uaminifukazi
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 1,481
- 928
Naona POMPO ameenda kuchukua maelekezo zaidi.
Hao ni walevi na watumwa wa wanasiasa tu wala wasikupotezee muda wako ndg.
Last edited by a moderator:
Naona POMPO ameenda kuchukua maelekezo zaidi.
Jamani, kwani Zitto alipoweka hoja hapa tulipaswa kukaa kimya? Je, si haki ya kila mmoja kufikiria kwa namna anayoona?NGURUV3,MCHAMBUZI na Pro-Chadema wanazi nyie ndo hamna hoja zaidi ya kutuletea ushabiki mandazi. Tatizo mna mahaba mazito na chama badala ya nchi na inawezekana hata hayo mahaba yapo ki maigizo zaidi ajenda kuu ikawa ni kusaka tonge tu.
Popote pale jina la Zitto linapokua likijitokeza mmekua mstari wa mbele kumshambulia na viroja uchwara vyenu. Hakuna mahali mliwahi kumuunga mkono siku zote mmekua ni watu wa kumkosoa na kumponda wakati wapuuzi kama akina Lema,Mnyika na sugu mmekua mstari wa mbele kupalilia hoja zao hata kama ni za kipuuzi.
Bshaka mmeamua watu waibe bilioni 200 kuliko kuipa hoja nguvu kwani mmehisi kuna watu itawang'alisha!!! Dah siasa za Bongo ni majanga.
Hiyo (red) hata mimi naiunga mkono maana kila ninaposoma upuuzi wa watu fulani humu natamani tungepata nafasi ya kutambuana japo kidogo tuone kama wangeendelea kuandika kama wanavyoandika hawa watu. Mi nadhani huu utaratibu wa anonymity unachochea sana kupost pumba na bangi kwenye jamii forum.
Bora 200Bil ziibiwe lakini si Zitto kuwa shujaa kwenye hili SAGA, teh teh teh
Hao ni walevi na watumwa tu wa wanasiasa wala wasikusumbue ndg.
swali zuri sana mkuu!
kwanza ni wazi unaonyesha unatambua na kukubali juhudi na jitihada zinazofanywa na mzalendo zzk.
kuhusu swali lako ni kukumbushe tu kitu kimoja watanzania tutakua tunafanya dhambi kubwa na takatifu sana kama majukumu mazito kama hayo tutayaacha kwa mtu mmoja tu! mtu ambae cheo na dhamana ya cheo chake havina nguvu ya kutosha kufanya kila kitu, habari ya ufisadi si ya kumwachia mtu mmoja mkuu
lingine mkuu lazima ujue kwamba zzk anafanya lile lililo ndani ya uwezo wake mengine anawaachia wengine wenye mamlaka nayo!
Agree with you 100%Bora 200Bil ziibiwe lakini si Zitto kuwa shujaa kwenye hili SAGA, teh teh teh
Loading .........nimesoma taarifa za kibenki za Mkombozi ni fedheha sana ........still loading.........
If you want to kill a dog... call it a bad name
NGURUV3,MCHAMBUZI na Pro-Chadema wanazi nyie ndo hamna hoja zaidi ya kutuletea ushabiki mandazi. Tatizo mna mahaba mazito na chama badala ya nchi na inawezekana hata hayo mahaba yapo ki maigizo zaidi ajenda kuu ikawa ni kusaka tonge tu.
Popote pale jina la Zitto linapokua likijitokeza mmekua mstari wa mbele kumshambulia na viroja uchwara vyenu. Hakuna mahali mliwahi kumuunga mkono siku zote mmekua ni watu wa kumkosoa na kumponda wakati wapuuzi kama akina Lema,Mnyika na sugu mmekua mstari wa mbele kupalilia hoja zao hata kama ni za kipuuzi.
Bshaka mmeamua watu waibe bilioni 200 kuliko kuipa hoja nguvu kwani mmehisi kuna watu itawang'alisha!!! Dah siasa za Bongo ni majanga.
Jamaa anataka watu wote wachangie kwa kumsifia Zitto, Wachangie kwa namna moja yaani pambio liwe lilelile kwa style tofauti lakini lengo liwe moja, watu wakihoji wanaambiwa wana chuki...Jamani, kwani Zitto alipoweka hoja hapa tulipaswa kukaa kimya? Je, si haki ya kila mmoja kufikiria kwa namna anayoona?
Nimeweka hoja, ingekuweka vema basi zingejibiwa ili ujinga na viroja uchwara wangu uonekane.
Ingekuwa vema ukaonyesha wapi wengine tumepalalia hoja za kina Manyika.
Hivi Mnyika ameandika chochote au kutajwa katika sakata hili?
Laiti zitto asingeweka habari hii, 'tungemshambuliaje''
Naikuombe, kwa niaba ya Zitto hebu tufahamishe maswali na hoja zetu tulizosema.
Tunajifunza kutoka kwa kila mmoja, badala ya kusema ni msaliti au mzalendo ni muhimu tukatafuta ukweli.
Kwa mfano, Zitto amesema kampuni ya Gombe ni ya ushauri. Tumeuliza hii kampuni na ile ya Laketugite zinafanya kazi moja zikiwa na wamiliki wale wale?
Pili, Zitto ametuhumiwa kutumia kampuni ya Gombe na Ongangi.
Tunauliza, je ni kweli Ongangi ni mshiriki wa kampuni ya Gombe? Kumbuka aliyeleta hoja hizi ni Zitto, sasa tusaidieni tuelewe kwa uchache tu kama Ongangi ana ushiriki au la! Mbona ni mambo rahisi.
Waberoya , CCM ni mafisadi hilo halina mjadala, lakini je kuna makosa watu wakitaka usahihi wa maelezo aliyetoa Zitto?Grant! kutwa kucha hawahawa ndio wanapiga kelele CCM mafisadi, mafisadi, matusi kibao wengine wanaandika atricle ndefu kama biblia klaumu CCM!
wanapotokea watu wachache kusimamia vilio vyetu, walewale wanaoonekana vinara wa mabadiliko wanaCHAGUA nani angesema hili walasio zitto! ila angekuwa Lissu au Mnyika ungeshangaa mioyo yao inavyofurahi
wengine wanataka zitto akiisha anzisha hili, awakamate hao mafisadi na awaweke ndani kabisa, kana kamba zitto ni mtu pekee nchi hii anayeawa kuwajibika na mafisadi! akisema jambo akashindwa katikati kwa kukosa support, wale wale wataamka na kusema mnafii huyu...anataka political gain au popularity!!!!
huwa siwaelewagi watanzania....unaweza ukafikiri ni swala la elimu..no, tatizo letu liko damuni kabisa, liko ndani kabisa ya genes na bongo zetu; hatujielewi hatujijui
kwa bora 200bn ziende ila zitto akae kimya!!! this is a shame of this generation
Tuhuma #1 : Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee'. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
wakuu kuweni na huruma na nchi yenu, hata kama mna chuki na zitto, haiwasaidii
As long ataokoa pesa za walipa kodi basi hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea kwa mungu
Huyu mwizi na tapeli siyo mtu wa kusamehewa hata chembe anahongwa na waingereza kuvuruga nchi yake halafu useme tumsamehe kwa kipi,msaliti na mnafiki kamwe hasamehewi kamwe akafie mbali kabisa....Nafikiri ifike mahali watanzania na vijana wenzangu tujifunze kusamehe na kusema(Let it go)..Jamani dunia unatucheka...Hata kama kuna mahala Mh:Zitto amewakwaza tusamehe twende mbele kwa masilahi mapana ya nchi yetu Tanzania...Hatuwezi kuwaacha hawa mafisadi/wezi wa rasimali zetu watambee na kutembea vifua mbele...Kuna watu humu Jf mungu kawapa(God gifted) upeo wa kipekee sana kujadili na kujenga hoja kwa hamasa,mashiko na weledi wa hali ya juu kwa mfano:MCHAMBUZI na wengine ila leo hii wamweshindwa kabisa kutuunganisha kwa pamoja kwa hoja zao makini dhidi ya wizi huu wa Tegeta Escrow wamebaki kumjadili Mh:zitto tu na kuacha hoja ya msingi, Kila binadamu ana mapungufu na hakuna binadamu aliyekamilika...Yatosha sasa ya Mh:Zitto yamepita tusonge mbele tuna mengi ya msingi sana ya kujadili...tunavyoongea sasa hakuna dawa mahospitalini Msd(Bohari ya dawa) wanaidai serikali zaidi ya billion 90 na wahisani wamegoma kabisa kuchangia budget yetu mpaka uchunguzi wa sakata hili la Tegeta Escrow utakapokamilika...Mwisho kama Taifa tusipojenga utamaduni wa kusameheana na kuamaniana siku zote adui yetu atakuwa anatumia udhaifu huo....Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Tena basi watu tunahoji kwa kutumia maneno ya Zitto, hakuna neno la pembeni.Jamaa anataka watu wote wachangie kwa kumsifia Zitto, Wachangie kwa namna moja yaani pambio liwe lilelile kwa style tofauti lakini lengo liwe moja, watu wakihoji wanaambiwa wana chuki...
Waberoya , CCM ni mafisadi hilo halina mjadala, lakini je kuna makosa watu wakitaka usahihi wa maelezo aliyetoa Zitto?
Kwamba, tulitakiwa tushangilie tu bila kutumia chembe ya fikra.
Kuna maswali yanayotokana na hoja za Zitto, si hoja za watu na hapo ndipo watu wajikite.
Endapo wewe umeamini kuwa anachosema ni sahihi hilo si kosa.
Ni mtazamo wako, na wala wale wanaohoji hawana maana ya kupingana na anayosema.
Wanachotaka ni kujiridhisha kuwa kinachosemwa ni sahihi na kutoka vyanzo clean.
Hapa ni mfano tu wa kukumbusha nini wengine tunahoji
Tuhuma dhidi ya Zitto na Ongangi zinahusu kuanzishwa kwa kampuni ya Gombe.
Anasema hivi
Swali ni kuwa, pamoja na Gombe kutojihusisha na biashara ya mafuta na gesi,na kuwa ni kampuni ya ushauri, je, kuna ukweli au uongo gani kuhusiana na Ongangi kuwa mshiriki wa kampuni?
Hilo tu. Anatakiwa aeleze kama Ongangi ni mshiriki au la, je, kuna tatizo gani kuhoji hilo?
Hebu tuanzie hapo halafu tutaendelea kuangalia maelezo yake moja baada ya jingine.