Kumbe Sitta aliwahi kumsomesha Zitto

Kumbe Sitta aliwahi kumsomesha Zitto

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,548
"Sitta ndiye aliyenisomesha kidato cha tano na sita. Wakati huo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na ofisi yake ilikuwa jirani na jengo la Benjamin Mkapa Tower. Nilienda ofisini kwake na kumwambia kuwa nataka kuhama kwa sababu kule Galanos hakuna walimu, nikamwambia nataka kusoma hesabu kwa sababu nilikuwa nachukua masomo ya Historia, Jiografia na Uchumi (HGE) na nilitaka kubadilisha na kusoma uchumi, jiografia na hesabu (EGM). Kutokana na Sitta kufurahishwa na matokeo yangu, kila likizo kabla sijaenda shule nilikuwa napita kwake na alinipatia ada na fedha za matumizi, kuanzia kidato cha tano hadi sita na baadaye tulikuja kukutana naye bungeni"-Zitto
=======================================

Ni mengi yamesemwa kuhusu mwanasiasa huyu kijana ambaye ameongoza harakati za kisiasa katika chama chake, Chadema kwa mafanikio, ingawa safari yake ndani ya chama hicho inaelekea kuishia mahali pasipo salama. Pia, ameongoza kamati muhimu za Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mafanikio makubwa. Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Zitto ana lipi la kueleza?

Swali: Hivi ukiacha siasa unatarajia kufanya shughuli gani?

Jibu: Mimi ni mchumi na mtakumbuka baada ya hoja ya Buzwagi mwaka 2007, kamati ya Jaji Bomani (Mark) 2007/08 tulivyo-submit (wasilisha), ripoti ya Bomani iligundua kwamba sina maarifa ya kutosha kwenye uchumi wa madini, hivyo nikaamua kwenda kusoma Ujerumani Masters ya pili ya Law in Business (Shahada ya Uzamili ya Sheria za Biashara), nikiwa bado mbunge mwaka 2009/10.

Katika Masters ile andiko langu lilihusu mfumo wa kodi kwenye sekta ya madini, mafuta na gesi. Kwa hiyo nimekuwa nikifanya chambuzi mbalimbali kama huu nilioufanya leo na kutumika katika gazeti dada la Mwananchi, The Citizen kuonyesha ni kiwango gani cha mapato ambacho Tanzania itapoteza katika kipindi cha miaka 15 ya uchimbaji wa gesi, ambayo ni Dola 55 bilioni ambayo ni zaidi ya mara mbili ya uchumi wa Tanzania.

Kwa hiyo, ninashiriki katika hizo professional associations (vyama vya kitaaluma), mimi sina biashara na sijui biashara na sina interest (nia) na biashara. Kazi ninayoipenda ni kufanya chambuzi na kufundisha.

Nimeombwa na mmoja wa maprofesa Chuo Kikuu Dar es Salaam kumsaidia katika darasa lake la Masters ya International Trade, pili Chuo cha Taifa cha Masuala ya Ulinzi (National Defense College) kule Kunduchi nimehadhiri kwenye masuala haya ya madini, gesi na mafuta.

Swali: Vipi kuhusu familia, umeoa na una mtoto?

Jibu: Nina mtoto mmoja lakini sijaoa. Mtoto wangu anaitwa Chachage na nilimwita jina hilo kwa sababu Chachage (Profesa Sethy, marehemu) alikuwa mwalimu wangu Chuo Kikuu na alifariki Julai, 2006 na mtoto wangu alizaliwa Novemba 2006.

Mimi ni mjamaa kiitikadi. Watu wangu ni kina Chachage na Profesa Issa Shivji. Tangu nikiwa chuo, Profesa Shivji anafundisha sheria, lakini most of the time (muda mwingi) niko ofisini kwake wakati mimi nilikuwa nasoma uchumi. Chachage alikuwa anafundisha sosholojia.

Sababu inayonifanya nisioe mpaka sasa ni kutotaka kuanza kujenga familia yangu wakati nina jukumu la kuhakikisha wadogo zangu wanalelewa properly (vyema).

Swali: Marehemu mama yako (Shida Salum) amewahi kukushauri kuacha siasa na ufanye kazi unayoipenda ya kufundisha, ushauri huu unauzingatia vipi?

Jibu: Mama ni mama, mama alikuwa anajua jinsi nilivyojitoa kuhakikisha Chadema inakuwa mpaka hapa ilipofikia kwa hiyo alipokuwa akiona migogoro ile na anajua kabisa kwamba these people are not fair (watu hawa hawakunitendea haki) kwa mwanangu kwa nini sasa mwanangu apoteze muda wake kwa watu ambao hawajali kazi alizofanya.

Mama alikuwa anajua kuwa napenda kufundisha na nilikuwa namwambia kuwa siasa ni wito na mimi wajibu wangu ni kuona kwamba tunaibadilisha nchi. Mimi nimesomeshwa bure, mfano ningezaliwa sasa pengine nisingepata elimu niliyoipata sasa hivi.

Sera za wakati ule mtu alisoma kwa uwezo wa kichwa chake na siyo uwezo wako wa mali, kwa hiyo siwezi kukubali kuiacha nchi wakati imenifikisha mbali.

Swali: Umefukuzwa uongozi na uanachama wa Chadema baada ya kuibuka kwa migogoro, unadhani ulionewa katika uamuzi uliochukuliwa?

Jibu: Kwanza, migogoro ni sehemu ya maisha na kwangu mimi nachukulia migogoro kama changamoto kwa kuwa hamna njia ambayo inanyooka moja kwa moja, njia zina kona. Changamoto na migogoro iliyotokea Chadema kwangu naona ilikuwa kunikomaza zaidi.

Bahati nzuri nimejenga uhusiano mzuri na watu na viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mmoja wa viongozi ambao ni role model (mtu wa kupigiwa mfano) wangu nje ya nchi ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir Mohamad ambaye kila mwezi Oktoba huwa nakwenda Malaysia kuonana naye.

Swali: Watu wanajiuliza Zitto Kabwe ni nani hasa, unaweza kusemaje?

Jibu: Kimaisha, Zitto ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya watoto 10, wasichana wanne na wavulana sita. Nimezaliwa katika Kijiji cha Mwandiga mkoani Kigoma na nimelelewa na babu yangu wa upande wa mama, ila wenzangu walipata bahati ya kulelewa na wazazi, mimi babu yangu, mzee Salum Mohammed alinichukua nikiwa na umri wa miaka minne na kuishi naye katika eneo la Mwanga Wilaya ya Kigoma, mkoani Kigoma.

Kukua kwangu kisiasa kunatokana na malezi ya babu ambaye alikuwa mwanasiasa. Alikuwa kiongozi katika ngazi za wilaya na mkoa wakati ule wa mfumo wa chama kimoja akiwa Mwana-Tanu na baadaye CCM.

Kitu kimoja ambacho watu wengi hawakifahamu, mimi nimejua kusoma na kuandika hata kabla sijaanza darasa la kwanza, kwa sababu babu yangu alikuwa hajui kusoma wala kuandika na alikuwa akiletewa barua za mikutano na kuchukua vijana wa jirani ili wamsomee, wakati mwingine vijana hao walimkatalia na hivyo babu aliniwekea mwalimu nyumbani kunifundisha kusoma na kuandika.

Nilianza darasa la kwanza nikiwa na miaka minane mwaka 1984 katika Shule ya Msingi Kigoma. Mapema, nikiwa na umri wa miaka mitano nilikuwa namsomea babu yangu barua zake za mialiko kwenda kwenye mikutano. Hii ilinijenga kisiasa tangu nikiwa mdogo kwa sababu barua zake nyingi zilikuwa za kisiasa, wakati mwingine yalikuwa ni makabrasha makubwa na sikuelewa, lakini nilikuwa nasoma tu ila yeye alielewa.

Kupenda kusoma tangu nikiwa mdogo ndiyo kumenijenga kwa muda wote na hivyo kuwa na discipline (nidhamu) kubwa ya kupenda kusoma.

Nilivyomaliza darasa la saba, nikaenda Shule ya Sekondari Kigoma na baadaye Sekondari ya Kibohehe iliyoko Moshi mkoani Kilimanjaro. Kulitokea mgomo Shule ya Sekondari Kigoma, mimi nikiwa kiongozi wa wanafunzi (kiranja) na ikawa wanatakiwa wanafunzi 20 walioanzisha mgogo ule wafukuzwe, nikakataa kuwataja majina na kuamua kuwajibika, nilifukuzwa shule nikiwa nimebakiza mwezi mmoja na nusu tu kabla ya kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Ilikuwa nimalize kidato cha nne mwaka 1994, lakini ikabidi niende kurudia kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kibohehe, nilifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 1995 na nilivyomaliza nikaenda Shule ya Sekondari Galanos, Tanga. Kwa jumla, matokeo yangu ya kidato cha nne yalikuwa mazuri sana na nilipata daraja la kwanza, karibu masomo yote nilipata alama A. Nilivyoenda Tanga sikupapenda sana, nikaomba kuhama.

Nikiwa kidato cha nne kule Kibohehe mwaka 1995, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati ule aligombea ubunge kwa mara ya kwanza Jimbo la Hai. Sisi ndiyo tulikuwa tukimsaidia katika kampeni zake.

Nilivyokuwa nataka kuhama shule, kutoka Galanosi kwenda Tosamaganga mtu ambaye alinitafutia uhamisho alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo, Samwel Sitta.

Sitta ndiye aliyenisomesha kidato cha tano na sita. Wakati huo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na ofisi yake ilikuwa jirani na jengo la Benjamin Mkapa Tower.

Nilienda ofisini kwake na kumwambia kuwa nataka kuhama kwa sababu kule Galanos hakuna walimu, nikamwambia nataka kusoma hesabu kwa sababu nilikuwa nachukua masomo ya Historia, Jiografia na Uchumi (HGE) na nilitaka kubadilisha na kusoma uchumi, jiografia na hesabu (EGM).

Kutokana na Sitta kufurahishwa na matokeo yangu, kila likizo kabla sijaenda shule nilikuwa napita kwake na alinipatia ada na fedha za matumizi, kuanzia kidato cha tano hadi sita na baadaye tulikuja kukutana naye bungeni.

Baadaye nilijiunga na chuo kikuu na nilipomaliza, nilikwenda kufanya kazi za kujitolea Chadema kama ofisa utafiti na baadaye nikaanzisha Idara ya Mambo ya Nje ambayo ilianzisha uhusiano wote ambao Chadema inao kwa sasa na Ujerumani, kwa sababu chama hakikuwa na idara ya mambo ya nje.

Wakati nasoma Ujerumani nilikuwa na-connect (mawasiliano) chama na vyama vingine internationally (kimataifa) na tukafanikiwa sana, nilivyorudi na kuajiriwa na FES niliomba nifanye kazi kwa asilimia hamsini, kati ya saa nane za kazi kwa siku ili nusu nyingine niweze kujitolea Chadema.

Mwaka 2005 nilikuwa campaign director (mkurugenzi wa kampeni) wa Chadema na nikaongoza kampeni za chama mwaka 2005 na tukapata wabunge wa kuchaguliwa watano na wabunge wa viti maalumu sita, nami nikawa mbunge na nikafanya kazi kuanzia mwaka huo hadi sasa.

Swali: Ilikuwaje ukamjua Sitta?

Jibu: Nilienda ofisini kwake, kama utakumbuka mwaka 1995 Sitta alishindwa ubunge wa Urambo na akawa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), kumbuka kuwa Ndeki (Alexander) naye anatokea Tabora. Nilivyoenda kuomba uhamisho nikakataliwa na nilikuwa nikitafuta mtu ambaye anaweza kunisaidia kupata uhamisho na nikaambiwa kwamba Ndeki ni wa Tabora na Sitta wa Tabora, mtafute Sitta.

Swali: Wewe haupo Ukawa, lakini umesusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba. Ukawa wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama wewe, kwa nini hujiungi nao?

Jibu: Siwezi kuwa Ukawa na nina sababu za msingi. Siyo kila mtu anayetaka serikali tatu anaupenda Muungano, kuna watu ambao wanaotaka serikali tatu hawautaki muungano na wamejificha nyuma ya pazia la serikali tatu.

Ndiyo maana msimamo wangu mimi wa serikali tatu siyo msimamo wa marais watatu kwa sababu najua msimamo wa marais watatu utavunja nchi. Msimamo wangu mimi ni rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano, mkuu wa Serikali Zanzibar na mkuu wa Serikali ya Tanganyika.

Chama chenye wawakilishi wengi kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitatoa Mkuu wa Serikali Zanzibar na chama chenye wabunge wengi Baraza la Wawakilishi Tanganyika kitatoa Mkuu wa Serikali Tanganyika na Bunge liwe moja, ndiyo msimamo wangu.

Baadhi ya watu wa Ukawa wanasema njia nyepesi ya kubakia na Zanzibar yetu ni serikali tatu, wengine wanasema njia nyepesi ya kubakia na Tanganyika yetu ni serikali tatu, mimi ni muumini wa Muungano na dola duniani kote hazivunjwi, bali zinaimarishwa. Mimi natakiwa nifikirie namna gani Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya zinakuwa sehemu yetu na siyo namna gani tunavyotengana.

Swali: Kama wewe siyo Ukawa, kwa nini huendi bungeni?

Jibu: Siko bungeni kwa sababu kule ni kupoteza muda, hauwezi kutengeneza Katiba ya nchi bila maridhiano. Lazima mridhiane ndiyo mkae mtengeneze Katiba kwa sababu Katiba haina mshindi.

Sasa leo karibu robo ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wapo nje na wengine wapo ndani ya Bunge wanaandika Katiba. Katiba itakuwa ya nani? Inaweza kupata uhalali wa kisheria lakini haitapata uhalali wa kisiasa. Nikasema siwezi kuwa rubber stamp ya mchakato ambao najua huko baadaye utarudiwa tu na ushauri wangu ni kwamba we need to stop (lazima tusitishe).

Chanzo:Mwananchi
 
Ndio maana ddogo ni ccm damu. Halafu dogo kama anachanganyikiwa vile. juzi kati kasema wapambe ndio wamewagombanisha na kamanda Mbowe. Mambo ya ajabu sana. Arudi kwao ccm tu CDM hatumhitaji ba hilo analijua.
 
Sasa hivi Zito anatapa tapa. mara aseme hivi mara vile. hata haeleweki ila ukweli ni kwamba. KISIASA ZITTO AMEKWISHA.
 
Kumbee! Me nlidhani alisomeshwa na UWT!!!!!!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Kwa jamii yetu ya kitanzania mtu kusomeshwa na mtu mwingine wala sijambo la ajabu, hongera ulipata mtu wa kukusomesha kuna watu wanatamani kusoma lakini wamekosa watu wa kuwasomesha
 
Hivi WAHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI HUWA WANAMPIGIA SIMU NA KUMUULIZA BOSI LEO UNATAKA KUZUNGUMZA NINI? TUKUANDIKE AU INAKUWAJE MIMI SIELEWI MAANA KILA SIKU HABARI ZA ZITO.
 
Aache kutumika,atumie haki yake kikamilifu.Ahamie mahali anapopataka ili awe huru.Kuliko sasa hajielewi anajifanya kusoma upepo unaelekea wapi.Inazidi kumpunguzia hadhi yake aliyoijenga kwa kipindi kirefu.Siasa za Tanzania zinahitaji umakini sana kutokana na Watanzania wengi sasa kufunguka kiakili.
 
Hivi WAHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI HUWA WANAMPIGIA SIMU NA KUMUULIZA BOSI LEO UNATAKA KUZUNGUMZA NINI? TUKUANDIKE AU INAKUWAJE MIMI SIELEWI MAANA KILA SIKU HABARI ZA ZITO.

Na yeye mwenyewe anakubali, na anaongea ili aandikwe..!!!
 
Hivi WAHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI HUWA WANAMPIGIA SIMU NA KUMUULIZA BOSI LEO UNATAKA KUZUNGUMZA NINI? TUKUANDIKE AU INAKUWAJE MIMI SIELEWI MAANA KILA SIKU HABARI ZA ZITO.

Mkuu mwananchi lilimtembelea zitto nyumbani kwake....na mahojiano yalikuwa marefu....hivyo huchapisha sehemu ya majadiliano hayo mpaka yatakapofika kikomo
 
mwanaccm damu huyo awez mchachafya mzaz wake mlezi
 
Sasa hivi Zito anatapa tapa. mara aseme hivi mara vile. hata haeleweki ila ukweli ni kwamba. KISIASA ZITTO AMEKWISHA.
Hizi correlation mnazofanya si za GT hata kidogo. Tazama Haya: Makongoro nyerere aligombea ubunge Arusha kwa opposition party, lakini baba yake alikuwa Nani?, vipi mabinti wa Wasira kuwa makada wa CHADEMA???!!, na Shemeji yake Karume kuwa kada wa CUF??!!
 
Sasa hivi Zito anatapa tapa. mara aseme hivi mara vile. hata haeleweki ila ukweli ni kwamba. KISIASA ZITTO AMEKWISHA.


Design ya Mrema Mrema hivi

Halafu hata majina yanaelekeana sana
Sitta
Zitto
 
Ukisoma habari za Zitto, unaona kabisa amejengwa kupitia mikono ya watu kadhaa wa kadhaa katika medani ya siasa. Lakini msimamo wake kisiasa umekuwa wa kuyumbayumba.
 
Zitto anawaumiza vichwa?? subirini anakuja mtatafuta pa kujificha
 
Hivi kweli ni ajabu Freeman Mbowe kumsomesha mtoto wa kada wa ccm..kama hana uwezo...siasa inawachanganya sana wanasiasa wachanga!,,,,,?
 
Back
Top Bottom