Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
Hapa ZZK amepotoka! Nadhani aipime vizuri kauli yake. Kuna watu wengi sana tu waliozaliwa kabla ya uhuru wenye uwezo na fikra madhubuti za kulikomboa taifa hili kiuchumi. Tatizo ni moja tu, wamekosa fursa kutokana na utawala wa kidhalimu wa CCM!
 
Hela zimeshamlevya, mara vogue, mara hammer 3, mara kilimo kwanza, mara ghorofa Dom? Si yule niliemjua pale Nkhuruma enzi za kunji la 2000. Zito huna personality ya kuwa Rais stop mocking, Mnyika ile vits yako naipenda sana, najua una uwezo wa kununua gari lolote la kifahari lakini image kwenye public ni kitu muhimu sana. Ulitia aibu na budget yako kivuli watu wakakupotezea naona unafikiri mapembe yako yamefika angani kumbe hata nchi moja hayana. Im very sory 4 you coz i can feel n see the outcome. Mara amiri jeshi mkuu, mara vijana its 2012 man, come on!
 
as if Zitto is not entitled to own make statements. I don't think that everytime Zitto makes a statement then we should correllate to Chadema operations. We should also understand this person is a Tanzanian too, he has equally all rights as any other Tanzania citizen....Give him a break neh!

With a view like this CCM will never be defeated, we'll only be taking one step forward and two steps back
 
Hivi wana Chadema mna tatizo gani Zitto kugombea URAIS ikiwa ni nyie ndio wenye turufu ya kumchagua au laa?.. inakuwaje mnaanza siasa za kutukana watu ambao wanaitumia haki yao ya msingi waktifuata anuni za chama. Hata wewe unaweza na unaruhusiwa kuweka jina lako kugombea Urais na likipita unaweza kuwa rais vile vile kwa nini iwe shida kwa Zitto.

Mimi nitasimama na Zitto wakati wowote ktk hili maana haki hiyo anayo na mtu mwingine yeyote iwe hata Shibuda maadam najua kazi ya kuengua majina ya wagombea itafanywa kwa utaratibu unaotakiwa.

Hamtaki Shibuda, jina lake litaondolewa, hammtaki Zitto, jina lake litaondolewa, Hamtaki Mbowe au Slaa litaondolewa vile vile. Na pengine hata huyo mnaye mdhania kuwa ndiye hataki kugombea Urais, sasa mnatabakiwa na nani?
 
Ukweli husemwa:

Mleta thread unasema nyinyi ndiyo wapiga kura, kwani Zitto siyo mpiga kura?. Hayo ni mawazo yake kama mwananchi wa kawaida na ni mpiga kura kama wananchi wengine.

Demokrasia inatuasa kukubali kutokubaliana na ndiyo maana kukawepo upigaji kura

Ninaamini demokrasia nayo ina taratibu na busara pia mkuu. Kwanini asitangazie kwenye vikao mahsusi vya chama??ama basi hata akasubiri kidogo walau 2015 ijongee karibu ili kama chama kiamue kwa pamoja?...
 
Naam. Hatimaye amemwaga na mboga kabisa..ametangaza kuwa atagombea urais 2015..sasa nimeshaamini anatumiwa.

Hahhahahah. . . . Ameshahakikishiwa kwamba umri wa kugombea urais utapungizwa to 35 years.

Nani amemuhakikishia??!

Lakini stetements za Zitto haziaminiki. Sio mara ya kwanza kusema jambo na kutenda kunyume chake.
 
Ninaamini demokrasia nayo ina taratibu na busara pia mkuu. Kwanini asitangazie kwenye vikao mahsusi vya chama??ama basi hata akasubiri kidogo walau 2015 ijongee karibu ili kama chama kiamue kwa pamoja?...
katika Siasa Nia ya kugombea Urais hutangazwa kabla ya vikao vya chama, pale inakuwa huwashutukizi watu kutaka kugombea isipokuwa unaanza na kujitambulisha kwa wananchi wote maana hao ndio Utakao waongoza..Uchaguzi ndani ya chama ndio unasubiri ya ndani kuonyesha nia yako tena mnaweza kupanga usigombee kiti ambacho mwenza anakiwania. Ni chama kimoja kaa timu ya mpira vile.. lakini sio Kitaifa..
 
Ah Zitto nae ameanza kuwa kama Kibonde Ephraim. ngoja nivizie hotuba za UNGA.
Habari za Zitto zinakera kooni kama moshi wa ubani hasa kama anayeuvuta hana mahitaji nao
 
wazaliwa baada ya uhuru watasimamia ukuwaji wa uchumi?sawa!
Kwangu mimi Wazaliwa baada na kabla ya uhuru watasimamia ukuwaji wa demokrasia,siasa safi na uchumi.namtaka kiongozi anayeweza kutambua umihimu wa sekta zote katika kufikia ustawi wa Tanzania.
 
UDINI itakimaliza CHADEMA tatizo la zitto ni uislam wake chama anachokipigania kina mrengo wa kueneza UKRISTO na misaada wanapokea CDU ya ujerumani.
 
millard ayo
#AMPLIFAYA Sep27 #2 ZITTO KABWE: nitagombea Urais 2015 sitogombea tena Ubunge, kuna watu wanajiona ni CHADEMA zaidi kuliko mimi lakini hawajui. (Post sponsored by ZANTEL )
 
Ni kipengele kipi katika katiba ya cdm zitto amekivunja? kwanini nyie pro slaa mnakuwa na akili za kushikiwa?
 
"Aleee wazee wa zamani kwaheri eeee!!!......... Akudo impact. Kwa wale wazee walioshindwa kuitumikia nchi wakiwa vijana na nguvu zao basi hata uzeeni hatuwataki.
 
UDINI itakimaliza CHADEMA tatizo la zitto ni uislam wake chama anachokipigania kina mrengo wa kueneza UKRISTO na misaada wanapokea CDU ya ujerumani.
Inasikitisha sana kuona ndivyo itakavyo someka na wanaChadema wanaendelea kumpiga vita hata anapo exercise his right.. hapo ndipo napokoma na jamaa zangu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom