Ninakubalina nawe Mwanakijiji kwa kiasi kikubwa. Lakini pia ninatofautiana nawe kwa sehemu fulani. Labda nitoe hoja zangu kwanza kisha nitaeleza ni kwa namna gani tunatofautiana, na similarities will take care themselves.
Ikumbukwe kuwa kumuwajibisha kiongozi wa nchi kidemokrasia ni kama ni tukio la kipekee. Labda hata hizo fikra hazijawahi kuwepo achilia mbali uthubutu. Hii ndio imepelekea viongozi wengi, hasa katika ngazi ya uwaziri kujifanyia mambo watakavyo, ilimradi tu wana-uswahiba na Rais. Mara kadhaa tumemsikia Pinda akisema Mamlaka yangekuwa yangu ningemuondoa huyo mtu leo. Kwamba yupo mtu juu yake ambaye ni rafiki wa mkosefu huyu na ndiye aliye muweka. Mimi sina jeuri ya kumuwajibisha.
Maana yake ni hii. Watendaji wakuu kama Makatibu wakuu kwa upande mmoja, na Mawaziri kwa upande mwingine, maadam wana-uswahiba na rais, kamwe hawatafiria kuwajibika kwa maslahi ya taifa. Watafanya kazi kwa maslahi yao binafsi au kikundi kidogo cha watu.
Hoja kama hii ya Zitto, kwa kiasi fulani inawakumbusha hawa miungu watu, ikiwa ni pamoja na Rais kuwa kuna uwezekano wa kuwaondoa kama watu watachoshwa kabisa na madudu wanayoyafanya. Hii walau italeta nidhamu na kuongeza ufanisi.
Wakati tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo (ambayo ndiyo ndugu yangu Mwanakijiji unayalenga), tunahitaji pia kuonyesha nini kinawezekana kwa sasa. Lengo letu kuu ni kuwa na taifa bora, lenye kutumia rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi wote. Ikiwa tendo kama hili linaweza kubadilisha mwelelkeo wa watawala, na kuwa na ufanisi, hilo tunalikubali. Ikiwa hakuna mabadiliko, we go for the great change. The good thing is we have all we need for both. Immediate and planned great future change.
Kwahiyo tofauti zetu Mkuu mwanakijiji ni kuwa, kile kidogo kinachowezekana, na kifanyike sasa wakati tunajipanga kufanya makubwa zaidi. Who knows, inawezekana hata hiki kidogo kikalipa!