Zitto ndani ya kumekucha ITV

ZZK was my mentor in those days...tatizo simuamini tena....matendo yake ya kuwa very independent yananikatisha tamaa..
I wish angeshirikiana vzuri na Dr na Mbowe na wananchi tukaona pasi na shaka kwamba wanashirikiana.

Wanao uwezo wa kubadilisha mengi ktk nchi hii.
Wala sio lazima any of them awe Rais..Kuna weakness ktk CDM ktk TEAM SPIRIT. Wengi wanategemea individual efforts..

UMOJA NI NGUVU..
 
We are not Kids! Huyu ndiye alikuwa anamtetea Mhando na huyo ndiye aliruhusu huo wizi bila wasiwasi wowote. Sasa anakimbilia kwenye TV huku uso umepauka kwa Hofu ya sakata lote kumuhusisha yeye mwenyewe siku zijazo!

Zitto hawezi kuaminika ana agenda mia moja ambazo hazifikishi popote bali misifa. Mara fedha zilizoko nje ana hataki kuwataja eti anasema ni kupoteza muda wakati huo huo anaonyesha hana imani na utekelezaji wa serikali sasa anachosema ni nini?

Siku zote alikuwa wapi kujua Tanesco kuna wizi hadi Mkaguzi ameonyesha. Wizarani walipo mwambia yeye akakimbia kumtetea Mhando tatizo ka kuwa Mnafiki litamfuata . Halafu etui anamalizia kwa kusema kuwa anataka urais sasa kichekesho cha mwaka!! Uliwahi kuona chama gani cha upinzani wakamteua a double agent kupeperusha bendera yao?
 
Tarehe 10 mwezi disemba nitakuwa Swiss kufuatilia zaidi hili swala na wachunguzi ambao wananisaidia kwenye hili.
Alhamdulillah, nilitoa maoni kama hayo hapa
Azipa 20:03 22nd November 2012
Kwanini ZZK asilisimamie hilo suala yeye mwenyewe? Nani alisema raia hawezi kwenda kufungua kesi Uswiss ili pesa zirudi. Prof. Mark Pieth ni raia wa Uswiss ambaye alifungua kesi kupinga uamuzi wa serikali ya Uswiss kutaka kurudisha pesa kwa familia ya Mobutu badala ya serikali ya DRC. Bahati mbaya kesi ilitupiliwa mbali kwakuwa yeye hakuwa ni raia wa DRC

Asijeakawa anaenda baada ya deadline. Maana huyu ZZK ni full usanii
 
Zitto is just a normal human being. Hawezi kutoa maoni au kauli ambazo zitamfurahisha kila mtu.
Ni vema tukaheshimu mawazo yake.
 
waache kujadili vitu vidogo hivyo vya maneno tu ambayo hayan athari katika uchumi wetu
 
Mimi nimependa jinsi alivyo ipaisha JF.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe ameipaisha JF, kupitia mahojiano yake live on ITV!.

Huyu ndio kiongozi wa kwanza wa level hiyo ku express appreciation kwa JF kupitia mahojiano yake ya saa 8 na jf, hivyo kuwataka viongozi wengine wawe accessible kuhojiwa!.

My Take:
Nimemsikiliza ZZK kwa makini sana!. Kiukweli Chadema has a "jewel" tatizo ni lile lile la "nabii" hathaminiwi nyumbani!.

Pasco.
 
"Waziri wa fedha nataka atoe taarifa ni kiwango gani cha fedha kimetoka kwa ajili ya kununua fedha, sasa hivi kwa sasa tunatumia zaidi ya bilioni 172 kwa ajili ya kununulia mafuta mazito ya umeme wa dharura" duhh halafu kuna wajinga wanasema elimu bure haiwezekani! Kina chama na Ritz aibi yenu.

Waungwana kwanza tunasalimiana; Asalaam aleykum; bibi Rehema hajambo?
Sasa turudi kwenye mada; sasa muulize huyo waziri wako fedha Zitto je kwa wakati huu ni lipi bora inabidi tuchague kati ya moja kati ya mawili nchi iwe kizani au tuzalishe umeme ili shughuli za kiuchumi ziendelee; na kingine muullize Tanesco haitoi umeme wake bure wananchi walipia umeme kwa maana hiyo hizo bilioni 172; hazipotei kama anavyotaka kubainisha; kiuchumi hatuwezi kuiweka nchi kizani kwa kisingio eti tunatumia bilioni 172; kuwa kizani gharama zake ni kubwa kuliko hiyo bilioni 172; muulize je tukiwa kizani GDP yetu itaathirika kiasi gani? Nadhani unaalewa nini maana ya dharura; gridi yetu ya Taifa imezidiwa tatizo hili ni kwa nchi nyingi za Afrika hivi sana Egypt wameweka sheria maduka yafungwe saa 3 za usiku kuokoa umeme; Zipo jitihada zinafanyika hivi sasa moja wapo ni kuleta gesi Dar es Salaam ili itumike kuzalisha umeme hizo zote ni jitihada za serikali; mkuu umeing`ang`ania sana bure tumeshakupa bi Rehama bure bado hujaridhika tu? Mkuu hapa hakuna wajinga JFkuna hekima nyingi punguza wahka!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
M/Kiti ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma POAC, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, amesema serikali lazima ifanye kazi ya ziada ili kupata majina ya walioficha mabilioni nje ya nchi!, na sio fedha za Uswiss.

Mhe. ZZK ameyazungumza hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na ITV asubuhi ya leo.

ZZK amesema kauli ya serikali ya Uswiss kiitaka serikali ya Tanzania ndio ipeleke maombi rasmi ni hadaa!. Amesema serikali ya Uswiss inaendeshwa kwa kutegemea faida ya mabenki, hivyo usiri ndio lengo la mabenki ya Uswiss.

Amesema lazima serikali iajiri mchunguzi huru azame ndani na kuibuka na majina na ni jukumu la serikali yetu kufanya uchunguzi wa wenye fedha hizo wamezipata vipi kama ikithibitisha wizi ndipo wayapeleke Uswiss.
 
Kwa hili namuunga mkono ZZK na Kinana.

By the way mi siwaitagi WAHESHIMIWA tangu kitambo...
kuna watu siwaheshimu...
 
hivi hawa watu na ccm yao hawajachoka tu kuiba???? wanasema hakuna mgao wakati tunashinda giza kila siku na na kumbe kuna pesa zinaibwa!! shame upon this government!
 
kumbe kina ritz na chama wakisema wamechoka na singel ya ufisadi kumbe kuna kitu wanakilinda
 
Kutoka kipindi cha mahojiano asubuhi hii ITV Zitto Kabwe ametangaza kumuunga mkono Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana kwa uamuzi wake wa kukataa na kukataza wanaccm kuitana waheshimiwa. Anasema tulipoacha kuitana Ndugu ndipo matabaka na kasi ya kujilimbikizia Mali na madaraja katika utoaji huduma ilipoanza. Je, Ndugu ni physchological factor katika kujenga nchi moja. Tuendelee na mjadala.

Nakubaliana na neno Mheshimiwa kuondoka kwenye jamii yetu.Linaleta ubaguzi wa wazi wazi sababu yake ni madaraka .Hata makanisani tulizoea kusikia ndugu zangu watu au wanafamilia wa Mungu , ndugu zangu wakristo nk lakini these days utasikia waheshimiwa Mapadre , Maaskofu, Mheshimiwa Baba Askofu , na mwisho anasema kwa wengine waheshimiwa watawa na wana familia ya Mungu .This is not the way .

Kinana hajaanzisha hili hata sisi wenyewe tumesha wahi kupinga hili neno maana sie watun wazima tulisha ona madhara mbeleni kabla Kinana akiwa kwenye tembo na EPA now Zitto joining him is not a taboo maana si kila jambo ni kupinga kwa kuwa aliyelitamka in bold ni CCM no.
 
Kutoka kipindi cha mahojiano asubuhi hii ITV Zitto Kabwe ametangaza kumuunga mkono Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana kwa uamuzi wake wa kukataa na kukataza wanaccm kuitana waheshimiwa. Anasema tulipoacha kuitana Ndugu ndipo matabaka na kasi ya kujilimbikizia Mali na madaraja katika utoaji huduma ilipoanza. Je, Ndugu ni physchological factor katika kujenga nchi moja. Tuendelee na mjadala.

Kumbe 'mheshimiwa' inaendana na wizi wa mali za wananchi, hivyo kutokuita waheshimiwa ufisadi utaisha. Je, na yeye ile kampuni yake ya wakala wa meli/ meli itaacha kubeba meno ya tembo kwa kutoitwa mheshimiwa?!!
 
hakuna mwanasiasa anayejua kutumia media vizuri kama Zitto.he is smart
 
Hilo Dr.alilisisitiza kwenye kampeni za 2010 ,siyo jipya ,kama kinana kaona zuri kuiga siyo mbaya
 
Hilo Dr.alilisisitiza kwenye kampeni za 2010 ,siyo jipya ,kama kinana kaona zuri kuiga siyo mbaya

Kabisa ndugu yangu. Tumelisema sana hili. Mwaka 2006 niliwahi kuhojiwa na kutamka sitaki kuitwa mheshimiwa. Ukisoma maandishi yangu au hotuba zangu bungeni ninaita watu ndugu. Hata interview ya juzi JF nimeita watu ndugu. Dkt. Slaa alilisema pia hili.

Tulipinge kwa kuwa Kinana kasema? Kinana ndio kasema baada ya sisi kusema, hivyo yeye katuiga sisi.
 
Hivi tukiwafahamu hao walioficha fedha Uswisi, tukajua na kiasi walichoficha, halafu itakuwaje? Chenge tulimfanya nini tuliposaidiwa kufahamu kuwa ana dola milioni moja kule Jersey? Tuliisha ichakachua sana ile sheria iliyoanzisha TAKUKURU. Sheria ile ya enzi za Mwalimu mtu kama Chenge angesimama yeye mahakamani kutueleza amezipataje zile pesa. Sheria ya sasa inaitaka TAKUKURU ndio ichunguze, itafute ushahidi mzito sio wa kimazingira. Itaupata wapi?

Mwacheni Zitto aendelee kujikusanyia umaarufu wa bure tu.
 
We are not Kids! Huyu ndiye alikuwa anamtetea Mhando na huyo ndiye aliruhusu huo wizi bila wasiwasi wowote. Sasa anakimbilia kwenye TV huku uso umepauka kwa Hofu ya sakata lote kumuhusisha yeye mwenyewe siku zijazo!

Zitto hawezi kuaminika ana agenda mia moja ambazo hazifikishi popote bali misifa. Mara fedha zilizoko nje ana hataki kuwataja eti anasema ni kupoteza muda wakati huo huo anaonyesha hana imani na utekelezaji wa serikali sasa anachosema ni nini?

Siku zote alikuwa wapi kujua Tanesco kuna wizi hadi Mkaguzi ameonyesha. Wizarani walipo mwambia yeye akakimbia kumtetea Mhando tatizo ka kuwa Mnafiki litamfuata . Halafu etui anamalizia kwa kusema kuwa anataka urais sasa kichekesho cha mwaka!! Uliwahi kuona chama gani cha upinzani wakamteua a double agent kupeperusha bendera yao?


Matatizo ya TANESCO si ya waziri wa sasa, ni matatizo ya siku nyingi. kama mkuu unataka amebebeshwe matatizo yote waziri mhong'o sidhani kama ni sahihi. kama una vijisent uswisi basi una haki ya kuongea hivyo. Zito alipoanzisha hoja ya buzwagi watu walisema ana taka sifa, lakini yaliyokuja baadae hope unayakumbuka. Zito alianzisha kampeni ya kutokuwa na imani na waziri mkuu matokeo yake Rais alifanya mabadiliko ya baraza la mawaziri, je huoni nalo muhimu kwa taifa? wote tunajua kuwa Zito kuwa zito hawezi kuwa Rais kwa Tanzania kwa sasa hata yeye nafikiri anajua, nafikiri anajipanga kwa baadae kwa sasa anataka kujipima. hata Rais wetu Kikwete alianzia mbali.
 
Back
Top Bottom