Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto kama uko serious katika hili sakata tunakuomba uweke bayana majina ya wahusika! Bado tuna kumbukumbu ya zile trillions za Uswis ulivyoipotezea ...
 
- You know, I don’t get my super friend and brother Zitto Kabwe. Mara leo unakiunga mkono CCM, mara anaishambulia. I mean I don’t get unless someone helps me. You can’t eat from two enemies. Either you are with us or against us.

-Ha! ha! ha! ha! ha! ha! Watanzania, msidanganyike. Hizi kujitetea na kujaribu kujisafisha kwa huyu bwana. Kuna jambo, na ni kwa nini atumie nguvu nyingi kabla ya report ya CAG kutolewa? Jiulize………Mnakumbuka kuna viongozi wa upinzania wametajwa? Tuone Zitto atachomokaje . Kumbuka Albert msando alipokea fedha kwa niamba ya…………….? Ushahidi hupo

- Sam Sholei alikuwa Managing Director wa Mwananchi Communication. Baada ya kugundulika kwamba permit yake kuisha, alilazimika kurudi kwao. Zitto Kabwe aliingia kati na kupiga kelele sana, akimtetea Mr. Sholei kwa nguvu zake zote. Je ni kwa nini Zitto alifanya hivyo? Ni kwa sababu, Zitto alipewa fedha nyingi sana na Mwanamke mmoja anayeitwa Gladys Sholei ambaye ni mke wa Sam. Zitto alipewa offer ya kwenda vacation kwenye moja ya visiwa ndani ya bahari ya Indi.

- My super friend Zitto leo anaishambulia CCM sana tu akitafuta attention, kana kwamba amesahau fadhila za CCM kwake. You know, mara nyingi Mbwa kamwe amng’ati anayemlisha. Zitto you know historia yako ndani ya CCM ni ndefu. Ulipotaka uwaziri wa nishati na madini tena kwa kulazimisha unadhani ni vitu ambavyo tumeshavisahau? ACT-Inapumua kutokana na fadhila za CCM sasa kelele za nini kutuma watu kukusafisha wakati unajua umechafuka pasipo kusafishika. Sasa nakubaliana ni kwa nini CHADEMA walikufukuza, sababu Kubwa UNAFIKI.

Wewe njoo na I'd yako hakuna Sababu ya kujificha wakati muandiko unaonekana!
 
Kwanza, nisisitize Tena Kwamba Nilikuwa shabiki wa zitto, sikuwa muumini wa philosophy yake kwani sioni any political or economic philosophy on zitto Bali nilichoona ilikuwa ni hoja zilizokuwa Zimejaa uzalendo na uchungu kwa nchi yake, zikiambatana na clean sheet when it comes to kujihusisha na hujuma za aina yoyote, basi.

Pili, najisikia Faraja sana unaponihusisha na Nguruvi3 Kwamba ninamtegemea sana kwa hoja. Mimi ni mtu wa Kujifunza constantly na Jamiiforums ni sehemu kubwa sana ya Shule Kwangu. Kwahiyo Mimi kutegemea mawazo Kama ya nguruvi3 ni kweli Tupu, kwani Watu Kama yeye Ndio wamenifungua sana akili na kuwa mwelewa zaidi wa masuala mengi sana ya kisiasa nchini.

Tatu, nashukuru angalau Leo umejibu hoja zangu kwani siku zote umekuwa ni mtu wa kukimbia hoja, rejea mijadala mingi ya zitto ambapo tumekuwa tukijadili masuala mbalimbali, hasa juu ya zitto na wenzake kuamua kuwa wasaliti wa mabadiliko for personal gain, huku washauri wake Kama wewe, lakini hasa prof kitila akiweka wazi Kwamba mikakati ya ACT ni kuanzisha upinzani wa kupambana na chama cha upinzani "chadema, badala ya a common enemy - chama tawala cha CCM.

Nne, Katika mchango wako hapo juu, by reading between the lines, unashambulia badala ya kutoa hoja huku ukiweka mazingira ya kukimbia my counter arguments kwa hoja za kitoto Kwamba 'hauna muda wa Kujadiliana na Mimi'. Kama kweli ulikuwa hauoni maana Katika hoja zangu, ungezipuuza tu Kama Wengine na kujadili hoja nyingine au ungebakia Msomaji tu Kama Wengine.

Tano, Kama kumkosoa zitto ni "kuchemka", na kumuunga Mkono zitto ni kuwa intelligence & enlightened", basi let me remain to belong in the former (mchemkaji), lakini Kama ambavyo tumekuwa tukiwaeleza Hapa na elsewhere, Nendeni mkawadanganye Wengine, sio sisi. Sisi Kama vijana bila ya kujalisha itikadi zetu, Tulimkubali sana zitto - hoja zake na tulimuunga Mkono, lakini sasa tumeona his true colors, na hatumtaki Tena, kwani historia imeshaandikwa Kwamba zitto ni msaliti wa mabadiliko, sio Shujaa au kiongozi wa mabadiliko. Tumejadili kwanini kwa kirefu, na Kama mnapinga Hilo, mleteni kwenye mdahalo.

Nimalizie kwa msisitizo Tena Kwamba "zitto wa buzwagi sio zitto wa escrow." Kama nyie "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".

Cc Ritz


Sent from my iPhone using JamiiForums

shida ni hii mkuu! kwenye kundi la vipofu chongo ni mfalme
zzk ni chongo na wanaobakia ni vipofu so automatically hata kama hutaki hakuna mbadala wake kwa tuliokua nao

nikuulize swali moja mkuu sasa hivi unamshabikia nani baada ya kuacha kumshabikia zzk!?
 
Last edited by a moderator:
Unapoteza muda wako, Zitto sio level yako na ata alipoanza siasa sio wewe uliyempandisha na vivyovivyo huna uwezo wa kumshusha, kwani umechaguliwa lini kuwa msemaji wa vijana wa Watanzania?hivi si wewe uliyeshindwa ata kuwashawishi wana Kinondoini ukaangukia pua?sasa kama uliwashindwa hao ndio utaweza leo kuwashawishi Watanzania kuhusu Zitto?endelea na chuki zenu sie tunaendelea na taifa letu.

Nadhani saizi unahangaika kupalilia kwa Mbowe, endelea kutumika tu, wakati wewe unatumika na kusubiri kula kwa fadhira vijan wenzako wanapigana wenyewe kutengeneza historia zao za kisiasa, na kwa hili mtabaki kuandika tu jf.

Hamuwezi kuongea hadharani maana mtapigwa mawe kwani kwenye hili umma wa wazalendo wa Tanzania upo na PAC inayoongozwa na Zitto.

Naona huu ujumbe umemuingia vizuri sana Mchambuzi! Watanzani chuki zinatupofusha hadi tuko tayari kuungana na maadui kuhakisha tunao wachukia hawafanikiwa hata kama walilo libeba lina maslai kwa Umma!

Hivi kweli kama mnataka hili jambo alibebe kafulila mwenyewe na apigane mwenyewe bila support kweli atafanikiwa? Mna uhakika hapati support ya mtu yeyote? Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.. kwenye maswala ya msingi watu wanatakiwa kupunguza chuki na kusikiliza engine bila kusahau kuwavumilia!

Kafulila hii vita haiwezi mwenyewe bila support ya wengine!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wala sitishii Bali nasubiri wakati ufike na na kuhakishishieni kama nipo hai lazima niuweke ushahidi wa zitto kuwa ni mnafiki sio mzalendo hata kidogo na nayajua hadi ya Kigali anayoyafanya

Wakuu nasubiri hizo ripoti zikabidhiwe ila narudia kusema Taifa hili linahitaji wazalendo sio chini ya 10000 nchi nzima na wenye nia ya dhati na si maneno kama ya zitto.

Baada ya ripoti nitaweka ushahidi huo kwa I D ya jina langu kamili humu tumo watu Tofauti na tunaishi maisha Tofauti na kazi Tofauti name pia uwezo wa kuamua na kuthubutu ni tofauti..

Wahalifu wa wizi wa Mali za umma wanadhani Jf ndo mahali pa kushitakia na kudanganyia watanzania ili Leo na kesho waje waseme zitto alisema hivi kamati yake ilifanya haya..

Tatizo tunahitaji mabadiliko ya watanzania wengiii na sio mmoja mmoja,Mimi pia msishangae nikanunuliwa nisije tenaa humu kwani Pesa ni balaaa cha msingi watanzania tubadilike Tuamue maamuzi magumu Tuna weza ila Hatujaamua...

Thanks

Keisha habari yako huna hoja! kumbe una price tag!?
 
Zitto unawaumiza wahafidhina, yaani wewe ni mwiba mchungu sijapata kuona.
 
Safari hakika ni ndefu sana maana watu wako tayari kuona Swala linakwama kuliko Zitto kuonekana ametoa mchango!

Bora hata vichwa panzi wafata mikumbo na ushabiki mandazi waliojaa hapa jukwaani ukiwakuta kwenye siasa za ushabiki mav.i huwezi kushangaa na unawachukulia poa tu kwasababu tumeshawazoe kila siku hapa jf wao ni kutema pumba tu. Sio Ccm wala Chadema kote wamejazana.

Tatizo linakuja pale unapokuta watu tunaowaheshimu hapa jukwaani kwa chambuzi zao makini na shule tunayoipata(ga) unapowakuta kwenye hizi siasa za majitaka,chuki na visasi visivyoisha vya kumchukia mtu na kuanza kumjadili mtu badala ya hoja zake.

Sawa hata kama tunatofautiana katika mambo mbalimbali lakini yapo baadhi ya mambo inabidi yatuunganishe kama watanzania mf kama huu wizi wa escow. Mtu kama MCHAMBUZI sio wakujitoa ufahamu kiasi hiki na kuanza kumjadili Zitto badala ya hoja iliyoko mezani na zaidi kutoa sapoti. Inasikitisha kwakweli unapokua na watu kama hawa kwani ugonjwa wao ni mbaya sana. Bora uishi na wagonjwa wa UKIMWI kuliko kukaa na WANAFIKI kama akina Mchambuzi.
 
Zitto unawaumiza wahafidhina, yaani wewe ni mwiba mchungu sijapata kuona.

Wivu tu ndo unawasumbua na baadhi yao wametafuna hii fedha ya escow ndio maana wako busy kupanga namna ya kugawana vyeo kwenye serikali ya kusadikika 2015 badala ya kupiga kelele nchi nzima huu wizi wa escow.

Hii agender ingebebwa na mnyika, msigwa au lema ndo ungewaona jinsi wanavyoishkia bango hii agender.... hao watu wanafiki sana.
 
....

Tatizo linakuja pale unapokuta watu tunaowaheshimu hapa jukwaani kwa chambuzi zao makini na shule tunayoipata(ga) unapowakuta kwenye hizi siasa za majitaka,chuki na visasi visivyoisha vya kumchukia mtu na kuanza kumjadili mtu badala ya hoja zake.

.....
Unatakiwa ume mmoja wa wanatafakuri yakinifu/fikira pevu ama kwa lugha nyingine Great thinker kama sijakosea mantiki....kugundua kile ambacho Zitto analenga kukifanya kwa kuteka mjadala/mkakati wa kuwashughulikia wezi wa mali za watanzania. Sisi ambao tuna tafakuri za wastani ama chini (Rejea Fig.1 Revised Blooms Taxonomy) lazima tupate wakati mgumu kujua kitu anachokifanya Zitto kwa sasa.

mfano anapoandika "...Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege! ...." unajua maana yake nini ?

Kumbuka hii sentensi ndiyo ambayo amefungia maelezo yake. Unajua umuhimu wa sentensi ya mwisho kwenye maelezo marefu kama hayo aliyoyatoa? Zitto anashahada mbili za masomo(Bachelor na Masters) tena aliwahi kusema alihitimu shahada hizo kwa good grades. Hivyo anapomalizia maelezo yake kama yale kwa sentensi ile. Lazima uwe katika level 4 ya Revised Bloom's Taxonomy na kuendelea ndiyo unaweza kujua ana maanisha nini. Wadau wengi wameeleza vya kutosha...juu ya kile anacholenga. Ebu soma tena maelezo ya Mchambuzi kwenye post zake za awali kwa makini kwenye uzi huu.

Ninachofurahi sasa hivi hata sisi tulioko chini ya level 4 tunaanza kutambua kwa urahisi nia za watu kama yeye.


M9e7ce7cdee8631f8fd5754a0bed68f59.png
 
Mkuu umejishusha sana, na ndio mana una m copy Nguruvi

imefikia muda huna akili zako, ila unashikiwa na akina Nguruvi ambao wanarukaruka tu na hoja za kujikomba

kumbe unakuwa mshabiki wa watu humu?? na sio philosophy za watu?

Yet unataka mabadiliko??

Hoja iko mezani take it positive jadili kama mzalendo kweli, kuwa ulikuwa unampenda zito na leo unamchukia kana kwamba una una ushahidi na eti anajisafisha ni kuishiwa hoja na haukupaswa kusoma; kubali kuwa umechemka na Mr. Waberoya hatakuacha upite bila kuelezwa kuwa umechemka!!
Waberoya , sijui kwanini inakukera mtu akini copy. Nadhani hiyo ni uhuru wa mtu na wala haiingiliani na hoja iliyopo mezani. Kuna kosa gani Mchambuzi au Sangarara wakini copy?
Inaingilanaje na hoja za Zitto, Harbinder Singh au StatOil?

Pili, hoja iliyopo mbele ni tuhuma na majibu ya Zitto, wala siyo Nguruvi3 ambaye hajachangia chochote hadi wakati huu.

Ni muhimu tukajikita katika hoja kuliko kufanya character assassination bila sababu za maana wala za kujenga.
Kama lipo linalomhusu Nguruvi, ni vema ukaliekeleza kwake katika uzi unaomhusu na si kumchanganya na hoja zilizo mbel yatu.

Tkukirudi katika hoja za Zitto
1. Kwamba Harbinder Singh aliangusha serikali ya KANU na CCM wakimukubatia ataangusha serikali yao.
Mkuu Zitto, kwani hoja zako ni masilahi ya taifa au ni kulinda CCM?

Unachokifanya kinaweza kuangusha serikali ya CCM, hapo huoni iunajichanganya mkuu.

Kwani kashfa ikiangusha serikali wewe una hofu gani hasa tukijua ni 'mpinzani''.
Kitu gani kinakutia hofu, kashfa hii ikiangusha CCM?

2. Kuna hoja ilitolewa mitandaoni kuwa ulipewa kiasi cha pesa kwenda kumtibu marehemu mama yako mzazi.

Hapa ulitakiwa ukanushe tu kuwa hujapewa kiasi hicho. Maelezo yako mengi hayajatoa jibu tarajiwa.
Habari ya kwenda kwenye vyombo vya sheria ni yako, watu walitaka kusikia ulichukua au hukuchukua.

3. Umesema bwana Ongangi amesomea Tanzania, ameoa na watoto, hivyo basi watu walete ushahidi wa passport ya Tanzania.
Sidhani kama ulipaswa kutueleza maisha ya Ongangi katika family level.

Hapa inaonyesha unajenga uhalali wa Ongani kuwa Mtanzania.
Tatizo ni kuwa hujajibu hoja zinazomhusu Ongangi na wala hatukuhitaji kujua Ongangi ana wake wangapi au wajukuu wangapi.
Je, mnafahamiana na Ongangi? Na mnfahaminiana katika kiwango gani?

4. Umesema kampuni ya Gombe haifanyi biashara ya mafuta na gesi.
Kumbuka kuwa si lazima iwe biashara ya gesi na mafuta.

Tumeona makampuni yakianzishwa mengine ya ulimbende lakini pia yakitumika kama 'conduit' ya dili nje ya malengo yake.
Hivyo haitoshi tu kusema Gombe haishughuliki na mafuta, unapaswa kuisafisha Gombe kama haihusiki kwa namna yoyote na transaction zinazoweza kutokea nje ya shughuli zake za ushauri.

Pia unapaswa kutueleza kama ni kweli au si kweli kuwa wewe na Ongangi ni washirika wa Gombe company.

Hili hujalifananua umetueleza kuhusu kazi za Gombe, wakati tuhuma zinaelekea katika uwepo wa ushirika katika kampuni hii.
Hili liwekwe sawa kama lilivyotuhumiwa kuliko ufafanuzi wa kazi za Gombe

5. Kama sitakuwa nimekosea, kuna wakati umehojiwa na kituo kimoja cha TV na kueleza kuhusu shughuli za kampuni ya Lakelitugike kama mshauri wa Kigoma all star( nisahihishwe kama nimekosea).
Sasa kuna hili la Gombe. Hizi kampuni zinafanyaje kazi katika mtindo mmoja

6. Kuna tuhuma kuhusu mbunge Mkono. Huko nyuma tuliambiwa umechukua gari.
Leo unasema haya ni mambo madogo ya kutuondoa katika mstari.
Ni kweli, lakini pia kumbuka mambo haya yana mlolongo mkubwa.

Pengine hili ungeliweka wazi zaidi kuliko kusema ni propaganda tu.
 
Sasa Zitto kuwaambia CCM kuwa huyo singasinga aliiangusha serikali ya KANU na ndo anakoelekea kuiangusha serikali ya CCM kosa linakua wapi? Jaman mbona mnapenda kuifanya siasa ni vita kwa vihoja vya kipuuzi kama hivi????

Yaani wewe maelezo yote ya Zitto umeona hilo la KANU tu??? Kweli ukiamua kuishi kwa kuendeshwa kama remote taabu tupu.
 
Sasa Zitto kuwaambia CCM kuwa huyo singasinga aliiangusha serikali ya KANU na ndo anakoelekea kuiangusha serikali ya CCM kosa linakua wapi? Jaman mbona mnapenda kuifanya siasa ni vita kwa vihoja vya kipuuzi kama hivi????

Yaani wewe maelezo yote ya Zitto umeona hilo la KANU tu??? Kweli ukiamua kuishi kwa kuendeshwa kama remote taabu tupu.
Ndugu yangu, nisome vizuri. Ninaomba ufafanuzi kuhusu aliyosema. Kaweka mada, tunaijadili. Inategemea mtu ameisoma na kuielewa vipi. Kuna sehemu sijaelewa ndio maana nimeweka alama za kuuliza, na pia kumsihi afafanue.
Hayo ambayo sikuuliza, ima nimeyaelewa au la, nimekuabaliana nayo au la. Kwa vile sina ground nimeyaacha kama yalivyo. Yel yanayotatiza ndiyo nimeyaeleza, tatizo liko wapi ?

Ukweli hautafutwi kwa herufi moja au neno moja. Hebu tujenge hoja tuache ushabiki
 
Ukweli una tabia ya kubaki ukweli milele. It is just a matter of time, kama wanakuzulia jambo we endelea tu ukweli utakupigania hata utakapokuwa kaburini na uongo utakufukua hata ukiwa kaburini pia na kupata adhabu japo kwa vizazi vyako vitakavyosalia. Usihofu, umezaliwa siku moja na siku moja utakufa pia.
 
Sakata hili la Zitto + IPTL linanikumbusha play moja nilisoma kidato cha tano iliyoitwa "AN ENEMY OF THE PEOPLE" yani ukisoma mule ndani utamkuta Dr.Thomas Stockman ambaye ndiyo mamfananisha na Zitto, Kitendo cha Dr.Thomas stockman kusimama na kupinga urasimu na ufisadi wa municipal pipe kulimfanya awe baptized thus as an enemy of the people, lengo la watawala wale lilikuwa ni kubadili upepo kutoka allegation zinazowakabili juu ya ubadhilifu na kuamua kumuattack Dr.stockman kwa personal issues ili kubadili tension ya watu.
 
Last edited by a moderator:
NGURUV3,MCHAMBUZI na Pro-Chadema wanazi nyie ndo hamna hoja zaidi ya kutuletea ushabiki mandazi. Tatizo mna mahaba mazito na chama badala ya nchi na inawezekana hata hayo mahaba yapo ki maigizo zaidi ajenda kuu ikawa ni kusaka tonge tu.

Popote pale jina la Zitto linapokua likijitokeza mmekua mstari wa mbele kumshambulia na viroja uchwara vyenu. Hakuna mahali mliwahi kumuunga mkono siku zote mmekua ni watu wa kumkosoa na kumponda wakati wapuuzi kama akina Lema,Mnyika na sugu mmekua mstari wa mbele kupalilia hoja zao hata kama ni za kipuuzi.

Bshaka mmeamua watu waibe bilioni 200 kuliko kuipa hoja nguvu kwani mmehisi kuna watu itawang'alisha!!! Dah siasa za Bongo ni majanga.
 
Back
Top Bottom