Wingi wa mistari/maneno si kipimo cha uthabiti wa hoja,aliyekuwa anahutubia hotuba ndefu majukwaani kiasi cha kuaminishwa kuwa umahiri wake wa kuhutubia hotuba ndefu utalisaidia Taifa amefanya nini hadi sasa zaidi ya kuligawa Taifa?Maneno huishi,hotuba za Baba wa Taifa hadi leo bado zinatumika kuchota busara na maadili ya uongozi,ikitokea leo hii Mungu akampenda "Mwenye heri " wetu na kumuita ili akampe daraja kamili la "utakatifu",ni neno gani lililotoka katika kinywa chake chenye wingi wa maneno liwezalo kutumika kama kielelezo cha busara na hekima zake?