Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
Ni LAANA kutangaza nia ya urais kabla ya wakati ,ni kinyume na taratibu za chama na ni dalili ya kutumiwa na magamba:
HATA KAMA KUOA NA KUOLEWA NI HAKI YA KILA MTU LAKINI MTOTO WAKO WA MIAKA 7 AKITANGAZA NIA YA KUOLEWA NA FULANI KABLA YA UMRI NA MUDA MWAFAKA, HUKUMBANA NA ADHABU KALI KUTOKA KWA WAZAZI.
 
Suala la wakati haliwezi kuwa tatizo hapa as far as nia yake hii haiwezi kuathiri chochote wala kuvunja katiba, kanuni na taratibu ndani ya CDM na ukweli kwamba kwa mujibu wa katiba ya JMT ni haki ya kila raia mwenye akili timamu kugombea nafasi yoyote.

Hata hivyo, hapa kuna kuna hoja tatu zinajitokeza. Mosi ni suala la kipengele cha umri kumnyima haki hiyo Zitto. Anachokifanya ZZK ni kutegemea muujiza wa kipengele cha umri kufanyiwa marekebisho ili kiweze kuaccomodate umri wake huo ambao utakuwa umefikia miaka 39 ifikapo mwaka 2015. Sasa kama hivyo ndivyo kwamba Zitto hana sifa za kiumri kugombea nafasi hiyo kwa katiba ya sasa na pengine hiyo mpya inayotarajiwa maana kwa kweli hakuna guarantee wala ulazima kwamba kipengele hicho kitabadilishwa (Wenye mamlaka ya kushusha na hata kupandisha umri huo ni wananchi walio wengi) ni kwa nini kila mara Zitto amekuwa akisisitiza nia yake hiyo ya kugombea urais? Anafanya hivyo akilenga nini hasa? Maana anajua fika kwa sasa hana sifa.

Lakini suala la pili ambalo linatia mashaka ni aina ya watu wanaounga mkono juhudi hizo za ZZK hasa za kushusha umri ili kuwapa fursa vijana kugombea. Itakumbukwa wakati akiwa Kigoma jimboni kwa Zitto, Rais Kikwete alieleza nia yake ya kuona Rais ajaye wa JMT anakuwa kijana na ghafla tukamuona Zitto na J Makamba wanavalia njuga suala hilo. Mara likawa agenda kuu vichwani mwa watu. Kwa wachunguzi wa mambo ni kama kuna mkakati unaratibiwa wa kigezo hicho cha umri kushushwa ili kuruhusu Zitto aombe kugombea urais CDM ama kwa kuutaka kweli au kupitia sera ya Andrew Chenge dhidi ya Samwel Sitta kwenye nafasi ya Uspika ya Tukose Wote.

Sasa hili la mwisho la Tukose Wote lina nguvu zaidi kwani linaweza kutekelezwa kwa Zitto kuwa ndani ya CDM kupitia kuimarisha kambi dhidi ya mgombea atakayepitishwa na chama chake (Linawezekana sana, ni fedha tu kumwagwa na tayari Zitto ana wafuasi wake ndani ya CDM na CCM pia) au kuhamia chama kingine cha Siasa hasa cha NCCR Mageuzi kutokana na aina ya Mwenyekiti aliyepo (James Mbatia ambaye tayari ameshazawadiwa nafasi ya ubunge na JK). Zitto akiwa chama kingine atapewa fursa ya kugombea urais na atatumiwa kumshambulia mgombea atakayepitishwa na CDM hivyo mgawanyo wa kura.

Vinginevyo uhakika wa haya yote tutaujua kadri siku zinavyosogea maana tayari watu wengi hata wananchi wa kawaida wameshaanza kumuangalia Zitto kwa jicho tofauti hasa lile la kusaliti harakati za mageuzi kwa kujiweka kando na ngwamba/mihenyeko inayowakumba viongozi wenzake wa CDM katika kukijenga chama na tetesi za yeye kujikita katika kuvuna fedha tu. Time will tell on this though CDM need to be very precautious
 
Mie nina shida na hayo maneno ya kusema hakuna wakuleta maendeleo zaidi ya vijana tu......sikubaliani nae....it is wrong.....wazee ni chemchem ya hekima pia wapo vijana. ni mbumbumbu tu.....ajenge hoja nyingine ya kutuaminisha sio la umri.
 
uchambuzi mzuri WOWOWO, wasiwasi wangu vipi atapitishwa wakati hawaungi mkono katika ujenzi wa chama? nani atamwona kuwa anafaa kuwakilisha watanzania kupitia CDM chama ambacho amejitenga kwa kiasi kikubwa? nina mashaka
 
Wakuu,

Sekunde chache zilizopita nimemsikia zito kwenye exclusive interview na Millard Ayo wa Clouds FM akitamka yafuatayo ..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."

Swali: Zitto anataka nini hasa?ana haja gani ya kuendeleza siasa za controversy namna hii kila siku?Je anatafuta umaarufu?

Binafsi ninamshauri aamke. Sisi ndio wapiga kura, atuache tuamue.

Naam, Hatimaye amemwaga na mboga kabisa... Ametangaza kuwa atagombea urais 2015 kupitia CHADEMA.

Zitto anasumbuliwa na ujana. Ni kwamba tu anajua sana kujieleza na ana haiba ya konekana anafahamu analosema. Ukweli ni kwamba uelewa wake, na mtazamo wake, kwa ujumla, hauendi mbali zaidi ya kujiangalia yeye mwenyewe na hisia zake kuhusu dunia inavyozunguka. Namfananisha kabis ana Julius Malema.

Hii haiba yake imeacha wahanga wengi wa kisiasa. Angalia akina Mkono walivyoaibika na saini zao za kumuengua Waziri Mkuu - moja ya miradi hewa ya Zitto. Angalia alivyochangia kujenga chuki dhidhi ya wawekezaji wakubwa wa migodi ya dhahabu, hata pale alipogundua amekosea ameshindwa kurudi na kuwaambia watu kuwa hii miradi siyo uadui. Yeye ameelewa, lakini kawaacha wananchi kule kule alipowapeleka - kwenye jamii inayochukia wawekezaji.
 
Nawashauri CDM wasimjibu chochote wala kujishughulisha na huyu dogo .

Mimi ningeshauri ili ku-neutralize hii kitu, hata kama hawamaanishi, Mnyika, Lema, Heche, Mdee nao watangaze ili kwamba atakapochaguliwa mgombea; lengo la Zitto la kusema ameachwa kwa udini na ukanda lisiwe na nguvu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
cdm tusiwe kama cuf. Kule hatumjui mwingine zaidi ya lipumba. Hiki ni chama cha demokrasia na maendeleo. Tujue nini maana ya demokrasia. Alijaribu mbowe akakosa. Akaja slaa akakosa. Sasa huyu kijana zitto naye huu ni wakati wake, apewe hii nafasi. Tofauti ya zitto na jk ni kuwa zitto ni mwelewa zaidi na ni mtu wa vitendo. Jk ilikuwa ni upepo tu. Zitto apewe nafasi
 
Zitto nakuunga mkono kwa kauli yako kwa asilimia 100. Umekuwa mwalimu wa ufunuo katika jamii kwa mambo ya kisiasa kwa muda mrefu, na sasa naona unajikita sana kwenye uchumi kupitia makala mbali mbali. Umekuwa ukiendelea kutoa ufunuo huo huo kwa kuifahamisha jamii uhusiano kati ya rasilimali ya tuliyonayo dhidi ya umasikini/ufukara tulionao. Naona sasa unahama kutoka kwenye upinzani tu wa kisiasa kiitikadi na kujikita zaidi kuelimisha jamii kuwa kujadili zaidi itikadi za kisiasa, tofauti ya mtu na mtu wa itikadi tofauti ni kupoteza muda. Sasa umehamia kwenye kutafuta zaidi mafanikio ya kiuchumi kupitia njia sahihi chini ya sera za chama chako cha chadema. Ninaamini Mungu akikujalia ukaja kushuka uongozi wa taifa hili, utatafsiri kwa vitendo nini kinatakiwa kufanyika ili twende ambapo panastahili. Mungu atakujalia na utafanikiwa.
 
uchambuzi mzuri WOWOWO, wasiwasi wangu vipi atapitishwa wakati hawaungi mkono katika ujenzi wa chama? nani atamwona kuwa anafaa kuwakilisha watanzania kupitia CDM chama ambacho amejitenga kwa kiasi kikubwa? nina mashaka

Well, asipopitishwa na CDM (Wengi tunategemea hivyo maana hashiriki ujenzi wa chama kwa sasa) maana yake plan A imekwama then ata opt plan B ambayo ni kukihama CDM na kupewa fursa ya kugombea urais kupitia chama kingine. Hapo ndipo yeye na makuwadi wake wataanza kuitupia madongo CDM mwishowe ni wapinzani kugawana kura na kurahisisha ushindi wa CCM. Ndiyo maana nasisitiza CDM need to be very precautious na ZZK hasa kuweka mikakati ya udhibiti mbinu na mianya yote inayotiliwa shaka kuelekea 2015.
 
Kwakuwa mwenzenu ametangaza nia tayari, na amesema asipopata ridhaa ya chama chake hakuna shida. Lkn inside anajua shida itakuwepo hasa madhara Makubwa ni kwenye propaganda ya 'udini na ukanda'; Zitto being that smart anajua kabisa reaction ya 'baadhi' ya watu itakavyokuwa.

Hivyo ili kupunguza nguvu ya hii kitu, vijana wengine nao watangaze nia za Urais hata kama hawamaanishi; vijana kama Lema, Mnyika, Mdee, Heche n.k. Ili pale chama kitakapompitisha mgombea; hao 'wenye mahaba Makubwa' na Zitto wasipate cha kusemea.

Ni maoni yangu tu, maana reaction yoyote ya chama ni mtaji wa Zitto na walio nyuma yake.
 
mara nyingi vijana wa CDM wanakubali ushaur wa slaa tu.subiri matusi
 
Kwa kiasi Fulani Zitto ameanza kuvuna alichokipanda hapa. Ona sasa tunaanza kujadili uraisi wa Zitto badala ya ufisadi wa CCM. What a waste of effort!

Naamini hii ni mbinu mbadala ya kudhoofisha CDM. CCM hawawezi kuwa na mbinu ya kutumia FFU peke yake. Lazima wajaribu kupandikiza malumbano ya wenyewe kwa wenyewe pia. Ni mbinu iliyofanikiwa huko nyuma kumdhibiti Lyatonga, lakini natabiri kwamba hapa kwa Slaa, Mbowe na Lissu hawataweza.

Tuachane na haya ya kupandikiziwa, turudi kwenye shughuli kubwa inayotukabili; shughuli ya kurudisha utawala wa kisheria Tanzania.
 
cdm tusiwe kama cuf. Kule hatumjui mwingine zaidi ya lipumba. Hiki ni chama cha demokrasia na maendeleo. Tujue nini maana ya demokrasia. Alijaribu mbowe akakosa. Akaja slaa akakosa. Sasa huyu kijana zitto naye huu ni wakati wake, apewe hii nafasi. Tofauti ya zitto na jk ni kuwa zitto ni mwelewa zaidi na ni mtu wa vitendo. Jk ilikuwa ni upepo tu. Zitto apewe nafasi
Hili nalo neno!. Mwenye masikio na asikie!.
P.
 
freedom of expression mkuu. kwani kavunja sheria kusema hvyo?
Huyu jamaa yuko huru kutoa maoni yake, si katiba ya CDM wala ya nchi inayoweza kumzuia. Hata hivyo, kwa mwanasiasa makini timing is everything na hapo ndo anapokosea. The time is or may not be right. Labda ZZK hajakuwa makini ya kutosha katika uana siasa wake, na hilo ni tatizo lake la muda mrefu! apart from that the guy's fine!
 
Haya ni mawazo ya Jemedari Zitto,sizani kama kuna tatizo kutangaza nia . Kama amekosea jamii itamuhukumu kivitendo. Tumuombee Mungu kamanda apewe hekima zaidi katika uongozi wake.
 
cdm tusiwe kama cuf. Kule hatumjui mwingine zaidi ya lipumba. Hiki ni chama cha demokrasia na maendeleo. Tujue nini maana ya demokrasia. Alijaribu mbowe akakosa. Akaja slaa akakosa. Sasa huyu kijana zitto naye huu ni wakati wake, apewe hii nafasi. Tofauti ya zitto na jk ni kuwa zitto ni mwelewa zaidi na ni mtu wa vitendo. Jk ilikuwa ni upepo tu. Zitto apewe nafasi
CHADEMA 2015 Hatufanyi majaribio!
 
Moja kati ya makosa makubwa tunayoyafanya watz ni kuamini kwamba mtu aliyefanya vizuri kwenye post flan anaweza pia kufanya vizuri kwenye nafasi nyingine ya juu zaidi! Mifano mingi imethibitisha kuwa ni makosa makubwa. Tumwangalie Sita, Stella Manyanya, Nape nk. Waangalie maprofesa waliokuwa wazuri chuoni baada ya kupata uwaziri. Wengi wamechemsha. Hata wale tuliodhani ni wazuri, tuwekuja kugundua ni wanafiki tu. Mfano Magufuli..
Hata Zito anakosea sana. Mchezaji anayefanya vizuri nafasi ya ushambuliaji, ni makosa makubwa kudhani kwamba anaweza kuwa mlinzi mzuri. Na kocha akimwamishia golini, ataishia kujuta! Swali la msingi la kujiuliza ni kwamba, kama anafanya vizuri kwenye nafasi yake, kwanini tumwamishie pengine? Ni sahihi kufanya hivyo!? Mimi nadhani tumwache Zito abaki bungeni, aendelee kuwa mshambuliaji mzuri kuliko kumweka position nyingine kwa "kudhani" kwamba atafanya vizuri!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom