Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Hadithi ni zile zile. kwanini umeiba kuku,......... jibu, mbona fulani kaiba ng'ombe,.............
CCM wanautaratibu wao tuliouchoka na uliotufiksha hapa tulipo, sasa je CDM nao wanafuata utaratibu huo huo
Ndio maana naamini Tz hakuna mkombozi wote wasanii tu
 
Asante kwaheri....... heri mimi sijasema kwamba akina Zitto Kabwe ni wasanii tu!!
 
Hii ni mind game. Iko kitu ingine hapa na wala sii urais. Wa TZ kaeni chonjo!.
 
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025

Nelsweeter,
Acha uvivu wa kufikiri,usikurupuke kujibu mambo ambayo hujui msingi wake. Unaposema ni zamu ya Wakristo,una-refer katiba ya nchi gani au chama gani,CCM,CDM,CUF..??Kwamba kama zamu hii katawala Muislam basi next time atawale mkristo?..BTW,unajua maana ya Mujahidina au unaropoka tu! Jibu hoja na sio kum-attack Zitto!
 
If wishes were horses even beggars would ride horses. Yericho endelea kuwaumbua
 
Ni Obvious Dr Slaa now yuko kwenye take off stage,Zitto anafaa lakini sio kwa sasa,Asubiri.Hata Zitto hajafanya kosa jamani.Amesema endapo chama chake kitamwona anafaa,na kama atapendekezwa mwanachama mwingine atamuunga mkono.Zitto yuko sahihi.Hata hivyo hatuwezi kumlinganisha na dakratr slaa kwa sababu daktari hajawahi kuthubutu kusema atagombea.

Kasoro ya zitto ni kuwa mbinafsi,anadhani kwamba he can fight the war alone.Kosa kubwa alilofanya la kuhamisha attention ya Chama kule Arumeru na kumjia yeye ,hajafanya timing ya kutoa makala yake,namfananisha na TUNTEMEKE.Always huwa hashirikiani na harakati za chama chake,Hakuna maandamano Zitto ameshiriki.ANASIFIWA NA WATU WA CCM,Kweli kweli jamani hata kama ni wewe adui yako anakusifia ,huoni kasoro hapo? Dr Slaa anashsmbuliwa kutwa kuchwa,huyu ni mpinzani sahihi.
 

Mwandishi katika habari uliyoileta nimeikubali hii paragraph, huko kwingine :hand::hand:

Holy c.r.a.p!!!!

He was saying his dreams!!! He even said if his party will ALLOW HIM!!! if not he will support any one endorsed by his party!! WHATS WRONG WITH THAT???

Mkuu Wabs! nakubaliana na wewe, watanzania tumekuwa na uvivu wa kufikirisha akili zetu...

 

Mkuu mimi siku zote huwa nashangaa na najiuliza maswali mengi tu mojawapo likiwa hili: CDM wanasema ni chama mbadala wa CCM lakini kila kitu wanataka kujilinganisha na CCM; huo ubadala utatoka wapi sasa? Bilal alikataliwa kugombea basi na Zitto akataliwe! Shibuda alikataliwa basi hakuna mtu wa kuchukua form dhidi ya Dr. Slaa; heee jamani tunataka chama mbadala chenye mitazamo tofauti kabisa na CCM na siyo chama ninachojilinganisha na ku copy ubaya wa CCM. Afadhali kingekuwa kina copy mazuri ya CCm lakini chenyewe kinacopy mabaya tuuuuu! Nashindwa kuona tofauti hapo.
 

Nikikuuliza ni wapi wazee walisema Ben Saanane huna maadili utanijibu?Do credibility a favour na uje uthibitishe hilo.Tuache upotoshaji.

Matola,
Just as everyone is entitled to their opinion then everyone should be entitled to their own actions(good or bad).
Unajua ukitaka kuheshimika ni lazima pia uwe na nidhamu.Heshima na nidhamu ni two way traffic.
Kuhusu Mnyika,sina utamaduni wa kujadili watu kama unataka kujadili watu jadili mwenyewe.Mnyika ni kiongozi wangu,ni rafiki yangu tunaheshimiana.Kuhusu suala la vyeo mimi sipo hapa kujadili hilo kuna mamlaka ya uteuzi kawaulize maswala hayo

Kuhusua Alliance ndani ya chama,ni alliance ipi niliyoitetea? Nakiri uchaguzi wa BAVICHA nilifanya Alliance.Je hilo ni tatizo? kuna political theory yoyote inayokataza aliance?chama kinakataza makundi,ofcourse makundi si healthy kwa mustakabali wa chama..Na hilo naunga mkono.hakuna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na makundi ila cha msingi ni jinsi ambavyo kila mmoaja anakuwa tayari kuvunja makundi baada ya uchaguzi

Nilipomaliza uchaguzi wa BAVICHA nilisema nitaendelea kutetea zoezi la demokrasia ndani ya chama changu.Kama ilivyo kwa mimi kutokuwa tayari kuona Dr.Slaa anazushiwa tuhuma za uongo au Kamanda mbowe ndivyo hivyo nitakavyopambana na upotoshaji unaofanywa dhidi ya kamanda Zitto na wanachadema wengine wa CHADEMA kwa ujumla.



Comrade Kimbunga,

I had thought that with more education and analytical thinking, our people would get past these narrow highly subjective conclusions about our reality. Unadhani baadhi ya watu hawajaelewa hili suala?wengine ndiyo hivyo hawewezi kuelewa lolote,na wengine wameelewa ila ni husda zao tu.Wengine wapo kazini.lol


Matola,
Kuhusu suala la kuwa Interested na zitto kuja hapa akueleze sijui nini siwezi kulijadili,atalijadili yeye mwenyewe.

Kwa hiyo suala la katiba kujadiliwa watu wanazuiwa kusema wanachoamini? Kweli hata katiba mpya itaandikwa hakuna mabadiliko yoyote kama tunafikia hatua kuchagulia watu marafiki na kitu cha kusema.

Tuna safari ndefu huko mbele.Guys,let us be matured,tatizo la hii hoja ni nini?mara wengine wanasema kuna uchaguzi Arumeru kwa hiyo timing ni mbaya.Nguvu zinazotumika ku-condemn hili kwa nini zisitumike kuelewesha watu kama unadhani hili lina athari kwenye hizi chaguzi?


Mwakalinga,

Well, Apologies if i don't paint out my wishes concisely.

Nikikuuliza ulete uthibitisho wa kukigawa chama,unaweza kuleta? Wanaonituhumu ?

You are basing all your accusation on a hearsay plus you jumped into conclusion. We'll damage ourselves before we can able to fix ourselves.

Bora umenipa benefit of doubt.Mara nganpi tumekosoana na kubishana sana hapa JF tangu niwe member 5 years ago na sijawahi kumkosea heshima yeyote anayenipinga kistaarabu? Akina Mugongo Mugongo,ACID,MTM,Field Marshal,Waberoya,Kimbunga,Kasheshe,Mwanakijiji,Mkandara na wengineo wengi watakushangaa sana kwa kauli hii ya kwamba ninaweza kuwa sikubali kukosolewa.

Nitasema kile ninachoamini na nitasimamia kile ninachoamini.Upotoshaji wowote utakaofanywa kwa maslahi ya wachache siwezi kuvumilia,siogopi kuchafuliwa na siogopi matusi wala vitisho.Ninachojali ni maslahi ya watanzania kupitia dira sahihi,najali maslahi ya vijana na nitapigania kwa gharama yoyote ile.Mkuu waangu pengine haupo ground kujua kinachoendelea,vijana wanatumika kama daraja la watu kisiasa.busara za viongozi wetu waliokuwa above 40 ndizo zilizozalisha hili bomu ambalo wanafiki wanajaribu kujifanya kwamba linawaumiza.Leo hii wanapita wanasiasa waliosababisha lindi la umaskini na wengine walioshindwa kuishinikiza serikali ilifanyie kazi tataizo la ajira kwa vijana leo hii wanalia machozi ya mamba.siwezi kucheka naoa

Umeongelea kuhusu kuheshimu mawazo ya wengine,huwa ninaheshimu mawazo ya wengine sana hasa wale ambao wanaonipinga.Wnaonipinga huwa ninawasikiliza zaidi,hata katika maisha yangu ya Uongozi vyuo vikuu na Eneo langu la kazi wanajua hivyo.Anayenipinga namsikiliza zaidi


Mkuu,kwa hiyo hata majukumu yake ya kamati ya hesabu za serikali na mashirika ya umma anayafanya kwa msukumo?suala la Posho anafanya kwa msukumo?


Field Marsha ES,
Bravo mkuu,Unajua tangu upotee na akina Mugongo mugongo jukwaa hili limepwaya sana .Wamebaki akina Mkandara,Mwanakijiji,na wakuu wengine wachache kutetea heshima ya JF kwa hoja.

Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?


Nuclear1,

Naomba ulete uthibitisho wa hayo uliyoandika.Ongeza list kabisa Willy malecela,Baraka Kange,Makongoro Nyerere,Ole Millya,Julius Mtatiro,David kafulila na wengineo! Tujadili mada iliyoko mezani achana na personal vendatta na kuchafua majina ya watu.Kwa bahati mbaya sijengi hoja au kusimamia hoja katika kufurahisha watu.Usidhani kila mtu yuko kama wewe mkuu

Remove the hatred induced politics of Tanzania and misguided priorities.Throw away your "no victor, no vanquished" mantra. It does not exist in practise. Surely, it does not exist in the minds of CHADEMA elites

The problem with most guys including you is that they are selectively hypermetropic. They see only what they want to see and blank-out others from their view. You are assertions are just inflammatory. Well you have the right to your opinion but not to your facts.

In reality you think you are doing good and giving Opposition what they want but in reality you are just hurting the Opposition camp legacy and most importantly the CHADEMA name with you silly fact fixing games.
 
Ni kweli kwamba Zito ana ajenda ya siri..? Na ni kwa manufaa ya nani..? Jee haya magari ya kifahari anayoyamiliki ameyapata kwa njia gani..? Ni kweli Zito na JK wako so close..? Kwa nini amekuwa na kauli ambazo ni very controversial..? Na mwisho ya yote anataka ku-achieve nini..? ni kweli anataka uraisi au anatumika kujaribu kukisambaratisha chama..? Kwa nini atangaze nia kipindi hiki ambako nguvu zote ziko Arumeru..? Na jee hii kauli yake ina uhusiano wowote na post moja ambayo iliwekwa hapa JF ilio (supposedly) mnukuu Dr Kitilah kuhusu mpasuko wa uongozi CDM..? Duh.. Kamanda Zito mbona wanipasua kichwa..? ntapata wapi majibu haya mie..?
 
MBONA hamsemi ukweli tu kwamba ZITTO ni immaterial kwenye urais?
=upapeti mwingiii!
=watanzania wengi mtamjua tu kabla ya 2015
=ana kaugonjwa kanakoitwa mega-mania
=kuhusu ugomvi wake na MBOWE si urais bali wale watu wa viti maalum mle cdm.kila mmoja wao anataka awe juu ya mwingine we subiri mpaka watauana labda hizo nafas ziondolewe.
 
Urafiki wa Zitto Kabwe na Jack Nzoka Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa wewe unataka kutuaminisha ni wa kawaida? hivi si wewe chama chako ndio kilisema Usalama wa Taifa ndio waliokuwa wanachakachuwa kura za CHADEMA? je inaingia akilini wakati chama kiko vitani kwenye uchaguzi mkuu halafu Zitto Kabwe anakuwa na mawasiliano ya karibu sana na one of your party enemy? (TISS)

Zitto Kabwe ni rafiki yako na kama alitoa makala hii ili kumjibu huyo mwandishi sasa mfikishie na ujumbe huu, aje hapa atupe ufafanuzi wa yeye kuwa karibu na Usalama wa Taifa. nitamuhesabu Zitto Kabwe kama ni Double Agent until he proves otherwise without resonable dought.
 
Hivi yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana umri gani vile...??

Yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana miaka 28 ila uongozi wa nchi yao ni tofauti na sisi yeye hajachaguliwa ki-domocrasia karithi urais.Mimi binafsi nakubaliana na wale wanaosema kwamba Zitto Kabwe bado hajapevuka kisiasa.The right time for him to run for presidency is 2020 or 2025.
 

Mkuu hivi ukiambiwa kwamba hao TISS, achilia mbali Zitto, wamejikita ndani ya CDM na wana madaraka utajisikiaje? Hivi mkuu mtu kuwa na urafiki na watu inakuwa ni jambo la kumhukumu? Kwa hiyo unataka Zitto awe na marafiki ambao ni wana CDM tu?

Nakumbuka Dr. Slaa alikuwa akiishi na Diwani wa CCM. Hapo unasemaje?
 
Umetumwa? wewe ndio Zitto Kabwe, unadhani sifahamu ninachokiuliza au unadhani wote humu viherehere vya wanasiasa? Mabere Marando alishajibu siku nyingi Mahusiano yake na TISS, hapa yanahitajika maelezo ya Zitto Kabwe na siyo maelezo ya wapambe wa Zitto Kabwe. tena ningekushauri kama unampenda kaa mbali na hili.
 
=BARRICK walikuwa wanamlipa $25000 kila mwez for 6 months in2009.
=Kwa kuitetea DOWANS alilipwa 80mil (TSH)
=Kuhusu post ya Mkumbo alikuwa sahihi kwa sababu hata yeye KITILA pale cdm yuko kwa ZITTO na anamfahamu vizuri ZITTO kwani ni KITILA aliyemleta Zito UDSM akitokea ZANZBAR UNIVERSITY wakati ule KITILA alikuwa RAIS wa DARUSO
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…