Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
Naam. Hatimaye amemwaga na mboga kabisa..ametangaza kuwa atagombea urais 2015..sasa nimeshaamini anatumiwa.
sijawahi kuona mwanasiasa aliye poteza mwelekeo haraka kama huyu dogo wa kitusi. let us wait and see his down fall politically.
 
Ingawa ni haki yake kikatiba kugombea urais, Zitto Kabwe anatia shaka kuanza kutangaza azma ya kugombea urais kupitia CHADEMA hata kabla ya wakati kuwadia. Je ni halali kuzungumzia mbio za urais kabla ya muda muafaka? Je Zitto anafanya hivyo makusudi akijua fiki kauli yake italeta mgawanyiko chamani na hivyo kukidhoofisha? Je ni kweli kuwa Zitto anautaka urais au ndiyo anaanza kazi yake aliyopewa na akina Koka wa Uhasama wa Taifa na CCM?
Haya hapa maneno ya Zitto mwenyewe
“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
 
Sarakasi zake, ana haki lakini kuna mechanism inayoweza ku-deal na kitu kama hicho. Zito si presidential material, hana personality hiyo, leave alone personality ya uwaziri. So good luck for him.
 
Kuna ubaya gani lakini mbona nilichoelewa ni kwamba Wazee wang'atuke waachie vijana. Ebu jiulize wewe mtu alikuwepo madarakani toka tupate Uhuru ina maana huyu alikuwa kijana wa miaka 18 kuendelea, leo hii miaka 50 baadaye bado anataka kuwa madarakani... Come on now ukishafika miaka 70 kuwa mlezi wa chama, pilka pilka hutaziweza, kubali kuitwa babu waachie wengine waiendeleze familia.
naona watusi mmekuwa wengi. huyu zitto anatumiwa.akitaka kujua kuwa yeye siyo maarufu atoke ndani ya chadema aende ccm aone atakavyo puuzwa .
 
Mods,

Tafadhali msiiunganishe hii na ile ya Mohamed Mtoi ili kuepusha mkanganyiko kwa wasomaji. Hili ni tamko la Jana alilotoa huko Kigoma na ile ya Mtoi ni ya Mwezi Machi. Tujadili hili jipya kwa sasa. Naileta Habari nzima kama ilivyoandikwa na Gazeti la Mwananchi Leo Ijumaa

Zitto: Ubunge sasa basi

rank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.

Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.

Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.

“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.

“Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.”

Atangaza kugombea urais

Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto

Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46.

Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.

“Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.

Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.

MY TAKE:

Hivi ni wakati muafaka kutangaza hii kitu sasa? Mbona simuoni Zitto kushiriki kikamilifu ujenzi wa chama kupitia M4C lakini katika urais anakuwa wa kwanza??
 
Huyu dogo naona sasa analewa sifa. Wakati wenzake wakipambana kukijenga chama yeye anapambana kujijenga binafsi kupitia migongo ya wenzake. Natamani Mwahalisi lingekuwepo nafikiri lingeweza kumsawazisha yeye na aliyemtuma. Nahisi kama ni pandikizi. Nakubaliana na mtoa hoja hii kuwa simuoni Zitto akikijenga chama, sioni akisifu chama bali zaidi naona majigambo binafsi yasiyo na tija. Wakati yeye akikosa usingizi kwa ajiri ya urais wa 2015, sijasikia hata mwenzake mmoja akiwaza HATA ubunge kwa mwaka huo. Wote wamefocus kukijenga chama kitaifa kuanzia mashinani. Ngoja tuone mwisho wake ukoje. Ila kama ataendelea hivi, namtabiria anguko kubwa la kisiasa.
 
Nakubaliana nawe kabisa Mkuu

Kwakweli CDM inabidi wafanye kitu kwa Zitto, sijui kitu gani lakini ili kuwe shwari mwaka 2015 na lengo la kuchukua dola lifikiwe, Zitto ni kikwazo kikubwa.

Ana Uhuru wa kugombea urais anaoutaka kama mtazanzania, lakini hiki kipindi ni cha kujenga chama zaidi na sio kujijenga kibinafsi.
 
Lengo lake asipopitishwa anataka wenye mawazo finyu waconclude kuwa wamemkatalia kwakuwa ni muislamu na ni muha (kanda fulani).

Kila siku nazidi kudelete kabisa. Lkn ndio tabia zao waswahili wa Kigoma-Ujiji.
 
afanywe kama chacha wangwe
 
Hapa zitto,pale slaa huku mbowe,huko shibuda mbona patamu apo.
 
Ni haki yake kikatiba,mwacheni aseme na atimize azma yake na dhamira yake
 
Kuna ubaya gani lakini mbona nilichoelewa ni kwamba Wazee wang'atuke waachie vijana. Ebu jiulize wewe mtu alikuwepo madarakani toka tupate Uhuru ina maana huyu alikuwa kijana wa miaka 18 kuendelea, leo hii miaka 50 baadaye bado anataka kuwa madarakani... Come on now ukishafika miaka 70 kuwa mlezi wa chama, pilka pilka hutaziweza, kubali kuitwa babu waachie wengine waiendeleze familia.

Huo ni ubaguzi, kuweni making kuna sheria zinazuia ubaguzi.
Maneno hayo yakitoka kwa kijana wangu wa kijiweni ntaelewa lakini kwa mtu anayejigamba ni rahisi ajaye....mmmh mashaka sana. Hats hivyo kila la kheri.
 
Lengo lake asipopitishwa anataka wenye mawazo finyu waconclude kuwa wamemkatalia kwakuwa ni muislamu na ni muha (kanda fulani).

Kila siku nazidi kudelete kabisa. Lkn ndio tabia zao waswahili wa Kigoma-Ujiji.

Aisee nimelipenda hili kwenye RED, hebu ngoja nilifanyie kazi inawezekana tukawa tunamlaumu bure kumbe asili yake
 
Mimi nashangaa watu wanaomshambulia Zitto kwa kutangaza nia yake. Zitto kama mtanzania na mwanachadema anapaswa kuongelea yale aliyonayo moyoni mwake, kosa lake lipo wapi?yeye anataka kugombea urais wanachama, wananchi na chama chake ndiyo wataamua nani agombee 2015. Kama ataweza/ameweza kupata ridhaa ya chama tatizo litakuwa wapi? Jambo la msingi tuwe na mfumo huru ambao hauna mizingwe kuhusu mgombea urais 2015 kupitia chadema maana hivi sasa chadema imeanza kukubalika-Chadema ni kama binti ambaye amependeza/au amevunja ungo kila akipita mtaani vijana wa kiume wanaona pale kuna mwali. Chadema wanachopaswa kufanya ni kuonyesha misingi ya chama kilichokomaa na kunaweza kuchukua dola. Watu huko CCM wanakimbia kwa sababu hakuna uhuru wa kutoa mawazo binafsi,pia mawazo mbadala yana nafasi kidogo huko CCM. Tukitaka kuwa na demokrasia nzuri lazima kwenye chama tuwe na watu wenye mawazo tofauti. Wafuasi wa chadema tusiwe too pre-emtive kwa kila kitu, tuwaachie kina zito na wengine watangaze nia ili tuweze kuchuja wagombea kwa misingi ya hoja. kumbuka wazee kina malichela waliishia wapi na mbio zao za kuwania Urais. Kutangaza nia na kuutaka urais sio kuupata urais. Ushauri wangu kwa Chadema wawe makini maana mwaka 2013-2014 aidha chadema itakufa au itabakia tumaini la watanzania kuelekea ukombozi wa kweli. Maana mtihani wa kwanza uchaguzi wa ndani wa chama utawaonyesha Chadema ni chama cha aina gani na 2014 uchaguzi wa serikali za mtaa ni kipimo cha pili kama watanzania wataipa chadema Dola. Ila Kama 2014 chadema ikishindwa kupata 45% ya uwakilishi wa serikali za mtaa lazima pia ijiandee kushindwa 2015.
 
Nawashauri CDM wasimjibu chochote wala kujishughulisha na huyu dogo .
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom