Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.

Tuhuma #1 :

Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

Majibu:

Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.

Tuhuma #2 :

Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.

Majibu:

Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.


Tuhuma #3 :

Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.

Majibu:

Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!

Tuhuma #4 :

Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.

Majibu:

Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.

Tuhuma 5:

Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.

Majibu:

Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.

Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):

Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

Majibu:

Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “Right or wrong, my country first". Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.

Aidha, wanatuhumu kuwa “Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa”

Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.

Tuhuma #7 :

Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.

Majibu:

Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.


Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila”.

Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.

Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:

Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.

Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).

Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.

Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!

Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC

Dodoma, 9 Novemba 2014

Uongozi si lelemama ni kujitoa mhanga kimwili na kiroho.
Mkimaliza hlo anzisheni huko Tanapa, Ngorongoro, TRA, Madini, Balozi zetu, Bomba la Gesi, Mmalizie na Halmashauri za miji na Wilaya mtamkamata mchawi wa Maendeleo yetu.

uko sahihi natamn siku moja nchi hii kila raia alipwe mshahara kwa kuwa tuna rasimali za kutosha ila tatixo ni familia chache tu
 
Bwana Zitto Ruyagwa Kabwe kwa nini usivuke daraja ukilifikia??? unachofanya sasa ni sawa na kuvuka daraja ukingali mbali na kingo za mto...Na hii inadhihirisha wazi kuwa siku zote mtoto mchokozi ndiye huwa wa kwanza kukimbilia kwa wazazi kushtaki...Bwana Ruyagwa kwanza ulikosea sana tena sana na umejishushia hadhi yako sana pale ulipotamka ati viongozi wa TPDC wapelekwe Polisi, lakini pili pamoja na kupelekwa Polisi wewe kama mlalamikaji (mtetezi wa unachokiita rasilmali za umma) ulipaswa kwenda kituoni na kufungua shauri pale..kwa kuwa ulikuwa unajua wazi kuwa unajaribu kujijengea umaarufu wa rejareja ndio maana hukuthubutu kwenda na wakaachiwa na baadaye tukapata taarifa kuwa umekiuka taratibu za kibunge...Nikija kwenye utetezi wako wote huu naona ni yale yale ya kuvuka mto kabla..Mmekwishakubaliana bungeni CAG na Dr.Hosea wafanye uchunguzi...wamefanya na kabla hawajamaliza mnakuwa watu wa mwanzo kubwatuka bungeni kwa kuwa tu mna kinga za kibunge ili muudanganye umma wa Tanzania kuwa kweli kuna ufisadi.

Kama mnao uhakika wa ufisadi huo tulieni tuliii..subirini ripoti itakuja kamati yako itapewa na bungeni itasomwa, hapo ndipo pa kuanzia kwani mbivu na mbichi zitakuwa tayari zimejulikana...Mimi nawaona wewe na Kafulila kama mnatumiwa na mna maslahi binafsi na ndio maana hamuachi vyombo vilivyopewa kazi hii vikamilishe kazi yake...Zile zama za Mbunge kuropoka na serikali kumwajibisha waziri zimepitwa na wakati kwani mawaziri wa sasa sio wale unaowadhani wapenda mshiko..hawa ni wazalendo kuliko wewe na wanafanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu...historia yao na yako zinaweza kulinganishwa ukaona wazi kuwa wewe umeibuka haraka katika kipindi kifupi tu

Bwana Zitto na Kafulila wacheni kupiga mayowe...tuachieni sisi tuone wenyewe. Zitto
hivi nyie watu huo upumbavu wenu utaishia lini? hivi kwa akili yako unafikiri zzk ni mtu wa kukaa nakuandaa kitu ili awe maarufu!? kajipange huna hoja mkuu!
 
Last edited by a moderator:
hivi nyie watu huo upumbavu wenu utaishia lini? hivi kwa akili yako unafikiri zzk ni mtu wa kukaa nakuandaa kitu ili awe maarufu!? kajipange huna hoja mkuu!
Sasa kwa mfano hii post yake, ina substance gani?
 
Pamoja na kuwa si mpambe wako tena kwa hili nakuombea mungu akulinde.
 
TUONYESHE RAFIKI ZAKO,TUTAKWAMBIA WEWE NI MTU WA AINA GANI-Hahaha-Soon true Colour za wanafiki zitajulikana-Prof.Muhongo Kafunga Maduka ya majambazi na wahujumu wa Wizara ya nishati na madini,VIBARAKA WANATAPATAPA !!!
Hao majambazi ni kina nani tofauti na hawa wanaopora 400 m kila siku? U-DC uliopewa umekufanya mtumwa na kipofu kiasi cha kushindwa kujua PAP kaingia vipi kwenye hii mikataba?!
 
Wamefikia hatua gani mkuu?

Kwani nchi uliwahi kisikia miccm imeibua uozo wanaoufanya kufisadi mali ya wananchi? Kama Si kafulila Na kamati ya Bw.Zito unafikiri haya yote yangejulikkana. Msipende kutetea mambo ya kijinga nyie ccm.wewe hapo si ajabu hata kumi hujapewa kwenye hizo fedha ila bado Tu Una ng'ang'ana kutetea majizi.
 
Kwani nchi uliwahi kisikia miccm imeibua uozo wanaoufanya kufisadi mali ya wananchi? Kama Si kafulila Na kamati ya Bw.Zito unafikiri haya yote myangejulikkana. Msipende kutetea mambo ya kijinga nyie ccm.wewe hapo si ajabu hata kumi hujapewa kwenye hizo fedha ila bado Tu Una ng'ang'ana kutetea majizi.

Ni wapi nimetetea wizi? Na haujanijibu wamefikia wapi?
 
ngozimbili usinawe vijijini tupo, nilikuwa Nakwa Babati jana maandalizi Uchaguzi wa Serikali za vijiji!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa utamaduni wa Viongozi wa Serikali ya Tanzania, tutasikia waziri fulani kajiuzulu ndio imetoka. kinacho onekana hapa Escrow A/C ni pipeline ya baadhi ya watawala kufanikisha mambo yao. Nimependa kufahamu kwako Zitto utachukua hatua ngani pale swala hili NYETI litakapo ishia kama vile la EPA baadhi ya wahusika wameachiwa huru bila hata kurudisha SENT?????????????? AU NI:yell:
 
hivi nyie watu huo upumbavu wenu utaishia lini? hivi kwa akili yako unafikiri zzk ni mtu wa kukaa nakuandaa kitu ili awe maarufu!? kajipange huna hoja mkuu!

Mkuu haya Ni majitu ya ccm achana nayo. Yatakuja hapa kupinga kila kitu we shangaa waziri wao Pinda kakiri kuwa Kuna watu wameiba lakini lijitu linakuja hapa linakanusha. Mambo ya ajabu kabisa
 
Hapa ndo aliponichekesha huyu jamaa. Anajiita mpinzani huku akiionya CCM itaanguka. Sasa yeye anataka ibaki ili iweje?

Hapo zito anataka wale wabunge wa ccm wamuunge mkono we hujamjuwa tu
 
Zitto kabwe,
kwanza umefanya vema kujitokeza kujibu tuhuma zinazokukabili lakini unaonekana kutumia akili pana sana kujibu tuhuma zako hasa kwa kutumia maneno ya kulaghai badala ya kumibu hoja asilia,ninashaka na maneno yako hasa kwenye maeneo haya,

kwanza,umesema kampuni ya shell haifanyi biashara hivi kunakampuni ambayo inaweza kuanzishwa siyo kufanya biashara? Kama haifanyi biashara inafanya kazi gani sasa.

Pili utakumbuka kwenye tuhuma zako unatuhumiwa kuazimwa au kukopeshwa kiasi cha milioni sita na kampuni moja wapo hapa nchini pesa hiyo ilitumika kwenda kumtibia mama yako kwanini hujasema hiyo pesa ulipewa kwa makubaliano gani au ulipewa kama msaada au kama mikopo mingine ili urudishe.

suala lako la kupewa hela na ubarozi wa uingeleza siyo jipya hata wakili wako ambaye sote tunamjua anayetokea mkoa wa kaskazini unamtumia sana kwenda kuchukua pesa zako za madili kutoka kwenye makampuni kadhaa unachofanya pesa nyingi huchukui wewe unatuma watu kwaniaba yako.

zipo sehemu mbili ambazo wakili wako amechukua pesa kwa maelekezo yako na amesainishwa siku moja hiyo document utawekewa hapa ila mnamuaibisha sana wakili wako japo hapendi unavyofanya lakini wewe unasema huwezi kuacha kuwasaidia waingeleza umetoka nao mbali.

jambo lingine ni wewe kutumiwa na nimrod mkono kiukweli hili unavyokataa binafsi mimi nakuona kituko mkono hajaanza leo kukutumia mpaka anakununulia ile gari ambayo kwasasa umeikodisha ni katika makubaliano yenu ya baadhi ya kazi unazomfanyia za kutumika kiukweli zitto nilikuwa shabiki wako sana tangu nijue kuwa wewe mla rushwa nakuweka kundi moja na wachumia tumbo wengine na hii tabia ya rushwa na wizi sasa umemfundisha hata deo filikunjombe.

ushauri wangu kwako fanyeni yote mnayofanya watanzania wasije kuwajua lakini siku moja wakijua mtachomwa moto mchana kweupe.

account yako imekuwa hacked?
 
....
Sina hakika kama kweli ZZK ana dhamila safi ya kupambana na mfumo wa wezi na mafisadi waliokuwa wanamfadhiri huko nyuma!!
Ana nunua kesi...ili aizime. Rejea kesi ambazo amewahi kushiriki kikamilifu....nini kilitokea kwenye kesi hizo(Ela zimefichwa uswizi,inflated gas contracts).

Hapa chakufanya...ni kutumia hizi baadhi ya taarifa anazozitoa tuzifanyie kazi...kwa ajili ya kuwashughulikia wahusika ama kwa njia rasimi ama zisizo rasimi. Huyu asipewe nafasi ya kununua suala hili.
 
Kwa niaba ya familia yangu yote na maskini wote Tanzania nasema Zitto Mungu awe nawe wala usikatishwe tamaa na hawa walio nacho wanaotaka kuturudisha nyuma ktk kila hatua tunayosogea. Pigana pigana mkuu you have our backup.
 
Last edited by a moderator:
Kwa utamaduni wa Viongozi wa Serikali ya Tanzania, tutasikia waziri fulani kajiuzulu ndio imetoka. kinacho onekana hapa Escrow A/C ni pipeline ya baadhi ya watawala kufanikisha mambo yao. Nimependa kufahamu kwako Zitto utachukua hatua ngani pale swala hili NYETI litakapo ishia kama vile la EPA baadhi ya wahusika wameachiwa huru bila hata kurudisha SENT?????????????? AU NI:yell:
Good question?

mara ya mwisho kumuona zitto amechukua hatua zaidi baada ya wabunge wa ccm kutetea ufisadi bungeni ni kwenye issue ya mkataba wa buzwagi.

Alipanda chopa na wenzake akakimbilia kwa wananchi

Siku hizi hana ujasiri wa kukimbilia kwa wananchi, sana sana anakwenda german kumalizia phd yake which is better still ama sivyo huenda facebook.

Ngoja tuone hili litaishaje,sababu uwezekano wa hiyo report kwenda bungeni mpaka sasa ni mdogo sana
 
Ni wapi nimetetea wizi? Na haujanijibu wamefikia wapi?

Unapoonekana kukwamisha hii habari ya zito Na kila kith nipo wazi mpaka waziri mkuu ameshasema.kwanini nisiseme unatetea wezi? Kuhusu hatua iliyofikiwa Ni kwamba tayari ripoti ipo kwa waziri mkuu anajipanga namna ya kuitoa kwa Bunge. Kamati ya Bw.Zitto ilishamaliza kazi take.
 
Mkuu haya Ni majitu ya ccm achana nayo. Yatakuja hapa kupinga kila kitu we shangaa waziri wao Pinda kakiri kuwa Kuna watu wameiba lakini lijitu linakuja hapa linakanusha. Mambo ya ajabu kabisa

We nae wa wspi wewe.

Nani kasema hela hazijaibiwa,au unaota?
 
We kweli Popo, kwann mnaandaa vijarida, vipeperushi, mnanunua magazeti, sijui maninini makorokocho ujinga mtupu, mara ooo kakopa mil.6 ...! Ujinga huu yaani Zitto anayetuhumiwa kupokea bil.3 kwa maCCM ili aiuwe CDM leo hana hata mil6... Akili mgando kabisa

Akili mgando.
Hata gavana wa BOT anaweza kukusa million moja.

Kuwa na pesa nyingi na kukosa kidogo ni kawaida tu katika maisha ya kila mmoja wetu.

Zitto ni fisadi ila ni mpiga dilli hata la buku kumi. Tunamjua.

Mara ngapi tunakunywa nae anaomba kulipiwa round?

Tena ya castle lite siyo jack Daniel.

Usiwe na akili mgando kama GT
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom