Zitto,
Kwanza Karibu tena JF, binafsi nashukuru kwa Maelezo yako Maridhawa, usiishie hapa tu, umekuwa kimya sana tokea Saga lako na CHADEMA, kuanzishwa ACT na Matamshi yako ya hapa na pale juu ya uanzishwaji wa UKAWA.
Back to the Main topic, Naomba kutoa comments zangu kama ifuatavyo based on your response dhidi ya kutuhumiwa Kwako kwenye issue ya escraw account
Tuhuma #1 :
Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:
Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee'. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
Kuna Madai kuwa unaitumia Gombe Advisors kuchota fedha kwenye mifuko ya akiba ya Jamii sio tu kwa Maslahi ya Wasanii kutoka Kigoma, bali ni kwa Manufaa ya kwako binafsi, Pia wadadisi wa Masuala ya Conflict of interest wanakosoa Kampuni hiyo kwenda kukopa kwenye Mifuko ya Hifadhi ikiwa wewe mmiliki wake unaiwajibisha hiyo Mifuko kupitia Kofia yako ya ueneyekiti wa PAC, some sort of kutumia Madaraka vibaya kunaweza kutafsiriwa hapa, hizi shutuma hujazijibu Mpaka Leo.
Bottom Line, Hapa hujakanusha kuwa huyo Bwana Rapahel Ongangi kuwa unafahamiana nae kwa namna yoyote
Tuhuma #2 :
Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.
Majibu:
Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.
Hapa unaonesha kuwa unamfahamu huyu mtu vyema sana.
Lakini kwanini Bwana Raphael asikanushe hayo yeye Mwenyewe?, je, wewe ni Msemaji wake, siku akijitokeza yeye Mwenyewe ama ama watu wakileta huo ushahidi utauweka wapi uso wako ?
Reffer to China wakiwanyonga some of their officials kwa kubeba Ivory kwenye their Diplomatic Bags, Membe wetu atauweka wapi uso wake ???
Tuhuma #3 :
Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.
Majibu:
Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!
Tutajuaje kama wewe ndo ulichambua ???, we need Facts, tuletee uchambuzi wako na wa Norwaay tupembue wenyewe.
Siamini kuwa wa Noorway walivujisha tu bila kuchambua
Tuhuma #4 :
Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.
Majibu:
Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.
Hapa unarudia Makosa ya hapo Juu ya kuwa Msemaji wa Bwana Raphael.
Hapa unajipachika usemaji wa Kampuni ya SHELL
Tuhuma 5:
Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.
Majibu:
Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.
Hapa tena unajipa Kazi ya usemaji wa Serikali ya Kenya katika kuisafisha na Kumsafisha Bwana Raphael.
Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):
Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.
Majibu:
Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile.
Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu', ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema "Right or wrong, my country first". Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.
Aidha, wanatuhumu kuwa "Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa"
Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.
Hapo kwenye RED and BOLD, inaelekea kuna unachojua dhidi ya hao wana Siasa, huenda nao kuna wanachojua dhidi yako.
Waarabu wa Pemba wajuana kwa Vilemba
Tuhuma #7 :
Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.
Majibu:
Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.
Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa "Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila".
Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.
Intentionally left Blank
Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:
Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.
Then what happened baada ya hawa jamaa kusekwa ndani ??
Je, kuna ambaye amajiuzulu ?, je wakishinda hii kesi wewe na Kamati yako mko tayari kuwajibika ???
Naoma hili tuliweke kwenye kumbu kumbu Tutahitaji Mrejesho kutoka kwenye kamati yako regarding this.
.
Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiende
Hapa unaonekana kuihurumia CCM na Serikali yake kwa kuipa anaglizo.
WTF !!!!!!!!!!! ????????????????
===============================
Nachelea Kusema Pia maelezo yako mengi ni ya Jumla jumla sana na hayana facts akama ambazo umetaka kupewa na unaodai wana kuchafua.
Pia, na wewe Kama msomi, akili Kubwa kama unavyojinadi / nadiwa, umerudia Makosa yale yale aliyoyfanya MFA jana kwa kujigeuza Msemaji wa China bila facts kwa kukanusa tuhumua za EIA kuwa Kwenye Dimplomatic Bags az Msafara wa Rais, Pembe za Ndovu zilibebwa.