ibaki ikitarajia huruma ya wabunge wao wa CCM ambao wengine wako kikazi zaidi na ukichukulia kura ni za siri, sipati picha itakuwaje..
 
Bravo wabunge.. sogezeni ukuni Jumatatu .. kisha serikali ibaki ikitarajia huruma ya wabunge wao wa CCM ambao wengine wako kikazi zaidi na ukichukulia kura ni za siri, sipati picha itakuwaje..

Siku ndugu zangu mtakapoelewa kuwa hii ni vita - tunapigania nchi yetu kuirudisha mikononi mwa wananchi - ndio mtatambua siyo kila neno lazima lisemwe, siyo kila silaha itumiwe na siyo kila kita kipigwe. Hivi mnafikiria suala la Arusha kwa mfano lilikuwa la lazima? Lema asingekuwa loose canon wala kusingekuwa na ulazima wa ile kesi; sasa mkiipeleka hii hoja J'tatu na CCM wakaikubali mnapoteza nafasi kama hiyo kwa miezi mingine sita kwa sababu hakuna kura 178!

Sasa wengi wanataka 'symbolic victory' kwamba 'tumethubutu'. Thats fine and dundee lakini vitani hakuna "ushindi wa symbolic"! Target ya Waziri Mkuu ilitakiwa ichukuliwe strategically; kwa sababu, mawaziri wakijiuzulu kama inavyosemwa na nyie mnaleta j'tatu hoja yenu guess what; wabunge wote wa CCM waliobakia WILL RALLY behind the prime minister, wale 5 or so waliotia sahii watakuwa pariah na japo wananchi watasifia uamuzi huo lakini the real target - Prime Minister hatopatikana.

Now, Kikwete akipenda just to outplay everybody atatangaza tu kuvunja baraza na akaunda baraza jipya chini ya PInda huyo huyo. Halafu itabidi ipigwe kura ya kumkubali kama waziri mkuu (namna nyingine ya kuwalazimisha watu kupiga kura ya kuwa na imani naye au la).. It is a war, na vita vinapiganwa kwa strategy! Thats all I'm saying. Hii hoja ikipelekwa j'tatu the oppossion WILL lose the argument ya change.
 
Kaka au Dada (sielewi ipi sahihi) unaejiita MzeeMwanakijiji, ngoja chama chako cha CCK ndio ukipe ushauri huo. Zitto anapeleka Jumatatu na yeye anakijuwa akifanyacho zaidi yako. Ushauri wako hauna mshiko.
 
Ni muhimu kura ibakie ya kutokuwa na imani na waziri mkuu hata kama wabunge wa CCM hawataipitisha.
Wabunge wa CCM watakuwa wako mahali pagumu kwa kila uamuzi watakaouchukua.
1. Wakipiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu basi angalao wananchi watapata imani kidogo kuwahusu CCM.
2. Wakipinga kupiga kura ya kutokuwa na imani - basi wananchi watajua wazi kuwa wizi unalindwa na CCM.

Inanikumbusha kijana aliyetaka kujifanya ana akili kubwa kuliko mzee mmoja wa hekima aliyekuwa akijibu maswali ya wanakijiji. Akamuendea yule mzee akiwa na ndege mkononi. Akamuuliza kama una hekima kweli basi sema.
Yuko hai au amekufa? Alijua akisema amekufa atamwachia aruke ili watu wamcheke. Akisema yuko hai atambonyeza afe ili watu wamcheke kuwa hana hekima. Hivyo mzee wa hekima akamjibu; "kuwa hai au kufa kupo mikononi mwako."

CCM wanapaswa kujua suala hili liko mikononi mwao. Kutokupiga kura ndiyo kura hatari zaidi against themselves.
 
Natafakari. Nakuja manake simu imeishiwa charge

Kwenye utafiti wetu tunajaribu kuleta teknolojia mpya ya kutengeza beteri zinazodumu karibu siku tano kabla hazijaomba juice mpya. Tumefadhiliwa na makampuni yanayotengeneza magari ya umeme na tumekaribia sana kufikia huko Kaanani kwa vile tumeshaongeza karibu asilimia 190 ya muda wa kawaida. Siku za mbeleni hutakuwa na wasiwasi wa kuishiwa chaji tena.

Nikirudi kwenye hii hoja ya Zito kutaka kumwondoa Waziri mkuu madarakani, ninadhani kuwa haikufikiriwa vya kutosha ingawa imeweka pressure ya kjutosha sana huko serikalini. Kwa hali ya kisiasa leo hii nchini, ninakuwa na wasiwasi sana kuona iwapo wabunge wa CCM watakuwa tayari kutumia nafasi zao kuipa Chadema umaarfu zaidi kwa kusupport kura ya kumwondoa waziri mkuu wao kutoka madarakani.
 
Siku ndugu zangu mtakapoelewa kuwa hii ni vita - tunapigania nchi yetu kuirudisha mikononi mwa wananchi - ndio mtatambua siyo kila neno lazima lisemwe, siyo kila silaha itumiwe na siyo kila kita kipigwe. Hivi mnafikiria suala la Arusha kwa mfano lilikuwa la lazima? Lema asingekuwa loose canon wala kusingekuwa na ulazima wa ile kesi; sasa mkiipeleka hii hoja J'tatu na CCM wakaikubali mnapoteza nafasi kama hiyo kwa miezi mingine sita kwa sababu hakuna kura 178!

Sasa wengi wanataka 'symbolic victory' kwamba 'tumethubutu'. Thats fine and dundee lakini vitani hakuna "ushindi wa symbolic"! Target ya Waziri Mkuu ilitakiwa ichukuliwe strategically; kwa sababu, mawaziri wakijiuzulu kama inavyosemwa na nyie mnaleta j'tatu hoja yenu guess what; wabunge wote wa CCM waliobakia WILL RALLY behind the prime minister, wale 5 or so waliotia sahii watakuwa pariah na japo wananchi watasifia uamuzi huo lakini the real target - Prime Minister hatopatikana.

Now, Kikwete akipenda just to outplay everybody atatangaza tu kuvunja baraza na akaunda baraza jipya chini ya PInda huyo huyo. Halafu itabidi ipigwe kura ya kumkubali kama waziri mkuu (namna nyingine ya kuwalazimisha watu kupiga kura ya kuwa na imani naye au la).. It is a war, na vita vinapiganwa kwa strategy! Thats all I'm saying. Hii hoja ikipelekwa j'tatu the oppossion WILL lose the argument ya change.

mm, nakubaliana nawe hii vita inahtaji akil ya ziada kuweza kuishnda. tayar taarifa za kujiuzuru kwa baadh ya mawazir zinaweza kuharibu au kudhoofisha dhana ya awali kwa kuwa nia ipo na dhamira yapasa kujipanga upya .
 
Mwanakijiji

Ninakubaliana sana na hoja zako lakini hili la kutaka raisi avunje bunge na kuilazimu nchi kuingia kwenye uchaguzi ni kitu kisichowezekana hata siku moja.
Wabunge wa ccm hawawezi kamwe kukubali hoja kama hiyo huku wakitambua vuguvugu la mabadiliko miongoni mwa wananchi kwa sasa, wataona ni bora wamalizie tu miaka yao mitano, kama wataangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 basi iwe hivyo lakini walau watakuwa wamejikusanyia vijisenti vya kundelea namaisha baada ya ubunge.

Kwa kuzingatia hali hiyo, sidhani kama hiyo proposal yako ni ya kuzingatiwa kwa sasa, labda ushauri kitu kingine, najua unaweza kushauri mbinu mbadala. Hivyo basi nadhani ni muhimu zitto ahakikishe anakamilisha saini sabini kwa ujibu wa kanuni na awasilishe hoja yake ofisi ya spika ili mchakato wa hoja hiyo uanze rasmi. Siamini kama wabunge wa ccm wanaweza kupiga kura ya kumtosa waziri mkuu wa serikali yao lakini kisiasa ina impact kubwa sana.

Niliwahi kushauri chadema ijikite katika kutafuta wabunge wa kutosha huku nikiwakumbusha kwamba ukiwa na wabunge wengi unaunda serikali,nikabezwa sana na nyie chadema kata,leo mnatanga tanga kila gesti bubu kusaka sahihi za mnaowaitaga magamba...!
 
MMKK binafsi nakubaliana nawe kuwa katika hili Zitto anapaswa kuwa strategic na ni kweli yupo Strategic. Hoja anayotaka kuiwasilisha Bungeni ni kutokuwa na imani na waziri Mkuu. Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni kwamba Bunge ambalo linawakilisha watanzania halina imani na Serikali yao kuanzia yule aliyemweka madarakani Waziri Mkuu kama kiongozi wa Mawaziri wote pamoja na Baraza zima la Mawaziri.

Zitto yupo Strategic, umeweza kuona mwenyewe kwa mfumo huu wa siasa tunaoendanao, kitendo cha Zitto kutoa hoja ya kuwataka wabunge kuachia kura zao ili zifikie asilimia 20 za wabunge wote kimeshtua hata kiti (SPIKA) ambacho kimantiki kimewekwa na CCM, spika amenza mizengw kabla ya kuieleewwa hoja, Spika kama mwanachama wa CCM ambae pia aanpokea maelekezo ya chama chake ana hofu kuu .

Kitendo hiki kimepelekea wana CCM kusutana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Mawaziri (BLM) kujichomoa wenyewe kwa kujiona hawafai tena, jambo ambalo linadhirisha kuwa hata Waziri Mkuu mwenyewe hana sababu za kuendelea kukalia kiti hicho cha uwaziri mkuu kwani ameshindwa, ameshindwa na atashindwa kabisa kuwasimamia mawaziri wake kwa sasa (tukumbuke ni muda mfupi umebaikia kuingia kwenye uchaguzi mkuu na CCM imeshapoteza matumaini kwa wananchi hata kwa maeneo ambayo ilijivunia ni nyumbani kama kule Songea, Mtwara na kwingineko).

Haiiingii akilini tuhuma zikawagusa mawaziri zaidi ya saba na bado kiranja wao Waziri Mkuu akasimama na kujinadi kuwa anao uwezo wa kuendelea kuongoza darasa la Mawaziri waliobakia..Waziri Mkuu hata kama hataondolewa na Umma kupitia Bunge, amepoteza sifa, hafai tena hataweza kuheshimika, wasifu wake umechafuak, sio mwajibikaji, hawezi kuwajibika kwa kipindi kilichobakia. Sio mwajibikaji kwa takwimu, ameshindwa kusimamia mengi, Halmasahuri za Wilaya, Fedha (bajeti inaielewewki na watu wanafuja fedha za umma), Elimu ( kukosekana kwa walimu na thamani mashuleni, kushuka kwa kiwango vya ufaulu, matatizo ya vyuo vikuuu na Bodi za mikopo) kilimo (KILIMO KWAZAN isiyo na tizaj, pembejeo na ruzuku za kilimo, mbolea zisizo na viwango, matatizo ya Bodi ya Pamba, Chai, Korosho, Mkonge, Tumbaku nk); huduma za nishati (maji, umeme hakuna) Maliasili (twiga wanaibiwa, madini yanachotwa kwa manufaa ya wageni). Hayo ni sehemu tu ya mengine mengi.

Ni kweli kuwa Bunge lijalo shughuli kubwa itakayofanyika ni kujadili Bajeti, lakini hoja ikiwasilishwa bado haina maana kuwa hata kama haitaungwa mkono na wabunge wanaotakiwa Kikatiba , lakini itaonyesha dhairi kuwa waziri Mkuu hakubaliki na hii itaweka historia kwa mara nyingine kuwa mawaziri wakuu wote chaguo la Mhe. Kikwete hawakubaliki tukianza na yule aliyejiuzulu kwa hiyari yake Mhe. Lowassa.

Hata hapa tulipofikia kwa kuweza kuwachonganisha wana CCM wakaanza kuvurugana wenyewe kwa wenyewe ni makakti tosha wa kuhesabu ushindi..haijawai kutokea mawaziri wakajipukutisha kwa kiasi hiki kikubwa katika historia ya nchi hii.. Rais hawezi leo kusimama hadharani na kujinadi kuwa Serikali yake imeweza kwa hali hii ambayo mawziri wake wamekiri kwa mioyo yao kuwa wameshindwa. Vyovyote itakavyokuwa, kuna la kujifunza katika hili na binafsi naamini kuwa kwa strategy iliyotumika Bunge limeweza kuonyesha ni jinsi gani linaweza kuiwajibisha Serikali kiufasaha zaidi...

Binafsi naamini kama kweli mawaziri watajiuzulu inavyosemwa itaharibu kwa kiasi hoja ya kutikuwa na imani na waziri mkuu. Think about it!
 
Kaka au Dada (sielewi ipi sahihi) unaejiita MzeeMwanakijiji, ngoja chama chako cha CCK ndio ukipe ushauri huo. Zitto anapeleka Jumatatu na yeye anakijuwa akifanyacho zaidi yako. Ushauri wako hauna mshiko.

lakini zitto si alitoa ultimatum;? kwamba mpaka kufika J3 kama mawaziri waliotajwa na CAG hawajajiuzulu atapeleka hoja bungeni? sasa si wamejiuzulu!
 
Nakubaliana nawe (taking into consideration thread yangu juu ya jambo hili hili). Ila bado nasisitiza kuwa tatizo kuu ni ccm na si individuals, hata kama hakutakuwa na kura ya kutokuwa na imani juu (ya iwe Pinda au aliemteua) bado CHADEMA waitumie fursa hii kuelimisha wananchi juu ya ccm kutokuwa na utashi wa kutatua shida zilizopo kwa wananchi. Proof ndio hii: hawako tayari kuwaajibisha wezi wa fedha za umma! CHADEMA wanahitaji nini tena?

Kweli kabisa maana itakuwa ni point muhimu sana ya kuja kuwaishtaki ccm kwa wananchi mwaka 2015 kwani wananchi wenyewe tumeliona na tunalifuatilia hili suala
 
Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?

Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?

Hapo kila mmoja ana mtazamo wake maana huwezijua anachowaza
 
Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?

Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?

Nia ya upinzani ni MASLAHI YA NCHI KWANZA, kuwaachia waboronge ili kupita kirahisi 2015 ni kukosa uzalendo, Kikizidi kuboronge, ni hela za walipa kodi ndo zinazoliwa.
 
Tuna kama miezi miwili tu kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza; endapo hoja ya kutokuwa na imani itatolewa sasa na kama Spika atakubali kuitisha kikao maalum ndani ya siku 14 (kwani haiwezi kutolewa kwenye kikao cha sasa) manake ni kuwa hoja kama hiyo haiwezi kuletwa ndani ya miezi sita. Ukishapata kura hizo sabini au zaidi basi unapanga kuleta hoja hiyo kwenye kikao kijacho na kuondoa kuzuiwa na muda kufanya hivyo.

Lakini zaidi watu wasije wakachanganya vitu viwili - kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ili hoja iweze kuletwa Bungeni zinahitajika asilimia 20 tu ya wabunge (ndipo namba ya kura 70 inapokuja). Kura 70 HAZIWEZI kumuondoa Waziri Mkuu; zinaweza tu kufanya hoja iletwe Bungeni. Baada ya kuletwa bungeni na wabunge kupiga kura inahitajika asilimia 50+1 kwa Bunge kupitisha Azimio la kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Hii ina maana ili azimio lipitishwe ZINAHITAJIKA kura 178 na siyo 70!

Sasa haitoshi kufanya hoja iletwe Bungeni tu (kwa kura 70) lakini tunataka inapoletwa Bungeni ni kweli kuna uwezekano wa ku-effect the removal of the Prime Minister. Jambo zuri ambalo limetokea ni kuwa kwa mara ya kwanza Watanzania tunazungumzia njia ya kidemokrasia ya kumuondoa Waziri Mkuu. Kwa hili Zitto amethubutisha watu kufikiria uwezekano huo na hili litaingia kwenye historia vizuri kabisa. Lakini pia linafanya watu wazungumzie juu ya madaraka ya Waziri Mkuu kusimamia serikali yanakoma wapi na kama ni mtu sahihi kumwajibisha.

Ikumbukwe pia kuwa hoja ya kumshtaki Rais chini ya article 46 ni RAHISI zaidi kwani nayo inahitaji kura 70 kuweza kuletwa mezani na sababu za kumshtaki Rais Bungeni ni za chini kidogo - mojawapo ni kuwa amedhalilisha ofisi ya Urais! Nimesema mahali pengine kuwa kutokuwa na imani naWaziri Mkuu ni kutokuwa na imani na rais hivi viwili kwa mfumo wetu havitenganishwi. Wote ambao wameunga mkono kwa kutia sahihi kura 70+ ina maana hawana imani na rais hakuna tafsiri nyingine. Kwa vile hili ni kweli ni muhimu basi kwenda moja kwa moja for the "jugular" yaani kuleta mashtaka dhidi ya Rais katika kikao kijacho!

Kwa kuleta mashtaka dhidi ya Rais na yakathibitika basi rais atajiuzulu na Makamu wa Rais atashika madaraka na atapewa nafasi ya kuunda serikali mpya bila kulazimisha uchaguzi mpya. Lakini kama tunataka mabadiliko ya kweli hadi Bungnei (kwa sababu wengine tunaamini matatizo hayako kwa Waziri Mkuu au Rais peke yake bali hadi Bungeni) basi azimio la kumtaka Rais avunje Bunge litolewe ili WOTE (kuanzia Rais hadi wabunge) warudi kwa wananchi ili kupata ridhaa mpya (a new mandate). Tusitake mabadiliko nusu kwani hakuna mapinduzi nusu (there is no half-revolutions)! Kama tunataka kubadilisha TUBADILI KITU CHOTE KIZIMA!

So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!

Inabidi uje bungeni na wewe sasa, kudandia au ku-improvove hoja za watu si vizuri sana na hasa unapoongelea impossibilities...

you have written utopia
 
Du...Siku hizi watu wanapeana staregy katika mitandao ya wazi....... Hizi PR hizi!!!
 
Binafsi naamini kama kweli mawaziri watajiuzulu inavyosemwa itaharibu kwa kiasi hoja ya kutikuwa na imani na waziri mkuu. Think about it!

Hoja ya Zitto na Wabunge wengi ilikuwa ni Mawaziri Waliotuhumiwa katika taarifa za kamati Wajiuzulu, lakini kwa kuwa Bunge halina uwezo wa kuwaondoa Mawaziri hivyo solution pekee ilikuwa ni kuviunjwa baraza zima la Mawaziri kupitia kura ya kutokuwa na imani na kiongozi wao, Waziri Mkuu.

Sasa kama Mawaziri hao waliotakiwa kujiuzulu wameshajiuzulu kabla ya hoja kupelekwa mezani, then hoja ya Zitto itakuwa imeshatekelezwa in advance.
 
Mawazo Bora ndani ya mawazo Bora ni uchakachuaji

nakumbuka tulipokuwa shule, kwenye ile elimu ya sekondari kubwa ya miaka miwili, mkaka mmoja ambaye mara zote alipenda group discussion ambayo ladies wako kibao, yeye alijifanya mtaalam sana wa hesabu za minyororo, na mkipata kipande cha swali na mkakukuruka nalo kwa muda na kupata jibu, yeye huchomoka akajitenga pembeni na kukukuruka nalo zaidi ili tu apate njia nyingine mbadala wa kulifanya swali hilo hata kama njia yake ni ya kubuni ili mradi jibu analijua basi ataungaunga mpaka nae aonekane kidume flan wa mafiga hayo yaliyoitwa mase au mets au 'nyuma ya nyumba' (backhouse). Basi akishajitengenezea njia yake anavamia kwenye group ambapo nyie that time mmeshasolve mafiga kama kumi hivi..utaskia.. 'eheee nimeshapata njia nyingine ya kufanya lile swali'.. basi atawabugudhi mpaka awaonyeshee na sometimes anasahau anarudi kuundaunda jibu anakuja tena.. yaaani kero tu.. hatimae aliruka na Div Zero ukingoni mwa shule..

..

....With all due respect to Mwanakijiji, nasikitika kuwa hiki ndicho nilichokiona kwenye hoja yake hii, na endapo Zitto atadanganyika kuifuata hoja ya Mwanakijiji, then mwisho wa siku ategemee matokeo yake kuwa "zero" kama ilivyotokea kwa rafiki yako, go Zitto go...
 
Mwanakijiji

Ninakubaliana sana na hoja zako lakini hili la kutaka raisi avunje bunge na kuilazimu nchi kuingia kwenye uchaguzi ni kitu kisichowezekana hata siku moja.
Wabunge wa ccm hawawezi kamwe kukubali hoja kama hiyo huku wakitambua vuguvugu la mabadiliko miongoni mwa wananchi kwa sasa, wataona ni bora wamalizie tu miaka yao mitano, kama wataangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 basi iwe hivyo lakini walau watakuwa wamejikusanyia vijisenti vya kundelea namaisha baada ya ubunge.

Kwa kuzingatia hali hiyo, sidhani kama hiyo proposal yako ni ya kuzingatiwa kwa sasa, labda ushauri kitu kingine, najua unaweza kushauri mbinu mbadala. Hivyo basi nadhani ni muhimu zitto ahakikishe anakamilisha saini sabini kwa ujibu wa kanuni na awasilishe hoja yake ofisi ya spika ili mchakato wa hoja hiyo uanze rasmi. Siamini kama wabunge wa ccm wanaweza kupiga kura ya kumtosa waziri mkuu wa serikali yao lakini kisiasa ina impact kubwa sana.

Mkuu uko sawa wasia. Hii process pekee ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ina impact na ujumbe mkubwa kwa serikali. Hata kama haitapita lakini a strong message itakuwa sent kwenye ofisi kuu ya nchi hii na kikao cha Baraza la Mawaziri lazima kitajadili hili suala na watu watatoana kafara tu.
 
mwanakijiji, kama ni macho huenda unayo manne, kama ni masikio nadhani yako 4 pia, ubongo kawaida umegawanyika sehemu kuu tatu lakini wewe sina hofu, wewe ni sehemu sita. Hii inapelekea wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, wengine wakifikiri mbili wewe unafikiri zaidi.
HOJA YA ZITTO KWELI SIO KUPIGA KURA BALI NI KUWASILISHA HOJA BUNGENI.

USHAURI WAKO WAKIUFANYIA KAZI, WATAFANIKIWA

Kumbe huyu mtu ni mlemavu - japo ana ulemavu unaoifaa jamii!
 
Back
Top Bottom