Mkuu umejishusha sana, na ndio mana una m copy Nguruvi
imefikia muda huna akili zako, ila unashikiwa na akina Nguruvi ambao wanarukaruka tu na hoja za kujikomba
kumbe unakuwa mshabiki wa watu humu?? na sio philosophy za watu?
Yet unataka mabadiliko??
Hoja iko mezani take it positive jadili kama mzalendo kweli, kuwa ulikuwa unampenda zito na leo unamchukia kana kwamba una una ushahidi na eti anajisafisha ni kuishiwa hoja na haukupaswa kusoma; kubali kuwa umechemka na Mr. Waberoya hatakuacha upite bila kuelezwa kuwa umechemka!!
I thought uko tofauti na akina Mbowe, kumbe hata wewe walikupata??
looser!! kumbuka hicho ni kidonge sina muda wa kujibishana na mgonjwa, meza au tema mimi simo
Kwanza, nisisitize Tena Kwamba Nilikuwa shabiki wa zitto, sikuwa muumini wa philosophy yake kwani sioni any political or economic philosophy on zitto Bali nilichoona ilikuwa ni hoja zilizokuwa Zimejaa uzalendo na uchungu kwa nchi yake, zikiambatana na clean sheet when it comes to kujihusisha na hujuma za aina yoyote, basi.
Pili, najisikia Faraja sana unaponihusisha na
Nguruvi3 Kwamba ninamtegemea sana kwa hoja. Mimi ni mtu wa Kujifunza constantly na Jamiiforums ni sehemu kubwa sana ya Shule Kwangu. Kwahiyo Mimi kutegemea mawazo Kama ya nguruvi3 ni kweli Tupu, kwani Watu Kama yeye Ndio wamenifungua sana akili na kuwa mwelewa zaidi wa masuala mengi sana ya kisiasa nchini.
Tatu, nashukuru angalau Leo umejibu hoja zangu kwani siku zote umekuwa ni mtu wa kukimbia hoja, rejea mijadala mingi ya zitto ambapo tumekuwa tukijadili masuala mbalimbali, hasa juu ya zitto na wenzake kuamua kuwa wasaliti wa mabadiliko for personal gain, huku washauri wake Kama wewe, lakini hasa prof kitila akiweka wazi Kwamba mikakati ya ACT ni kuanzisha upinzani wa kupambana na chama cha upinzani "chadema, badala ya a common enemy - chama tawala cha CCM.
Nne, Katika mchango wako hapo juu, by reading between the lines, unashambulia badala ya kutoa hoja huku ukiweka mazingira ya kukimbia my counter arguments kwa hoja za kitoto Kwamba 'hauna muda wa Kujadiliana na Mimi'. Kama kweli ulikuwa hauoni maana Katika hoja zangu, ungezipuuza tu Kama Wengine na kujadili hoja nyingine au ungebakia Msomaji tu Kama Wengine.
Tano, Kama kumkosoa zitto ni "kuchemka", na kumuunga Mkono zitto ni kuwa intelligence & enlightened", basi let me remain to belong in the former (mchemkaji), lakini Kama ambavyo tumekuwa tukiwaeleza Hapa na elsewhere, Nendeni mkawadanganye Wengine, sio sisi. Sisi Kama vijana bila ya kujalisha itikadi zetu, Tulimkubali sana zitto - hoja zake na tulimuunga Mkono, lakini sasa tumeona his true colors, na hatumtaki Tena, kwani historia imeshaandikwa Kwamba zitto ni msaliti wa mabadiliko, sio Shujaa au kiongozi wa mabadiliko. Tumejadili kwanini kwa kirefu, na Kama mnapinga Hilo, mleteni kwenye mdahalo.
Nimalizie kwa msisitizo Tena Kwamba "zitto wa buzwagi sio zitto wa escrow." Kama nyie "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".
Cc
Ritz
Sent from my iPhone using JamiiForums