Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 20, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tuna kama miezi miwili tu kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza; endapo hoja ya kutokuwa na imani itatolewa sasa na kama Spika atakubali kuitisha kikao maalum ndani ya siku 14 (kwani haiwezi kutolewa kwenye kikao cha sasa) manake ni kuwa hoja kama hiyo haiwezi kuletwa ndani ya miezi sita. Ukishapata kura hizo sabini au zaidi basi unapanga kuleta hoja hiyo kwenye kikao kijacho na kuondoa kuzuiwa na muda kufanya hivyo.

  Lakini zaidi watu wasije wakachanganya vitu viwili - kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ili hoja iweze kuletwa Bungeni zinahitajika asilimia 20 tu ya wabunge (ndipo namba ya kura 70 inapokuja). Kura 70 HAZIWEZI kumuondoa Waziri Mkuu; zinaweza tu kufanya hoja iletwe Bungeni. Baada ya kuletwa bungeni na wabunge kupiga kura inahitajika asilimia 50+1 kwa Bunge kupitisha Azimio la kutokuwa na imani na waziri mkuu.

  Hii ina maana ili azimio lipitishwe ZINAHITAJIKA kura 178 na siyo 70!

  Sasa haitoshi kufanya hoja iletwe Bungeni tu (kwa kura 70) lakini tunataka inapoletwa Bungeni ni kweli kuna uwezekano wa ku-effect the removal of the Prime Minister. Jambo zuri ambalo limetokea ni kuwa kwa mara ya kwanza Watanzania tunazungumzia njia ya kidemokrasia ya kumuondoa Waziri Mkuu. Kwa hili Zitto amethubutisha watu kufikiria uwezekano huo na hili litaingia kwenye historia vizuri kabisa. Lakini pia linafanya watu wazungumzie juu ya madaraka ya Waziri Mkuu kusimamia serikali yanakoma wapi na kama ni mtu sahihi kumwajibisha.

  Ikumbukwe pia kuwa hoja ya kumshtaki Rais chini ya article 46 ni RAHISI zaidi kwani nayo inahitaji kura 70 kuweza kuletwa mezani na sababu za kumshtaki Rais Bungeni ni za chini kidogo - mojawapo ni kuwa amedhalilisha ofisi ya Urais! Nimesema mahali pengine kuwa kutokuwa na imani naWaziri Mkuu ni kutokuwa na imani na rais hivi viwili kwa mfumo wetu havitenganishwi. Wote ambao wameunga mkono kwa kutia sahihi kura 70+ ina maana hawana imani na rais hakuna tafsiri nyingine. Kwa vile hili ni kweli ni muhimu basi kwenda moja kwa moja for the "jugular" yaani kuleta mashtaka dhidi ya Rais katika kikao kijacho!

  Kwa kuleta mashtaka dhidi ya Rais na yakathibitika basi rais atajiuzulu na Makamu wa Rais atashika madaraka na atapewa nafasi ya kuunda serikali mpya bila kulazimisha uchaguzi mpya. Lakini kama tunataka mabadiliko ya kweli hadi Bungnei (kwa sababu wengine tunaamini matatizo hayako kwa Waziri Mkuu au Rais peke yake bali hadi Bungeni) basi azimio la kumtaka Rais avunje Bunge litolewe ili WOTE (kuanzia Rais hadi wabunge) warudi kwa wananchi ili kupata ridhaa mpya (a new mandate). Tusitake mabadiliko nusu kwani hakuna mapinduzi nusu (there is no half-revolutions)! Kama tunataka kubadilisha TUBADILI KITU CHOTE KIZIMA!

  So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!
   
 2. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  TUBADILI KITU CHOTE KIZIMA! - naunga mkono hoja asilimia 100

  Lets remove the source - the big guy himself! - nashauri tuanze kuandaa mashtaka ya kumshtakia - tukusanye makosa yake!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji

  Ninakubaliana sana na hoja zako lakini hili la kutaka raisi avunje bunge na kuilazimu nchi kuingia kwenye uchaguzi ni kitu kisichowezekana hata siku moja.
  Wabunge wa ccm hawawezi kamwe kukubali hoja kama hiyo huku wakitambua vuguvugu la mabadiliko miongoni mwa wananchi kwa sasa, wataona ni bora wamalizie tu miaka yao mitano, kama wataangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 basi iwe hivyo lakini walau watakuwa wamejikusanyia vijisenti vya kundelea namaisha baada ya ubunge.

  Kwa kuzingatia hali hiyo, sidhani kama hiyo proposal yako ni ya kuzingatiwa kwa sasa, labda ushauri kitu kingine, najua unaweza kushauri mbinu mbadala. Hivyo basi nadhani ni muhimu zitto ahakikishe anakamilisha saini sabini kwa ujibu wa kanuni na awasilishe hoja yake ofisi ya spika ili mchakato wa hoja hiyo uanze rasmi. Siamini kama wabunge wa ccm wanaweza kupiga kura ya kumtosa waziri mkuu wa serikali yao lakini kisiasa ina impact kubwa sana.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Natafakari. Nakuja manake simu imeishiwa charge
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe (taking into consideration thread yangu juu ya jambo hili hili). Ila bado nasisitiza kuwa tatizo kuu ni ccm na si individuals, hata kama hakutakuwa na kura ya kutokuwa na imani juu (ya iwe Pinda au aliemteua) bado CHADEMA waitumie fursa hii kuelimisha wananchi juu ya ccm kutokuwa na utashi wa kutatua shida zilizopo kwa wananchi. Proof ndio hii: hawako tayari kuwaajibisha wezi wa fedha za umma! CHADEMA wanahitaji nini tena?
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Good point.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kwa vile imebaki siku 4 napendekeza hivyo, lakini la msingi apate hizo sahihi 70 akomae nazo hadi bunge lijalo!
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?

  Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
  1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
  2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?
   
 9. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji nimekukubali watahangaika pa kutokea watashindwa hata hapa tu ni fundisho tosha kwa magamba.
   
 10. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Ninavyomjua mkuu wa Kaya kabla ya hicho kikao atabadilisha baraza la Mawaziri na Pinda ataamua kujiuzulu kwa sababu za kiafya...

  Nashauri kama akifanya hivyo waamie kwa Spika.., na yeye ni wa kupiga chini.., (Hafai Kabisa), Hopefully tungeweza kumuondoa mkuu wa Kaya (lakini this is not possible.., not in Africa, not with these wapenda Posho), Ila spika anaweza kuondoka kutokana na makundi ya CCM)
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Namba moja mkuu ndio sahihi...na kwa staili hii katu hatutafika mahala. Kwa bahati mbaya hata wale wasuo kwenye mfumo wa vyama nao wanafurahia staili badala ya kufurahia staili yenye maslahi kwa taifa ambayo ni hiyo namba 2 ingawaje haimaanishi ni kuifanya CCM iendelee kushika hatamu!
   
 12. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Mabadiliko hayawezi kuanzia kwa PM pekee.Huyu kama mshauri na msimamizi mkuu wa serikali bungeni ina maana lolote litakaloamriwa hapo ni la serikali nzima.Kama ni kuachia Pinda eti kwa sababu ya kutowajibika kwake basi tatizo hilo huanzia kwa rais mwenyewe.Yeye naye anaona lakini huwa ni mvivu wa kutoa maamuzi mapema.Suala la kina Mponda na Mkulo na wengine hilo halikuhitaji mijadala.Kumbukeni wakati wa mgomo wa madaktari huyo Mponda na mwenezake walipolazimishwa kujiuzulu waligoma na Rais pia kagoma kumwondoa kwa kumwona hana hatia.Serilkali nzima imeoza.
   
 13. D

  Don The Great Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Hili naliunga mkono,bunge lijalo ndio hii hoja iwe presented.It is a good start kwa muheshimiwa Zitto.Something is better than nothing.
   
 14. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu sahihi zimeshatosha,zipo 73
   
 15. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama huamini hilo hata kumwondoa Pinda ni ndoto ama hasithi za Pwagu na Pwaguzi
   
 16. T

  Tenths Senior Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mh Zitto usife moyo, remember no one is 100% perfect, chukua orodha yako na andaa hoja tayari kutimiza adhma yetu kwa bunge lijalo. Kwa Wah. Deo na Lugora ujasiri wenu umeonekana kwa wtz na kwa hakika umma wa wtz upo pamoja nanyi.
   
 17. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaah kumbe ndo maana huyu bibi kiroboto kapinga!kwa maelezo hayo Mwanakijiji ulioyanisha hapo juu inatosha dhahili kuzuia kupiga hiyo kura,CCM ni wajinga
   
 18. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  siamini kama ccm na wabunge wake wanaweza kumpigia kura waziri mkuu ya kutokuwa na imani naye (vote of no confidence)achilia mbali raisi wao, na kama unavyojua raisi wako naye hawezi kuvunja bunge...hana uwezo wala maamuzi hayo, atavunjaje ili uchaguzi urudiwe wakati inajulikana kuwa hawezi kurudi pale magogoni? si bora afabye liende?
  then hii ya kuvunja bunge huwa nu kama timing, especiaally kama chama tawala hakina wabunge wengi lakini kinakubalika mtaani...so ikitokea risk ya vote of no confidence, maybe kwa sababy za kisisasa au kishabiki...raisi kwa kujua kuwa anakubalika mtaani, anaweza kuvunja bunge...
   
 19. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Babu alipofika miaka 100 hakuacha kulamba mfupa wa kuku japo hakuweza kutafuna. Ukimrukia footballer kumkanyaga utahukumiwa kwa bad intent.. hata kama hukumpata. Zitto ameonyesha nia ya kumuondoa waziri mkuu/rais asiyefaa hata kama haingewezekana kupata 70 vote and later percent 50+1; CCM na Serikali yake kama siyo sikio la kufa watajifunza kutenda kwa busara siku zijazo
   
 20. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mmmh hili ni gumu saana kwa chama cha magamba! kwa sasa jambo ambalo wanaweza ni kubadilisha kikosi cha mashambulizi, maana wengine wamesign hoja ya zitto ili nao wapate ulaji!
   
Loading...