Duh?????????
Ama kweli kazi ipo... Ati wanapendelewa????
Moja, Kama ni kweli wanapendelewa, na nadhani si kisiasa tu kama mnavyotaka kutuaminisha wengi wenu humu ndani. La hasha tuanze kujiuliza maswali kwanza,
1. Mlima mrefu kupita wote afrika, wenye kutoa theluji uko wapi???
2. Na ni kwa nini mwenye mamlaka ya kuiumba Dunia aliamua kuupeleka Kilimanjaro na si Tandahimba, Mtwara ama Matombo, Morogoroau Kibandamaiti, Zanzibar???
Basi kama ni upendeleo haujaanza baada ya Siasa zetu tunazotaka kuzileta hapa, Hata upendeleo umeanza tangu kwa Muumba wa mbingu na Dunia.
Mbili, nina uhakika leo hii pale bungeni mkipiga takwimu ni wangapi wasiosoma Kilimanjaro ama wengi wetu tunaosoma hii post ambao miaka ya 1995 kurudi nyuma mlikuwa mko Olevel kama haukuwa unasoma Mbeya ama Iringa basi angukio kubwa zaidi lilikuwa ni Kilimanjaro. Mfano, Zitto nakumbuka alikuwa vidato viwili mbele yangu Kibohehe, Hai. Iliweza wasomesha wazawa na wasio wazawa wa mkoa husika pasipo shaka Leo hii mnasema wanapendelewa????
Taasisi nyingi sana zakidini zimejenga zaidi Kilimanjaro kuanzia Mashule, mahospitali n.k kuna Mashule kama Hiyo Kibohehe iko chini ya jumuiya ya Kiisilamu, Majengo Sec. Uru, Maua Seminary n.k zilizo chini ya ya wakatoliki, kuna Kolila iliyokuwa chini ya Walutheri ambayo hivi sasa iko mbioni kurejeshwa chini ya Serikali, Mahospitali kama KCMC........ Tangia miaka hiyo ya themanini leo hii mnasema wamependelewa na Serikali?????
Tatu, uchapakazi wa wahusika wa mkoa huo nao ni wamependelewa na Serikali??? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Hawa majamaa walikuwa na shule karibia kila kata kabla hata Serikali haijaamua kutekeleza sera hiyo. walisimama kidogo katika sekta ya kuukuza mkoa wao kwa kuukimbia lakini hivi sasa nafasi pekee Moja ya UPENDELEO kutoka Serikalini ambayo ni kuvipandisha hadhi vyuo vingi vya Mkoani Kilimanjaro kuwa vyuo vikuu ndo vitairudisha tena kasi ya mkoa ule kama zamani.
Angalia karibia kila wilaya wana Chuo kikuu ama Chuo cha maendeleo kiliko chini ya Tengeru. Sasa kwa nini wasiendeleeee????? Moshi Mjini wana Ushirika na Veta , Moshi vijijini wana Stefano Moshi, Singa Chini na vya Maendeleo kibao, Hai wana vya taasisi vya dini pale Boma ya ngombe chenye Hadhi karibia na Veta,Marangu Teaching Collage huko Kwa Mbatia, Rombo........!
Kah.....! bado mnasema upendeleo umetokana na Serikali?????
Naamini kama upendeleo kwa Mkoa ule umeanzia toka Kwa Mwenyezi Mungu na si Serikali kama mnavyotaka kutuubiria hapa.
Kwa kumalizia kuna msemo wa kimatani zaidi wanasema kama ukienda popote Tanzania hii ukamkosa Mchagga kimbia hapo maana hilo eneo halifai kuishi. japo ni maneno ya kiutani Je, ni kwa nini hawakusema Kama hakuna Mndengereko??? Kwa hiyo hata watunzi wa matani wanawapendelea Wachagga???
Hongereni wachagga, Kazeni buti.