Zitto: Sitagombea uongozi CHADEMA

Zitto: Sitagombea uongozi CHADEMA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.

Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.

“Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.


Chanzo: Gazeti la Nipashe
Simwamini sana huyu dogo. Akiwa India aliwahi kudai hanampango wa kugombea urais na kusisitiza hata katiba haimruhusu. Juzi kayala matapishi yake akidai anautaka urais. Tusubiri tuone
 
Wanaowasiliana naye wampe ushauri. Azungumze vitu vizito kama jina lake. Kwanini anajuzungumzia yeye tuuuuuuuu. Na tena wakati huuuuuuuuuuu !!! Hapo alipo tayari ni Kiongozi kwanini anacheza na manenoooooo !!! Mara nataka kuwa Rais mara nataka kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CDM !!! Anahangaika na nini???
Mara anataka kuwa lecturer.
 
Kama walivyosema wachangiaji wengine, sasa hivi tumeelekeza macho na masikio yetu Arumeru mashariki hadi tarehe 01.04.2012, sasa baada ya hapo tutaweza kuanza kuulizana nani atagombea na nani hatogombea, na sababu za kugombea/kutogombea.
 
Bravo sana kama nikwl koz apo utaonesha kuwa we ni realy state man na ucwasikilize ambao awa kuelewi unacho kisema na kudakia upande wapl bila kukujaji kiwakinifuzaid
 
zito ni kipenzi chetu
wana chadema, ana
mawazo mazuri
tuache maneno
maneno yasiyo na tija
 
geita labda kamuachia ben saanane.ni muda nasikia yupo huko na alipost picha huku

Mmeanzisha thread kule tangu jana na cha moto mmekiona bado una kiwewe.Focus kwenye thread za maana acha mawenge na majungu !
 
Exactly mkuu, walianza kumpima Mbowe wameona maji marefu
Maji marefu yalitokana na kuzuiwa Zitto asigombee.,Sio kwamba Mbowe na maji marefu..Ila subirini safari hii "nahisi" kamanda John Magale Shibuda atagombea uenyekiti..
 
Hapo sasa ameshaelewa kuwa Watu hawaombi kuchaguliwa, bali Mtu mwenye uwezo huombwa na Watu kugombea kwa maslahi ya wengi
 
na wewe unamuunga mkono?acha ujinga wewe
Wewe ndio uache ujinga EMT kumuunga mkono au kutomuunga mkono ni haki yake ya kuchagua na uhuru wake. Mimi simwamini Zito kuwa anasifa za kuwa Rais lakini nafikri ana haki ya kugombea. Alishasema wanachama na chama chake wakiamua ndipo atakuwa mgombea. Hiyo ni ambition ila sisi ndio tutajua anafaa au hafai kugombea urais lakini ni haki yake ya kidemokrasia.
Huu unazi wa kutotaka mwingine kuwa na ndoto za kuwa kiongozi wa CDM au kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia CDM utaipa CDM sura mbaya kuliko tunavodhani.
Inatakiwa watu waweke taratibu nzuri za kupata viongozi kisha hizo taratibu ndizo zitakazochuja nani anafaa nafasi gani katika uongozi wa chama au kugombea vyeo vya siasa kuliko kuwaamini watu. Mimi namwamini Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika na Zito lakini najua ni binadamu hawa tusiwafanye Miungu watu.
Hili tatizo la kuamini watu na kutotaka wengine wasogelee uongozi ndilo linalofanya viongozi wang'ang'anie kuwa madarakani hasa wakishapata uongozi wa dola kwa kuwa wanajua kuna wajinga wanaowaona Miungu watu. Wanaojifanya wanazi ndio wanaoua vyama.
 
Alishawahi kunukuliwa kuwa hatagombea ubunge tena 2010. Gafla akaja kivikine. anataka kugombea majimbo matano tofauti.. HUYU NDIO ZITTO KABWE. Haitanishangaza akibadili na akisema anagombea u wenyekiti
 
Maji marefu yalitokana na kuzuiwa Zitto asigombee.,Sio kwamba Mbowe na maji marefu..Ila subirini safari hii "nahisi" kamanda John Magale Shibuda atagombea uenyekiti..
Alizuiwa na nani asigombee.
 
Ben Saanane huyu Masalia ya Zitto yaliyopukutishwa CHADEMA?.........Yaani mtu ambaye hana sifa za kuwa kiongozi kwenye Baraza la vijana atapata wapi sifa za kuwa kiongozi wa chama? hapa ndipo ninapomkumbuka Makamba Sr visisimizi kama hivi alikuwa anaviponda kwa nyundo nzito.

Imeandikwa....Ben Saa 8 anajitahidi kupoteza Muda wake.
 
acho sio baadaye anaamuka na kupalulana na wakuu wake waliomkuza.
 
mkuu hilo kundi haliaminiki.hapo kuna hesabu kali sana mwana.chadema watimueni tu hao

may be anataka amwachie Nafasi ya kugombea uwenyekiti BENARD SANANE. bkoz we cant know

It's a vengeful decree for sure designed by maniacal undemocratic coward characters out there not only to silence freedom of expression and of the youths but also to silence radical movement underway......

Unataka niseme unachotaka kusikia.Ok,Let my signature below,confirm your doubts.It's very clear and loud !
 
Back
Top Bottom