Ruppy karenston
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 412
- 73
Zitto ana mbwembwe aiseee.
Sikatai inawezekana, lakini ninavyofahamu mimi if you want to win a game you have to be involved, you can't play cards by looking through the window, kama ataamua kuwa nje ya ulingo sijui ataweza vipi.It could be the other way too. Labda hataki tena kugombea ili nae aunde informal timu yake nje ya uongozi ujao?
Tatizo Matola uandishi wako wa shule za kata haujifichi hata ukitumia ID mia, mnatakuna humu JF mnafanya JF sehemu ya kutolea matusi yenu Mods kuweni makini na hii ID ni muendelezo wa makusudi kuichafua JF kwa Multiple ID's
Mnatakiwa kumzoeya, alishatangaza kugombea ubunge kwenye majimbo matano mwaka 2010......Zitto ana mbwembwe aiseee.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama, alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
Naona umeamka nazo kichwani..thread imepostiwa Today 09:58 ikarudiwa Today 10:22(full doc). Post yako imekuja 15min baada ya habari nzima kuwa hewani, wewe umepost Today 10:37, sioni unacholalamika, nafikiri ni frustrations fulani.ETM hebu kuwa realistic hata wewe. Ukisoma post yake ya pili imejieleza vizuri kwa kifupi. Hiyo ndiyo ilistahili kuwa post ya kwanza. Si vizuri kuchukulia mistari miwili kubeba kichwa cha habari. Tuendelee na mjadala.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Gazeti la Nipashe.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
"Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Uvivu wa kusoma na kuelewa. Umesoma hadi mwisho na kuelewa? Acha kukurupuka.
Karudie kusoma post yangu ya mwanzo.
Acha utata basi kama una full Info si uziweke hapa? unafikiri wote tupo town?Mpuuzi ni wewe uliyeleta habari nusunusu, kama unashindwa kufupisha habari ni bora usilete habari kulingana na hisia zako. Hebu karudie kusoma habari yote then ujiangalie mapungufu yako.
Aisee una akili sana, ila sijui sheria za usajili wa mitandao zinasemaje, Mtandao unaweza kufungiwa au ni bann tu hasa kwa wale wanaoshambulia CHADEMA?SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS
Tafadhali jiepushe na mambo yafuatayo:
1. Kumvunjia heshima, kumkejeli, kumtukana, mjumbe yeyote.
2. Kuleta katika JAMII FORUMS maelezo yenye maudhui mabaya, au kuweza kuleta maudhi yoyote kwa wajumbe ama kwa wingi wake, ukubwa wake, au mfumo wake.
3. Kuleta makala au kuendeleza mijadala yenye kuleta ugomvi, uchochezi na yenye muelekeo wa kutengenishana badala ya kuungana miongoni mwa wajumbe wa JAMII FORUMS na Watanzania wote kwa ujumla.
4. Kuleta maongezi binafsi baina ya mwanachama na mwanachama (waliojisajili) waliyoongea kwa kuaminiana kutoka katika Private Messages (PM) au barua pepe (Emails) na kuyaanika hadharani kwa nia ya kuchafuana.
5. Kusambaza kwa makusudi au kwa uzembe barua zenye virusi vya kompyuta.
6. Kutoa maelezo au shutuma dhidi ya mwanachama mwenzako, kiongozi wa au watu wenye hadhi kijamii bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwa lengo la kuchafua rekodi safi ya mhusika kijamii.
7. Ni sharti kwa kila mwanachama kutoa maelezo au mchango wake kwa uwazi na ukweli na kutomuogopa yeyote wala kumpendelea yeyote bali kuweka mbele maslahi ya taifa.
8. Kila mwanachama yupo huru kutoa maoni yake mradi yaliyotajwa hapo juu yanazingatiwa.
Duh! Nami najiweka pembeni.Big up Prezdaaaaaaaaaaaaa, jiweke pembeni na makundi ndani ya chadema
Ebwanae , kumbe uko mbwinde wakati siku zote unajidai hapa JF kuwa kuko Dar, kaz kweli kweli. Usije ukajisahau tena siku nyingine ukatwambia uko kwenye tukio fulani linaloendelea mjini manake ndo zako hizo..Acha utata basi kama una full Info si uziweke hapa? unafikiri wote tupo town?
Mnatakiwa kumzoeya, alishatangaza kugombea ubunge kwenye majimbo matano mwaka 2010......
Mimi Nilisikia anagombea Geita!....huyu jamaa sasa ndio naanza kumuelewa kumbe anatamani sana ile mirahaba ya madini!..Halafu si alikuwa anaumwa kipanda uso hivi hiki akina madhara yoyote kwa akili za binadamu?nilisikia la kinondoni kumbe kuna mengine?anatakiwa aangaliwe kwa ukaribu sana