Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic...

KWA VILE SIKU 14 AU ZAIDI NOTICE, TOA NOTICE JTATU NA IJADILIWE SIKU YA KWANZA YA KIKAO CHA JUNE. sIRIKALI ITAKAA BILA RAHA MUDA WOTE HUO NA PIA MTAPATA MUDA WA KWENDA KUWAELEZA WANANCHI SABABU ZA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI
 
Hapana, kilichofanywa na Zitto ni kufire a "warning shot' na kutuma ujumbe kuwa we can fight to the very end. La maana nikutambua kuwa hii ni vita na hupigani tu alimradi kupigana; unapigana ili kufikia matokeo fulani. Sasa mimi sitaki matokeo ambayo yatarudisha Waziri Mkuu wa CCM, baraza jipya la CCM, na rais wa CCM tutakuwa hatujabadilisha kitu zaidi ya kubadilisha tu upande wa shilingi - thamani yake ni ile ile.

sasa kama lengo ni kumuondoa tu waziri mkuu ili waziri mkuu mwingine wa CCM aje well that fine and dundee lakini kubadilisha tu waziri mkuu kumetusaidia vipi baada ya kuondoka kwa Lowassa? Hivi katika wabunge wote wa CCM leo hii mnafikiria yupo ambaye atakuwa tofauti sana? na kwamba ndani ya wabunge wa CCM linaweza kuundwa baraza tofauti na mabaraza yaliyopita?

Mabadiliko sahihi niyale yatakayoiondoa CCM madarakani au kuipunguzia nguvu yake!
 
M.mwanakijiji nakubaliana sana na mawazo yako,na ifahamike kuwa mawazo haya yanazingatia sheria,nadhani njia iliyopo sasa ni hili la aidha mawaziri wanaohusika kufisidi nchi waondoke kwa maana ya kujiuzuru au wawajibishwe na aliewateua,wakishindwa kufanya wenyewe basi mh.zito atapeleka hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa mujibu wa sheria,ambapo bunge litapiga kura.sasa kilichopo ni aidha zito asubiri bunge lijalo au apeleke jtatu,nadhani njia njema ni bunge lijalo kwa kuwa nao wataendelea kujipanga kwa namna mbalimbali hivyo mwezi juni si mbali na huyu ni kuku wetu hatuhitaji manati kumpata,atarudi bandani nasi tutampata.kimsingi nimeshuhudia viongozi wakiendelea kuchukulia mambo ktk wepesi yaani kujaribu kuwafunga midomo wabunge wa chama chao ambapo hiyo ni hatari zaidi kuliko wangewaacha,kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu haipingiki na nina amini litatimia kwa kuwa hii ni njia ya kidemokrasia ya kuonesha serikali kuwa haturidhiki na utendaji wao.
 
Tuna kama miezi miwili tu kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza; endapo hoja ya kutokuwa na imani itatolewa sasa na kama Spika atakubali kuitisha kikao maalum ndani ya siku 14 (kwani haiwezi kutolewa kwenye kikao cha sasa) manake ni kuwa hoja kama hiyo haiwezi kuletwa ndani ya miezi sita. Ukishapata kura hizo sabini au zaidi basi unapanga kuleta hoja hiyo kwenye kikao kijacho na kuondoa kuzuiwa na muda kufanya hivyo.

Lakini zaidi watu wasije wakachanganya vitu viwili - kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ili hoja iweze kuletwa Bungeni zinahitajika asilimia 20 tu ya wabunge (ndipo namba ya kura 70 inapokuja). Kura 70 HAZIWEZI kumuondoa Waziri Mkuu; zinaweza tu kufanya hoja iletwe Bungeni. Baada ya kuletwa bungeni na wabunge kupiga kura inahitajika asilimia 50+1 kwa Bunge kupitisha Azimio la kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Hii ina maana ili azimio lipitishwe ZINAHITAJIKA kura 178 na siyo 70!

Sasa haitoshi kufanya hoja iletwe Bungeni tu (kwa kura 70) lakini tunataka inapoletwa Bungeni ni kweli kuna uwezekano wa ku-effect the removal of the Prime Minister. Jambo zuri ambalo limetokea ni kuwa kwa mara ya kwanza Watanzania tunazungumzia njia ya kidemokrasia ya kumuondoa Waziri Mkuu. Kwa hili Zitto amethubutisha watu kufikiria uwezekano huo na hili litaingia kwenye historia vizuri kabisa. Lakini pia linafanya watu wazungumzie juu ya madaraka ya Waziri Mkuu kusimamia serikali yanakoma wapi na kama ni mtu sahihi kumwajibisha.

Ikumbukwe pia kuwa hoja ya kumshtaki Rais chini ya article 46 ni RAHISI zaidi kwani nayo inahitaji kura 70 kuweza kuletwa mezani na sababu za kumshtaki Rais Bungeni ni za chini kidogo - mojawapo ni kuwa amedhalilisha ofisi ya Urais! Nimesema mahali pengine kuwa kutokuwa na imani naWaziri Mkuu ni kutokuwa na imani na rais hivi viwili kwa mfumo wetu havitenganishwi. Wote ambao wameunga mkono kwa kutia sahihi kura 70+ ina maana hawana imani na rais hakuna tafsiri nyingine. Kwa vile hili ni kweli ni muhimu basi kwenda moja kwa moja for the "jugular" yaani kuleta mashtaka dhidi ya Rais katika kikao kijacho!

Kwa kuleta mashtaka dhidi ya Rais na yakathibitika basi rais atajiuzulu na Makamu wa Rais atashika madaraka na atapewa nafasi ya kuunda serikali mpya bila kulazimisha uchaguzi mpya. Lakini kama tunataka mabadiliko ya kweli hadi Bungnei (kwa sababu wengine tunaamini matatizo hayako kwa Waziri Mkuu au Rais peke yake bali hadi Bungeni) basi azimio la kumtaka Rais avunje Bunge litolewe ili WOTE (kuanzia Rais hadi wabunge) warudi kwa wananchi ili kupata ridhaa mpya (a new mandate). Tusitake mabadiliko nusu kwani hakuna mapinduzi nusu (there is no half-revolutions)! Kama tunataka kubadilisha TUBADILI KITU CHOTE KIZIMA!

So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!
Hili umetoa wapi? Thibitisha....
 
mzee mm, ok nakubaliana na mawazo yako, lakini kwa vyovyote vile, mawazo yako ya mabadilliko yanategemea uamuzi wa ccm yenyewe!!!yaani aidha wabunge waamue kuvote kutokuwa na imani na raisi au, raisi aamue kuvunja serikali....none of these itaweza kutekelezwa na ccm!! so ni mbaya kwamba tunategemea mabadiliko, au tunayataka, lakini utaratibu wa kisheria hauruhusu, unless ccm wenyewe waamue, au tuvunje sheria kwa kuandamana na kufanya vurugu nchi nzima, na hapo watatuua kwa risasi, kutugawanya, untill utajikuta peke yako au mko watano na hakuna badiliko mliloleta
 
Lakini vile vile CDM wanaweza kuitisha maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuhusiana na ufujaji na ubadhirifu wa mali za umma; hii ndio njia yenye nguvu zaidi kwani inarudisha nguvu kwa wananchi na siyo wabunge. Badala ya kuandamana tu hivi hivi wanaitisha maandamano makubwa ya kusema kuwa wananchi "wamechoka" na ikibidi ni maandamano yasiyokoma hadi mawaziri au waziri mkuu ajiuzulu!
 
Kwa mazingira yetu mie nashauri tujipime na PM kwanza.

Hata kama akibadilishwa tukapewa Lusinde inatosha kuonyesha kwamba inawezekana.
Siku za mbele we can refer hilo kumng'oa mkulu bila kujali atakuwa wa chama gani.

By the way kura zitakuwa za siri, bora kushindwa huku ukijaribu!
 
Lakini vile vile CDM wanaweza kuitisha maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuhusiana na ufujaji na ubadhirifu wa mali za umma; hii ndio njia yenye nguvu zaidi kwani inarudisha nguvu kwa wananchi na siyo wabunge. Badala ya kuandamana tu hivi hivi wanaitisha maandamano makubwa ya kusema kuwa wananchi "wamechoka" na ikibidi ni maandamano yasiyokoma hadi mawaziri au waziri mkuu ajiuzulu!
nilisikia mbowe jana anatoa wazo kama hilo, anyway labda tujaribu hili, tushinikize serikali ijiuzulu...lakini wasiwasi wangu ni kuwa, baada ya maandamano na kuanguka kwa ccm, nchi itaingia katika mgogoro wa kisiasa, hasa ukizingatia kuwa raisi amechaguliwa (kama tunavyoaminishwa)!!!! na maandamano yatategemea support ya 'wakubwa' wa nje...so labda cdm waangalie hayo kwanza, maana maandamano yana cost zake...zisiwe incurred for nothing!!
 
Lakini vile vile CDM wanaweza kuitisha maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuhusiana na ufujaji na ubadhirifu wa mali za umma; hii ndio njia yenye nguvu zaidi kwani inarudisha nguvu kwa wananchi na siyo wabunge. Badala ya kuandamana tu hivi hivi wanaitisha maandamano makubwa ya kusema kuwa wananchi "wamechoka" na ikibidi ni maandamano yasiyokoma hadi mawaziri au waziri mkuu ajiuzulu!

Mwanakijiji,

..hata mimi na-prefer option ya kuwashtaki CCM kwa wananchi kutokana na madudu haya.

..sidhani kama CCM wanaweza kuchukua hatua kutokana na shinikizo la CDM ndani ya bunge.

..kinachoweza kuwashtua CCM ni pale tu wananchi watakapoanza kuwakataa waziwazi kama walivyofanya wananchi wa Arumeru.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Lakini vile vile CDM wanaweza kuitisha maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuhusiana na ufujaji na ubadhirifu wa mali za umma; hii ndio njia yenye nguvu zaidi kwani inarudisha nguvu kwa wananchi na siyo wabunge. Badala ya kuandamana tu hivi hivi wanaitisha maandamano makubwa ya kusema kuwa wananchi "wamechoka" na ikibidi ni maandamano yasiyokoma hadi mawaziri au waziri mkuu ajiuzulu!

Hapa ndio nadhan withdrawal ya hoja ya Zitto si ushauri mwafaka.

Sahihi zilizopatikana ni kwa hoja against PM kubadili mwelekeo juu kwa juu itamaanisha tupate ridhaa mpya ya waliotia saini which may equally be difficult.

Tuanza na Pinda, no turning back
 
Mkuu MMKJ,
Kila mtu anajua kuwa katika mazingira ya sasa kisiasa wanaccm hawatakuwa tayari kumpigia kura waziri mkuu kuwa hawana imani naye, na pia kwa rais kama kutakuwa na hoja ya aina hiyo. Utamu wa hoja ya Mh Zitto kwa sasa ni kuwa wabunge wamehubiri sana ufisadi ulioripotiwa na CAG na iko wazi kuwa serikali ni ya kifisadi. Wakati wa kupiga kura dhidi ya waziri mkuu watakaomuunga mkono Zitto wataonekana mashujaa mbele ya umma na watakaoimpinga wataonekana wasaliti kwa wananchi. Kwa mazingira ya sasa ya kisiasa na uelewa wa wananchi inatakiwa wabunge wote wanafiki wajulikane na siku zao tuanze kuzihesabu sambamba na chama chao. Kwa bunge la sasa haiwezekani kumng'oa waziri mkuu but hoja ya kumng'oa ni strategy nzuri mno kupata political gain
 
Kwa niaba ya JF na wanamageuzi na mabadiliko ya kweli naunga Mkono hoja Kubadili Kitu Chote.
 
CDM wanachukua nchi kama wanasukuma mlevi vile............so funny
 
kimsingi nakubaliana nawe Mwanakijiji ila sikubaliani na conclusion yako. Sababu zangu ni

Kwanza, kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa vyovyote vile ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi. nafuu iliyopo tu ni kuwa kwa sasa rais ataendelea kuwa madarakani. ila raisi huyu atakayeendelea kubaki madarakani atakuwa raisi tofauti kabisa na aliyekuwepo kabla ya kura ya kutokuw ana imani ya waziri mkuu wake aliyepita. lazima atajuajkuwa sasa hali ni tofauti sana na asipoangalia safari ijayo dhahma itahamia kwake. na hilo ndo somo la leo, kwa kuanzia.

pili, kwanza kura ya namna hii itamuongezea nguvu sana waziri mkuu mpya atakayekuja. huyu wa sasa anaonekana alikuwa tu political expediency of the time pale EL apojiuzulu. so hana mashiko na hana nguvu za kusimamia kiukweli shughuli za serikali. ndio maana hana la kujibu ktk mazingira haya manake yuko sawa tu na hawa mawaziri watuhumiwa mbele ya mkuu wao wa kazi. lakini baada ya somo la leo, PM ajaye lazima atakuwa mkali manake kitumbua chake kinaweza potea wakati wowote kupitia bungeni na yeye kugeuka kichekesho. si ajabu kwa sasa Mhe Pinda anaonekana kichekesho tu machoni mwa jamii yetu, manake hana akifanyacho wala awezacho. Next PM hatokubali kuwekwa kwenye hali kama hiyo. akiona anashindwa kuwawajibisha mawaziri wake kwa vile wana kinga ya Raisi, yeye mwenyewe atakuwa wa kwanza kutangaza kujiuzulu, na kumwachia Rais nchi yake. Kwa hili Rais nae ataonekana hafai na atatolewa kwa urahisi zaidi.

tatu, baada ya kutengeneza utamaduni wa kidemokrasia wa kuwaondoa wakuu wa nchi kupitia bunge, itawajaza nguvu wabunge kuwa kumbe inawezekana kuung'oa mbuyu na mzizi wa fitina. na ile dhana ya kung'ang'ania party loyalty itakuwa haipo tena. na wale waoga watapata ujasiri. tunahitaji hiki kitu.

nne, kwa hali ilivyo, Raisi atavunja baraza la mawaziri very soon. atakuwa mtu wa ajabu sana akiendelea kumsubiri asha rose come june, kama tulivyosikia. anapambana na tide ya muda na inazidi kula kwake. akiamua kulivunja baraza la mawaziri ni wazi kuwa hoja ya zitto itakuwa imepitwa na wakati. kumbuka kuna faida nyingi sana za kisiasa kuona mwisho wa hoja ya zitto ndani ya bunge kuliko kupigwa chenga ya mwili na JK.

Hitimisho langu ni kuwa Zitto aendelee na hoja yake ktk kikao hiki au kingine chochote cha karibuni. there is everything to gain and nothing to lose! Alluta Continua!
 
Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?

Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?
Ndugu yangu hapo alipofikia Mhe Zito ni pazuri kwa maana hawa wanamaghamba hawawezi kujitia kitanzi kwa namna yoyote ile!!! Hivyo CHADEMA ikishindikana wanayo sababu ya kuwashitaki kwa wananchi, wahukumiwe na umma!! A wonderful strategy of liberation!!!VIVA PEOPLES POWER VIVA UKOMBOZI WA MTANZANIA!!!!!!

 
Ndugu yangu hapo alipofikia Mhe Zito ni pazuri kwa maana hawa wanamaghamba hawawezi kujitia kitanzi kwa namna yoyote ile!!! Hivyo CHADEMA ikishindikana wanayo sababu ya kuwashitaki kwa wananchi, wahukumiwe na umma!! A wonderful strategy of liberation!!!VIVA PEOPLES POWER VIVA UKOMBOZI WA MTANZANIA!!!!!!

Ana sahihi ngapi mpaka sasa??
 
Back
Top Bottom