Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
1,948
Reaction score
1,238
Wakuu,

Sekunde chache zilizopita nimemsikia zito kwenye exclusive interview na Millard Ayo wa Clouds FM akitamka yafuatayo ..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."

Swali: Zitto anataka nini hasa?ana haja gani ya kuendeleza siasa za controversy namna hii kila siku?Je anatafuta umaarufu?

Binafsi ninamshauri aamke. Sisi ndio wapiga kura, atuache tuamue.

Naam, Hatimaye amemwaga na mboga kabisa... Ametangaza kuwa atagombea urais 2015 kupitia CHADEMA.

Zitto: Ubunge sasa basi

Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma | Mwananchi | Sept 28, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.

Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.

Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

"Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.

"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.

"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.

"Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi."

Atangaza kugombea urais

Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

"Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii," Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; "Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya."

"Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo," alisema Zitto

Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46.

Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.

"Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu," alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

"CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?" Alihoji Zitto.

Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
 
hii kauli nzito sana "aliyezaliwa kabla ya uhuru"....bidae narudi
 
Zitto sasa afurushwe rasmi nje ya cdm.TUMEMCHOKA.

Nadhani kauli yake haina tatizo japo chadema wanamjua tabia na matatizo yake,kitu cha msingi wala msikurupuke na kauli yake mda ukifika anayo haki kama wanachama wengine ya kugombea kwenye mchujo wa chama na akipita ndo chaguo la chama hivo wananchi wataamua awe rais au laa.
 
Amejisemea bila kufikiri. Ana maanisha hata kama mtu ni msomi kama akina Lipumba hawezi kusaidia isipokuwa wale waliozaliwa baada ya uhuru? Huu ni uhuni wa kawaida wa Zitto ambaye hujitahidi kujionyesha kama thinker wakati siyo hasa ikizingatiwa hata akiwa shule alipita hivyo hivyo. Nadhani kwa thinker mzuri hana haja ya kuwatenga watu kwa umri wao bali tabia zao hasa linapokuja suala zima la ujenzi wa taifa. Mbona tuna vijana waliozaliwa baada ya uhuru kama akina Masha, Ngeleja, Maige, Mosha, Ridhiwan, Bashe, Malegesi, Salma Kikwete na wengine lakini bado ni mafisadi wa kaiwada?
 
Akiongea clouds fm katika kipindi cha amplifier,ZK amesisitiza NI LAZIMA AGOMBEE URAIS 2015,na amesisitiza chama atakachogombea ni Chadema,yeye ana damu ya Chadema kwa kua yupo Chadema toka ana miaka 16,japo kuna watu sasa wanajifanya wao ni Chadema zaidi yake!
 
mkuu kutangaza nia sio kutumiwa.

Please nawaombeni sana wanaCDM wenzangu kwamba tuachane minyukano ya ndani kwa ndani kwani tutakiua chama chetu na tushindwe kufikia lengo letu.

Kweli kwenye vyombo vya habari ndio sehemu ifaayo kutangazia hii nia? Ukiwa kiongozi mwenye busara kabisa??

Ninaamini anatumiwa. Maana lengo kuu la wanaomtumia ni kutengeneza nyufa za kutokuelewana ndani ya cdm. Njia rahisi zaidi ya kufikia lengo hili ni hii aliyoitumia bwana ZZK...tunayakumbuka sana haya wakati ule wa akina Mrema na Marando kule NCCR.
 
kwanza amewatukana wazee wote Tanzania huku ni kukosa busara na hana sifa ya Uongozi kwani ni mbaguzi. Wapo Wazee waliozaliwa kabla ya uhuru na wanailetea Tanzania maendeleo na wapo wapuuzi waliozaliwa baada ya uhuru ni wapuuzi wa kutisha . Zitto hana busara kwa hili
 
Wakuu,

Sekunde chache zilizopita nimemsikia zito kwenye exclusive interview na Millard Ayo wa clouds fm akitamka yafuatayo ..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."

Swali: Zitto anataka nini hasa?ana haja gani ya kuendeleza siasa za controversy namna hii kila siku?Je anatafuta umaarufu?

Binafsi ninamshauri aamke. Sisi ndio wapiga kura, atuache tuamue.

Kama haujamuandika "out of context" Zitto anapaswa atuombe radhi tuliozaliwa kabla ya Uhuru, awaombe radhi na wazazi wake ambao bila wao, nna uhakika wote walizaliwa kabla ya Uhuru, asingekuwepo hapo alipo.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli husemwa:

Mleta thread unasema nyinyi ndiyo wapiga kura, kwani Zitto siyo mpiga kura?. Hayo ni mawazo yake kama mwananchi wa kawaida na ni mpiga kura kama wananchi wengine.

Demokrasia inatuasa kukubali kutokubaliana na ndiyo maana kukawepo upigaji kura
 
mkuu chama chetu kinaongozwa na katiba ya chama, so hakuna kipengele chochote ambacho Zitto amevunja, pia inabidi tufike mahali tusiwe sensitive sana ktk kila neno koz tutajikuta tunapoteza lengo la kupigana na adui (CCM).

Plz lets buld our CDM.
Umenena,
nitashangaa sana chadema kama kauli ya Zzt itaonekana tatizo japo matatizo na tabia zake mnazijua na kauli yake najua ni ngao kwa kinachoweza kutokea kwenye chama kwa sababu ya ukigeugeu wake!
 
as if Zitto is not entitled to own make statements. I don't think that everytime Zitto makes a statement then we should correllate to Chadema operations. We should also understand this person is a Tanzanian too, he has equally all rights as any other Tanzania citizen....Give him a break neh!
 
Wakuu,

Sekunde chache zilizopita nimemsikia zito kwenye exclusive interview na Millard Ayo wa clouds fm akitamka yafuatayo ..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."

Swali: Zitto anataka nini hasa?ana haja gani ya kuendeleza siasa za controversy namna hii kila siku?Je anatafuta umaarufu?

Binafsi ninamshauri aamke. Sisi ndio wapiga kura, atuache tuamue.
Kuna ubaya gani lakini mbona nilichoelewa ni kwamba Wazee wang'atuke waachie vijana. Ebu jiulize wewe mtu alikuwepo madarakani toka tupate Uhuru ina maana huyu alikuwa kijana wa miaka 18 kuendelea, leo hii miaka 50 baadaye bado anataka kuwa madarakani... Come on now ukishafika miaka 70 kuwa mlezi wa chama, pilka pilka hutaziweza, kubali kuitwa babu waachie wengine waiendeleze familia.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom