Zitto: Mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa na Serikali

Zitto: Mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa na Serikali

kwa taarifa yako wewe chali. Wachaga wanao uwezo wa kuweka lami na kujega majumba watakayo. Nyie jengeni dar wao wanajenga kwao.
Kingine,ni haki ya watz wote kupata maendeleo bila kujali chama. Huwezi kukaa na kusifia ccm kwa lipi lillofanya? kuwagawa watz kwa manufaa yao binafsi? kusafirisha twiga? dhuluma?
sisi watu wa kaskazini hatubabaishwi na wajinga wa ccm wala mtu yoyote. Katika mikoa yenye watu werevu wanatoka kaskizini.
kuna barabara gani kule imewekewa lami na mtu binafsi mkuu?
 
Maendeleo moja ya hulka ya watu.wa kilimanjaro na wamelelewa hivyo maendeleo huletwa na wao na si serekali.Mtu akipata hela popote kwanza ni jinsi gani anabadilisha mazingira ya kwao.Katika usafi wanaongoza kwa kuweka mazingira vizuri,juzi kwenye ya Afya kati ya mikoa miwili ambayo haijaripoti kipindupindu mpaka sasa.
 
Maendeleo ya Kilimanjaro hayajatokana na wakoloni Bali watu wake ....kumbuka hawa walikuwa na Native Gorverment " chagga council " ambayo ilikuwa na mandate kamili ha kuwaletea watu Maendeleo ...serikali ya mkoloni ilikuwa ikitoa allocations Kama serikali inavyofanya Sasa lakini tofauti "serikali " ya Kikimanjaro ilikuwa inaenda mbali zaidi kutoza Kodi kwenye mazao ....na kuweza kwa kutumia fedha zake yenyewe ..kujenga
Barabara za lami
Mifereji ya asili
Kuhudumia shule ( wanafunzi walipata chakula,madaftari,uniforms, bure kwa kutumia Kodi za kahawa ")
Kujenga Kasri Palace
Kujenga Legislative Assembly ( bunge ) la kisasa
Kuweka Mfumo Rasmi wa "mahakama"
Kuwa na walinzi wake
Kusomesha wanafunzi nje ya Nchi
Kujenga hotel Kati Ya kisasa kuliko zote wakati huo Afrika mashariki "kncu" ...pia ndio lift ya kwanza
Kujenga Chuo cha ushirika
Kujenga Kituo cha utafiti wa kahawa ..
Kujenga shule ya secondary ya Kisasa kuliko zote "lyamungo" ambayo ilikuwa kila chumba anakaa mwanafunzi mmoja au wawili ....na ilikuwa na facilities za kimataifa ikiwamo Bwawa la Kuogelea .
Kuwa na Akiba ya fedha za kigeni nje .....
Etc

Hayo yote yalifanywa na wananchi wenyewe kupitia Native Gorverment Kabla ya uhuru .....iweje Leo kuanza kuwaonea watu hawa kusema wanapendelewa?????????
Kilimanjaro ,Mji wake wa Moshi ilikuwa the same line as Nairobi Kabla ya Uhuru ........watu walikuwa wanatoka Nairobi Kuja kula raha moshi ....Native Gorverment ya Kilimanjaaro ilikuwa ni ya pili yenye nguvu Afrika mashariki baada ya Buganda ....iweje ionekane walipendelewa........zaidi wazee wengi wanaona MAENDELEO YA KILIMANJARO YAMESIMAMA AU KWENDA TARATIBU...KAMA YANGEENDA KWA KASI ILE BASI LEO HII SIJUI WATU WANGESEMAJE....
TAZAMA HATA MKOA WA TANGA HUU ULIKUWA MANISPAA KABLA HATA YA DAR ES SALAAM LAKINI NAO WAKASIMAMA .....NI LAZIMA TUWE WAKWELI
Watu kama zito haya mambo hawajui wanabwabwaja tu
 
Ndo maana tunazidi kuwa na maendeleo sasa wewe mgogo endelea kufa njaa hapo Dodoma kwwnu kwa kuishabikia ccm
Ndio naishabikia ili ilete maendeleo kama ilivyokuwa huko kwenu halafu tukishaendelea tutachagua upawa kama ninyi. Hapo vipi. Kiss kiss
 
Wachaga wana desturi ya kurudi kwao kila decembar kwa ni lazma wajenge kwao sasa haya makabila mengine yakishafika mjini yanasahau kwao nani ataenda kujenga huko? Ni vizuri mkamuuliza zito kabla hajalalamika kajenga kwao?
 
Imetafunaje mkuu wakati mimi kijijini kwangu kuoga asubuhi nawasha heater then naoga kwa shower angali wewe kijijini kwenu unatembea kilomita 5 kusaka maji na bado ukiyapata unayachemsha kwa kuni...
Haaaaahaaaaaa kama ndivyo mbona mnahangaika sana ili mchukue nji hiii. Tutawakata tu ccm ilishaleta maendeleo huko sasa kuleni bata na upawa. Ccm nzuri jamani hebu ona mnavyonjoi matunda ya uhuru
 
Mangi marialle alikuwa anafanya kazi UN kabla ya Uhuru mkumbuke pia Moshi ilikuwa na almashauri kabla ya Uhuru bila kusahau huduma nyingi kama SHULE MAJI BARABARA UMEME HUDUMA ZA AFYA nyingi zilikuwepo kabla ya Uhuru WAMISIONARI walituletea dini na maendeleo
 
Mzee wa kijijini kule uchagani ukimleta mjini ndio kwanza anaona anateseka kwa kua kule alikotoka analala bila msongamano mjini huku chumba kimoja watu 10 hata hewa utapatia wapi
 
Haaaaahaaaaaa kama ndivyo mbona mnahangaika sana ili mchukue nji hiii. Tutawakata tu ccm ilishaleta maendeleo huko sasa kuleni bata na upawa. Ccm nzuri jamani hebu ona mnavyonjoi matunda ya uhuru


Tunataka tuichukue nchi ili tuwaletee maendeleo coz hamjitambui.
"" UPINZANI KWA MAENDELEO""
 
Leo wakichangia mpango wa maendeleo wa miaka 5 baadhi ya wabunge akiwemo Zitto Kabwe,Amesema serikali imekuwa ikipendelea mkoa wa Kilimanjaro kwa miaka mingi na kuisahau baadhi ya mikoa mingine.

Zitto ameyasema hayo baada ya mbunge wa Rombo Joseph Selasini kuomba mwongozo kwa Chenge na kusema,Serekali inatoa tamko gani kwa hii tabia ya wabunge kuona mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa?

Mwenyekiti wa bunge ameiagiza serikali itoe tamko juu ya suala hilo,Maana linaweza kuligawa taifa na kuleta mtafaruku.

Hivi mi najiulizaga,maendeleo ya Kilimanjaro ni ya asili au ni ya upendeleo?
g
Mimi ni mkristo, na katika mikoa niliyoishi nje ya kilimanjaro hata katika nyumba za ibada niliona watu wa Kilimanjaro wakijitoa zaidi kuchangia huduma mbalimbali ikiwemo hata sadaka. Kanini imekuwa hivi sijui kama ni kujipendelea au vipi.

Lakini nadhani historia ina mengi ya kutufundisha, labda ni mazingira tuliyokulia (jiografia), wageni tuliokutana nao (Wamsionari na wengineo), changamoto za maisha, elimu na mtizamo wa serikali; vyote vyaweza kuwa na mchango. Kwanini hadi leo miaka zaidi ya 50 bado wahazabe wanaishi kwa kutegemea mizizi na uwindaji sina jibu, huenda serikali imewatelekeza kwa kiwango hicho. Mwaka wa 1990, mkoa mdogo sana wa Kilimanjaro ulikuwa na shule za Sekondari 93, na kati ya hizo za serikali zilikuwa kama 10 hivi. Lakini hata hizo chache za serikali, hazikujengwa na Serikali, ila zilitaifishwa kutoka kwenye mashirika na nyingine kutoka chama cha ushirika.

Kilimanjaro hususan wachaga ni mkusanyiko wa vikabila vidogo vidogo tofauti (different ethnic groups) kwenye mteremko wa mlima kilimanjaro, lakini waliweza kujenga mila na desturi ambazo ziliwaunganisha kwa kiwango kikubwa na waliungwanishwa na kuitia kwa watawala wao (Mangi), ambae miaka ya mwisho kabla ya uhuru waliweza kufikia hatua ya kuwa na mtawala mmoja miongoni mwa hao machifu kuwa chief mkuu (Mangi Mkuu), na kufanikiwa kuunda hata serikali ya wachaga by then. Waliweka mikakati ya matumizi bora ya ardhi, ikiwepo kilimo ya matuta (terracing) kwenye miteremko, walichimba mifereji kwa , ajili ya kilimo cha umwagiliaji (mifereji hii ilichimbwa kabla ya 1900). Hivyo, unaweza kujione hawa watu walikuwa wakipata maji karibu sana na majumbani mwao hata kabla za zama hizi za bomba. Walianzisha chama cha ushirika cha kwanza kabisa Africa KNCU (1930) ambacho kilichachua sana maendeleo ya zao la kahawa na jamii hii kwa ujumla. Chama hiki baadae kilijataifishwa na serikali na shughuli zote za kiuchumi kuhodhiwa na serikali ikiwepo kununua na kuuza kahawa.

Kwa upande mwingine Watu wa Kilimanjaro (hususan Wachaga) wanaamini kuwa walinyimwa fursa za kuendelea kwa muda mrefu na Serikali, na laiti kama wangetendewa haki basi wangekuwa mbali kuliko waliko sana.

Kwa mtizamo mwepesi, kila mkoa palipo na watu wa Kilimanjaro kumekuwa na tofauti na uhai zaidi kwa shughuli za kiuchumi, na sina hakika kama serikali ndio inayofanikisha haya.

Hivyo basi, inawezekana kukawa na ukweli kuwa serikali inawependelea watu wa Kilimanjaro kwa mtizamo mwepesi kwa kuwa tayari wanaishi Juu ya Mstari kulinganisha na Watanzania walio wengi. Inawezekana pia wakawa na lobbing kubwa kuliko Watanzania walio wengi, kwani wakati wengine wakililia shida ya msaada wa mahindi kwa ajili ya njaa, wao kilio chao kikawa barabara ambayo ni hatu moja zaidi. Kumbuka kilimanjaro, watu hawahamasishwi jinsi ya kuhifadhi chakula cha msimu, kama wanavyohamisishwa wengine kwani kwao hiyo sio issue kwao.

Kitabu "Life in Tanganyika in the Fifties" kilichoandikwa na "Godfrey Mwakikagile" kinaweza kutupatia japo harakati za watu wa sehemu mbalimbali Tanganyika katika harakati za kujiletea maendeleo yao.
 
kuna barabara gani kule imewekewa lami na mtu binafsi mkuu?
Barabara ya kutoka Kalali mpaka Nronga (Machame) inawekwa lami na watu wa Nronga... Ni kama Kilomita 5 mpaka 6 hivi... Na kampuni inayojenga ni Elerai Constructions.. Na barabara ya kutoka Makoa mpaka Nkuu ilishawekwa moramu na kutaka kuwekwa lami na wananchi wenyewe lakini kuna mambo yaliingiliana wakahairisha...

Hizi ni barabara za vichochoroni, sio barabara kuu... Ni kama tuseme kujenga lami kutoka pale kituo cha basi makonde mbezi kuingia huko ndani mpaka Mbezi juu..
 
..kitu kingine ni MOBILITY ya wananchi wa maeneo mbalimbali ya Tz.

..Wachaga wanaongoza kwa kuhama Kilimanjaro kwenda kutafuta fursa maeneo mengine ya Tz.

..sasa watu wanalalamika kuwa Wachaga wanapendelewa, wakati Wachaga wenyewe wanakimbia Kilimanjaro.

..kuna haja ya kubadili mentality ya wa-Tz. Kama eneo unaloishi halina fursa au serikali imesahau kupelekea maendeleo basi ni vizuri mtu akahama kwenda kuishi kule kwenye huduma nzuri.

..Chukulia mfano Marekani. Obama amezaliwa Hawaii, amesoma New York, amekwenda kufanya kazi Chicago/Illinois. Alipokuwa anagombea Uraisi alikuwa anajulikana kama the junior senator frm Illinois.
Umesahau akienda kutafuta fursa lazima arudi kwake ajenge nyumba aweke umeme na maji na fensi alafu anarudi tena mkoani kutafuta shilingi na hata kama ajasoma usishangae kumkuta kwa juhudi zake za kuuza hata bucha ya nyama lakini mtoto wake atasoma mpaka chuo kikuuu au atampeleka kusoma nje najua wengi watasema wanaibaa ukweli ni kwamba ukijitahidi kufanya kazi kwa bidii pasipo kuchagua kazi baada ya mda unakuwa na maendeleo. Tafuta historia ya wachaga walivyo teseka wakitafuta kipato ndio utaelewa maana ya kujituma. Pia zao la kahawa liliwainua sana.Jiulize kwa nini ukioa mwanamke wa kichaga hata kama wewe ni milionea hata yeye atataka ajishughulishe kuongeza mtaji au anakuwa meneja mkuu kwenye biashara zako yahani bega kwa bega.
 
Hila maajabu haya yameibuka bungeni pasipo kutarajiwa.
 
Mimi leo nimejiuliza maswali mengi baada ya kuona kwenye taarifa ya habari kwamba kuna mkoa shule ya msingi darasa la kwanza lina wanafunzi 300 mwalimu mkuu anambiwa wasipojua kusoma kuandika na kuesabu anashushwa cheo wakati hao wanafunzi 300 ni shule ya msingi yenye darasa la 1-7 kwa mkoa wa kilimanjaro.Hapo ndio tofauti ya ubora wa elimu inaanzia kweli darasa la 1 wanafunzi 300 mwalimu mmoja tena darasa uwanjani kweli kitaeleweka.
 
Mimi leo nimejiuliza maswali mengi baada ya kuona kwenye taarifa ya habari kwamba kuna mkoa shule ya msingi darasa la kwanza lina wanafunzi 300 mwalimu mkuu anambiwa wasipojua kusoma kuandika na kuesabu anashushwa cheo wakati hao wanafunzi 300 ni shule ya msingi yenye darasa la 1-7 kwa mkoa wa kilimanjaro.Hapo ndio tofauti ya ubora wa elimu inaanzia kweli darasa la 1 wanafunzi 300 mwalimu mmoja tena darasa uwanjani kweli kitaeleweka.
inabidi wahamie kilimanjaro, maana kule wachaga wanaondoka wanahamia mikoa yao
 
kuna barabara gani kule imewekewa lami na mtu binafsi mkuu?
Nyingi sana kuna barabara inayotoka makutano ya kuelekea sanya juu sokoni na kibongoto ile barabara ya kuelekea kibongoto hospital siyo serikali imeweka lami kuna barabara ya sambarai kwenda juu siyo serikali ile lami iliyowekwa
 
Nyingi sana kuna barabara inayotoka makutano ya kuelekea sanya juu sokoni na kibongoto ile barabara ya kuelekea kibongoto hospital siyo serikali imeweka lami kuna barabara ya sambarai kwenda juu siyo serikali ile lami iliyowekwa
shukrani kwa taarifa
 
Chagua upinzani banaaa hapo Moro majimbo 3 wamechagua upinzani baada ya miaka 5 morogoro yote itakuja kuchagua upinzani hawa wabunge wa upinzani uzuri wao hawakai kimya pale wanapoona shida jimboni kwao haijatatuliwa hii ndio inaipa upinzani ukuaji kila siku hata huko kilimanjaro ndugu zangu wasiha walistuka ndugu zangu wa same walistuka moshi vijijini wakastuka kuona maendeleo mbona yanadumaaa kulinganisha na majimbo mengine wakagundua shida ni ccm wakaitupa kwenye dastibini
 
Back
Top Bottom